Home
Unlabelled
new african
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Obviously, there is hope for Africa. But that will be achieved when imbeciles we have put in power will stop wasteful spending and stealing from poor folks.
ReplyDeleteKwa spichi za kupendeza tu, viongozi wa kiAfrika wamebobea. Lakini vitendo vyao viwadipresi tu wananchi.
“Hushangai watoto wa Kennedy unashangaa Ridhwani Kikwete kugombea uongozi wakati baba yake ni mwanachama wa CCM na kila siku ndani mwao anachojua ni CCM. Ukitembea na mhanga, utachimba,” -Yusuf Makamba.
ReplyDelete“Hushangai watoto wa Kennedy unashangaa Ridhwani Kikwete kugombea uongozi wakati baba yake ni mwanachama wa CCM na kila siku ndani mwao anachojua ni CCM. Ukitembea na mhanga, utachimba,” Yusuf Makamba.
ReplyDelete“Ninaye rafiki yangu mmoja Morogoro, yeye ni padri, ana watoto watano, wote pia ni mapadri,” Yusuf Makamba.
ReplyDeleteMapadri hawaruhusiwi kuoa au kuwa na watoto.
Viongozi wetu bwana!
kaka michuzi tuwekee hata picha moja ya mechi ya senego na tz.
ReplyDeleteJomo Kenyatta wa Kenya aliwahi kuulizwa tofauti ya Tanzania na Kenya ni nini akajibu kuwa "Kama unataka watendaji wazuri katika sekta mbalimbali njoo Kenya utawapata wengi sana na kama unataka wahutubiaji wazuri kwenye kila eneo liwe la siasa,uchumi,biashara,kilimo,maofisini n.k nenda Tanzania kamwambie Nyerere akupe anao wahutubiaji wengi sana wazuri kuanzia tawi hadi juu kwenye taifa.
ReplyDeleteMbele ya raia wengi awamu hii ya Uongozi wa Rais Kikwete ni awamu ya wahutubiaji wazuri sana kasoro mtu mmoja tu SAID MWEMA ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi ambaye ndiye pekee ambaye kagoma kuwa mhutubiaji, kaamua kuwa mtendaji.
Huyu hata Kenyatta angekuwa hai angemwomba samahani ila waliobaki angewaambia hata kama wanataka kwenda mahakamani waende wakitaka haombi samahani!
Tanzania bado haijapata Raisi ina Waziri wa Mambo ya nchi za nje ambaye amehama na katibu wake mkuu wakahamishia ofisi na majukumu yao ya wizara ya Mambo ya nchi za nje Ikulu na wanaendelea nayo wakiwa Ikulu.
ReplyDeleteMkapa kama awamu yako ilikuwa ni ya "uwazi na ukweli" vipi mkopo wako uliufanya siri?
ReplyDelete~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tangu kuondoka madarakani kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Bw. Benjamin Mkapa tuhuma na madai mbalimbali yamekuwa yakimuandama mstaafu huyo kila kukicha. Madai ya hivi karibuni ambayo yamekuwa ni kama chumvi kwenye kidonda na mafuta ya taa kwenye moto wa kuni, ni yale ya Bw. Mkapa kujipatia mkopo wa benki na hatimaye kuanzisha kampuni ya biashara wakati akiwa bado katika kiti cha urais. Kabla ya madai haya ya sasa kulikuwa na madai mengine mengi ambayo yanamhusisha Rais Mkapa mwenyewe, mkewe au familia yake ya karibu.
Mara hizo zote, juhudi za kumtaka Rais Mkapa azungumzie na kujibu madai na tuhuma zinazotolewa dhidi yake zimegonga mwamba. Lakini kwa vile Tanzania hatuna wafalme, na viongozi hutawala kwa ridhaa ya watu, na ya kuwa katika nchi ya kidemokrasia kama ya kwetu viongozi huwajibika kwa watu basi hatuna budi kwa mara nyingine tena kumtaka Rais mstaafu Bw. Benjamin William Mkapa kuzungumzia utajiri alioupata akiwa madarakani na kuonesha kwa vielelezo kamili kuwa utajiri wake kaupata kwa njia ya halali na siyo kwa sababu ya kutumia cheo na nafasi yake ya Urais.
