historia imewekwa leo baada ya taifa staaz kukaribishwa ndani ya ukumbi wa bunge na kupokea pongezi rasmi za serikali ya jamhuri ya muungano kwa kazi nzuri waliyofanya. vijana wetu walipata pia heshima ya kupiga msosi na wah. kabla ya kupaa kuja dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2007

    du vijana sasa wasivimbe vichwa tu maana hapo ninavyojua sisi wabongo na huo mkwanja huchelewi kumaliza mtaa mzima......

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2007

    oooooh what a day!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2007

    safiiii safiiii sanaaaaa!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2007

    safi sana!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2007

    Ongereni! Hila ilo la kuingia na Jezi Bungeni halifai...kunaitajika Taifa stazz kuwá na suti zao rasmi.Kufanya kosa sio kosa hila kurudia kosa ndio kosa..tujifunze kutoka kwa wenzetu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2007

    daa vijana kweli sijui mnajisikaje sasa kazi imebaki mjitume sept.mpate raha tena kama hii na sisi wadau tujimwage kwa furaha mjipange maana mechi ijayo itakuwa lala salama

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2007

    imependezaa hiyo safi sanaa yaani hamkuwahi kufikiria kama siku moja mtakuwa bungeni mnapata msosi na waheshimiwa sasa mkitaka kupata tena msosi hevi kama huo ikulu fanyeni mambo sept.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2007

    hili dili hili leo nikitoka kwenye box naenda park kujinoa miezi sita tu narudi kuchezea taifa stars.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2007

    ndio mwanangu mwenyewe shabani musa nditi,aminia babaake,mdau.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2007

    Kitu cha maana kusikia toka Bungeni toka mwaka umeanza.
    Ukija na medali bungeni...ukishinda hatua ya kwolifaing,bungeni...
    Safi sanaaaa!
    Ni mtazamo tuu,masela msijenge chuki.Ata na Majani...

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2007

    hututaki negativity jamani sisi leo tunafurahi tu, ndio saaaaaaaaaaaafi saaaaaaaaaaaaaaaaana.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2007

    Home News More in this Category!
    Stars clinch another victory in Dodoma
    DAILY NEWS Reporters
    Daily News; Tuesday,June 19, 2007 @00:02

    320m/- contributed for their upkeep

    A HERO'S welcome, fund-raising functions in which 322.5m/- was raised on the spot and in pledges; and a special luncheon were some of the highlights of the grand reception for the national soccer team, Taifa Stars, here yesterday.

    It was jubilation all the way from the airport, where the government plane that had ferried the players from Mwanza en route from Ouagadougou in Burkina Faso, had touched down in the morning, to the Parliament Buildings here.

    Stars beat Burkina Faso 1-0 in an Africa Cup of Nations qualifying match, reviving Tanzania’s hopes of reaching the finals to be played next year in Ghana for the first time since 1980.

    The Prime Minister, Mr Edward Lowassa, who officiated at a special fund raising function held during the luncheon, told the players that with proper planning, they could make better use of the money instead of spending it on luxuries.

    Head of the delegation, Zanzibar’s Deputy Information, Sports and Culture Minister Mahmoud Thabit Kombo, then stood up and told the prime minister on the players’ resolve to invest their money in personal housing projects through such organizations as the National Social Security Fund (NSSF).

    "Honourable prime minister, on our way here from the Parliament Buildings, the boys had a lengthy discussion in which they decided that if they get as much as 200m/-, ways should be found to help them build houses or even get cars,’’ Mr Kombo said.

    Mr Lowassa advised them to liaise with NSSF Director-General, Dr Ramadhan Dau, who was present, to see how they can invest their money more profitably.

    At the Bunge reception ceremony, all MPs contributed 33m/- while the prime minister said he had 47m/-, which he had collected from four people. The Ministry of Infrastructure Development pledged 70m/-, bringing the total to 150m/-.

    The ‘harambee’ continued during luncheon at which Infrastructure Development Minister Andrew Chenge said his ministry and institutions under it were topping up their earlier pledge (70m/-) by 30m/-.

    Other pledges were made by Industries and Trade Minister (30m/-), Labour, Employment and Youth Minister John Chiligati (10m/-) while Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi pledged 15m/-. He also pledged a further 15m/- from his personal companies.

    Singida Urban MP Mohammed Dewji gave 30m/- while the proprietor of TIOT Company pledged 10m/-. Dodoma residents contributed 25m/- on the spot at the airport. Team captain Shadrack Nsajigwa received the money from the prime minister on behalf of his colleagues.

