mechi ya staaz na senego imeisha dakika tano zilopita na matokeo ni droo 1-1 baada ya jamaa kukomboa bao kipindi cha lala unono walilopigwa kipindi cha kwanza na nizar khalfani. sasa tunao msumbiji na bukina faso kabla ya kujua hatma yetu katika kuelekea ghana...
Home
Unlabelled
droo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mr michuzi please may you gives us the highlights of the match, we would be very glad if you upload the video in our blog, thank you in advance
ReplyDeleteIlibaki kidogo jamaa wamtie aibu Rais wetu kwa kupigwa bao la pili. Watu wanajiuliza, mbele ya Rais vijana wameruhusu bao moja, je Rasi asingekuwepo? Kaazi kweli kweli!
ReplyDeletekwani position yetu ni wangapi katika group yetu? na timu ngapi zinatakiwa kuingia ktk fainali.
ReplyDeletetuweze kujua mipango ya baadae na mechi zilizo baki ni za ugeni au jumbani
Tusikate tamaa bado tunajenga timu.Tuna mechi na Burkina Faso after 2 weeks tugeuze macho yetu huko na tueendelee kuwasapoti vijana wetu.MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteBwana Michuzi...hebu rekebisha hiyo sentensi inayotusihi tusitumie lugha yenye matusi kwa ajili ya kujenga taifa lenye maadili!!!!
ReplyDelete"Karibu katika hii blog, Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Ila nawaomba tuweze kujieshimu kila mmoja wetu kwa kutumia lugha zisizo na matusi. Akhasante."
Kwa wale mnaoishi USA, You can have a free two weeks unlimited rental moviess from Blockbester. They ask you to keep a card on file so they know you are a real person and can mail you movies, but they don't charge you anything.All you have to do is to return them back or drop them at your nearest location.
ReplyDeletehttp://www.getblockbuster.com/trialexpire0610
(leave the promo code blank when they ask for it)
Have fun!
Asante Kaka Michuzi kwa matokeo,na Hongera kwa taifa stars japo ni droo ila wanastahili pongezi sana.
ReplyDeleteKwanza naomna nianze kwa kutoa hongera kwa kikosi hiki cha Taifa Stars, kweli vijana wamecheza game nzuri sana na matunda ya mwalimu Maximo tunaanza kuyaona vijana wamecheza game nzuri sana wanastahili pongezi, kinachotakiwa ni kutoa support ya kila namna kwa timu yetu hii ya Taifa,, kila mTanzania anapaswa kujivunia na kuonyesha utaifa wake. Burkina faso tutawakamata tu na Msumbiji wakija lazima wakione cha mtema kuni maana kwa soka iliyochezwa leo hawawezi kucoropoka hata iweje
ReplyDeleteniliicheki live hapa UK kupitia kwenye link moja aliyotao mdau wa blog yetu hii. Japo ilinimua jamaa kurudisha ila tuombe mungu ya kuwa best run up sasa. Ngoma ndo imetoka hiyo
ReplyDeleteNimefuatilia game LIVE online kupitia www.rewmi.com ambayo ilikuwa inarusha kandanda hilo kwa hisani ya TvT (Tanzania Television). Kwa kweli dogos wanahitaji pongezi, ila bado kazi tunayo. Wasenegal walitawala kipindi cha pili kiasi cha kututia tumbo joto. Anyways, kama Wamakonde wakiwapiga Bukina Faso, then tunakanafasi. Tuwaombee.
ReplyDeleteAnko Michuzi asante sana kwa kutupa matokeo faster faster... nilishangaa sana kutafuta radio ya kitanzania au TV online inayotoa matangazo live nikakuta hola yani bongo tech hii bado atuna. inasikitisha sana. lakini ukija kwa anko michuzi unapata just after the game hiyo nimependa kaka.
ReplyDeleteKwa anko aliyeuliza atima yetu ya starz... kazi tunayo sana na tena sio kazi rahisi.
Team 16 zinatakiwa kwenda Ghana
12 watakuwa washindi wa kwanza wa kila kundi
3 watakuwa ni washindi nafasi ya pili ambao ni watamu zahidi
1 ni ghana mwenyewe.
kwahiyo hadi now bongo ni nafasi ya pili lakini kama tunahitaji kwenda ghana basi tunaitaji kuwa wa kwanza katika kundi letu lakini tukiwa nafasi ya pili basi itakuwa ngumu kuwa katika wale watatu kwasababu ya yale magoli manne tuliochapwa na senegal (-3)
Kwenda ghana tunaitaji kushinda mechi zote mbili ili tupate point 6 na pia tusali na mola wengine wote wa droo ambayo ni kama ndoto ya alinacha au abunuasi kujenga nyumba hewani.
