Hi Michuzi!
Thanks again for your support! Nawashukuru Watanzania wote waliomwombea na kumtakia kila ya kheri mrembo Flavia. Nashangaa kukuta mjadala mreeeeefu kuhusu vazi la jioni la Flavia na baada ya kuona kuwa suala hili limeota mikono na miguu naomba niweke baadhi ya vitu sawa kabla ya press conference wiki ijayo ili wasomaji wako waheshimiwa ambao wamekuwa mashabiki wazuri waweze kuelewa vyema suala hili.
Miss Universe Tanzania ni tofauti na mashindano mengine kwani kamati ya maandalizi ya mrembo inahusika moja kwa moja na kila nguo anayovaa Flavia. Historia nzima ya mavazi ya Flavia ninayo mimi. Tuanze na mavazi yake ya kila siku: Magauni yote ya Flavia yamekaguliwa na kukubaliwa na kamati. Flavia hajavaa gauni ambalo hatujalikubali isipokuwa t-shirt au gauni ya masponza wa Miss Universe (eg. Hard Rock cafe, YMI jeans n.k)
Mavazi haya yalimvutia hata designer mkuu wa Miss Universe na designer maarufu wa USA - Tadashi ambaye alitaka kujua zaidi kuhusu kitambaa kilichotumika, na designs. Designer wa mavazi yake Flavia ya kila siku ni siri yetu but is local na fundi ni local. Bwana Michuzi naomba niweke wazi kwamba it's time sisi watanzania tujivunie utamaduni wetu vitenge na kanga vimemtoa sana Flavia na atasimulia mwenyewe jinsi alivyowavutia waandishi na mashabiki wa kimataifa kwa mavazi yake.
Vazi la taifa : Lilibuniwa na Farouque Abdela wa Zanzibar! Ni designer mwenye sifa kubwa na ana ubinifu wa hali ya juu! Vazi hili la Flavia lilikuwa limetokana na vazi la kimaasai na lilipata sifa nyingi sana. Nadhani niliandika mengi kuhusu vazi hili hapo awali.
Vazi la jioni la kitabu na website: Vazi hili la pinki lilibuniwa na designer ambaye jina lake tumelihifadhi, but ni wa hapa na fundi alikuwa wa hapa. Vazi hili pia lilisifiwa kwa kuwa ya kipekee.
Vazi la usiku la raundi ya kwanza (preliminary au presentation show) tarehe 23: Hii ni vazi lile la damu la mzee au maroon kwa kiingereza. Gauni hili lilibuniwa na Jamila Swai, designer mwenye uzoefu mkubwa anayejulikana kwa kudesgin hata magauni ya harusi. Gauni hili lilimbeba Flavia katika 15 bora ambayo ilitangazwa tarehe 28.
Vazi la usiku la fainali (tarehe 28): Katika siku chache kati ya preliminary na fainali, nilifuatwa na wataalam wa masuala ya urembo ambao walinieleza kuwa ni kawaida kubadili gauni la jioni kwa warembo wengi. Pia nilishauriwa na watalaam wengine kuwa ingekuwa vyema kutafuta gauni la rangi nyingine. Baada ya kutafakari, ilibidi nianze kuangalia uwezekano wa kupata gauni lingine. Ndipo nilipofuatwa na designer mkuu wa Miss Venezuela Miguel Aleman, ambaye ni designer wa washindi wengi wa Miss Venezuela (miss Venezuela mwaka huu pia amevalishwa na Miguel). Yeye alijitokeza bila kuambiwa akiomba amvishe gauni jeupe Flavia. Ilikuwa ni siri kali na hakuna mtu aliyejua hili, zaidi ya watu 2 wa Miss Universe waliomsaidia Flavia kubadili nguo. Miguel alifanya kazi usiku mzima kukamilisha gauni lile. Naomba nieleze watanzania kuwa Flavia alisifiwa sana na lile gauni na lilikuwa gauni ambalo lilimkaa vizuri. Alipotokea, watu ukumbini walitoa 'WOW!' kwa pamoja. NIlikuwa nimekaa katikati ya watu na kila mtu alishangaa kwa furaha wakinieleza kuwa Flavia alionekana kama malaika! Ile rangi nyeupe ilimtoa sana! Flavia pia alipenda kuwa na gauni simple, kitu ambacho wote tuliafiki kwani uzuri wake ni wa kipekee. Kila mtu alikuja kunipongeza wakisema kwamba Miss Angola ambaye nguo yake ilikuwa na nakshi nyingi alishindwa kumfikia Flavia kwani gauni la mrembo wetu iliongeza uzuri wake na haikumfunika kwa mimeremeto.
Pointi za vazi la usiku: Kama mashabiki mlifuatilia Flavia alipitwa na pointi 0.01 na Miss USA ambaye alidondoka stejini! Sasa swali, je lile gauni la Miss USA lilikuwa zuri zaidi au ni bahati mbaya au nzuri? Kwani siyo gauni tu ambalo linapewa pointi lakini jinsi mrembo anavyoivaa gauni na kuiwakilislisha (presentation and poise). Flavia hakudondoka, Miss USA alidondoka. MIss USA alivaa gauni nyeusi Flavia alivaa nyeupe. Hakuna jibu. Flavia alifanya vizuri sana lakini bado alishindwa kupenya 5 bora. hiyo 0.01 point ilikuwa nini? Jamani hayo tumwachie Mungu. Tusitake kutafuta sababu zisizo na maana.