Kwa watu wengi ambao wanafuatilia tuhuma zilizotolewa na zinazoendelea kutolewa kwa Rais Mkapa watakumbuka kuwa kati ya tuhuma zote kubwa ya zote ni ile tuhuma ya kuhusika kwake katika ununuzi wa rada ya kijeshi ambayo Benki ya Dunia ilisema ni ghali mno na haikufaa kwa matumizi ya Tanzania. Baada ya mamlaka za Uingereza kuanza kufanya uchunguzi wa kampuni iliyohusika na uuzaji wa rada hiyo, watu na taasisi mbalimbali hapa nyumbani na nje ya nchi walijenga hoja kuwa Bw. Mkapa azungumze na wananchi na awaambie ni kwa kiwango gani alishiriki katika ununuzi wa rada hiyo. Kelele hizo zilipozidi, Rais Kikwete akiwa katika moja ya ziara zake nje ya nchi (Brussels, Ubelgiji) aliingilia kati na kuwauliza Watanzania "Hivi mnataka mzee Mkapa atoe sauti, sauti kuhusu jambo gani? Mnataka aseme nini, mimi naona tumwache mzee wa watu".
Suala hili la uanzishaji wa kampuni uliofanywa na Rais Mkapa na mkewe mwaka wa nne tu wa Urais wao umezidi kuzua wasiwasi na hisia za kuwa Rais Mkapa hakuwa mtu "msafi" kama tulivyofanywa kuamini wakati wa uchaguzi wa 1995. Hata hivi sasa watu na taasisi mbalimbali zinapomtaka Rais mstaafu huyo kuzungumzia miradi yake wakati akiwa katika ofisi ya juu kabisa nchini, kelele za "mwacheni mzee wetu" zimeanza tena kusikika. Tahariri ya mojawapo ya magazeti ya serikali wiki iliyopita ililitamka bila haya au kigugumizi chochote kile kuwa "Mkapa amefanya mengi kwa taifa hili na tumpe nafasi ya kustaafu na kupumzika bila bughudha yoyote."
Kwa baadhi ya watu kumtaka Mtanzania mwenzetu huyo kutuambia na kututhibitishia kuwa hakutumia nafasi yake vibaya alipokuwa madarakani ni "bughdha" isiyo ya lazima na ni sawa na "kumuandama Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu kwa sababu ambazo hazina msingi zaidi ya chuki.". Kwa watetezi hawa wa usiri, kuulizia kiongozi aliyepita katikati yetu na kuomba kura zetu mara mbili akiahidi kupigana vita dhidi ya ufisadi huku akipepea bendera ya "uwazi na ukweli" basi imekuwa tatizo. Tunapouliza ni jinsi gani kiongozi tuliyemweka madarakani kwa kura alitumia ridhaa hiyo na kama hakuitumia ridhaa hiyo kujinufaisha yeye na familia yake imekuwa nongwa.
Ndugu zangu kama waswahili wasemavyo, "akutukanaye hakuchagulii tusi". Mtanzania mwenzetu tulimchagua atuongoze kwani tuliambiwa kuwa kati ya wale wote walioonesha nia ya kutaka kwenda Ikulu mwaka 1995 yeye ndiye aliyekuwa "msafi". Nakumbuka alivyonadishwa na Mwalimu Nyerere pale uwanja wa Nyamagana. Tukamchagua na kumpa dhamana ya uongozi wa nchi yetu. Miaka kumi baadaye Mtanzania huyo anaondoka Ikulu akiwa Bilionea na watetezi wake wanatuambia tusiulize kazipataje, kweli woga mwingine! Kiongozi ameondoka akiwa na majumba bwelele ya kupanga na makazi, ndani na nje, akiwa na akaunti za fedha hapa nyumbani na ugenini, na akiendelea "kutesa" kiulaini kwa pensheni na mafao kadha wa kadha yanayotokana na ofisi yake iweje kumuuliza kuwe kosa? Kumuuliza "mzee utuambie umevipataje vitu hivi vyote ndani ya miaka 10, wakati yule aliyetawala nchi yetu miaka 25 hakuweza" tunaambiwa ati tunambughudhi mzee. Hoja nyingine ni za kutupa zinapotolewa tu hadharani.
Ukweli ni kuwa watetezi wa Mkapa wanatutaka tukae kimya kwa vile hata tuulize vipi hatutapewa majibu. Binafsi naona kuwa wale wanaotutaka tunyamaze tusiulizie utajiri wa Rais Mkapa wanatumia visingizio vya "Amani ya Tanzania", "Kubadilisha uongozi kwa ustaarabu" na "uzee wa Mkapa" kama mbinu ya mazingaombwe ili tusione viini macho vinavyotendeka au vilivyokwisha tendeka. Mbinu zao hizo zinatokana na hofu moja tu, nayo ni hofu ya ukweli. Watetezi wa Rais Mkapa wanaogopa ukweli kujulikana na watu wa kawaida kwani sifa zote za "amefanya mengi kwa Taifa hili" zitapeperuka hewani kama vumbi kwenye jani kavu lipeperushwapo na upepo. Watetezi hawa siyo tu hawako tayari kuuacha ukweli ujulikane bali hawawezi kustahili kuona ukweli huo! utawaumbua.