    Coach Marcio Maximo thanked all Tanzanians for their moral and financial support for the team, saying his boys, unlike the highly paid professional players, are faced with life’s difficulties including lack of transport.

    "Ask them, they are here…they board 'daladala' to come to the training ground, they don’t have proper accommodation which makes them share rooms,’’ Maximo said as the players cheered.


    Comment on this Story






    Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved








    Contacts:
    TSN Daily News building, Samora Avenue, Plot No. 7, P.O.Box 9033, Dar es Salaam,
    E-mail: newsdesk@dailynews-tsn.com; Telephone: +255222110595, Fax: +255222135239 0r +255222112881

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2007

    Hivi Kaka Michuzi, mimi sio mpinga umoja wa nchi yetu au sio mpinga michezo, Lakini hebu tuzungumze ukweli-hivi kweli muda na risosez zote hizi tulizopoteza kwa ajili tu ya kuwapokea Taifa staz zilistahili kweli jamani!?! Au ni ulimbukeni wetu tu?
    Ushindi tulioupata sio UBINGWA bado tuna safari ndefu, kweli tulihitaji kup;oteza pesa na muda wote huo kushangilia ushindi ambao sio ubingwa jamani? Vandumwe!
    Bunge limepoteza muda wake wa maana wa kujadili maswala muhimu ya kitaifa eti kuwaona na kuwapongeza.
    Ule muda wa bunge uliopotea utafidiwa kwa kuongeza siku za bunge mbele. Siku hizo zikiongezwa maana yake ni kwamba wabunge wanalipwa hiyo siku ya ziada. Hiyo pesa inayolipwa ni kodi ya mwananchi wa kawaida. Let us be serious jamani Mweeh!
    Radio Tanzania inaacha kutangaza mambo ya muhimu inaiba muda eti kutangaza live mapokezi ya timu ya taifa kila wanakokwenda. Vitu kama matangazo ya vifo ambayo ndugu wanatakiwa wapate taarifa za haraka yamecheleweshwa eti kisa taifa staz. Gharama ya hii haionekani imidiateli lakini mwisho wa siku ni mwananchi wa kawaida/mlala hoi ndio anaibeba.
    Hivi Michuzi what was so special hapo. Je timu ya kriket au netboli ikifanya kama hivyo tutafanya kama hivi tulivyofanya?
    Narudia sio mpinzai wa michezo au umoja lakini nina uchungu sana na nchi yangu hasa nikiona risosez zinapotea bure kam hivi na m bebaji mzigo ni mlala hoi. Hivi hata hao wafadhili wanaotupa hela za kuendeshea inji hii wakituona hivyo tunavyofanya si wanatusikitikia sana jamani? Hivi hata vitu hivi ambavyo viko vere ovias tunasubiri kwanza mpaka tuje tufokewe au tutishiwe kusitishiwa misaada na wafadhili jamani kwamba wenyewe hatu reason kweli jamami! tutishiwe
    Nina uchungu sana na nina mengi sana ya kusema lakini wacha niwaachie nafasi na wenzangu. Mnaohusika naomba mlione hilo. Hiki ni "kilio cha mtu mzima" jamani! Ohoo!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 19, 2007

    .Mheshimiwa issa, HABARI ZA LEO MAALIM SHUKRANI KWA LUGHA YA PICHA HIZI NZURI VIONGOZI NA WACHEZAJI WETU WANAJITAHIDI .."..KADRI YA UWEZO WAO.."..SIO MBAYA...NAONA WAHISHIMIWA WANAPATA MLO VILEVILE.."..MLO KAMILI..??.."

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 19, 2007

    hongereji taifa stars

    peres naungana nawe kwa kiasi fulani coz inaonena sasa tunaover do. nadhani kiasi kingehijika licha ya kuwa tunahitaji kufurahia upya wa hatua za mafanikio ya soka.

    lakini kitu ambacho nimeadhimia kusema ni kwamba watanzania ni wanafiki, vinyonga, sijui nisemeje. leo hii wanashangilia hivi; ikitokea, siombei ila hawa watu wakifungwa utashudia uchungu na uchafu wa midomo ya watanzania. mimi kama mzazi wa wanasoka watarajiwa huwa inaniuma wachezaji wanapofungwa wakiwa wamepondeka hakuna kiongozi/mwananchi anayetoka kwenda kuwa-hagi. kwanini machungu wale peke yao ushindi tushee nao.??

    jamani hawa ni watu nadhani ifike mahali nasisi tuwatendee haki. hatuwezi kushangilia kufungwa lakini tutambue juhudi zao wanazokuwa wameonyesha. na hata wanapotuletea ushindi tusiache kuchambua makosa yao. mf. nani yule kababaika golini kapiga juu tukakosa goli la pili...eeeh.. au ukiangali vizuri mapunda ivo anafanya kazi ngumu sana mabeki bado hawafanyi vizuri. mi sijui mpira vizuri lakini sioni umaliziaji mzuri bado ktk timu yetu. tushangilie na kukosoa ili kuboresha. magoli ya kubahatisha sawa ila na magoli ya kimahesabu yanajenga cv nzuri.