Mustafa Hassanali: Flavia hakuvaa gauni hata moja la Mustafa Hassanali huko Mexico. Magauni yake yaliyopitishwa na kamati hayakuwa na gauni lolote la Mustafa. Mavazi na mengineyo: Mimi binafsi nawatetea sana madesigner wa Tanzania. Ilikuwa ni bahati mbaya tu kwamba Mexico ni mbali na nilikuwa sina muda wa kuomba design. Kwa kweli wengi wao ni wazuri na wanafanya kazi kubwa sana ku-promote design, vitambaa na utamaduni wetu. Sisi watanzania tusitake kushindana na Miss Japan ambaye alinunua gauni lake la Gucci kwa dola 3,000! Kushinda si thamani ya nguo. Jamani huu ndio mwanzo, tutafanikiwa tu kupata taji! Ningeomba kuchukua nafasi hii pia kuwaomba madesigner wa hapa wawe na uzalendo. Madesginer wa nchi zingine hutoa magauni bure kwa ajili ya warembo, na hujituma kwani wako radhi kukesha usiku kucha ili design zao zionekane duniani.
Nimejifunza mengi kwani hii ilikuwa ni mara yetu ya kwanza. Nadhani mwakani tutakuwa tumejitayarisha na magauni mazuri zaidi na mengi zaidi! Kwa wale madesigner wanaotaka kudesign magauni ya Miss Universe Tanzania tafadhali wajue, mambo ya kuwapa warembo wenyewe magauni si njia sahihi. Ni lazima ipitishwe na kamati. Flavia ataendelea kuvaa magauni ya kanga na vitenge kwani anajua thamani yake!
Tanzania tujipende na tupende utamaduni wetu! I am so proud to be Tanzanian! Flavia is so proud to be Tanzanian! TANZANIA JUU! Tumeweka historia at Miss Universe!
Asanteni sana!
Maria Sarungi-Tsehai
Maria - beauty is in the eyes of the beholder. Hakuna mtu anayemkataza Flaviana kuvaa vitenge. Avivae tu as long as vinamtosha.
ReplyDeleteUnafikiri kwa sababu Miguel ndiyo alimvalisha, iko guaranteed kwamba atapendeza? wewe mwenyewe umeshasema kwamba alimvalisha Ms. venezuela, unafikiri kwamba angetaka apendeze kuliko venezuela? c'mon man, be serious. ulimuona Ms. Venezuela alivyopendeza?
That white evening dress was just too simple, unaweza kuvaa ile nguo kwenda kulalia. Ile nguo ya maroon ilikuwa nzuri sana, sasa mngemvalisha nguo za namna ile.
Huu siyo wakati wa kuwa defensive Maria, chukua criticism and work on it. Sijaona hata mtu mmoja ambaye amemsema vibaya Flaviana as a person, watu wame comment on that dress. So, get that dress out of her wadrobe now!!
Dada Maria good job. Ila nina comment hapa.
ReplyDeleteKwa nini watanzania tunapenda vitu vya bure? Thats bad! We hujui hao madisigner ni kama anybody else, they are after making their ends meet. I really appreciate you, you are so professional and I admire what you have done, but tujifunze kuwa independent. There is nothing like free lunch in this world!!
Kama umeamua kuingia kwenye haya mashindano, just fight and get what it takes to be there. Naelewa uzalendo ni muhimu , ila Iam sure when you perform well, certainly in the process utaitangaza nchi yako for long time. Kama leo it will go in history..Miss Univ. 2007 alikuwa mjapani..na wala hakuna atakayeuliza miss univ. namba tano, saba nk.. Just like any other race. What we know today is JK is TZ President..kwamba kulikuwa na akina Mrema, Lipumba and others kwenye race..its immaterial....
When it comes to business? jifunze kuinvest in what you want. Ndo maana gauni la $$3000 lilimpa taji miss Japani. Na when you enter the race, jiamini kwamba uko on one level...ukishaanza kusema as you said..kwamba..tusijilinganishe na miss Japani anayevaa gauni la $$3000..Tayari umesha jigrade kama second class..au msindikizaji. And you cant win. Kumbuka majaji ni kama mimi na wewe, wana taste..just like any body. Surely, hutapewa taji just because "nguo yako ni cheap lakini nzuri"
Again, I applaud what you did, na Iam sure you will reach far-God allowing, but jua..kila mtu atavuna alichopanda. Ulipoenda Mexico, priority ilikuwa ni kushinda taji, kuitangaza nchi was secondary. Ndivyo binadamu tulivyo....Kama unataka watu wawe generous na fani zao for the sake ya kutangaza nchi..then the governemnt should foot the bill!
Again take this as a constructive criticism. Jua kwamba wengi wetu tunamtakia Flavia mafaniko in her career, just like you as an enterprenuer..Ila mimi sikupenda kitendo cha wewe kusema eti watu wawe wazalendo by donating nguo....This is capitalism where innovation and hard work like that of Mustafaa, Sawe, You and all SHOULD BE RECOGNIZED AND REWARDED! I hope I will live long enough to cast another vote for your efforts, just like I did last week in Mexico. Infact what you should do, anza sasa kukusanya masponsor and involve even the government kama TTB nk....to give you support you deserve, maana in the process unafanya wanayopaswa kufanya.
Nakutakia mafanikio mengi sana and keep up the good work.
Mdau,
SAWA TUMEMSIKIA DADA SARUNGI lakini mimi nina uhakika watu walikuwa wanamshangilia flaviana kipara chake na sio mavazi~~~ nina swali moja kwa dada sarungi je kwanza NI KWANINI CUPZ ZOOOTE za nguo za huyu binti kubwa>??tunaomba mtueloeweshe pili bado tuna utata ktk hilo gauni lake la blu bahari alilosafiri nalo(sijui mtu tangu lini anasafiri na mgauni kama ule) yani kwanza haukupendeza na ulikuwa na rangi mbaya sana.
