
mwandaaji wa miss universe tz maria sarungi-tsehai akiwa na flaviana matata na mtaalamu wa saikolojia mike lerch ambaye amekabidhiwa jukumu la kuwanoa washindi wanne bora wa miss universe tz katika kambi maalumu ya kuwatayalisha kisaikolojia inayoanza leo ijumaa hadi jumapili katika kuwaandaa kwa mashindano na majukumu mengine mbeleni. kambi hiyo, ambayo imedhaminiwa na kampuni ya roundtrip tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya matangazo na uhusiano ya lowe scanad pamoja na hoteli ya jangwani sea breeze, itatumika kuwapa warembo hao ambao ni pamoja na flaviana ushauri nasaha, mazoezi na ushauri ili kuwatayarisha kuwa warembo wa mfano wa kuigwa katika maisha yao ya baadae. kwa mujibu wa maria progamu hii imeandaliwa ili kuhakikisha warembo wote washindi wa miss universe tz hawatumbukii katika midomo ya mamba na pia kuwaandaa wawe maselebriti wenye kujiheshimju
ndo maana, kumbe maria mwenyewe ndo huyu anaonekana tu ni mbishi hata kwenye picha
ReplyDeleteWala huhitaji mafunzo yeyote...hao majibaba yanayopenda dogo dogo ndio yanatakiwa kupewa mafunzo.
ReplyDeleteLa muhimu huyu ni kumpeleka shule akapate degree na kazi nzuri ili aweze kusimama kwa miguu yake miwili bila kutegemea wanaume.... Itakua mfano kwa mamiss wengine wanaokimbia shule baada ya kuwin kidogo tu.
Na somo ni kwa wasichana wote wa kibongo MSIPENDE FREE RIDE....mambo ya fairy tail sio mazuri...wasichana wakibongo kuwin big kwao ni kuolewa na billioner. Kwa hiyo hata shule sio muhimu tena kwa wengi kwa vile still wana day dreams za kupata maTX au matajiri. Basi kazi iliyoko kwao ni kujipamba kutwa kucha na kwenda kwenye trapping clubs.
Tokeni kidogo muone wasichana wa ughaibuni wanavyochacharika na maisha.
Huyo "saikolojisti" mbona anaonekana MHANGA sana huyo? (UH++).
ReplyDeleteHao mabinti watapona hao kweli jamani!?!
mimi nadhani hawa wazee wanaojidai wanatoa sijui KANSELING, wao ndio wanatakiwa wapewe, maana hawa ndi waharibifu wa watoto wa watu.
ReplyDeleteAnaonekana ana njaa tena wazee wa kibongo, yaani hapo cha maana hakuna zaidi ya kuwapa sound. Mimi siwaamini kabisa, labda wangepewa mwanamke wawafanyie huo ushauri, otherwise kwanza huyo baba kashaniboa hapo.
Binti wa watu bado mdogo sana wasije MKIRA bure hao vijibabu
hahahahaaa dah wabongo kwa kuua ni noma
ReplyDeleteUnajua kila mtu huku kaenda shule kusoma psychology au sociology. Sasa saa hivi wako kila kona huku na wengine ndio wanakimbilia huko kwetu.
ReplyDeletejamani sisi culture yetu sio mambo ya counselling or therapisty.. Sisi tuna bibi na wakunga wa jadi... wasituchukulie kazi zetu bure
isijekua one session pound 300.
Bi kidude yuko wapi? tosha kuwacousel hao watoto na hiyo hela mngempa yeye anaelewa mazingira yetu na nini kinawafanya wasichana kukimbilia wanaume matajiri na kuacha shule....shida sio couseling uchumi mgumu na sort cut ya mbongo kufanikiwa sio kufanya kazi ni kuwa kupe.
Ukiona wafanyakazi wengi wanaenda kazini kila siku lakini hawawezi kulipa kodi ya mama mwenye nyumba nani atathamini kazi tena?