wadau naomba kuuliza. hivi raha ya champeni ni ipi - kufunguka kisailensa ama pooooouw! kama hivi?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2007

    Michu, tatizo ni ndugu zangu Watanzania, champagne ikimwagika ndio wanaona mtu anajua sana kufungua chupa hizo, hawaelewi kuwa kuna tukio na tukio la kumwaga champagne, na pia sio kumwagika kama wataalam wengi wamwagavyo, huwa ina style yake ee baba..., kama ni for car rally, football championship, thats understandable kumwaga BAADA ya kuifungua

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2007

    Mimi nafikiri kisailensa ndo user friendly pasipo kuwepo na wastage of resources. Ingawaje hiyo poooooooooow inaonekana kama fashion kwa wale wasiopenda kubadilika, lakini watu wengi hawa-maindishi hiyo wastage style. Hayo mambo ya poooooow tuwaachie formula one akina ALLONSO na BUTTON

    Michuzi tupe uzoefu wako kwani umeshahudhuria sherehe nyingi ingawa hulipi kiingilio bali camera yako ndo kiingilio chenyewe.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2007

    Kumwaga siyo lazima, kuzibua kwa mlio ni poa, ila mimi huwa inaniuma sana kuona yooote inaishia chini, mgeni rasmi anaambulia nusu glasi! noma zaidi ni pale mnapoambiwa kuwa eti kuna chupa moja tuuu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2007

    raha ya champagne kwa mwafrika ni ule utumwa wa kiakili unaoambatana na wazo zima la kunywa na kumwaga champagne

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2007

    Kumwagika ama kutomwagika inategemea na shughuli inayosheherekewa. Kama unasheherekea ushindi basi kumwaga inakubalika. Lakini kama ni harusi ama shughuli nyingine kama hizo basi kumwaga haikubaliki.
    Katika mila za wachaga huwa wanapenda kumwaga mbege na kinywaji chochote kile wakisema kuwa wanawapa wazee waliowatangulia. Kwa hiyo wao wanaweza kuendelea kumwaga huyo shampeini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2007

    Yote hii ni utumwa wa fikra. hizi mila sio zetu ni mambo ya kuiga.
    so kumwaga au kutomwagika sio issue.

    Kwani Mbege na Kangara huwa zinamwagika. Mimi najua ktk matambika kumwaga kinywaji ndio sehemu ya tambiko. Sasa mimi nashangaa watu kumwaga 'kilaji' ktk Sherehe as if wapo ktk tambiko. ni mkanganyikoa ambao inabidi uondolewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...