Kuhusu hili suala la Rais kupewa mkopo wa dola laki tano na kuweza kuanzisha biashara akiwa ofisini na kutajwa ati huo ni mfano mzuri wa kukopa kutoka benki na klipa. Wazo hilo kwanza linatuchekesha na linasikitisha mno. Kama alikuwa ni mfano mbona hatukuambiwa wakati anakopa na kurudisha fedha hizo ili tumuige? Kwanini awe mfano baada ya siri kufichuka? Hivi wanataka Watanzania tuamini kuwa Rais Mkapa alikwenda mwenyewe benki kimya kimya au waseme tu kuwa benki ilimfuata Ikulu.
Sitashangaa kabisa kuwa imekuwa vigumu kwa Rais Mkapa kufuatilia kwa makini na kwa uzito unaostahili tuhuma na madai yote yanatolewa dhidi yake binafsi na familia yake. Hili linawezekana aidha kutokana na wingi wake au kwa sababu nyingine yoyote, nimeona nijitolee basi kwa moyo wangu wa ukarimu kuorodhesha tuhuma na manung'uniko ambayo yamejaa mitaani kuhusu utawala wake na hasa kwenye suala hili la kujitengenezea utajiri wa haraka haraka ndani ya miaka kumi ya kukalia kiti urais wa jamhuri yetu. Madai hayo ni haya:
Kwamba akiwa Rais na kwa kutumia nafasi hiyo aliweza kujipatia mkopo mkubwa kutoka benki miaka minne tu ya utawala wake tena alifanya hivyo wakati watanzania wako katika kumuuguza baba wa Taifa. Kwa mtu aliyepewa kwa dezo nafasi hiyo na Mwalimu Nyerere kitendo hicho kinaonekana ni cha kisaliti na kuvunja vunja kila ambacho Mwalimu alisimamia.
Kwamba katika kipindi chake hicho kifupi aliweza kukusanya fedha kiasi cha kujenga jumba Lushoto, kufanyia matengenezo nyumba ya Sea View, kujenga jumba jipya Msasani, na kununua nyumba/hoteli huko Afrika ya Kusini na ikadaiwa alimuomba mzee Madiba aipe baraka zake, na mzee huyo akamkatalia.
Kwamba ilikuwa ni kutokana na baraka zake Taifa letu likaingia kwenye Mkataba wa kununua rada ya kijeshi ambayo kwa mujibu wa Benki ya Dunia ilikuwa ni "ghali na kwa Tanzania haifai". Baadaye imekuja kugundulika kuwa dalali aliyeshiriki kutuuzia rada hiyo alimegewa karibu dola milioni 12 kwa kazi yake huku akiwagawia watu wachache serikalini. Je yeye (Mkapa) alijua kuhusu mgao huu kwa "namna yoyote" ile.
Kwamba ilikuwa ni katika uongozi wake Taifa letu likaingizwa kwenye mikataba ya ajabu ya uwekezaji na ile ya ubinafsishaji. Ilikuwa vipi yeye kama Rais kushindwa kabisa kuweka maslahi ya Taifa mbele hadi mrithi wake anapokuja ndipo makosa yanaonekana hadi kudaiwa kuwa Tanzania "hatuna wataalam wa mikataba"? Kama alijua wataalam wetu hawajabobea katika mikataba hii mikubwa ya biashara kwanini hakuomba msaada mapema hadi leo tunalazimika kuwaomba watuonee huruma na kuanza "kupitia tena mikataba"?
Kwa vile alianza biashara zake na "ujasiriamali" akiwa bado Rais, ni kwa jinsi gani shughuli zake hizo ziliingilia utendaji kazi wa ofisi yake au yeye mwenyewe na hivyo kuathiri matokeo ya kazi zake alizoapishwa kikatiba. Je, haoni kuwa wazo la Rais kuanza kufanya biashara kubwa akiwa ofisini inaleta picha mbaya na hasa kuonesha mgongano wa maslahi?
Kama kweli katika kufanya biashara hizo akiwa Ikulu alitaka kuwa mfano kwa Watanzania wengine ni kwanini Watanzania hawakuambiwa kuwa Rais wao ni mjasiriamali na ameanzisha biashara kama wengine, na kwanini hakujitolea kuwa mfano wa kukopa kutoka benki na kulipa?
