
septemba 6, 1992: mzee oscar kambona akiwasili dar na binti yake neema baada ya kuwa uhamishoni kwa zaidi ya miaka 25. siisahau siku hii kwani tulifika uwanjani saa 11 alfajiri kusubiri ndege ya british airways itue saa 12 na kulikuwa na uvumi kwamba mzee kambona ambaye sasa ni marehemu angekamatwa mara tu atapofika, hivyo askari kibao walitanda uwanjani na wakawa wanatuzuia tusiingie ndani. mie na kaka james nhende wa mfanyakazi tulipenya na kuingia ndani kwa kutumia njia za panya. waandishi wengine kutuona sie tuko ndani na wao wako nje wakaanzisha zogo, virungu vikatembea. bahati mzee huyu hakukamatwa wala nini na mambo yakaisha salama. ila ni wachache walifanikiwa kuipata picha hii
Kwanza, nadhani huyu jamaa alikuwa more visionary katika mambo ya uchumi kuliko hata Nyerere. Sielewei uwezo wake katika mambo mengine ya kujenga taifa ambayo Nyerere alifanikiwa sana, ila katika kila jambo alilomwonya Nyerere katika kuongoza uchumi alikuwa right.
ReplyDeletePili, kumbe binti yake alikuwa mzuri vile. Yuko wapi siku hizi? Unaweza kuniungaishia? hata mimi nimekomaa kama yeye.
Tatu, ni afadhali tungeafuata sera za Kambona kiuchumi moja kwa moja kwa sababu tusingeashangaa sana wakati rais Mkapa alipoamua kufuata sera hizo baada ya kifo cha Nyerere kwa kuanzisha ANBEN LTD.
Samahani, nilisahau kukuilza kwa nini mwaka 1992 ulipga picha ya black and white. Ulikuwa bado na dinosaur camera?
ReplyDeleteNamjibia Michuzi kuhusu hilo swali la huyo ndugu hapo juu kuhusu kwa nini michuzi alipiga hii picha black and white jibu ni kwamba angepiga ya rangi ingeonekana na polisi thats why akapiga hii ya giza gizaa yani ilikuwa ni kimya kimyaa mtu wanguu camera ilikuw andani ya shati wangu.LoL
ReplyDeleteAjabu sana Harusi yake Kambona ilifungwa kanisani London na Nyerere ndiye alikuwa Best man wake wakiwa wamesafiri kwa hela za Walipa kodi miaka ile wakaenda kuzila kwenye harusi na Kambona na kuzinywea wine na pombe za Ulaya na kuzivutia sigara za Ulaya wakati ule Nyerere alikuwa mvuta sigara sana na mpenda raha.
ReplyDeleteHata sijui hawa marafiki wakaribu waligombaneje.
Labda mke wa Kambona aliwachonganisha.Maana naye alikuwa kiwembe hadi akamtelekeza mzee Kambona hadi akafa Bachelor pamoja na kuwa alizaa naye Huyo msichana.
Huyo Msichana Safi sana Kalitoa hotuba nzuri sana pale uwanja wa Jangwani Wakati vyama vingi vilikuwa ndio vinaanza.kalikuwa kanajiamini na kako fit sana kichwani.
Nilipendezewa nako sana kwa hoja zake.
Michuzi, hata mimi nilifanikiwa kuingia ndani pale Airport, lakini nikaotelewa nje. Nilidhani nitapelekwa lockupu.
ReplyDeleteIle boxi aliyoshika Neema ni fax machine. Alinyang'anywa na customs airport. Kambona alivyo-clear customs na kuruhusiwa kutoka alionekana kama ana mshangao fulani maana nadhani naye alitegemea kukamatwa.
Kambona alivyotoka nje kuna kundi la watu walimshangilia ile mbaya, na vilio vilisikika mpaka TAZARA. Ungeon uso wa Kambona alivyosikia anashangiliwa, karibu alie.
Yeah, siku ile Kambona alivyorudi Bongo ilikuwa historia.
neema....anaitwa neema kambona masika..... ameshaolewa na ana watoto wawili. kwa sasa yupo dar anafanya kazi european union kama public relations personnel wao...
ReplyDeleteMichuzi, kuhusu hizo "njia za panya"... je, ni rushwa kwa kuhonga walinzi pale airport?! Naomba ueleze, ahsante
ReplyDeleteMume wa Neema ni Dr. Richard Masika, Mkurugenzi wa mafunzo (Director of Studies) na vice principal pale DIT - Dar es Salaam Institute of Technology (zamani Dar Tech).
ReplyDeleteMume wa Neema (Dr Richard Masika), sasa ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha yaani Arusha Technical College
ReplyDelete