ridhiwani jakaya mrisho kikwete leo asubuhi amechukua fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa mkoa wa pwani katika mkutano mkuu wa taifa wa ccm mjini bagamoyo, na siyo sumbawanga ambako baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba anakwenda huko kuchukua fomu kugombea ujumbe wa halmashauri kuu ama nec. ridhiwani, ambaye kawasili bongo jana, anamalizia masomo yake ukerewe. picha juu inamuonesha ridhiwani na nduguze wakiwasili ofisi za ccm za wilaya ya bagamoyo leo asubuhi na chini akipokea fomu toka kwa katibu wa ccm wilaya ya bagamoyo bi. yasmin.
habari kamili soma daily news ama habari leo kupitia www.dailynews-tsn.com baada ya saa sita na dakika moja saa za afrika mashariki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 69 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2007

    haya bwana yangu macho tu...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2007

    sijui na mimi pangu pakavu nikitaka nitapewa?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2007

    SIYE TUNAUNGUA JUA, NAMBARI ONE.... NAMBARI ONE.... NAMBARI WANI

    WATU WAKITOKA UKEREWA DIRECT WANACHUKUWA FORM

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2007

    Ngoja na miye nirudi mapema. Hivi hizo form zinaisha lini kutolewa...Naona ulaji ni CCM....jaman recent graduate changamkeni ...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2007

    hmmmmmmm.....political dynasties in the making??/JK u need to do some serious work for the nation before working on your dynasty.Ari mpya and all that, vimeishia wapi? Umeme hamna[basi hatusemi tena] maji mhhh!! Usafiri ndio kafiri kabisa kuanzia petroli mpaka minyororo[hata solution ya mwenzako ya njia tatu doesnt work]
    samahanini kwa kutoka nje ya topic lakini vinakera sa ingine.
    For the young man: hope you know what you're getting into , if so good luck and DO THE RIGHT THING!Always

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2007

    kuchukua fomu ni rahisi je kutekeleza???Muulizeni JK

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2007

    Gari ameshuka nalo hilo au gari ya baba hiyo????...

    MWEE WATOTO WA BABA WANARAHA NDIO MAANA WAKIMALIZA SHULE WANARUDI MAPEMA TU BONGO

    Siye tuhangaike kukusanya vihela tuweke MOT halafu tena mpaka tukalifanyie hiyo gari PRE- INSPECTION

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2007

    Jamani atafanyaje hiyo kazi kwa vile kisheria yeye anahitaji kuwa na bodyguard kwa vile ajili ya kazi ya baba yake. Ina maana akisafiri kikazi na mabody guard wake watalipiwa na hela ya walala hoi....

    Au mimi sielewi how this works

    Naomba mnieleweshe

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2007

    Wote meongea pumba tupu mtu mwenye akili huwezi kuuliza gari la bab yake au lake mbona gari kitu kidogo tu, na hakuna anayezuiwa kuchukua fomu za kugombea ili mradi utimize masharti. Mwacheni dogo asonge mbele we need to stop talking rubish and focus nyie watu mtanzania akifanya kitu basi hakuna support yoyote utatukanwa utasemwa vibaya kulalamika tu kama kazi. kama mnaona mambo hayaendi sawasawa basi tumieni uhuru wenu wa kikatiba sio maneno maneno mtoto wa muhunzi anakuwa mhunzi, dereva dereva, mbeba boksi ulaya na watotot huko huko watarithi. tubadilike jamani tuone mbali. msifikirie kulithishwa tu hakuna mtu anaeymzuia mtoto wake akiamua kufuata nyayo zake kufanya hivyo ni uamuzi binafsi. Keep it up Riz

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2007

    Hivi yule mzee wa Utandawazi alikuwa hana watoto nini, mbona wao hawakuchuaga au walichukua haikutangazwa jamani, aya bwana maji hufuata mkono na viongozi huandaliwa kama wewe baba yako hajakuandaa basi usifirie hata siku moja kuja tawala nchi. Kingship. Halafu JK bado ana nafasi kama mbili au tatu hivi za kuteua wabunge, naona anamuandaa dogo amkabidhi moja sasa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2007

