
kunradhi: wadau ni kweli picha ya chini ni kikosi kilichocheza na bukina faso dar. ya juu ni kile kilichocheza na chipolopolo mji kasoro bahari. hapo kuina mwaikimba, njojhole, costa na maxiime ambao hawakwenda wagadugu. samahani kwa usumbufu uluiojitokeza kutokana na makosa ya kibinadamu. hongera wadau kwa kuwa shapu. mnanitia moyo wa kuwa makini. vile vile mfungaji wa bao kule wagadugu hakuwa henry joseph bali ni erasto nyoni. kwa niaba ya mapaparazi wa bongo tuliochemsha bila shaka kwa msisimko (hata juma nkamia wa tvt naye alisema henry joseph) naomba radhi wadau kwa usumbufu. vile vile huyu erasto hivi sasa anakwenda kuchezea vitalo ya burundi
taifa staaz usiku huu wametua mwanza wakitokea bukina faso na kupokewa kwa shangwe na maelfu ya wakazi wa jiji hilo la mawe. inasemekana kesho watapita dodoma kwa muda kusalimia wazee kabla ya kutua dar milango ya saa kumi jioni ambako mapokezi ya kufa mtu yameandaliwa. pichani ni kikosi kilichocheza mechi ya kirafiki na zambia 'chipolopolo' uwanja wa jamhuri mji kasoro bahari. na ni listi hiyo hiyo iliyowabenjua bukina faso. jk hatokuwepo kwani yuko kampala ambako anahudhuria kikao cha wakuu wa isti afrika mashariki na pia ataelekea burundi kwa ziara rasmi ya siku tatu.
toka shoto juu: erasto nyoni (ashanti), nadir Haroub 'kanavallo' (yanga), shaaban nditi (moro united) henry joseph (simba), salum swedi (mtibwa). chini toka shoto: nizar khalfani (mtibwa), saidi maulidi 'smg' (yanga), ivo mapunda (yanga), shadrack nsajigwa (yanga) na amir maftah (mtibwa).
huko maputo ngoma droo - si senego wala msumbiji waliopata bao. hivyo 'kinyekinye-kisonzo' bado kipo kwa safari yetu ya ghana....
Bro michuzi,samahani mbona huyo unaesema ni Amir Maftaha sio yeyeÉembu cheki vzr hiyo picha yeye huwa ana dred
ReplyDeleteHivi ni kweli mlima lkilimanjaro unayeyuka? Nimesikia leo kwenye usa fox channel new at 9 pm eastern time
ReplyDeleteMICHUZI HIYO PICHA ULIWEKA SIYO YA TEAM ILIYOCHEZA NA CHIPOLOPOLO.HUYO WA KWANZA KUSHOTO NI HENRY JOSEPH SIO ERASTO NYONI.. WAANDISHI WA BONGO MNA TABIA YA KUKURUPUKA SANA. MFANO KAMA WALE WATANGAZAJI WA RADIO NA TELEVISIONI WOTE WALIKOSEA MFUNGAJI WA BAO LA STARS JUZI!! BAO LILIFUNGWA NA ERASTO NYONI ILA WA TV ALISEMA HARUNA MOSHI NA WA RADIO AKASEMA HENRY JOSEPH. HUO NI UNAZI UNAWASUMBUA.. KWENYE HIYO PICHA WA KWANZA KUSHOTO NI HENRY JOSEPH NA SIO ERASTO NYONI.
ReplyDeleteMICHUZI MAJINA HAYAENDANI NA PICHA, REKEBISHA. INGEKUWA (BWAWA LA MAINI)LIVERPOOL USINGEKOSEA UNAWAJUA WACHEZAJI WOTE. LAKINI TEAM YAKO YA TAIFA HUWAFAHAMU, SOKA LETU LINAHITAJI UZALENDO HATA WAKUFUATILIA TU. Sio ajabu hata tukisema uimbe wimbo wa taifa utashindwa, lakini ngwasuma na twangapepeta unazijua nyimbo zao album moja baada nyingine- by Mtu wa Mpira.
ReplyDeleteWACHEZAJI ULIOWATAJA NA PICHA HAVIENDEANI.
ReplyDeleteAhsant michuzi, mbona picha inamuonyesha Mwaikimba ambaye hakuwepo Morogoro kwenye Mechi?