Kwamba, kwa kutumia vyombo vya dola alilazimisha mali ya Watanzania kuendeshwa na wageni ambao baadaye tukagundua kuwa hawakuwa na uwezo wa kutuendeshea kampuni yetu. Je haoni haja ya kuwaomba wananchi msamaha kwa kutudhalilisha kiasi hicho wakati mapolisi na mitutu yao walipowaingiza kwa nguvu watendaji wa Tanesco toka Afrika ya Kusini?
Kwamba, alipokuwa kwenye mkutano wa baraza la kiuchumi kule Davos, Uswisi ilipigwa haramba iliyoongozwa na mcheza filamu maarufu Bi. Sharon Stone ambapo kiasi cha dola milioni moja zilichangwa ndani ya dakika tano ili kumpa Rais Mkapa katika juhudi za "nchi yake kupambana na ugonjwa wa Malaria". Aliporudi na hata baadaye, Watanzania hatujaambiwa ahadi ya kiasi hicho ilitimizwa vipi? Ni kiasi gani kiliweza kupatikana taslimu na fedha hizo zilitumiwa vipi na kikundi gani katika juhudi za kuangamiza ugonjwa wa Malaria? Kwanini hakutuambia wakati huo?
Basi, hayo ni maswali machache ambayo yako mitaani na Watanzania kwa kweli wangependa wasikie majibu yake kwa ukweli na uwazi. Kwa kufanya hivyo atajijengea heshima kwa wananchi na kuonesha mfano wa ujasiri wa kiongozi kutoogopa maswali. Hata hivyo kama ataendelea kuwa kimya (kama ilivyo kawaida ya baadhi ya viongozi) basi anawapa Watanzania idhini ya kujaribu kutafuta ukweli kwa njia yoyote ile zikiwemo njia za kisheria. Itakuwa ni jambo la kusikitisha sana na la aibu endapo kesi itafunguliwa katika mahakama ya nyumbani au nje ya nchi ili kutafuta ukweli wa utawala wa Rais Mkapa. Viongozi wetu lazima waanze kubadilika kwani Watanzania waliowazoea miaka ya nyuma waoga oga hivi na wasiothubutu sasa hivi wameanza kuamka.
Kuendelea kukaa kimya na kupuuzia madai dhidi yake Rais Mkapa hajitendei fadhila, hawatendei haki wananchi waliomweka madarakani na haimsaidii kitu zaidi ya kuanza kuonekana amejiunga na jumuiya teule ya viongozi wa kiafrika ambao kwa nguvu zote wameingia Ikulu wakiwa masikini na wakatoka matajiri. Kwa kuendelea kuwa bubu kuhusu madai dhidi yake na familia yake Rais Mkapa ataanza kuonekana ni mmoja wa viongozi wa kiafrika waliotumia nafasi zao kujitajirisha kupitia migongo ya wananchi wao. Licha ya sifa ambazo amezipata nje ya nchi, wakati umefika "mzee wetu mstaafu" azungumze na wananchi wenzake ili aonekane mwenye hekima na siyo kiburi.
Vinginevyo sisi Watanzania wenzake tutaanza kupata jibu la lile swali alilouuliza Mwalimu wakati wa vuguvugu la uchaguzi wa mwaka 1995 baada ya vigogo wengi wa CCM na upinzani kujitokeza kutaka kugombea nafasi ya kuingia Ikulu. Mwalimu aliuliza "watu wengi wanakimbilia Ikulu, Ikulu kuna nini?" Hatujui kama Rais Kikwete naye ameshaanza biashara huko Ikulu au ana mpango huo, hata hivyo inaonekana Rais Mkapa ameanza kutupa jibu la hicho kilichoko Ikulu ambacho "watu wengi wanakimbilia". Tulichobaki kushangaa ni kama ule "utakatifu" wa Ikulu bado upo au uliondoka na Mkapa.
Naunga mkono Anon wa June 5, 2007 12:13:00. Watanzania tumekuwa watu wa bla bla nyingi. Mfano mzuri ni hiyo Anon wa
ReplyDeleteJune 5, 2007 4:01:00 AM EAT
Kuna ubaya gani rais kukopa!! au ulitaka aibe upate maneno mengi ya kuongea. Watu kama anon June 5, 2007 4:01:00, ndio wanapelekea watanzania kutuwa hapa tulipo, badara ya kutoa mawazo nini kifanyike, kila siku wanatafuta mtu wa kumlaumu.