    Mzalendo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2007

    Perez hapo juu,
    Nakuunga mkono sana. Hatukustahili kwenda mbali kiasi hicho kwa kushangilia kama tumefika mwisho. Hii inafanana na methali "masikini akipata ........"
    Kushangilia tu kulikooneshwa ni motisha tosha. Au kiongozi angetoa kauli kupitia vyombo vya habari kwaniamba ya watz wote kuipongeza timu ingekuwa ni busara. Unajua wenzetu waliofika mbali, kutumia 'resouces' na kodi za wananchi wanajiuliza mara 2. Nikupe mfano 1 tu. Mie hapa nasoma ugenini, na vyuo vingi vinatoa ufadhili kiasi kwa wanafunzi wasio na uwezo kusoma bure kwa kodi za wananchi toka serikalini. Mwaka jana wananchi wametoa kura za maoni kufuta kodi hizo, kwani wao hawataki kuendelea kuumia. Sasa nilichogundua serikali zetu kama TZ, ukishika rungu unachota tu fungu la pesa na kuandikia matumizi, bila hata ridhaa au ripoti kwa walipa kodi.
    Pili, nimesikitishwa kidogo na mheshimiwa wangu Spika kufuta swali la mbunge DODOMA, kisa anadai katumia lugha ya 'kijiweni'kwa kusema "BAJETI NI SAWA NA MWIBA WA MCHONGOMA". Mie mtaalamu wa lugha japo sijisifii kuwa nimefuzu kila kitu, na siiti hiyo ni lugha ya kijiweni. Hii ni lugha ya picha. Lugha ya picha haiwi tu ya kijiweni. Nina mashaka kama kweli Kiswahili tunakijua vema.
    Kama nimemwelewa kiundani, Spika alitaka lugha hiyo ipunguzwe ukali. Na si lugha ya kijiweni kama anavoita. Nadhani anatakiwa naye kutofautisha dhana anazotumia.
    Pia nimeona jinsi alivyo'biased' kama kiongozi wa Bunge kwa kuita hiyo ni lugha ya kejeli. Je, kama ikithibitika na Watz wengi kuwa ni bajeti chungu, atasema nini? Anatetea kwa kusema watu wametumia muda wake kuiandaa, hiyo si hoja. Je, anaijua gharama ya kuipokea bila kuibeza itawaaumiza wananchi kiasi gani? Kweli nadhani tunahitaji busara toka kwa wazee na kama kauli za hasira na kugawa watu kimatabaka.
    MNASEMAJE, WADAU? Mimi sina chama chochote, ila naipenda nchi yangu... Najisikia kuchangia mawazo ilimradi situkani.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 19, 2007

    UKISHINDWA KUKASIRIKA CHEKA

    The ‘harambee’ continued during luncheon at which Infrastructure Development Minister Andrew Chenge said his ministry and institutions under it were topping up their earlier pledge (70m/-) by 30m/-.

    Other pledges were made by Industries and Trade Minister (30m/-), Labour, Employment and Youth Minister John Chiligati (10m/-) while Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi pledged 15m/-. He also pledged a further 15m/- from his personal companies.

    Singida Urban MP Mohammed Dewji gave 30m/- while the proprietor of TIOT Company pledged 10m/-. Dodoma residents contributed 25m/- on the spot at the airport. Team captain Shadrack Nsajigwa received the money from the prime minister on behalf of his colleagues.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 19, 2007

    Shukrani kwa stars kwa kututoa watanzania kimasomaso, na vile vile shukrani kwa wizara, taasisi na watu binafsi waliojitolea kuchanga pesa kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji wetu.

    Hivi hizi pesa toka wizara ya miundombinu na ofisi ya waziri mkuu si pesa za walipa kodi au wizara siku hizi nazo zinazalisha kiasi cha kupata faida na kuweza kutoa mchango wa mamilioni kwa stars kwa snapshot? au katika bajeti either ya mwaka jana au mwaka huu wizara hizi ziliomba zipangiwe fungu maalum kwa ajili ya kuwapongeza starz? napenda uzalendo lakini kwa pesa toka wizarani!? hususan wizara ya miundombinu ambayo inashindwa kujenga au kukarabati barabara zetu kwa ajili ya ukosefu kwa pesa ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi???!!!