ReplyDeleteHAKUNA ALIESEMA HAPENDI MA MODEL WETU WASIVAE KANGA WALA VITENGE HAPO UMEWEKA WORDS IN OUR MOUTHS coz ktk comments zote hakuna aliesema hivo kwanza kwa taarifa tu sisi watz tuna fagilia sanaaa hivo vivazi shida ni kuwa LIBUNIWE VEMA ndo hicho tunachoomba na sikingine.!wananchi tutoe maoni yetu tafadhali bila uwoga wowoteeeeeeeeeeeeeeeee shukrani
Dada Maria hingera sana. Unajua katika maisha ya kawaida lazima kutakuwa na watu ambao hawawezi kuliona jema na wengine hawawezi kuliona baya. Hatua mliyofikia kweli mmeitangaza TZ kwa masuala ya urembo!!!HONGERENI tena. Watu wengine wanapiga domo tu na lawama tu bila kujua masuala yanakwendaje.
ReplyDeleteFC
aah, sarungi we, sisi mabox yanatungoja,time yetu is limited,wewe hadith ndefu,tutafika kweli ?
ReplyDeleteNANI KASEMA FLAVIANA ASIVAE KHANGA NA VITENGE?we sarungi unaanza kutubambika maneno sasa ndiyo avae khanga na vitenge ndiyo vinathamani hutakiwi kutukumbusha ilo tunalijua lakini VIBUNIWE VYEMA viwe na MVUTO sio mguo wa rangi ya ajabu anaovaa akienda kupanda ndege she looked absolutely UGLY!! mnamuharibia uyu mtoto nyie hamshangai kwann kila mtu anacomplain?ningekuwa wewe ningesikiliza ushauri ulikuboresha sio kuji-justify 2
ReplyDeleteMrs Sarungi Tsehai, congratulations on a job well done despite the outcome. Many felt the white dress was not adequate, and as one anony said, beauty is in the eyes of the beholder.
ReplyDeleteIla sikuelewi unaposema fundi wa nguo za Flaviana jina mnalihifadhi - I thought this pageant and many more like it are for the promotion of local artists? In the same article you said tujivunie utamaduni wetu, sasa madesigner na mafundi washonaji sio utamaduni tosha? Kwa nini unaliziba jina la designer huyo? Hataki publicity na wider soko la nguo zake? Don't you think more exposure to our up and coming designers etc is a good thing for all?
jamani cooments zote zilikwua zinazungumzia GAUNI sio material. Ukweli magauni anayovaa hayampendezi tunajua zanzibar wanavyovaa one way gauni ila kwa model wetu Flavia ana shape nzuri ya kupendeza hata kanga au kitenge ila wanavyomshonea hapana na wanamzidishia VIPIMO .
ReplyDeletehttp://www.missuniverse.com/delegates/2007/files/TZ-video-gown.html
TAKE A CLOSE LOOK OF THE GAUNI JAMANI AFU MSEME TULIMUONEA FLAVIANA KUSEMA GAUNI BAYA http://darhotwire.com/dar/Maisha/2007/06/04/33377.html
ReplyDeleteHuyu flavia wenu mimi sioni urembo wake, ila kama wembamba maji ndo maanake urembo siku hizi, basi inabidi tulazimishwe tuu kukubali. Mwanamke gani hana curvs? urembo wa mwafrika siyo huu.
ReplyDeleteMaria, that was a great CLASSY job! People, nauliza, hivi ni design ya nguo, rangi, kitambaa au size ndio mbaya? Or they didn't 'study' Flaviana's figure properly. Naona, tight fitting clothes zina-accentuate curves zake vizuri, nguo ikiwa loose especially kifuani, inharibu kabisa!
ReplyDeleteMama Tsheshai Sarungi hadithi ndefu ya kujidefend wont help for now,gauni lilikuwa baya na zile hereni jamani kweli?? hatuwezi kutetea ujinga,tunakupongeza u worked hard but gauni na hereni no way kusema tuvisifu huku twajua wazi ndio vilivyomuangusha,take critisms and work on them,thats it thats all.
ReplyDeleteWEWE ANONY hapo juu tunakuomba ukatafte kwenye google ujue ni vigezo vp vinatakiwa ktk miss universe! hii sio miss bantu!!
ReplyDeletewell, naona huyu Mustapha Hassanali ametumia hili zaga lote kwa publicity yake, kama Flaviana hakuvaa nguo yoyote aliyotengeneza yeye angekuja hapa tu na kusema hilo, lakini alileta blaa blaa nyingi kwa adverntage yake, na bili kuweka simple statement kwamba no dress was design by him.
ReplyDeleteMaria, maria yaani USD 3,000 ndio umeona pesa ya kukuintimidate? C'mon, u can't be that cheap! Ndio maana nani huyo .... huyo Mustafa Hassanali kakuchamba.
ReplyDeleteHata ungemtonya Kikwete wakati uko Mexico angekupiga tafu na hiyo hela.
Ndugu anan wa June 4, 2007 3:12:00 PM EAT huo ni urembo wa kimataifa sio wa Mwafrika. Ukitaka urembo wa Mwafrika anzisha shindano la kiafrika, (say, "Miss Black") usihangaike kushindania mashindano ya watu weupe.
ReplyDeleteMaria,
ReplyDeleteI think you're missing the point. Watu hawakulaumu wa-designer wakibongo. Wamelaumu lile gauni whoever decided kuwa Flaviana anatavaa hili gauni ndio mwenye kosa. Kama ulivyosema, Flaviana alikosa point 0.01 kumpita Miss USA. Watu walichosema ni kuwa lile gauni limechangia kukosekana kwa hizo point ambazo zingempa FLaviana uwezo wa kuwa tano bora.
Umesema Miss USA alianguka, wote tulimwona. Lakini pamoja na kuanguka kwake aliweza kumpita Flaviana 0.01. Watu wanachosema kuwa ni Flaviana had a chance. Gauni lingikuwa poa angeweza kupata hiyo 0.01 na kumpiku Miss USA.