    Bro Michu hao vigogo na watoto wao wanatuyeyusha tukianzia kwa wakina ipi,kinje na huyo dogo hapo,wao wanaona siasa ni mchezo wakujificha au kidali po,angalieni amini anafanya nini zaidi ya kuuza papa,lakini poa mshikaji wetu kapona babkubwa sasa tusubiri ya huyo bwa mdogo

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2007

    mbona mnalalamika sana nani aliwatuma baba zenu wakimbie umande,wakati baba zetu wanaenda shule nyie baba zenu walikuwa wanaendeleza ugoni sio basi ndio matunda yake na nyinyi mkibaki kulalamika hivyo watoto wenu watakuwa kama nyie sorry to be a pain.mnaona juzi violet mzindakaya amechukua form leo ridhiwani kesho it might be bob lowassa na nyie mkae msubiri mtaletewa kwenye mail box zenu hizo form.wazazi wawengine wanafikiria mbele.sina mengi mkitaka kunitukana tukaneni sijali

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2007

    Kuwa kiongozi nchi zingine ni pride.

    Na ukiwa kiongozi mzuri hata ukimaliza muda wako jina lako linakumbukwa milele.


    Sitaki kutaja majina lakini kuna viongozi wamesha anchia ngazi lakini hata jina halikumbukiwi. Pamoja na kuwapa majina katika kila mtaa, na sehemu nyinginezo lakini wapi. Watabakia kwenye vitabu vya historia tu na shule zenyewe ndio hizo haziendekei sijui nani atawakumbuka...

    Kwa mtindo huu watasahaulika wengi

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 06, 2007

    tatizo hapa ni kwamba watu hawana imani na watawala,hawaonyeshi kuwa wapo kututumikia. ... nadhani kama angechukua form za chama cha upinzani isingekuwa nongwa ,tena labda angesifiwa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 06, 2007

    Hii inaonyesha wazi jinsi serikali yetu ilivyojaa wasanii. Kilamtu anaona anaweza kuongoza. Matokeo yake ndio kama haya hata ripoti zinaandikwa kisanii sanii tu. Safi sana Kigoda kwa kuikataa. Enzi za Mkapa ukiambiwa uchumi umekuwa 6% inakuwa hivyo kweli. Sio sasa usanii tu umezidi.

    MPs reject economic review
    JIANG ALIPO
    Daily News; Tuesday,June 05, 2007 @00:02

    THE Parliamentary Standing Committee on Finance and Economic Affairs yesterday rejected the report on the State of the National Economy for 2006.

    Committee chairman Dr Abdallah Kigoda also rejected projections for fiscal 2007/08 and 2009/10 presented by the Minister for Planning, Economy and Empowerment, Dr Juma Ngasongwa.

    Dr Kigoda asked the minister, after a day’s deliberations to improve the report, saying it contained sweeping statements which were not validated.

    “We ask you to go and work on this report again and improve on the noted parts then we will arrange another meeting with you and the Ministry of Finance,” said Dr Kigoda.

    The committee rejected all paragraphs on efforts to reduce poverty under the 2006 National Strategy for Growth and Reduction of Poverty Status Report (commonly known as MKUKUTA).

    “We want a detailed and comprehensive status report. We are not satisfied with these three paragraphs. These three paragraphs have to be re-written,” explained Dr Kigoda.

    One of the paragraphs read in part as: “The government continued directing plenty of resources in sectors that stimulate economic growth, thus reducing income poverty.”

    It mentioned those sectors as agriculture, infrastructure, education, health and water supply.

    Earlier, Dr Ngasongwa said the government had identified five priority areas for 2007/08 and 2009/10 as part of the implementation of the MKUKUTA programme.

    “Areas identified are investment in infrastructure, agriculture development, human resource development, improvement of social services and implementation of the second phase of the improvement and liberalisation of the financial sector,” said Dr Ngasongwa.