Siyo siri Mkapa amejitahidi kujenga uchumi wa Tanzania, kuliko maraisi wote waliomtangulia. Ila malalamiko ya watu kama Anon June 5, 2007 4:01:00, mwisho mlimkatisha tamaa!!
Toa mawazo wa kwenda mbele, siyo tusiwe watu wa kulaumu tu.
Kama ni kuingia ofisini ukiwa maskini na kutoka tajiri si Mkapa Peke yake.Nyerere naye aliingia Ikulu akiwa lofa aliyezaliwa nyumba ya nyasi kule Butiama lakini baada ya kustaafu alikuwa na jumba la nguvu Msasani kando ya bahari,na lingine la nguvu kule kwao Butiama lilojengwa kwa nguvu na pesa za serikali na siyo mkopo kama Mkapa.Nani mtakatifu zaidi hapo aliyekopa au aliyetumia hela za serikali kujenga nyumba yake?
ReplyDeleteWako watu wengi tu mlizaliwa porini kabisa vijijini mkiwa hata ndala hamna sasa hivi mnaendesha magari baada ya kupata ajira na baada ya kustaafu hamtakuwa vile mlivyoingia.Mliingia kwenye ajira maskini mtatoka matajiri.
Suala la kuwa Mkapa aliingia mchovu na sasa hayuko vile is nonsense! Wabunge,mawaziri,wakuu wa mikoa,wa wilaya n.k wote wako hivyo huingia wachovu hutoka wako fit.
Please it is time to stop cheap politics.Tanzanians let us be real!
Anony...June 5, 4:01 AM EAT acha fitina. Kwani ukikopa hela benki ni lazima kila mtu ajue? Sheria gani inamkata raisi kukopa? Suala la rada tulishasikia kwamba serikali ya UK inafanya uchunguzi kuona kama kuna chembe ya rushwa. Ikibainika bila shaka wahusika watajulikana, iwe rais mstaafu au yeyote yule. Je unataka Mkapa aseme nini? Kwa mfano akisema hakuna rushwa ktk ununuzi wa rada au ndege ya raisi. Je kauli hiyo itakuwa imeondoa duku duku lako? au ni majungu tu kama ilivyo kwa bongo wengi?
ReplyDeleteWabongo blah kibao!
ReplyDeleteSasa wewe unadhani mtu akigombea urais anakwenda pale Ikulu kutangaz DINI? Hakuna mtu anakwenda pale kutangza Dini au kujipatia umaarufu, ila ni kuweka maisha yake vema. Sasa wewe Anon 4.01 hapo juu umeweka longo longo lefu na halina mpango juu ya tuhuma za Mkapa!
Hivi wewe ulitegemea nini? Kwamba Mkapa ataoke pale hohehae? Nini matarajio yako?
Mkapa kafanya vitu vizuri tu na sisi watanzania tunajivunia kwa sana. Mwache afanya biashara na kuchukua mkopo atakavyo. Wewe nani amekukataza kuchukua mkopo? Nenda sasa hivi mikopo kibao na iko mingi sana sana. Ni wewe tu.
Usilielie bila sababu. Changamka. Changamka sana sana maisha yanakwenda na yatakuacha bureee!
I think all this fuss about Mkapa taking a loan while in office is kind of funny. First of all, any Tanzanian is qualified to apply for a loan , if they meet the requirements, they are able to receive one. You do not have to be a president to get a loan. Many civil servants including salaried workers receive loans, and many banks and institutions actively market their products to civil servants, the president is a civil servant and he like any other is entitled to a loan.
ReplyDeleteWhat would have happened if Mkapa had stolen the money to purchase, the neighboring residence? I think his actions were very transparent and legal, hajafanya kosa lolote. That he decided to register a company is quite logical, the loan amount was big and it makes sense, especially when you purchase valuable property.
The previous owner of the neighboring property probably decided to give the Mkapa's the first offer when he decided to sell it, Rais angelipa in cash , then we would be asking where did he get that money? Kwamba ameweza kukarabati nyumba na kujenga nyingine , is absolutely possible with loans.
Claire short alishatoa ufafanuuzi kuhusu rada. Mkapa alirithi hilo swala kutoka kwa awamu ya mwinyi. Alichofanya yeye ni kuweza kuokoa millions of dollars, by stopping the deal, kwa hiyo sasa we have a aradar system that uses obsolete technology and does not cover the entire country. Ila nashindwa kuelewa kwanini Mkapa alitetea saaaana rada wakati wa utawala wake. It seems to me that many of the uncontroversial deals were done under mwinyi.
Ila sasa wote, Mkapa na kikwete walikuwa cabinet members and every major contract goes through the cabinet. Which means they both had knowledge of phoney contracts, but we do not know if they supported them , afterall cabinet meetings are secretive.