Kumbuka kuwa watu wameangalia hiyo Miss Univere Live wengine walikuwa huko huko Mexico. Sasa unapopata mawazo ya watu toka UK,USA, Mexico hata huko Tanzania kila mtu kwa wakati wake ameona kasoro ambao imempunguzia Flaviana uwezo wa kusonga mbele huwezi kuzuia watu wasiongelee, bali wewe chukulia hii kama Challenge kwa wakati mwingine mfanye vizuri. Take this as learning experience. Kama ulivyosema kwenye mesage yako kuwa umejifunza mengi, basi chukua mawazo ya wadu mbalimbali ambao kwa wakati wao wote wameliona tatizo moja kubwa lilimkosesha uwezo wa kwenye tano bora mrembo wa Tanzania. Mimi binafsi nataka kukuuliza swali je umeangalia clips za miss universe? Kama bado angalia tena halafu jibu swali langu. Wakati Flaviana anatoka kwenye steji baada ya vazi la jioni, kwanini alikuwa anakimbia na anajishika matiti?
Maria mimi nina wasiwasi na huyo designer wa Miss Venezuela aliyekushauri. Kwa mtazamo wangu hapo ulipigwa bao la kisaikolojia, kama zile mind games za "The Survivor", au hata corporate world. Hapo ukute mzee mzima USA baada ya kuona Wamexico wanamzomea sana na wanamshangilia sana Miss Tanzania dizaini alicheza dili na timu ya Miss Venezuela wakushushe comfo. Bahati mbaya na wewe ukaingia laini kwa sababu tu Venezuela wana uzoefu, ukasahau pia kuna wivu wa kibiniadamu mtu akiona "dogo" anapanda chati fasta fasta.
ReplyDeleteTake Care my sister. But you hv done a great job.
Bravo, Hongera na Asante Flaviana for having contributed to the fantastic and awesome winning moment!
ReplyDeleteKwenye mashindano kuna mshindi/washindi na mshindwa/washindwa!
Acheni ulimbukeni wa kuwa "experts" baada ya jambo kutukia! Hii ni tabia watu wenye akili finyu!
Hayo mawazo yenu mazuri na mabaya, mbona hamkuyawakilisha kwa Maria Sarungi-Tsehai kabla ya mashindano?
Dada Maria asante sana kwa maelezo yako. Poleni na kazi kubwa mliyoifanya. Na kama ulivyosema madisigner wajifunze kwa hili. Kutoa nguo zao nyingi na bure ili washiriki wawe na nguo nyingi za kuchagua baada ya kupitishwa na kamati ya maandalizi. Wakivaa nguo zao kwenye international standard pageant ni sifa kwao na kujiongezea CV zao.
ReplyDeleteKwa wale msiojua hii ndio inaitwa damage contol sio yule Hassanalli alivyokuja na maneno yake baada ya mashindano kuisha watu wakasema ni damage contol.
Ila mimi kama mmoja wa watazamaji live wa hili shindano, ukweli ni kuwa labda hilo gauni lilionekana nzuri kwa karibu. Lakini kwa sisi tuliyokua tunaangalia kwenye TV hapa USA ...Mh....ukweli lilionekana kama kubwa kidogo na too simple kwa kweli, na sijui reflection ya ile color akafade kabisa hakung'aa tena.
Nilikua najiuliza vikoi vyetu vilikua wapi mpaka wamvalishe ile satin material?
Ingawaje mjapani hiyo gauni aligharamikia sana lakini style yake kweli ni ya vimono vyao na ukizingatia kila habari na news tulizokua tunasoma walikua wanamfagilia mkorea huku. Na mjapani alikua hata hayuko kwenye chart lakini still alivyopita mjapani watu wakawa impressed. Na wala hawajui lolote kuhusu yeye zaidi ya lile gauni lake walilomwona nalo kwa sekunde mbili.
Mimi kwa ushauri wangu ni kuwa
1. Hawa watu wanaadmire sana vitu vya culture za watu majudge wote wale uliowaona wengi wameishi au wanaishi USA na wanareperesent majority of the people we live and see them all days.... Na kila siku tukivaa tu vinguo vyetu kutoka Africa na kwenda mfano kanisani wanashangaa, wanapenda na wanauliza wapi nitapata hiki.
Hivyo mkumbuke kwenye mashindano mengine kuwa the more the original the better the game.
2. Wanapenda unique thing...kama hivyo Flavia alivyokua bold ..ile ilikua the plus thing sana tu ingawaje najua pamoja na mengine mengi yalimfanya akafikia hapo lakini nakuambia trust me... if other things remain equal na urudie hilo shindano na flavia awe na nywele kichwani asingefikia hapo.
Kwa hiyo maana yangu ni kuwa hawa watu wanajali sana original na unique things. Kwa hiyo mashindano mengine muweke hiyo kichwani.
Da maria Tatizo lako siko zote unajua kila kitu, mbishi kama walivyo wajomba zako warusi. Umefika muda sasa to sit down and look in the mirror and ask yourself kwanini watu wote hawa wanlipigia gauni kelele. wala hatuhitaji uanze kujihami mimi nilizania umekuwa kumbe bado akili mbovu mbovu kama zamani maana nakufahamu vizuri sana na ukiacha hizo dharau na kujiona wajua kila kitu then u will make it ila ukingangania kujihami basi kau na huo ushamba wako. Samahani kwa kutumia maneno makali ila ni kwa faida yako mimi sikutegemea mtu kama wewe useme eti mwalihifadhi jina la designer, tatizo pesa mnapata ila mnapenda vitu bei rahisi. Ukiangalai vitu vyako vingi viko hivyo hivyo kumbuka watu wanaona na wanajua kipi bora na kipi si sahihi kama ni kwa ajili ya wewe na mumeao sawa lakini for public it is not good enough kaza mkanda dada yangu and stop being defencive lady.