    ReplyDelete
  19. wabongo bana hapo hata hio safari ya kwenda Ghana bado si ya uhakika lakini mapokezi utasema vijana wamechukua world cup.

    Sasa subiri wakirudi kweni vilabu vyao hao vijana si vichwa kuvimba na kuwazarau wenzio wao na makocha wa timu zao. Kwani hamuwakumbuki akina Mwaikimba hadi ajaifanya Cantona na kuwapiga mashabiki? Juma kaseja je? na rafiki yake mgosi kama sikosei wakaenda zao kuoa kabisa huko Tanga na wakakwepa kwenda kwene kambi ya simba.

    Wabongo bwana!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 19, 2007

    mie nafikiri hizi shamrashmara zingesubiri tukapata ticketi ya kwenda Ghana. Kwa jinsi mambo yalivyo sasa ticket sio guranteed.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 19, 2007

    I AM WITH YOU PEREZ, 110%

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 19, 2007

    E bwana MIchuzi, this is from the bottom(est) of my heart. Unatusaidia sana tulio nje. Sikuhizi sisomi tena ippmedia.com na web zingine mshenzi za bongo. Big up man. Hatujuani ila nikija bongo nitakutafutia zawadi na nitakutafuta.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 19, 2007

    acheni kufakamia mwisho mtavimbiwa buree mshindwe kufanya mazoezi. Angalieni diet pia, mafuta mengi sio mazuri kwa afya.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 19, 2007

    Jamani ndugu wa TZ tulio juu, tumeshindwa hata kutoa dola 1 kuonyesha nasisi tuko na wenzetu TZ,au pesa ya huku ni taaaaaaaaaamu,
    nawakilisha.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 19, 2007

    minyoo imeshtuka baada ya kuona huo msosi.Huku kambini wanakula hovyo hovyo.

    hongereni sana.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 19, 2007

    " Rewards can (Sometimes) squelch motivation"

    Mimi hili bado sijalielewa bado.Hivi nani aliwaroga watanzania? Hamjifunzi historia? Mankumbuka mechi ya simba fainali Dar na Stella At.

    Hayo wanayotendewa wachezaji sio yatakayokuwa nadni ya mioyo katika mechi zijazo.

    Nasikitika kwa hayo kuwa tumeondowa uwezo wa "ndani wa wachezaji" na kuwapa "uwezo wa nje"

    Kwa nini "Overjustification" ya namna hii??!

    Pole watanzania.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 19, 2007

    Michuziiiiiii naomba kukuuliza hivi hawataki fund raising kutoka raia walio nje ya nchi? Tungesupport kishenzi hizo jersey zao wangetengeneza nyingi na kutuuzia huku na pia Tracksuit.....

    Jamani hawana website tunaweza kununua huko....Tanzania ulimwengu wa e-commerce changamkieni tenda hiyo...hii sio lazima ipitishwe na TBS anyobe can open a site ansd sell this things online.

    Tukitaka kanda za nyumbani mpaka tukija au tumuagize mtu changamkieni hii biashara ulaji hapa

    Sijui hata kama serikali yatu ina keep data za raia wake walio nje ya nchi lakini ukweli tuko wengi na soko liko kubwa tu..

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 20, 2007

    Mheshimiwa Issa..VIPI MZEE..NI FURAHA TUPU i hope ..TUNASHUKURU SANA.."..NESHNO ASEMBLI GOZ GEY.."

    ReplyDelete
  29. Perez, nimeupenda uchambuzi wako. kama ulivyosema, ingetosha tu kiongozi wa serikali kutoa tamko la kuwashukuru vijana na kama ni kuwakaribisha makulaji wangefanya hivyo jioni baada ya shughuli za kawaida za Bunge. bila shaka siku moja ya shughuli za Bunge iliyopotea itafidiwa na walipa kodi watakuwa wamekamuliwa shs Milioni 33 za ziada za posho ya wazee wetu.
    Hivi hii ya kuonekana ni kitu cha ajabu timu yetu kushinda itakwisha lini? si timu ya taifa inatakiwa ishinde jamani? ina maana kila tutakaposhinda nje basi ni sherehe kama hizi? mbona naona kama hii ni aina fulani ya Inferiolity Complex?
    kama alivyoainisha Perez, kuandika haya hakumaanishi kukosa uzalendo....!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 20, 2007

    Machozi yanitoka saizi..have had dreams of our national team being well funded in other to make it to the next level..about time!! even if this cud be govt propaganda to cover their other blunders...Money well spent..

