
salamu za shukrani toka makunduchi zimeingia sasa hivi
Bwana Michuzi,
Tunakushukuru kwa jitihada zako za kuwaelimisha Watanzania wenzetu. Kujitokeza kwa wadau wengi kutoa maoni yao juu ya ule mjadala wa 'amarula, na ndovu ni dalili kuwa ujumbe wetu umefika. Tunawashukuru Watanzania wote waliotoa maoni yao. Hii ni dalili njema ya kupevuka kwa demokrasia nchini. Hatuna nia ya kuanzisha mjadala mwengine lakini tunategemea Watanzania walio wengi watakuwa pamoja nasi. Mwisho tunawakaribisha Watanzania wote katika Sherehe yetu ya jadi ya kusherehekea 'Mwaka Kogwa' yaani mwaka mpya wa kiswahili huko Makunduchi itakayofanyika mwezi wa Julai 22.
Mwenye kutaka habari zaidi kuhusu mwakakogwa afungue mtandao wetu wa kijiji http://www.mzuri-kaja.or.tz/
Ahsante sanaMuombwa
Watu wa Makunduchi siwawezi .... kumbe longo longo lote lile ilkuwa ni "Nitoke vipi?"
ReplyDeleteHaya bwana mmeshapata "attention" yetu.
Tunaogopa kuja huko: POPOBAWA!!
ReplyDeleteWaungwana umefika wakati wa kuziacha mila nyengine zisizo na value added kwa jamii .hayo mambo ya mwaka kogwa kwa kweli si mazuri kwa kipindi hichi kilichoshamiri hili janga la ukimwi, kwani nikichocheo kikubwa cha maambukizi ya ukimwi.kwa kweli watu hufurika kufanya ufuska tu.ukimwai utatumaliza tukiendelea kukumbatia mila potofu.
ReplyDeletesijabahatika kufika kisiwa cha pemba,sijui hapo makunduchi au mwanakwereke ndo mjini kabisa? au nje ya mji,
ReplyDeletehongereni kwa mwaka mpya wa kiswahili,japo sijaelewa mnamaanisha nini?na hepi bethdei zenu zinafata mwaka huo? au?
Kamtu-Chui/Paris
hahahhah! Haya tena Muombwa kaja na mamabo ya mzuri kajaaaaa huyu jamaa kweli kibokoo pwanii full maneno yake yantia wlakini wadau tusijekuwa tumeingiliwa na popo bawa kweny blog yetu Michuzi angalia hii mammbo.
ReplyDeleteWeb yenu kaandaa mzungu "The local traditional medicine man call it "Mkuu hapingwa", literally meaning "the leader is not opposed"" au HAPINGWA ndo HAPINGWI kwa ki makundu chi
ReplyDeleteDUH..MICHUZI HUYO JAMAA ALIYEKUPA PICHA AMENIKUMBUSHA MBALI SAANA.
ReplyDeleteHUU NDIYO MBUYU NILIYOCHEZWA NGOMA YANGU YA JANDO BAADA YA KUTAHIRIWA.
HIVI BADO UPO MPAKA LEO. MIAKA AROBAINI SASA SIJAFIKA ZENJI LAKINI HAPA SIJAPASAHAU KWANI NILIKUWA NIKIPITA KILA SIKU. BRAVOOOOOO JAMAAAA
Vipi mzee msosi, na wewe unafika huko makundu uchi?
ReplyDeleteMichuzi hii website ya mzuri kaja...Nimeipeda sana!!! Ina touch maisha ya mwananchi wa kawaida!
ReplyDeleteBest,
Gina la village linafurahi "Mzuri kaja"
ReplyDeleteCulture celebration yao iko so rich nafikiri hizi ndio sehemu bali Tanzania still zina keep original traditions.
nakupitisha michuzi, hizi culture ni muhimu kutunzwa. Huwa nafikiria kwa nini Ukanda wa Pwani usijaribu kutunza traditional swahili. Kuna weza kuwa na Traditional swahili na modern swahili kama ilivyo ktk Chinese. Sijui kwa nini sisi hatuna hamu ya kuhifadhi historia yetu, wakenya wataendelea kudai kiswahili kimeazia kwao kwa vili sisi hatuthamini hata historia na utamaduni watu.
ReplyDelete