……bruuum bruum bruuuum…. taxi ya Kengeja inakuja….mbele kuna polisi wa trafiki….……..mara polisi akaisimamisha gari…..


Polisi: "assalaam alaykum mzee"


Dereva: "walaykum salaam"


Polisi: "nakushtaki……kushajua kusolo?"


Dereva: "abaa hadi sasa sijajua…..na kwanjionavyo leo sinakosa"


Polisi: "kunzidisha watu abaa…wakubaliana nami?"


Dereva: "yakhe mie sijazidisha….nionyeshe huyo ntu aliezidi humu"


Polisi: "gariyo inruhusiwa kuchukua watu wanne….hebu esabu watuwo n'wangapi?"


Dereva "n'wanane"


Polisi: "kutokana hesabuyo huoni kama watu wanne wanzidi hapo?"


Dereva: "nasematena abaa sijazidisha…ila weye wajuakusoma?....subirintoke uko nje"….dereva akatoka nje ya gari….


Dereva: "soma apa n'langoni panaandikwaje?"


Polisi: "licensed to carry four passengers"Dereva: "ha kunjua maanaye?"


Polisi: "enhe…..imeruhusiwa kuchukua abiria wanne….ndio n'kakwambiakun'zidisha abaa"


Dereve: "zunguka na nlango wa huku…uje usome…"……dereva na polisi wakazunguka mlango wa mbele wa pili wa gari…"


Dereva: "ha soma na hapa"


Polisi: "licensed to carry four passengers"


Dereva: "ha abaa nne na nne n'ngapi?"


Polisi: "n'nane"


Dereva: "ha sin'kwambia sijazidisha ila nawe ukaidi un'kushika"…..


dereva akaingia kwenye gari, akatia moto gari nakuondoka…..akimuacha polisi kapigwa na butwaa akiwa hajua hata asemenini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2007

    hahahaha michuuu leo kweli umeleta kituuu yaani siku yangu naona itakuwa ni ya kucheka tuuuu.....weka vichekesho vingi km hivi!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2007

    no offence meant,hiki kiswahili sio cha pemba kweli!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2007

    Brother Michu mie hizo ANTIQUES za magari huwa nazihusudisha sana hizo, unakatiza nalo kule coco beach au Mlimani city just for fun!
    Kama analiuza mi ntalinunua hilo Michu.
    Au kama unajua mtu anaeuza PEUGEOT 403, lina pua mbele, halafu milango yake ya mbele inafunguka kwa upande wa mbele huo huo! Mwee! Nalizimia sana!

    ReplyDelete
  4. si mchezo nimependa sana, heee more idea kwanini kusiwa na blog ya jokes pekee yake kama hivi. au ipo mi sijui

    ReplyDelete
  5. natokwa na machozi kwa kucheka!

    ReplyDelete
  6. kwa kiluga kagari kama hako tunakaita 'kabyuku'. Nimeipenda hiyo humour. Nimerudi mzee mtandao ulikuwaga unasumbuwaga kule kwetu Mbeya.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 12, 2007

    Michuzi,

    Mimi ni mmoja ya wageni wa mwanzo katika blog yako (tangu picha za helsinki october 2005, wakati huo sikuwa hata nakufahamu kwa sura zaid ya jina in fact kwenye ile picha ya helsinki nilifikiri ndesenjo ndio wewe). Nimekuwa nikitembelea blog yako na kupitia comments kila siku ya Mungu ila leo ndio itakuwa ya mwanzo kusoma comment nilioiandika binafsi. Mara zote nilijiona sina cha kuchangia hivyo nilibaki msomaji tu. Leo nimefurahishwa sana na nimeshindwa kujizuia na huu ucheshi uliopost, mimi ni mpemba wa asili inaonesha alieandika sio mpemba kweli kwani kachemsha sehemu kadhaa ila kajitahidi.
    Natumia hii fursa pia kutoa ushauri kwako upunguze ucheshi hasa ule uliosheheni adult-content. Hali kadhalika nahamasisha watoa maoni waachane na uanonymous unaharibu hii blog, pongezi kwa mashujaa kama mwaipopo!!!

    A. Ayoub,
    Canada.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2007

    ..Sir Issa..hiyo gari inafaa.."..PIMP MY RIDE.."

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 16, 2007

    Michuzi mbavu zinauma kwa kucheka, my god! mswahili ni mswahili kweli, very funny!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...