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 21, 2007

    anoni wa June 19, 2007 11:36:00 pm
    Iko mbona iko juu tuu! Search for "bongo radio" then nenda links; utakutana na internets sites za kumwaga ambao wanauza miziki ya wabongo.Pia kwenye blog hii kuna tangazo la "Mahusiano.com" unafikiri ni site ya dating?La hasha ni ngoma mtindo mmoja. Miezi michache ilopita "tzuk.org" walikuwa wanauza trakisuti za Tanzania tembelea huko labda bado wanazo.
    Kuhusu kuchangia staz, we watumie ela kutumia wstern money uone kama hazitawafikia.
    Mwisho anoni naomba kujua uko mkoa gani wa Iraq?Na Afriganstani ulihama lini?Au uko visiwa vya ukelewe?
    Nitafurahi nikisoma comments za Mbunge kuhusiana na hili la staz kwenda kujadili majeti.
    Muheshimiwa aliunda Tume ya mishahara kwa Civil Servants, staz ndo wamefaidika.Wafanyikazi wa sirikali labda msubiri kukiundwa Tume ya Taifa Staz, labda na nyie ndio mtafikiriwa.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 21, 2007

    SAWA KABISA MZEE PEREZ. NIMESHANGAZWA NA MOHAMMED DEWJI KUISAIDIA STARS MILIONI 30 WAKATI BARABARA YA DODOMA-SINGIDA HAIPITIKI HAWA WAKATI MVUA.
    NIMESHANGAZWA NA WABUNGE KUCHANGIA MAMILIONI YA FEDHA KWA AJILI YA TAIFA STARS TUU. TENA NDANI YA SAA 24, WAMEPATA ZAIDI YA MILIONI 300 HUKU WANANCHI WANAOJENGA NCHI WAKIUWANA KIGAMBONI.
    NDIYO! HAKUNA USAFIRI NA KIVUKO KILICHOPO (MV ALINA) HAKINA UWEZO WA KUMUDU VISHINDO NA MAHITAJI YA SASA YA KUSAFIRISHA ABIRIA.
    SISHANGAI KUONA SERIKALI KUINGIA MKATABA WA SERIKALI YA CHINA KUJENGA UWANJA MPYA WA TAIFA WAKATI WATU WALIKUWA WANAKUFA KILA MWAKA KIVUKONI/KIGAMBONI...KISA HAKUNA USAFIRI WA UHAKIKA.
    HIVI LINI SISI WASHAMBA TUTAAMKA TOKA KWENYE MABLANKETI NA KUANDAMANA KAMA MLIVYOFANYA JUZI KUISIMAMIA KIDEDEA SERIKALI NA KUTOA KAULI KUHUSU MASUALA MUHIMU?
    WATU MNAANDAMANA KWENDA KUPOKEA TIMU ILIYOSHINDA MOJA KATI YA MECHI ZA KUFUZU KWENYE MASHINDANO YA KUWANIA TIKETI ZA FAINALI ZA AFRIKA WAKATI HAMJUI MTAKULA NINI, MTAAMKIA WAPI?
    FURAHA KUBWA MLIYOONYESHA KWENDA IKULU STARS ILIPOSHINDA, IMEWAPA KICHWA WABUNGE WENU NA KUONYESHA JINSI WANAVYOWEZA KUTUMBUA MAMILIONI YA FEDHA HUKU WALALAHOI WAKIFA NJAA!
    LINI JAMANII TUTAAMKA. INATIA KICHEFU CHEFU KWELI HASA IKITILIWA MAANANI NCHI IMEJAA UMASIKINI, RUSHWA NGAZI ZOTE, MADAWA HAKUNA HOSPITALI, WAGONJWA WANALALA CHINI, BARABARA MBOVU, USAFIRI WA SHIDA NA MENGI TUU.
    MILIONI 300 ZINGENUNUA VITANDA VINGAPI KWA AJILI YA HOSPITALI. MILIONI 300 ZINGENUNUA MADAWATI AU VITABU VINGAPI KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI HUKO VIJIJINI...SIYO MJINI. JUST VIJIJINI TUUU.
    EEH MOLA WEEEE. WAAMSHE WAJA WAKO, WALIOKUMBWA NA HUYU SHETANI MKUBWA (S0KA), UWAPE FAHAMU NA KUANGALIA HALI ZAO ZA MAISHA. MAMBO YA TEGEMEZI YATAISHA LINI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...