ReplyDeleteNarudia ubishi acha bado wajifunza wewe ndio kwanza waanza kuingia mjini safari ndefu hiyo listen to comment and work out something good. Hakuna anayekuchukia ni kwa faida yako.
Dada yangu wa June 4, 2007 3:12:00 PM EAT uckonde. Uzuri wa Flaviana ni uzuri wa kimashindano tu. Yaani ana vigezo vya kushindana kwenye mashindano ya urembo.
ReplyDeleteUkitaka kujua uzuri ambao tunazimikia walume wa kibongo wewe simama pale stendi ya basi Posta Mpya utaona vifaa. Angalia wanaume wanageuza shingo (tena kwa staili ya kujifichaficha) kwa nani na nani hapo utajua viwango vya uzuri Bongo.
Kama ni michango tangazeni mapema najua wapo wengi tu wana moyo na watatoa japo kidogo lakini kitapush na kuongeza quality yetu katika kushiriki mashindano hayo.
ReplyDeleteNa pia mjaribu kushirikisha watu wanaoishi nje ya nchi pia kwa mawazo na ideas. Blog ya Michuzi imeshatuunganisha na kutufanya kuwa wote tuwe karibu zaidi.
Unajua labda wewe una bahati ya kutembea nje ya nchi mara kwa mara, lakini ukumbuke kuna madisigner wengine hawana bahati hiyo...always their perception will base on what they see hapo nyumbani. Always when you go out of your town or your country you real start to see, view and jusge things in different ways compare to before.
Colaboration ya watu wa TZ na nje ya nchi ita make a bid difference.
Eg..mimi sio professional desingner lakini I could be a fashion stylist. Na toka mdogo nina good taste ya color na fashion na nimekulia kwenye nyumba ya mama anayependa craft stuffs sana tu na mpaka leo mama yangu ni seamstrees. Nikija bongo ni vikoi na material nyingine za nyumbani lakini namchorea nguo zangu ninavyotaka, tunakata pamoja ananishonea. Nikurudi huku vitambaa ni hivyo hivyo vya bongo lakini kwa vile naujulia mwili wangu na najua nini kiko kwenye fashion na najua color zinazonipendeza basi mchanganyiko kidogo tu watu macho yanawatoka na wanazitamani hizo nguo sana tu.
Madisiger wanavipaji vya kudisign nguo lakini fashion stylist wanavipaji vya kukuangalia na kujua hata kama wewe ni mzuri au mbaya kiasi gani ukivaa hii nguo ina rangi hii itakupendeza sana au itakuchukiza sana. Sasa kwa nchi yetu clothing disigner ndio huyo huyo anakua fashion stylist. Ni wachache wenye vipanyi hivyo viwili kwa pamoja.
No sweat no doubt najua siku moja tutaenda all the way.
wabongo bwana mi ndo maana uzalendo huwa unanishinda, kwa hiyo huyu maria kaona wote hapa ni vilaza tunaongea pumba tu kuhusu gauni? anapinga comment zote kuwa gauni lilikuwa baya kwa hiyo wote tulioona gauni ni baya ni wivu wetu tu au labda sisi ni vichwa maji au tv zetu zilionyesha mchelemchele?
ReplyDeleteI am not wasting my time for this no more, i cant believe she's against the majorities opinion? may be because she is the sponsor trying to make a bunch $$ for less
thats bongo, mi sina uzalendo wa kijinga I go for the reality
kama yeye anaona gauni lilikuwa zuri labda hiyo ndo standard yake siwezi kumlaumu sana
we huwezi kumtaja jina dizaina mmoja halafu wengine usiwataje majina yao.we unaonekana sio fair person at all na hujiamini katika mambo yako.ushauri wa bure tafuta career nyingine na huwezi ukawa spokeswoman unae faa.
ReplyDeleteHONGERA FLAVIAN.
I LOVE YOU SO MUCH.
Bi. Maria,
ReplyDeleteUsijidanganye kabisa kuwa lile gauni lilikuwa zuri!... Gauni baya sana na kama Miss USA asingeanguka basi Bi.Flaviana angekuwa nyuma kwa point 10. Gauni lile humviki mtu yeyote kama unamtakia ushindi. Huyo Designer wa Venezuela kawavikeni Mkenge, Flaviana alikuwa tishio kwa Miss wao na hapakuwa na njama nzuri zaidi ya kumwondoa kwa vazi..
Sasa wewe twambie ni kitu gani kimemfanya ashindwe? maanake kwenye mambo meninge yote mazito aliweza kupita.... Vazi tu la jioni!
Bi. maria kila Mtazania aliyetazama mashindano yale tulijua Flaviana kachemsha baada tu ya kutokea na lile vazi. Na hata vazi alilorudi nalo tanzania ni mchemsho. Kuwa designer haina ndio kipaji. Wapo Madesigner millioni duniani na wachache sana huwavutia watu!...Designer mzuri ni mbunifu sio elimu ya darasa peke yake!
Kubali mlifanya makosa na mtajaribu kujirekebisha baadaye!
Samahani jamani hivi hilo vazi la usiku lilitokana na Khanga ama Kitenge?
ReplyDeleteIkiwa kama mwenyewe Maria uliwasili uwanja wa ndege ukiwa umevaa kiatu chekundu, jacket la pinki na rangi nyingine kadhaa za ajabu, unadhani unatoa mfano gani kwa wasimamizi wa mambo ya urembo?
ReplyDeleteNadhani baadaye ujitahidi dada yetu kufanya mambo tofauti na hii safari ya kwanza.
Nimesoma comments zote. I want to make the following clear:
ReplyDeleteSisi hatutaki vitu vya bure, ila madesginer nao inabidi waelewe kuwa kuna investment needed. I have good relationship with many of them. Cha ajabu nimeshapata response yao leo hii baada ya kusoma this blog. Baadhi wamenielewa na tuko tayari kufanya kazi pamoja. Kwa hili nakushukuru Mr Michuzi for enabling this blog kuwa platform for healthy discussion.