Mungu Ibariki Blog yetu
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Taifa stars.
watarudishaje bao wakati wa dakika za majeruhi? hawa madogo hawakutangaza emergency nini? hata kama wamecheza vizuri ni makosa makubwa sana kurudisha bao dakika za majeruhi bora afe mtu wangerudisha mwanzoni sawa
ReplyDeleteinabidi wajue kuna wakati inabidi watangaze emergency na kipindi hicho unajituma beyond your ability
Kocha wetu feki, tazama kocha wa wenzetu waganda? na kweli wamefanya
ReplyDeleteNilikupo uwanjani Michu, kwakweli hata kama mechi ilikuwa 1:1 lakini Stars wameshinda kwa maana ya uchezaji.Hatuna wachezaji professional katika line up yetu,lakini hata Wasenegali wamekubali kuwa Stars ni timu bora kwa jinsi ilivyoweza kutandaza kabumbu katika idara zote. Asiye wafahamu kwa majina wachezaji wa timu zote na ukamuuliza timu ipi ina wachezaji wengi professional angekuambia TAIFA STARS.Huo ndio ukweli.
ReplyDeleteAnony June 2,2007,11:53 vipi bwana... Unajua maana ya professional football... wote hao ni wachezaji wa kulipwa mzee mwenzangu (kwa sababu ndio shughuli yao full time, sema senegal wanao wengi wanaocheza ulaya..... basi!!!
ReplyDeleteTuliobakiza mechi nao wanaonyeshana uwanjani hapo Machava stadium.
ReplyDeleteMpaka half time Msumbiji 2 - Burkinafaso 1
Nafasi ya pili inanukia ila inabidi tuwakandamize Burkinafaso kwao na kumkandamiza Msumbiji nyumbani kwetu uwanja mpya!!
Ooooopppss!! Tico Tico kaongeza la tatu! Msumbiji 3 Burkinafaso 1!
ReplyDeletenaomba nimkosoe mhariri wa sunday observer kuwa, timu ya senegal ina point 7 na siyo 9, tanzania bado tunayo nafasi, ninaangalia live mchakato kati wamakonde na Bukinafaso, mozambique inaongoza kwa mabao 3 kwa zero, hii inaonesha hata Tanzania tulipofungwa 4 senegal ilikuwa ni football!! tunao uwezo wa kushinda na bado tunayo chance nzuri.... mungu mbariki michuzi, ibariki taifa stars, mungu ibariki Tanzania...
ReplyDeleteKAMA MTANZANIA NAOMBA TFF, WASIRUHUSU MECHI KATI YA TAIFA STARS NA TIMU YA JANGWANI, NIMESOMA HABARI KWENYE GAZETI... MICHO ANATAKA KUTUHARIBIA TIMU YETU, HATUWEZI TIMU YETU YA TAIFA STARS KUJIPIMA NA YANGA, HII NI KWA SABABU YANGA INACHEZA MPIRA WA KISHAMBA!!!
ReplyDeleteTIMU YATAIFA INAPASWA KUJIPIMA NA TIMU ZILIZO LINGANA NA VIGOGO WA MPIA BARANI AFRICA KAMA SOUTH AFRICA NA SENEGAL.. AKHSANTENI
MLIAKUVANA
ReplyDeleteNAONA UMECHEMKA. HIVI HAYO MATOKEO YA 3-1 YAMETOKA WAPI?
KWA MATOKEO NIONAYO MIMI, MSUMBIJI IMEIFUNGA BURKINA FASO 3-0.
MAMBO YAWEZA KUWA MAZURI KWANI MECHI YA MARUDIANO NA BURKINA FASO JUNI 15/16 AU 17, HUENDA TUKAAMBULIA KITU.
TUOMBE MUNGU SENEGAL AENDELEZE UBABE WAKE DHIDI YA MSUMBIJI AMBAO SASA WAPO NAFASI YA PILI. WAO WAMEFUNGWA MABAO MACHACHE DHIDI YA STAZ. SOTE TUNA POINTI SAWA 5.
KUNA HABARI KWAMBA BURKINA FASO MAMBO SI MAZURI KWANI NAHODHA WAO MAHAMADOU KERE ANAYECHEZEA CHARLEROI YA UBELIGIJI, AMEJIUZULU TIMU BAADA YA KUTEMWA.
MAMBO YAKIENDELEA HIVYO, UONGO TUNAWEZA KULAMBA DUME HUKO KWAO NA PIA KUIGEUZA MBOGA MSUMBIJI KWENYE MECHI YA MWISHO JULAI 7/9.
PIA TUOMBE MUNGU MECHI YA MSUMBIJI NA SENEGAL WIKI MBILI ZIJAZO IWE SULUHU ILI KAMA TUKISHINDA, TUTAKUWA POINTI SAWA NA SENEGAL.
SENEGAL IKILALA KWA MSUMBIJI HUKO MAPUTO, HALINA INAWEZA KUWA MBAYA WADAU. TUOMBENI MUNGU STAZ ISHINDE HUKO BURKINA FASO NA MECHI YA MSUMBIJI NA SENEGAL IWE SARE.
