michuano ya timu za vijana chini ya umri wa miaka 17 ijulikanayo kama copa coca cola imeanza jana kwenye viwanja vinne dar - karume, chang'ombe ttc, kawe na mlimani - katika harakati za kuvumbua vipaji na pia kuunda timu ya taifa ya vijana ya umri huo ili kupata taifa staaz iliyopikwa na kuwivya toka awali. jumla ya timu toka mikoa 28 ikiwa ni pamoja na unguja na pemba zinashiriki. wilaya za ilala, temeke na kinondoni zimepewa hadi ya mikoa ambapo kocha wa taifa wa timu ya vijana mbrazili marcus tinocco atatumia fursa hii kuanza kazi rasmi. wadhamini ni kampuni ya coca cola ambayo ilianza kudhamini michuano ya mtoano mikoa yote na mabingwa ndo waliokuja kwenye fainali ambayo mshindi atanyakua dola 4,500. pichani ni uwanja wa karume ambapo jana uliwasha moto rasmi wa michuano hiyo inayofungua ukurasa mpya wa kabumbu nchini, tofauti na awali ambapo wachezaji wa timu za taifa walikuwa wakichaguliwa kiholela toka vilabuni. kama alivyo kocha wa staaz marcio maximo, ujio wa tinocco, ambaye kaja toka mwanzoni mwa mwaka huu, unadhaminiwa na serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mwanzo mzuri. hapa nina imani tutapata wechezaji wazuri tena si kwa ubabaishaji kama ilivyokuwa mwaka juzi ambapo Wambura alidanganya umri wa mchezaji mmoja wa U-17 kwa kuigeuza 3 (1983) iwe 8 (1988)kwa kuitazamisha kinyume nyingine kama 'E' ya mcharazo ili mchezaji yule acheze. Kumbe alikuwa kijeba wa haja.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2007

    safi sana hii ndo siri ya mafanikio ya soka popote pale duniani,kuanza kukuza vipaji vya watoto,na lazima wapelekwe na shule ili waweze kuwasiliana kimataifa,na tuwauze nje ya nchi,hapo kakosekana mkwasa na kayuni tu,
    Kamtu-Chui

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2007

    MICHUZI- FURAHA YANGU IMEISHIA JANGWANIII.....
    Duh. Ama kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.
    Siku mbili zilizopita nilikuwa natembea kifua mbele baada ya Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burkina Faso huko Ougadouguou.
    Nilijuwa Yes! angalau mwanangu Januari 20, nitaanza kujiweka sawa na kushuhudia michuano ya Afrika huko Ghana ikishirikisha miamba ya soka ikiwemo Tanzania.
    Lakini baada ya kuketi chini na kutafakari jinsi msimamo wa michuano hiyo ilivyo hivi sasa, Tanzania inawania nafasi hiyo ikichuana na mataifa mengine makubwa wakati nafasi zilizobaki ni mbili tu!
    Kuna Afrika ya Kusini yenye pointi 11, Uganda, Algeria, Benin na Zambia zote zikiwa na pointi nane.
    Eritrea hainitii hofu sana kwani hata ikishinda na kuwa pointi sawa na Taifa Stars, haina rekodi nzuri sana inayozidi Taifa Stars.
    Stars kama itaibuka na ushindi dhidi ya Msumbiji, itafikisha pointi 11 ambazo zinaweza kufikiwa na timu hizo tano.
    Nimezitaja Afrika Kusini, Zambia, Algeria na Benin kama tishio kwa sababu zimefungwa magoli machache kulinganisha na Taifa Stars iliyoruhusu mabao sita hadi sasa.
    Afrika Kusini imefungwa bao moja, Uganda imefungwa mabao mawili, Algeria na Benin zimeruhusu mabao manne kila mmoja hadi sasa.
    Kwa mtazamo wangu, endapo Zambia itailaza Afrika Kusini, Benin ikaifunga Cape Verde, Uganda ikainyuka Niger na Algeria kushinda mechi yake dhidi ya Gambia, zitafikisha pointi 11.
    Kwa hiyo kutakuwa na timu tano na Stars ikiwa ya sita kwenye kusaka timu mbili bora. Nafasi moja imechukuliwa na Sudan yenye pointi 12 hadi sasa.
    Kwa vyovyote itakavyokuwa, Stars na Watanzania wote licha ya kuomba ishinde kwa hali na mali dhidi ya Msumbiji, pia tuombe miujiza Senegal ifungwe tena na Burkina Faso huko kwao au watoke sare ya aina yoyote ile.
    Kila nikiwaza hivyo, ninakondaaa ile mbaya na kuona NDOTO YA KUIONA STARS kwenye viwanja vya SEKONDI NA ACCRA huko Ghana ni finyu.
    Sina raha kabisa na kama kuna mtu anadhani kwamba Stars imeshapita, inabidi afikirie siyo tu mara mbili.
    Kwa sababu katika soka lolote laweza kutokea. Lakini hili la timu tano kuwania nafasi mbili, linatia hofu kubwa.
    ALAMSIKI....Mwanasoka

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2007

    Hiyo programme ni nzuri sana kwa ajili ya kukuza soka letu. Sasa bwana Michu mimi nina ombi moja. Nina mtoto mwenye kipaji kikubwa cha soka akiwa na miaka 13 tu. Tukiwa hapa ughaibuni, amekuwa the best player kila timu aliyochezea, akiwa pia mfungaji bora. siku chache zijazo tutakuwa hapo mother land.Nitaanzia wapi au nimpeleke wapi ili apate nafasi ya kuonesha umahiri wake? Kama una info kuhusu jinsi ya kuwaandikisha watoto wenye soccer talent naomba uturushie hapa kwenye blog (wapi, nani wa kumuona, lini, nk.) Nitashukuru kwa response yako. Bravo Michuzi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2007

    Ghana tunakwenda hatuendi?Ebu tuelimishe wananchi waelewe!