Naomba niongeze kuwa kama wewe ni designer write and tell me. Usitumie jina la Mustafa au Ailinda Sawe maana wao wamenielewa. Tumia jina lako. Let's talk.
When we talk about investing in masuala ya urembo, I don't think anyone can really challenge me on that, because I have personally invested time and my money, and have achieved a lot with it. Talk about psychology na suala la kusema tunasindikiza also for me is not appropriate here, because kabla ya Flavia kufanya vizuri hatujawahi kuota hata kuingia 15 bora, now we are complaining about not winning the crown! I believed that we can make it before anyone else and we did it! First time tumeshiriki, we made it to Top 10, nchi nyingi zinapeleka warembo miaka 7, 11 na hawajawahi kuingia hata 15 bora. Hapo bado sijataja achievement za warembo wengine tuliowapeleka miaka ya nyuma, kama vile Best National Costume award in Miss International 2005 (vazi lililobuniwa na Farouque Abdela). Jamani let us think before we write.
Kuhusu ugly gowns mnazozungumzia, again wenyewe mmetetea beauty in the eyes of the beholder au siyo? Sasa kama ni hivyo kwa mfano hiyo nguo ya maroon mnayoisifia ilipondwa sana na critics wengi huko nje kabla ya preliminaries, but Flavia wore it and she made it. And I think it was a great gown! Sikujali. Nayo walisema ni simple sana! Waliiponda mpaka Flavia alishuka from namba 2 mpaka namba 7 after tarehe 23 (the preliminary show)katika grid ya Global beauties. So at times you have to make decisions, and it was the best at the given time. I stand by my decision. Also the simplicity of the gown was a strategy, we made a statement, it went with the naturalness and simplicity of Flavia. By the way, msichanganye simplicity with cheap. That gown is very expensive!
Also kusema kuwa desginer Miguel alitaka kumpunguzia makali Flaviana is a very unfair statement. Miguel alikesha usiku kucha kurekebisha gauni. The design tuliafiki wote. Pia kwa taarifa yenu, marekebisho mengine madogo yalifanywa na wataalam wa Miss Universe kabla ya shoo! Please tuache conspiracy theory zisizo za maana. Mashabiki wa Flavia walikuwa ni pamoja na watu kutoka Colombia, Mexico, Venezuela, Curacao, Bahamas, na nchi zingine. Tufurahie kwamba mrembo wetu kafika mbali. Mbona Miss Angola alivaa expensive gauni ya boutique na alikuwa nyuma ya Flavia?
Niko tayari kupokea maoni kuhusu suala hili na masuala mengine, kupitia email ya missuniversetz@hotmail.com
Asanteni kwa maoni yenu and for a healthy debate! Siku njema
Maria job well done. Umempresent mrembo wetu na kumfua vizuri na akaweza kuiwakilisha nchi yetu vizuri hasa.Dont listen to people with low IQ kama Mustapha Hassanali. Poor girl hakupata hilo tenda la nguo ndio maana.Nimesoma hilo tangazo lake nikaona tu kuwa ni mtu ambae he thinks so high of himself. Tanzania tumejitahidi sana na tujitahidi zaidi next time kwa kushirikiana na watu kama kina Maria. Mustapha too bad for you alafu wewe unajua ni shoga alafu unasubutu kuja hapa. TUTAKUCHAMBA!Chubby idiot!GET YOUR OWN BLOG UTANGAZE MITANDIO YAKO YA MINGARO!
ReplyDeleteNdugu yangu wavenezuela hawatuzidi chochote kwa nchi yao zaidi ya wao ni weupe na sisi ni weusi. Uliza tuliofika nchi yao tukwambie. Huyo designer alifurahi sana kufanya hiyo kazi kwa vile anajitafutia umaarufu kwenye international level. Hao wabongo wnataka walipwe ndio hivyo shauri lao.
ReplyDeleteah halafu nimeshaamini kumbe huyuu dada mbishi eh,kuna annoy hapo juu amekwambia uache ubishi dada,wakati ule unatuomba tumpigie kura flavia ulikuwa kama dada mzuri sasa hivi waleta za kuletwa sio.Piga ua gauni baya,halafu unajitia kelele next time uje kuomba kuraaaa,sijuiiiiii,kubali ulikosea dada,wala hutamegeka.
ReplyDeleteMARIA, JARIBU KUWA MKWELI, LOOK DEEP DOWN? LILE GAUNI LILIKUWA BAYA, FULL STOP. NA KAMA NI KWELI HUYO MVENUZUELA NDIO AMEKUPA MAWAZO YA KUMDEZINIA LILE GAUNI BASI ALIKUPIGA GOLI ZURI TU NA AMEWIN. HAYO NDIO MAWAZO YA KUWA COMPETATIVE, AMEKUPATA DADA YANGU. PILI, WATU WOTE TULIKUWA TUNATAKA DADA YETU ASHINDE, NA SASA HIVI TUNATOA COMMENTS TU HAKUNA CHA WIVU. UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUJIULIZA WEWE MWENYEWE WHY EVERONE IS COMPLAINING? MAY BE THERE IS TRUTH IN IN. THEREFOR ETAKE THE CRITICISM AND USE THEM FOR NEXT TIME. KAMA UTABAKI KUSPEND MUDA WAKO NA KUTUANDIKIA PUMBA HIZI AS TO WHY ALIVAA LILE GAUNI HONEY WE WILL NEVER SUCCEED, HATA HAPO TULIPOFIKIA NI KIBAHATI TU. PLEASE LETS' WORK UP, FLAVIANA CAN DO BETTER, SHE NEED A REAL DESIGNER AND PERSONAL STYLIST. nA LILE ALILOLIVAA AIRPORT LILIDEZINIWA NA NANI, MVENUZUELA PIA AU THIS TIME MMEXICO?