    Even that, Dr Kigoda said, lacked progressive report, which should show how future projections reflected last year’s implementation of the programme. Dr Kigoda held the planning portfolio before.

    Dr Kigoda also asked the ministry to give a comprehensive report on the National Insurance Corporation (NIC) saying, “This committee last year rejected NIC assets evaluation, so we want a thorough report on it.”

    Dr Ngasongwa was asked not to respond to the observations by the committee as the chairperson, Dr Kigoda, said that the ministry had to work on the report first before another meeting between the committee, the ministry and the Ministry of Finance.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 06, 2007

    CCM kimekuwa chama cha machifu, Viongozi wanahakikisha kwamba warithi wa nafasi zao ni watoto wao, hivyo wanaanza kuwaandaa mapema. Kama baba yako ni kapuku asiye na jina sahau kupata uongozi ndani ya CCM.

    Ukienda kuchukua form utaulizwa Baba yako jina lake nani, alikuwa na cheo gani ndani ya CCM? kama alikuwa ni "kapuku mpiga debe" ndani ya CCM basi wee URIEEEE TU! Ama kweli bongo inaliwa na wenye meno. Wamegundua kwamba makulaji yote yako CCM hawataki kuingia kwenye nyanja zozote zile bali uanasiasa tu!!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 06, 2007

    mtaumiza kichwa bure kumjadili huyu dogo kila mtu anajua siku zote maji yanafuata mkondo na hayapandi mlima hata siku moja, kwa hiyo si tulio mlimani tutakuwa tunayaangalia tu
    michuzi mwaga picha za maana hakuna tukio lolote huko bongo

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 06, 2007

    Na mimi mwenzenu leo nimeamua kuomba kadi ya CCM usikose makala yangu kwenye Tanzania Daima...

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 06, 2007

    sisi ngoja tukatafute pesa tukazamie kwenye meli za kwenda ulaya na South Africa maana hapa nimeishaona hakuna dili ni nchi za kisiasa tu.

    Watu wenye ethecx na hatutaki kuwa watu wa hira hatuwezi ishi nchi hii. Ngoja tutafute panapotufaa tuache nambari wanu na mabao ya visigino.

    Naona marais wote mpaka mwaka 3,000 wameisha jipanga.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 06, 2007

    Aah!niseme nini sasa.kila la heri bwana,ilimradi kuwe na usawa katika hizo kura.Halafu dogo angalia, si unakumbuka yaliyomkuta ndg yetu,rafiki Marehemu Ipyana?

    ReplyDelete
  21. haya dogo kanyaga twende!!....sio siri mwana wa nyoka nyoka...mie hata umonita sijawahi ushika...nitaweza wapi nadhani ni kutokana na baba hata balozi wa nyumba 10,10 sijawahi muona akigombea...so wenye uwezo wao wacha waendeleze libeneke...

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 06, 2007

    jamani huyo nyuma ya ridhiwani ,pembeni ya huyo mama sio HASSAN huyo!!!!!!!!!!!!rafiki yake mkubwa ridhiwani....mbona umekonda kaka?hadi sura!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 06, 2007

    JAMANI MIMI NATAFUTA KWENDA KUISHI NA KUFANYA KAZI NG'AMBO HUSUSANI USA, UK, GERMANY, JAPAN, AUSTRALIA, NORWAY NA NEW ZEALAND. MTANZANIA MWENZANGU ANAYEWEZA KUNISAIDIA kivyovyote KWA HILO NAOMBA AWASILIANE NAMI KWA KUWEKA e-mail address yake hapa kwa Michuzi nami nitacheck naye. Asanteni. Asante pia Bw. Michuzi samahani kwa kutochangia mada hapo juu.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 06, 2007

    NAOMBA NIULISE ILE PICHA YA MIPAJA IPO WAPI???

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 06, 2007

    SAWA WACHA WATOTO WENU WACHUKUWE FORM

    YULE MWANA MUZIKI PAMOJA NA WATOTO WAKE WALIOFUNGWA MILELE ?