ReplyDeleteMICHUZI KUNA KOSA HAPA,HICHO NI KIKOSI KILICHOCHEZA NA BURKINA FASO SEPTEMBER MWAKA JANA NA SIYO CHIPOLOPOLO
ReplyDeleteKWA MAONI YANGU TAIFA STARS INACHOHITAJI NI USHINDI TU DHIDI YA MOZAMBIQUE BILA KUJALI MATOKEO YA MECHI YA SENEGAL. NAFIKIRI KINACHOANGALIWA NI UWIANO WA POINTS KATI YA TIMU MBILI ZA KWANZA KATIKA KILA GROUP.SENEGAL NA TZ WAKISHINDA WOTE TUTAKUWA MA PTS 11 WAKATI KWA MFANO SUDAN AU TUNISIA MMOJA WAO AKISHINDA WATAPISHANA PTS 4 UKIANGALIA MFANO HUO UNAONA SISI NDIO TUTAKUWA BEST RUNNERS-UP.HAIWEZEKANI KUWA TIMU YOYOTE ILIYOZOA POINTI NYINGI NAFASI YA PILI NDIYO INAYOPITA MAANA KUNA GROUP AMBALO LINA TIMU TATU TU. MSHINDI WA PILI KWENYE KUNDI HILI KWA VYOVYOTE HAWEZI PATA ZAIDI YA PTS 9. WATAALAMU WA SOKA CHUNGUZENI ZAIDI MTUPE HALI HALISI.
kaka michuzi
ReplyDeletehapa umechemsha hii ni timu iliyokipiga na burkina dar, wachezaji kama huyo mrefu wa kwanza kulia waliosimama wima na njohole watatu kutoka kulia waliosimama wima hawakuwepo wagadugu.
Tunashukuru kwa kufanya masahihisho kwa kuweka picha muafaka !!!! Lakini hata kama haujaenda shule za kizungu HUWEZI KUSEMA naomaba nikunukuu kama ulivyoandika hapo juu "......... isti Afrika mashariki ....... ". Hiyo ni sawa sawa na kusema barabara ya Morogoro Road !!! Upo hapo ????? Jitahidi kuandika kitu ulichona uhakika nacho Bw. Misupu !!!
ReplyDeletekinachotakiwa ni pointi zote tatu na magoli dhidi ya msumbj. lakini utata ambao nadhani wengi hatujauelewa vizuri ni vile vigezo vya mshindi wa pili ... inakuwakuwaje hasa ktk kufuzu as best runners - up?
ReplyDeleteWADAU NI KUWA WANAANGALIA MWENYE MAXIMUM POINTS KATIKA KILA GROUP HASA KWA GROUP ZENYE TIMU 4 KWANI KAMA SUDAN WAMESHAJIKUSANYIA POINTS 12 HIVYO AUTOMATICALLY WANA WAMEKWALIFY. WE NEED TO BEET MOZAMBIQUE THEN TUOMBE MUNGU KUWA TUWE MIONGONI MWA WENYE POINTS 11 KATIKA NAFASI TATU ZILIZOBAKI
ReplyDeleteSomeni hapo mtaona ACN regualtions na second best anapatikana kwa criteria gani???
ReplyDeletehttp://www.cafonline.com/pdfs/NationsCup_E_2002_2004.pdf
JAMANI MNAOTAFUTA WACHUMBA MBONA HAJITOKEZI EMAIL YANGU NI don_1978@hotmail.com, TAFADHALI IKIWEZEKANA TUMA NAPICHA YAKO PIA.
Safi sana kwa marekebisho mjomba Michu.
ReplyDeleteHongera kwa Taifa Starz na UFAFANUZI wa Mh Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mgawanyo wa mchango wao fedha kwa timu ya taifa kama zawadi ya ushindi dhidi ya Burkina Faso. Hii ni moja kati ya changamoto muhimu sana kwa viongozi wa michezo Tanzania.
Tanzania Gooooo
umekosea kaka michuzi shaban nditi yupo mtibwa,amir maftaha yupo yanga,erasto nyoni yupo vitalo ya burundi, kwa taarifa tu nizar khalfan,amir maftah na erasto nyoni ni matunda ya serengeti boys ya king kibaden mputa.
ReplyDeletemsomaji morogoro
Michuzi, "isti afrika mashariki" ndio nini?
ReplyDeleteAnon, "global warming" haiogopi Mlima Kilimanjaro! Unapenda Fox TV Channel?
Lakini Michuzi mbona kwa muda mrefu imekuwa ikiandikwa kuwa Erasto Nyoni na Salvastory Ntebe wanachezea Vital'O ya Burundi? Nyoni alirudi na kujiunga na Ashanti na sasa anataka kwenda tena huko Burundi?
ReplyDeleteNaomba ufafanuzi. Pia Amir Maftah hachezei Mtibwa bali Yanga. Leo ni mara ya pili nakukosoa ndugu Michuzi.