ReplyDeleteMaria,
ReplyDeleteHukujibu swali langu "Wakati Flaviana anatoka kwenye steji baada ya vazi la jioni, kwanini alikuwa anakimbia na anajishika matiti?" Halafu wale camera men wa Miss Universe wasivyokuwa na adabu wakaionyesha kama dakika mbili hivi binti wa watu anajaribu kujisetiri kwenye matiti.
Chukua ushauri wa watu, hatukutakii mabaya ila jifunze kutokana na hili shindano.
Wow!!!! This is too deep.... "When we talk about investing in masuala ya urembo, I don't think anyone can really challenge me on that, because I have personally invested time and my money, and have achieved a lot with it." I wish you could take this sentence back. Remember that is our country's name we are talking about here. Nobody is talking about Flavia, Miguela or you in personal but the truth has to be told..
ReplyDeleteYou worked yourself so much and you need to chill out. People do appreciate what you have done so far but if it is too much, next time you guys need to ask for advice and monetary help from Tanzanian citizen in and out the country. Unless you want to do it by yourself for your personal or business reason but no matter the reasons behind remember you represent our country's name. And (we) as citizens we have the right to question or say the truth.
Remember public relationship is very good too. You don't want to put in drain all that you have accomplished so far with unintentional comments.
Nyinyi Watanzania, Kiswahili ya kwagu si sanifu, kama ya kwenu.
ReplyDeleteLakini wacheni Kiswahili murefu! Msaindieni Maria! Maneno maneno migi sana pana leta a viable solution to what your kamurebo kazuri kenu encountered in Mexico City, Mexico.
Asiyekumbali kushidwa si mshidani!
Na wewe, Maria Sarungi-Lethai, una mbahati ya kuweza kupata lawama na sifa kutoka kila upade wa dunia kuliko na Watanzania, kwa njia ya mtadao via Michuzi.
Kumbali kupokea hizo lawama na sifa zote. Zi-analyse. Na u-synthesize mazuri ya kujifuza.
Nyinyi Watanzania, kubukeni kuwa the competitive edge demands that you purposefully learn to persevere under defeat. But pick up the courage to stand up and fight again!
Flaviana (abaye anafanana na ndito ya Kimaasai)amekosa kwa wa kwaza, lakini Tanzania imepata ndanda yeke mndogo wa Alek Wek!
Ushauri kutoka kwa wa Ujirani Mwema Nchi ya Kasikazini!
dada maria kubali kupokea hizo construcive criticisms, hamna haja ya ´malumbano, mwenye macho haambiwi tazama, watu wameona na wanatoa mawazo ya kujenga. Kubali kukosolewa ili next time iwe perfect.
ReplyDeleteHuyu Maria Sarungi anaonekana ni mtu mbishi sana na pia anajifanya anajua kila kitu kuhusu mambo ya urembo na mavazi. Hivi watu wangapi wakuambie kuwa lile gown lilikuwa baya ndio utakubali??
ReplyDeleteMimi nakumbuka nilivyokuwa naangalia haya mashindano kwenye TV haikunichukua hata sekunde 5 kujua gauni litamharibia Flaviana hata kabla ya matokeo kuwekwa hadharani. Na pia nilikuwa naangalia na watu wengine ambao sio Watanzania nao wote walisema hilo hilo kuhusiana na hilo gown. Ukweli ni kwamba mlichemsha kwenye lile gown hata kama huyo Mvenezuela Miguel alilishona/kulifanyia fitting usiku mzima.
Kama wengi wanavyosema chukua criticism na uzifanyie kazi ili mwaka ujao kusiwe na makosa kama haya.
The absurd part about this argument is the implication that "the gown" won the competition for the Japanese lady and lost it for Flavia, and the fact that no Flavia without Maria!
ReplyDeleteIt looks like all new Flavia suitors will have to go through Maria...the Stalinista! Just kidding!
Sasa jamani...binti kafikia hapa alipofika...let us move on...mwishowe mtakuja kumfanya awe Mwisho Mwampamba mwingine...overwhelmed by new fame and totally unecessary publicity. Kuna mambo ya msingi zaidi. Kazi ya kupiga vita mimba za watoto wa darasa la sita kule Tunduru na Nkasi tusimuachie Ananilea Nkya pekee.
Maria, good job on a job well done. Now you have to come up with another unique Tanzania girl for next year!! Kaaazi kwelkweli!
ReplyDeleteI bald girl worked for you this time - are you to keep it up next year???? Are you to incorporate the tons and tons of constructive criticism you got here and on other blogs and websites? Or are you going to continue being defensive (and for what?)????
In either case, good luck next year (na angalia usijepata vicheche vichache vitakavyoharibu jina lako na la nchi!!)
michuzi una roho mbaya, umeniudhi sana! kubana coment yangu. ningekuwa nimetukana ningeelewa kwanini umebana! mimi najiheshimu na nimeandika point unabana ili iweje? yaani muda wangu wa kuandika si kitu? inavunja moyo! kuna watu humu wametaja mpaka wajomba wa maria kuwa ni wabishi lakini umepost. not fair at all. najua nahii utaiminya sawa tu!
ReplyDeletemaria bisha uwezavyo lakini huu mshono "MWANAMEKA" sijui 'Nguva" ulomvisha mrembo wetu na unaambiwa lakini huna hata dalili kujufunza wala kukubali shauri yako.
mdau mza
Jamani, mimi kila siku nasema hivi, sisi waswahili huwa mdomo ni mrefu sana sana. Mtani wetu wa jadi, Muthoni, katuambia ukweli. Sioni kama kuna ubaya kwa maelezo ya Sarungi kuhusu mchakato mzima wa Miss Universe.