    LINI WATAPEWA MSAMAHA, NAONA KUWA INATOSHA..........

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 06, 2007

    Hakiyanani Baba wa Taifa Nyerere yuko mbinguni

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 06, 2007

    Unasema kweli Nyerere yuko mbinguni

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 06, 2007

    HIVI WATANZANIA TUNAKWENDA TUNAPOANGALIA AU TUNAANGALIA TUNAPOKWENDA???????

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 06, 2007

    Balali ni mtaalamu au mwanasiasa?

    Chris Alan


    KUELEKEA mwishoni mwa miaka ya 80, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, alijikuta katika mvutano mkali na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Makerere. Hoja iliyokuwako kama ilivyo ada ya taasisi za huduma za kijamii katika bara la Afrika, ilikuwa maslahi duni ya wahadhiri hao.
    Kilichotokea, kilikuwa ni watawala, yaani serikali, kushindwa kuthamini mchango wa chuo hicho kwa ustawi wa taifa la Uganda kiasi cha kuachwa kama kimetelekezwa hivi. Katika mijadala ya kujaribu kurejesha hadhi ya chuo hicho maarufu duniani, na hasa Afrika Mashariki, kikiwa ndicho chuo kikuu kikongwe kilichozalisha wasomi katika ukanda huu tangu na hata baada ya uhuru wa nchi za Afrika Mashariki, Museveni na wahadhiri walifikia hatua ya kushindwa kuelewana.

    Ikumbukwe kwamba, Museveni aliingia madarakani nchini Uganda mwaka 1986 kwa njia ya mtutu. Pia ikumbukwe kwamba, kwa takribani miaka 15 tangu 1971, Idi Amin alipotwaa madaraka kwa kumpindua Milton Obote, taifa hilo liliishi katika msukosuko mkubwa mno.

    Hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba, Museveni aliyekuwa ni rais msomi akiwa amehitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyekuwa wakiishi chumba kimoja na mwasiasa mkongwe wa Tanzania ambaye alikuwa waziri katika awamu tatu za utawala wa nchi hii, Jackson Makwetta, hakuweza kuwafurahisha wasomi wa Makerere.

    Habari zinasema katika mojawapo ya majadiliano makali, Museveni alielezwa yafuatayo: ‘Any rebel from the bush can become a president, but not any rebel from the bush can become a lecturer’. Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba: Kila muasi kutoka msituni anaweza kuwa rais, lakini si kila muasi kutoka msituni anaweza kuwa muhadhiri. Kauli hii ilimuudhi Museveni.

    Ujumbe aliokuwa akipewa Rais Museveni wakati huo ni kwamba, zipo kazi ambazo watu hawazipati hivi hivi tu, si kwa kutumia nguvu au aina nyingine ya njama ila kwa kuvumilia kwa muda mrefu darasani, kupekua vitabu na kujenga uwezo wa kutenda kazi fulani. Kwa maneno mengine, ujumbe ulilenga kumweleza kwamba, kuwa rais ni mafanikio katika maisha, lakini hakika urais unaweza kumwangukia mtu yeyote ilhali kazi kama ya uhadhiri haina bahati, ni lazima kujituma na kupekua vitabu na hivyo walioamua kupitia mkondo wa kazi hiyo, ni lazima waheshimiwe na kutuzwa.

    Hivi karibuni, nimekumbuka mfano huu baada ya kuangalia na kusoma mwenendo mzima wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Balali. Kila nikisoma majibu na maelezo yake anayotoa kwa umma, ninashindwa kusadiki kama huyu yuko kundi gani hasa. Hivi huyu ni yule wa kundi la awaye yeyote anaweza kupata nafasi hiyo au ni watu wenye taaluma fulani tu?

    Kinachoendelea ndani ya BoT ni kana kwamba wanatayarisha maelezo kwa ajili ya kuwafurahisha wanasiasa. Yaani Gavana ameamua kuwa mwanasiasa kuliko pengine alivyo Waziri wa Fedha.