    Sport | June 21, 2007



    Here is the maths
    innocent ndawula & fred musisi
    MASERU/KAMPALA
    Cranes will qualify for the MTN Africa Cup of Nations finals in Ghana next year if they beat Niger in the last Group 3 tie at Namboole Stadium on September 8, and results elsewhere go Uganda’s way.


    NAIL-BITING TIMES: Cranes' star David Obua
    The three key matches Ugandans will monitor closely are South Africa-Zambia, Sierra Leone-Benin and Gambia-Algeria. Tanzania and Eritrea, despite having 8 points, are realistically out of contention.

    The ideal result for Uganda in the Togo-Mali game is a draw. If one of the teams wins and Benin picks three points in Sierra Leone, Uganda could be squeezed out of the picture.

    After failing to impress away from home, Cranes will be backing on it’s resilience at home in the last group game against Niger where Uganda has scored five goals and conceded just one.

    Sudan who last played in the Nations Cup finals in 1976 in Ethiopia has already grabbed at least one of the three best-placed runner-up positions following their 2-0 win away to Seychelles.

    Remaining key matches
    S. Africa v Zambia
    Gambia v Algeria
    Swaziland v Eritrea
    Uganda v Niger
    Togo v Mali
    Tanzania v Mozambique

    Runners-up table

    P W D L F A Pts
    * Sudan 5 4 0 1 10 2 12
    Togo 5 3 0 2 7 7 9
    Zambia 5 2 2 1 6 2 8
    Uganda 5 2 2 1 5 2 8
    Algeria 5 2 2 1 5 4 8
    Tanzania 5 2 2 1 4 6 8
    Eritrea 5 2 2 1 5 8 8
    Namibia 5 2 1 2 6 6 7
    Eq. Guinea 5 2 1 2 5 7 7
    Botswana 5 2 1 2 3 6 7
    Burundi 4 2 0 2 5 6 6

    * Already qualified

    • Note: 12 group winners qualify automatically. The best three teams shall be determined according to:
    • 1- Higher number of points
    • 2- Better goal difference
    • 3- Higher no. of goals scored
    • 4- Play off game

    CAF reserves the right to amend the kick-off times and dates of any group matches to have them played at the same time in order to guarantee the sporting equity if necessary.

    GHANA 2008: HOW CRANES CAN QUALIFY

    Cranes will go through on September 8th if Uganda beats Niger’s Mena and..

    Zambia is beaten or held by S. Africa

    And Algeria’s Desert Warriors fail to win or win by not more than two goals. Uganda could eventually qualify with Benin if the latter wins in Sierra Leone. Algeria +1 goal difference makes Uganda’s position healthy

    Benin draws or loses in Sierra Leone

    And a winner emerges from the Togo-Mali game, Uganda could qualify on goal difference. The determining games will be Gambia v Algeria and South Africa v Zambia. Goals are therefore paramount.

    Algeia draws/loses/gets small win

    And either Zambia or Benin fails to win, Cranes will definitely be one of the three best losers thus reaching Ghana 2008. The likelihood of Algeria qualifying is certainly not as bright as Uganda’s anyway.

    Tanzania fails to maul Mozambique

    In all fairness, Tanzania is virtually out of the picture. They need to score eight, nine or ten hoping that the scores of Uganda, Benin, Algeria and Zambia go their way. There is just a 0.01% possibility of this happenining.

    Eritrea demolishes Swaziland away

    That Tanzania at 0.01% stand a better chance than Eritrea speaks volumes on the improbable hurdle facing the North East Africans. Mathematically, Eritrea is in the picture. Realistically, they have no chance.

    • Note that Sudan or Tunisia will qualify as best runner up so there are only two slots up for grabs

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2007

    Mgosi, ukienda Bongo onana na Jeki ""Jac"" Pemba..LOL

    Well, nijuavyo hakuna kitu unachoongelea huko Bongo, ukizingatia hata michezo ya Mashuleni ilifutwa kitambo..Sana sana mtoto atachezea Team ya Shule yake ambapo ni kama kujifurahisha tu. Ila cha kufanya, onana na wadau wa Klabu za Dar es Salaama kama Simba, Yanga na kadhalika, mtoto kama atakuwa na muda saa ambazo Teams hizo zinafanya mazoezi(asubuhi na jioni), anaweza pata nafasi ya kufanya nao mazoezi, ila sio kila siku, watamruhusu tu pale ambapo team haitakuwa kambini au pale ambapo team haina mechi katika siku za karibuni..All in all, ni ngumu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2007

    MDAU MWENYE MTOTO MWENYE KIPAJI MUONE BONIFACE MKWASA, DR LIKI NA AKINA MTEMI RAMADHANI AU KIBADENI WANA TEAM ZA WATOTO WANAZIFUNDISHA NA KUZILEA. UNAWEZA PIA KUWAONA AKINA JACK PEMBA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2007

    Mdau mwenye mtoto ampeleke pale Jangwani (Yanga), Jack Chamangwana anaandaa timu za vijana/watoto na bila shaka atamjaribu aone kipaji chake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...