ReplyDeleteMimi nadhani watoa mada hapa juu wangetoa pongezi za dhati na kumshukuru Maria na waandaji kwa binti yetu kufika hapo alipofika. Walikuwepo Warembo kibao, katika hao binti yetu kafikia 10 bora. Je, hao wengine pia mavazi yao yalikuwa na kasoro zaidi ya Flaviana? Hao wengine ina maana walikuwa uchi mpaka night dress ya Flaviana ikaonekana mbaya na bado akashika moja ya nafasi kumi?!!
Hii nailinganisha na wadau wa soka hapa Nchini. Miezi miwili iliyopita Coach mkuu Maximo alivunjavunja na kuunda team ya Taifa Stars upya. La ajabu wadau wakubwa, wakiwemo waliobobea kwenye mpira, kama Mziray na Gulio, walilaumu sana kwa kisingizio kuwa eti serikali imeingia gharama kubwa sana kuwapeleke Brazil wachezaji na isingekuwa vema kuibadilisha team. Pia waliidai kuwa wachezaji walioongezwa ni wachanga zaidi na waliotolewa ni wazoefu sana. La ajabu mpira ulipopigwa Mwanza hao hao ndo wamekuwa wa kwanza kumpongeza coach! Pia walikuwa wa kwanza kumpongeza Haruna Moshi kwa kudhibiti wa-senegali kwa nguvu na akili zote! Haruna Moshi hajawahi kucheza mechi yoyote ya kimataifa!!
Hii Maana yake nini basi. Hapa ina maana kuwa sisi Wabongo huwa wagumu sana wa kuelewa na kukubali matokeo pia na mabadiliko. Wabongo wakikomalia issue inakuwa aibu tupu! Hakuna mabadiliko ya kufikiria wala ubinifu wala hata akili mbadala. No Suggestions! Lawama tu mtindo mmoja!
Hii inadhihirishwa na comments za hovyo hovyo hapo juu. Wote akili imelala kwa kulaumu tu na bila kuchuja. Hakuna wazo mbadala ila eti ...Maria kubali mawazo, yapi hayo?!!
Jamani, tumpogezee Maria na Flaviana. Angalau hata Mexico wametufahamu sasa. Nimewahi kuishi na Wa-South America huko Europe, walikuwa wananishangaa ni nimetoka Tanzania,,, ndiyo wapi!. Lakini Sasa angalau wanajua kuwa kumbe kuna vibinti vizuri na wanaweza kuja kuchangaia kwenye gene pool yetu!!
Ujumbe kwa Maria:
ReplyDeleteNaingia sana kwenye blog ya Michu na nimesoma uchangiaji kuhusu issue mbali mbali, watanzania hawamkopeshi mtu. Kwa issue ya Flavy wamekuwa na umoja wa ajabu sana hakukuwa na negative comments, matusi wala nini wote tulikuwa bega kwa bega binti yetu ashinde.
Comments wanazotoa wote hapo juu ni very very constructive, maana hata kama wewe ndiye uliye m-sponsor Flavy lakini kawakilisha taifa letu, therefore acha ubishi mi ninge kuwa wewe ningesema: "Asanteni sana kwa maoni yenu wote next time nitajitahidi kusahihisha pale tulipo kosea na kufanya vizuri zaidi" PERIOD!
Kwa watanzania wote: kwa issue ya Falvy umoja wenu ulinigusa sana kumbe huwa mnafanya makusudi kuleta fujo....now I know deep down u all love our beautifull country/people.. I love u all
Mungu ibariki Tanzania, viongozi na watu wake.
Waridi
MJADALA UISHE WARIDI AMESEMA YOTE. MWENYE MASIKIO ASIKIE...
ReplyDeleteHONGERA FLAVIA NA HONGERA MARIA KWA YOTE MLIYOYAFANYA. NA NEXT TIME CHUKUA MAZURI NA UYATUMIE NA MABAYA WEKA KWENYE KAPU UJUE NI MATOKEO YA KUWASILISHA NCHI
WACHA KUTUTIA AIBU WATANZANIA, WEWE UMEONA DOLA 3000 NYINGI KUMNUNULIA NGUO MISS TANZANIA KTK SHINDANO. KAMA UMEONA NYINGI HAKUNA UMUHIMU WA KUSHIRIKI, KAMA NI NCHI DOLA 3000 NI MBUZI TU...
ReplyDeleteUKITAKA UZURI UZURIKE...
MTOA MADA UMEJITAHIDI KUELEZA KASORO YAKO MOJA KUBWA NI KUENDELEA TU KUTAMIA MAWAZO YA KIZAMANI KAMA VILE "JAMBO FULANI NI SIRI", "JINA TUNALIHIFADHI" na mengineyo kama hayo. Dunia ya leo ni ya uwazi na kweli achana na tabia hiyo ambayo msingi wake ni watu kupenda kusifiwa tu na inapotokea kuwa-challenged au critized basi huyo nii adui, au ni wivu. Tutumie mawazo ya wengine kama kichocheyo cha maendeleo na siyo vinginevyo
ReplyDeletemaria alitoa siri uwanjani: "Miguel alifanya kazi usiku mzima kukamilisha gauni lile."
ReplyDeleteHiyo shonwa shonwa hadi usiku mzima! ndio maana kifua cha Flaviana hakikuvailiana na gauni hilo!
Mrembo wetu alionekana kana kwamba kwamba kavaa gauni la mama yake!
Kulikuwa na mapakizi mengi ya kitambaa kenye mshono wa matiti kwa sababu gauni hiyo ilikuwa imeshonwa kwa wenye matiti makubwa kuliko Flaviana wetu!
Hata hivyo, tuache yaliyopita; tudunge yajayo!