Coverstory
ReplyDeleteTanzania
“There is hope for Africa“
President Jakaya Mrisho Kikwete, the fourth president of Tanzania, came to power on 21 December 2005. In this wide-ranging interview, he tells our editor, Baffour Ankomah, what his government has achieved in 15 months in office, how the country is marching boldly on to greatness, and how the future of Africa is very promising. “There is hope for Africa. I am optimistic,” he says.
Baffour: In July, the African Union summit in Ghana is going to discuss a union government for Africa. Looking at the complexities on the ground today, do you think Africa will ever have a union government in a continent of 53 disparate countries?
President Kikwete: I believe Africa will have one government some day, but I cannot say when with certainty. Let’s see how the discussions in Ghana go. Certainly this is the dream that the founding fathers had for the OAU, that ultimately there is going to be African unity and this unity is symbolised by one African government. The issue has been how do we get there? The whole transformation of the OAU to the AU is to give greater focus to this trail.
Again, just like the debate on the East African Federation, we may come to a point where we will have to get a roadmap. Of course, while some countries think we can have a map, some think we need time. However, some time in the future, we will have to do as we did in East Africa – have a team of people come up with concrete proposals and targets that are time bound, and then we can discuss these targets and start a process of moving towards the implementation of those targets. I am confident that some day Africa will have one government and that government is desirable. The sooner the better.
Hmmm! Stephen Benjamin Mkapa...It is funny because Mkapa is your dad and you're afraid of so many scandals during his era including Net Group, Purchase od Radar and president's jet, minerals contracts and now doing business in Ikulu while he was still a president.
ReplyDeleteYeah! Jamaa ana hoja ya kujibu muda mrefu yatamkuta kama ya Chiluba ya kuonekana kujinufaisha kwa mabilioni ya pesa alipokuwa Ikulu na likitokea hili mtalia kilio cha mbwa midomo juu! Kama likuwa anajua anataka kuwa mfanya biashara kwa nini aliamua kuwa Rais wa Tanzania?
Chiluba of Bongo, soon this case will be in the court of law and all his bank accounts in Tanzania as well as foreign countries will be audited. How come you became a billionaire in 10 years? What type of business could make someone a billionaire in 10 years? Watanzania wengi wangependa wajue biashara hiyo ili nao waichangamkie. Mkapa tumbo kumoto...awamu ya uwazi na ukweli...ha ha ha vichekesho kweli kweli!!!!
ReplyDeleteNasikitika kwa comments za Stephen eti kila mtanzania ana haki ya kupata mkopo, hiyo ndio hoja yake. Anashindwa kuelewa kwamba Rais kwa nafasi yake ni tofauti na watanzania wengine hasa linapokuja suala la nani apewe kipaumbele. Jiulize swali dogo tu wewe na Mh. Rais muombe mkopo bank nani atakuwa wa kwanza kuupata hata kama wote mna sifa sawa za kukopa! Haihitaji kuwa na degree kutambua matumizi mabaya ya ofisi wanayofanya viongozi wetu. Yote haya ni matokeo ya kuua azimio la arusha, hakuna maadili ya viongozi tena. Kila mtu anatafutia tumbo lake kwa gharama yoyote ile. Kazi kwako Stephen u have to be an organized analyst usiende kwa mazoea tu!
ReplyDeleteACTIONS MATTERS THAN WORDS.WE ARE TIRED OF HIS WORDS,WILL NEVER WASTE MY TIME TO BUY THAT MAGAZINE.
ReplyDeleteWadau lioko marekani naomba mnisaidie ni duka gani naweza kupata hili gazeti ningependa sana kulisoma hili niweze kujua ni vitu gani vinamfanya huyu bwana awe optimistic but more importantly what his adminstrarion has achieved so far to make him feel that way .
ReplyDeleteI went to Barnes and Nobles but i couldn't find that magazine.
NAsikia Rais wetu alikuwa anarudi kufanya supp(Supplementary) ya mitihani yake kila mwaka pale UDSM.
ReplyDeleteMnaomfahamu nithibitishieni
HAYA MALALAMIKO YOOOOTE, ETI MKAPA KATUMIA FEDHA VIBAYA ALIPOKUWA RASI, ETI JK NAYE ANACHANA TU FEDHA ZA UMMA HUKO IKULU AU;
ReplyDeleteETI MWINYI NA NYERERE NAO WALINUFAIKA WALIPOKUWA MARAIS NA MAMBO MENGINE KIBAO NI KUPOTEZA MUDA TU.