Taifar Stars ina nafasi ndugu zanguni. Kitu muhimu ni kujihakikishia ushindi mnono mechi yao ya mwisho bila kujali kama Senegal watashinda au vipi. Naamini sisi tunaweza kupata "viti maalumu" kwenda Ghana kama tutalingana point na Senegal.
Lakini wasiwasi ni kama tutakuwa na magoli machache ya kufunga dhidi ya kufungwa na kukawa na mshindi mwingine wa pili ktk kundi lake mwenye point sawa na wa kwanza lakini mwenye wastani mzuri wa magoli ya kufungwa v kufunga.
Tukiamua tunaweza. Karibu Ghana 2008!
Hayaaaaaaaaaaaa!!! Mambo yameiva, kwa wale wasiojua criteria za best looser, mshindi wa pili, mnahabarishwa tena kwa uhakika kwamba kinachomata ni idadi ya point sio difference btn the group winners... salalaaaa!!! hio sio criteria nzuri lakini tutafanyaje ... kwa mantiki hiyo CAF washampitisha Sudan kama best looser, this is to say nafasi moja kwishakwenda... sasa ndugu zangu kuna haja ya kufanya triki hapa,,,, TFF wahakikishe mechi inachezwa wakati mmoja na ile ya Senegal kwa maana tuombe Senegal kama hawana liwanja kama la kwetu... ili wao wacheze kawaida jioni ... na sisi tucheze usiku,,, meaning iwe wakati mmoja kusiwe na kupanga matokeo kwa habari kamili kutoka CAF... hizi hapa wadau http://www.cafonline.com/news.php?id=60
ReplyDeleteHayaaaaaaaaaaaa!!! Mambo yameiva, kwa wale wasiojua criteria za best looser, mshindi wa pili, mnahabarishwa tena kwa uhakika kwamba kinachomata ni idadi ya point sio difference btn the group winners... salalaaaa!!! hio sio criteria nzuri lakini tutafanyaje ... kwa mantiki hiyo CAF washampitisha Sudan kama best looser, this is to say nafasi moja kwishakwenda... sasa ndugu zangu kuna haja ya kufanya triki hapa,,,, TFF wahakikishe mechi inachezwa wakati mmoja na ile ya Senegal kwa maana tuombe Senegal kama hawana liwanja kama la kwetu... ili wao wacheze kawaida jioni ... na sisi tucheze usiku,,, meaning iwe wakati mmoja kusiwe na kupanga matokeo kwa habari kamili kutoka CAF... hizi hapa wadau http://www.cafonline.com/news.php?id=60
ReplyDeleteMashabiki wa Kitanzania, pamoja na kwamba mimi sio mwanamichezo bora au Rick Abdallah mzuri, Naomba kuwapa tathimini ya kazi iliyo mbele yetu! Kwanza La muhimu ni kwamba tushinde kila mmoja anakubaliana na hilo pili je! Tukishinda alafu Senegal nayo ikishinda itakuwa je? Maana yake tutagombani nafasi mbili zilizobaki maana moja imeangukia kwa Sudan. Swali je ni nani hao wanagombani nafasi ya mbili: Jibu ni our THREAT ziko kwenye group 6, 8, 9 and 11. Kwa vipi uchambuzi huu hapa:
ReplyDeleteGroup 6: Threat is when
Eriteria Vs Swaziland:- hapa ni kama Eriteria Atashinda
Group 8: Threat is when:-
Gambia vs Algeria & Guinea vs Cape Verde :- hapa ni kama Guinea na Algeria watashinda mechi zao
Group 9: Threat is when:-
Benin vs Siera Leone, Togo Vs Mali: - Hapa ni kama Togo vs Mali watadraw alafu Benin washinde no issue, however if match btn Togo and Mali itakuwa sio draw na Benin akashinda --- kimbembe
Group 11: Threat is when:-
Zambia vs South Africa, problem is only when Zambia beat South Africa ... not very much likely!
Kwa hiyo kwa kifupi nafasi mbili zinagombaniwa na group 6,7,8,9 and 11... we are in group 7.
Our challenge ni kufungwa magoli mengi na Senegal, kwa hiyo ilitujiweke pazuri tushinde na pia kwa magoli mengi.
Mungu Ibariki Tanzania
Ahsante kwa kunisoma.
Habari hizi bila kubania waweza kuzifuatilia hapa
http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/6498881.stm
Jamani ehhh hizi nderemo zote tungengoja baada ya mechi yetu na msumbiji maana kimbembe bado kipo sasa naona watu wana ndoto za furaha hii sherehe mpaka kwenye bunge ingengoja mwezi Septemba na sio sasa au watu wanaogopa ya kuwa tutakuwa kwenye swaumu hivyo hawatoweza kushereheka kwa kukufuru
ReplyDelete