Anony wa Tarehe June 3, 2007 8:17:00 PM EAT, actually nilikuwa naangalia game live on a Mozambique channel my LNB & satelite dish picks up, it and UBC so I also watched live Nigeria go down 2-1 to Uganda.
ReplyDeleteSenegal anaongoza akiwa na pointi saba, sisi na Msumbiji tunafuata tukiwa na pointi tano ila wao wamefunga goli moja zaidi na na wamefungwa magoli mawili pungufu ya kwetu. Check this link for summary until this weekend's games: http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/6031899.stm
Final score from Msumbiji was Msumbiji beat Burkinafaso 3-1. Looks like Msumbiji is back in the hunt for a trip to Ghana!
Hongera Stars ila mpaka sasa hivi hali sio nzuri kwa mijubu wa msimamo wa makundi yote mpaka sasa hivi hatuna nafasi. Kuna makundi ambayo yana timu zenye pointi nyingi zaidi yetu hasa kwa kutegemea kuqualify kama best loosers! Kundi la nne Tunisia wana pointi 10 anayefuatia Sudan ana pointi 9, Kundi la tatu Nigeria ana point 9 Uganda wana point 7, Afrika Kusini wana pointi 10 Zambia wana pointi 7. Kwa ujumla hali sio nzuri. Tupiganie nafasi ya kwanza vinginevyo kwa kutegemea best loosers we are finished!
ReplyDeleteLIVE coverage ya mpira pale TvT bado sana hasa mpangilio wa kamera. Bora hii game wangefanya colabo na Star TV.
ReplyDeleteMbona hata hao Star TV nao bomu - dakika nzima inapita wakati kamera ya mpira inaangalia watazamaji huku mpira unaendelea! Na sio mara moja tu bali mara kibao! Nadhani wao wana kamera moja tu na ifanye kazi zote.
ReplyDeleteLakini ni mwanzo tu na tunajifunza kutokana na experience. UBC walimleta muingereza atangaze ile mechi na ilikuwa kama unatizama EPL vile, not kwamba ni nzuri but the familiar English twang was there.
kweli tvt bado kabisa wangeshirikiana na star tv..mara nyingi kulikuwa na interruption ya simu za watu waliokuwa karibu na mitambo yao ambayo haiko advanced....
ReplyDeleteTatizo siyo moja tu. wadau wenzangu, mengi tu. Kwanza vifaa vya kurekodi hiyo mechi hai popote pale sidhani kama ina viwango vinavyokubalika.
ReplyDeletePili hao wanaochukua matukio hai (live) sidhani kama wana ujuzi wa kutosha. Nadhani bado tuna ule mtindo wa kupeana kazi nzito eti kwa vile mtoto wa mjomba anajua kushika camcorder, baba mkurugenzi tvt, kapita huyo apewe kazi.
Hali hiyo ndiyo inayochangia. Watu wana elimu finyu ya kuchukua, kuchanganya na hata kuongoza uchukuaji wa picha lakini mtu analamba dume na kazi kubwa kama hiyo, aka...mpe mjomba. Hatufiki mbali.
Mambo ya ubwanga na unyamwela katika kazi, ndiyo yanayochangia viwango bora. Nalifahamu hilo tangu enzi hizo IPP, DTV zilipoanzisha vituo vyao vya TV.
Watangazaji wa RTD walipapatikiwa wakati TV na Radio ni vitu viwili tofauti katika masuala ya utangazaji.
Mtangaji wa TV anaweza kutangaza redioni bila matatizo, lakini wa Radio kwenda TV na kutangaza habari au matukio, ilikuwa mchemsho wa hali ya juu. Wengi wameachia.
Nadhani hata Michuzi naye alikuwa anachemsha katika kipindi chake cha soka. Kilikuwa hakiendani na kazi yake Ingawa ni mwanahabari, lakini amebobea zaidi katika kupiga picha.
Michuzi akiandika habari, nadhani haiwezi kufanana na mtu anayefanya kazi hiyo kila siku. Kadhalika mwandishi akipiga picha, huwa ni vituko. Utaona kuna tofauti kubwa.
Kwa hiyo wadau wenzangu msishangae na viwango vya TVT au STAR TV. Tunapata vitu kutokana na viwango vya hao wanaopiga picha za matukio yaliyo hai au kuonyeshwa baadaye. ALAMSIKI.
At the end of the day both are better than nothing!
ReplyDeleteUnajua enzi zile mtandao wa TV ulikuwa mdogo tulikuwas tunaambiwa tu matukio tuna amini tu. "Oh unajua Matumla alikuwa anoongoza raundi zote ila majaji wamemfanyia fitina tu na kupoteza pambano" Jamal Malinzi, boxing promoter. Au "Ikangaa ilibidi ashinde NY Marathon ila badala ya kupewa juice akawa anapewa maji akaishiwa nguvu" kumbe ni maji tu hutolewa wakati wa NY Marathon,etc etc etc