SI MARAIS TU WANAOTANUA NA FEDHA ZA WALALAHOI HAPA BONGO. VIBOSILE WA MAKAMPUNI YOTE BONGO NAO WANA TABIA HIYO.
IWE KWENYE SOKA (TFF), KWENYE KLABU ZA MPIRA, KWENYE TAASISI YOYOTE ILE, WATU WANALAMBA SANA FEDHA ZA WANANCHI.
NA PENGINE HATA WEWE MLALAMIKAJI KAMA SIYO WEWE MWENYEWE, BASI ATAKUA MMOJA KATI YA MZAZI WAKO ANAJINUFAISHA NA JASHO LA WALALAHOI.
HATA KAMA UNGEKUWA WEWE MWENYEWE UPO KWENYE USUKANI, LAZIMA UTAKE USITAKE UNGEITUMIA NAFASI HIYO TENA KWA VIABAYA MNOOOOO.
TUSIKAE KULALAMA NA KUTAKA KUMTIA MICHUZI MASHAKANI KWA KUTUMIA BLOG YAKE KUWATUKANA AU KUWALAUMU VIONGOZI KWA KISINGIZO CHA "MSEMA KWELI" WAKATI MNASHINDWA KUJITOKEZA HADHARANI NA KUTOA DUKUDUKU LENU.
WEWE MLALAMIKA UNA MBUNGE WAKO ANAYEHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE. MPE HAYO MAONI YAKO ATAYAFIKISHA KATIKA NGAZI HIYO AMBAYO INA UWEZO WA KUMSHTAKI MTU YEYOTE AU KUTOA MARI YA KUTAKA ASHTAKIWE.
WOTE TUNAFAHAMU KATIBA YA NCHI INASEMA HAKUNA MTU ALIYE JUU YA SHERIA NA KUFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA KATIBA YA NCHI.
MIMI NINGEPENDA KUMSHTUA MICHUZI AWE MAKINI SANA NA HAYA MALALAMIKO YASIYO NA MPANGO YANAWEZA KUMTIA MASHAKANI NA KUONEKANA ANAFANYA FITINA DHIDI YA JK AU BM.
NI MWAKA JANA TU KUNA BLOGGER MMOJA HUKO MISRI ALIPOJIKUTA AKIENDA JELA KWA KILE KINACHODAIWA KUCHOCHEA NA KUIKASHIFU SERIKALI YA HOSSAIN MOBARAK.
KUMBUKA KWAMBA HAWA NI VIONGOZI WA SERIKALI. WANASOMA YOTE HAYA YAANDIKWAYO HUMU NA KUANGALIA KAMA KUNA UKIUKWAJI WA SHERIA YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.
MIMI WALA SIMTISHI MICHUZI LAKINI SUALA LA KUKASHIFU, KUTUKANA NA KUDHIHAKI VIONGOZI, LINAWEZA KUMTIA MATATANI JAMAA NA KUJIKUTA AKIENDA LUPANGO HUKU WALIOANDIKA WAKILA RAHA NJE...SHAURI YENU
We mshamba hapo juu unayemkomalia Stephen, mikopo kila mtu ana access nayo. Wewe kama una uraia wa woga kwa kuamini kuwa ukipanga foleni na Rais nani atapata kwanza, shauri yako! Hakuna cha wa kwanza wala wa mwisho. Wewe changamka, mikopo iko kibao.
ReplyDeleteLabda tatizo lililopoa kwa wabongo wengi ni kwamba hawajui mikopo ni nini na wala hawana idea kwamba wakikopa watatumiaje. Uliza tu. Usiwe na wasi wasi. Nchi hi ni yako na kila mtu anaweza kopa. Usisinzie. Changamka na acha woga kwamba ukipanga foleni na Rais wewe utakuwa wa mwisho kupata mkopo. Hakuna mashindano. Mikopo iko nje nje. Lakini tu kama una akili ya kutumia.
Jamaa hapo juu usipoteze kupigiana kelele na stephen Mkapa, jamaa wamedata hao, yeye anachojua ni sketi na larger.
ReplyDeleteHivi wewe anonymous ulieandika habari ya Ridhwan inahusu nini??????? Watu bwana ili mradi tu uandike. Unachekesha lol next time andika kitu kinacho husiana na mjadala.
ReplyDeletemimi, namsupport anon wa jun 5..., kinachonishangaza zaidi, ni katika mining/madini,
ReplyDeleteiweje na itakuwa vipi... Tanzania wapate royalty kutoka kwa investors only 3% only 3% how com is this logic???
where is 97% ????
we have to understand royalty ni part ya profit, hii inamaana tayari imesha dedactiwa expenditure..
kama expenditure bado haija deductiwa , solution nzuri ni ku deduct expenditure and then the profit should be distributed between the government and th investors...
