hii ndo motel agip mtaa wa pamba dar. hapa ndipo disko la clouds lilipoanzia kabla ya kuhamia hoteli ya new africa miaka hiyo chini ya ma-dj emperor, joe johnson olela na bonny luv. jengo hili ambalo kwa sasa ni kama gofu kwa kukosa shughuli kwa miaka kibao ndimo chimbukoa la clouds 88.4 fm pamoja na prime time promotions na pia mawingu studio iliyoko mwenge na mawingu disco liliotesa sana a-taun wakati fulani. inasemekana zali la umiliki wa jengo hili lipo mahakamani na haijulikani litaisha lini ama hoteli hii itafunguliwa lini na nani ukizingatia mmiliki wake emmanuel manthiakis ambaye alikuwa pia balozi wa heshima wa ugiriki keshafariki kitambo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2007

    joe johnson olela hajawahi kuwa dj hapo na kama aliwahi basi sio na clouds tulikuwapo tokea siku disco linaanza, Boni Luv nadhani naye alianzia new africa seventh floor.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2007

    Michuzi Unapoteza historia ya hapo Motel Agip au shimoni kama palivyo julikana enzi hizo, Joe johnson Olela alikuwa space 2000 (Mbowe) wakati hapo pana boom.Waanzilishajii wa hapo walikuwa ni Mzee mzima mwenyewe Joseph Kusaga, Jese Mwalongo, Richard Mazula (Ebonite wall jack) na Stuwart Chiduo, baadaye akaja Bonny luv, baada ya wazee wazima kujikata. Rupia

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2007

    Maelezo ya hapo juu yote natumaini niya kweli. Kumbukumbu zangu nikuwa hiyo ilikuwa around 1988 hivi ndiyo Clouds ilianza ku hit kabla ya kwenda 7th floor New Africa Hotel. SteveD.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2007

    Nadhani Emmanue manthiakis bado yu hai.... Ukicheck na Movenpick Hotel utapata uhakika wa jambo hili

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2007

    brother Michuzi naona historia imekupita kidogo, lakini sio mbaya utu uzima na mambo mengi kichwani ukiangalia mara luku mara maji sometimes easy kuforget. my point is kuhusu holela akuwepo kabisa dsm wakati huo,pili ukitaka kujua historia ya clouds MOTEL AGIPmuhulize YUSUFU TARZAN,CARL LEWIS FANUEL LIGATI,WATOTO WA FOUR WAYS (ILALA)au waanzilishi wenyewe wa clouds yaani WATU WA UPANGA ambao tumeanza na JOSEPH tokea anapiga boogie HELLENIC CLUB.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2007

    jamani CLOUDS sio ndio ilikuwa BIRIBI, wakati justin kusaga alivyoshuka na vyombo toka holland,nakumbuka huu moto ulikuwa italian club, hii ni 79/80 kama sikosei

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2007

    SASA ANANY HAPO JUU WA JUNE7 SAA11:10 KWELI KUMBUKUMBU ZAKO KWAMBA CLOUDS NA BIRIBI NI KITU KIMOJA? HAYO NI MADISCO MAWILI TOFAUTI KWANZA BIRIBI ILKUWA HATA JOSEPH HAYUKO DSM ALIKUWA ANASOMA MOROGORO KIUMRI ALIKUWA BADO KABISA,PILI BIRIBI ILIKUWA NI VYOMBO VYA JUSTINE MWENYEWE,TATU CLOUDS ILANZA BAADA YA MZEE KUSAGA KUONA JOSEPH ANAHAING ANA MPANGO WOWOTE NDIO AKAMNUNULIA VYOMBO VYA DISCO NA NDIO MPAKA LEO UNAIONA HAPO ILIPO.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2007

    Nakubaliana na Anony wa 8.08, Manthiakis is still very much alive. He resides in Masaki as today!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...