SUPRISINGLY ONLY 3% GOES TO THE GOVERNMENT, UKIULIZA UTAAMBIWA KUWA TUNAOGOPA KUWA INVESTORS WATAHAMA... JEE HATUONI KUWA KUWA MADINI YA TANZNIA TUNAYAGAWA...
WHAT IS THE FUTURE OF TANZANIA...
WHAT IS THE FUTURE GENERARTION OF TANZANIA... NI KUBAKI NA MASHIMO...
MIMI NINAONA KUNA UMUHIMU WA MIKATABA YA MADINI KUPITIWA NA KUNA UMUHIMU WA KURISE ROYALTY...
KAMA HAIWEZEKANI NI BORA KUSTOPISHA KUGAWA MADIN... KWANI SIKU ZA MBELE YATAPANDA THAMANI
KUNA UMUHIMU KWA SERIKALI KUIMARISHA KILIMO
WEWE ANON WA JUN, 5:55 WACHA MAMBO YA KIKHANISI, WENZANKO WANaKUTAFUNA? HIZI NI ENZI ZA UKWELI NA UWAZI! WANAKUKANYAGA WENZAKO
ReplyDeletekwa taarifa yako we unaesema kikwete alikua anarudi kufanya supp hujui chuo kikuu wewe, magenious wote lazima msapishwe nenda kaulize wanafunzi wa sheria na sociology walimu gan wanasifika kwa kutoa masupp mpaka 150 wanajulikana kabisa wao mabigwa wa kutoa supp
ReplyDeleteMimi ninachowaambia hawa viongozi wapenda hela na kujitajirisha wenyewe kuwa kuna kufa…Utawanyonya walala hoi utakavyo lakini huendi na hata hiyo ndururu ukifa.
ReplyDeleteNa haka kanchi ketu life expectancy yake ni 45 yrs na ukiongeza nachozi ya walala hoi hamtalala usiku ng’o…. macho yatakuwa wazi tuu sijui hiyo miaka utaifikisha vipi. Wakati walala hoi wao wanalala na kuota ndoto nyie mtakua mnawanga usiku mzima na kuwaza wapi tena pa kunyonya.
nchi nyingine kuwa kiongozi ni pride
Here are their contacts:
ReplyDeletecontactseditorial@africasia.com
Advertisement:
advertising@africasia.com
Headquarters:
7 Coldbath Square
EC1R 4LQ
London
T: +44 (0)20 7713 7711
Fax Admin: + 44 (0)20 7713 7898
Fax Editorial: + 44 (0)20 7713 7970
Subscriptions: Email: subscriptions@africasia.com
T: +44 (0) 1858 438 792
F: +44 (0) 1858 461 739
USA:
World Media
Conover Brown
Ph: 212-244-5610
E-mail:conoverbrown@worldmediaonline.com
Try this link:
ReplyDeletehttp://www.africasia.com/newafrican/na.php?ID=1332
"Wadau lioko marekani naomba mnisaidie ni duka gani naweza kupata hili gazeti"
ReplyDeleteBarnes and noble has the magazine. If you are in New York nenda Barnes and Noble Union square 14th street. They usually have very few copies in stock. I read this issue three weeks ago and so I would think they have a new issue for this month. But try.
Matumizi mabaya ya madaraka na ofisi ndio mambo yanayoiua nchi yetu. Kingine ni uwezo mdogo wa wananchi kuchambua mambo bila kufikiri kwa mapana. Haiwezekani mwanachi wa kawaida akaamini ana fursa sawa na Rais ingawa Rais! Tukatae tukubali nchi yetu tunaimaliza wenyewe kwa sababu ya ubinafsi wetu na uvivu wa kufikiri wa baadhi ya wananchi. Pole Tanzania, kila mkuu wa nchi akiwa mjasiriamali by 2040 nadhani nchi itauzwa yote kwa wageni.
ReplyDeleteWewe unayesema blogger alikamatwa Misri na kushughulikiwa kaulize kilichompata Raisi wa Misri.Ile kesi ilimpeleka pabaya hana hamu na blogs na wanablog tena na hazigusi.
ReplyDeleteWewe ni mwoga na mjinga unafikiri watanzania bado ni kizazi kile cha waoga waliokuwa wakitishwa na maafisa usalama wa mataifa cha akina Nyerere wakati wa ubabe wa mkomunisti Nyerere.