    Kuna mlolongo wa mambo ambayo Balali ameyasimamia na kuyaeleza hadharani katika kipindi kisichozidi miezi mitatu iliyopita. Moja ni kule kujaribu kukanusha kitu kisichokanushika, kwamba serikali ilikuwa imetumia zaidi ya bajeti yake karibu shilingi trilioni moja (bilioni 978) ilipofika Februari, mwaka huu. Taarifa ya ufafanuzi ya matumizi ya serikali kuwa makubwa kiasi hicho ilikuwa ni kituko, hakuonyesha kwamba BoT imejipambanua vipi juu ya hisia na shinikizo za kisiasa. Zaidi sana alidhihirisha ni mtu wa kusukumwa na shinikizo tu, si mtaalamu, ni kada wa siasa.

    Lakini hata BoT hiyo hiyo ilipoficha taarifa ya matumzi ya serikali kwa mwezi Aprili, maelezo ya kujitetea yaliyotolewa kwa umma yalikuwa ni ya kushangaza kwa sababu, hayafanani na kuelekea kukaribia uzito wa taasisi hiyo nyeti ya kuratibu uchumi wa taifa. Eti taarifa ilichelewa ndiyo maana haikuwako kwenye ripoti yao.

    Sasa kinachonisukuma kuchambua mambo haya leo, ni ukweli kwamba takwimu za BoT zinazotolewa kila mwaka, hasa kuhusu mwelekeo wa uchumi, zinaacha maswali mengi kuliko majibu. Waziri wa Fedha, Zakia Meghji amekaririwa akisema kwamba, mfumuko wa bei uliokuwa umepanda kidogo hivi mwezi wa tatu na sasa umeshuka kutoka asilimia 7.2 hadi asilimia 6.1 mwezi Aprili.

    Tunajua kila wakati BoT imekuwa ikijivua wajibu wa takwimu hizi ikisingizia kwamba ni jukumu la Mamlaka ya Takwimu. Kama nitakuwa nimekosea sana, nitaomba kuelimishwa na pengine niombe radhi kabisa kungali mapema. Ninachokiona hapa ni kwamba, hata kama takwimu hizi zinatoka Takwimu kwa kuwa BoT wana wataalamu wao, wachumi waliobobea katika masuala ya uchumi, si ajabu wala jambo la kushangaza kama na wao wangejibidiisha kutafiti ili wajiridhishe kweli kwamba hizi takwimu za hali ya uchumi wanazoletewa kutoka Takwimu, zina usahihi wowote kulingana na hali halisi ya mambo mitaani.

    Ninasema haya kwa sababu wote walioko BoT au Takwimu si watu walioingia huko kwa bahati mbaya, kama wapo walioingia humo kwa bahati mbaya na si kwa vigezo vya sifa za kitaalamu, hapo si mahali pake, ndani ya taasisi hizi hakuna kupiga siasa, kama yuko awaye yeyote anayepiga siasa, tafadhali atafute chama cha siasa na aachane na taasisi hizi nyeti za kuratibu mwenendo wa uchumi wa taifa hili.

    Ukiangalia kwa makini sana takwimu hizi zinazoelezwa kwamba hali imekuwa nzuri zaidi kiuchumi kutokana na mfumuko wa bei kurudi chini, picha inayojengwa hapa ni kutaka kuonyesha kuwako kwa mafanikio ya kiuchumi nchini, ili wanasiasa wapate cha kujisifu kwamba wamefanya kazi. Lakini ukweli ni kinyume chake, hakuna mafanikio. Bei ya mafuta ya petroli kila kukicha inapaa na haiwezekani bidhaa hizi zipande bei halafu vitu vingine vyote vibakie pale pale.

    Hakuna kitu kimekuwa na nafuu ya bei katika siku za hivi karibuni, hata ile nyama ya ng’ombe (ambayo ilikuwa imedoda kutokana na hofu ya homa ya bonde la ufa – RVF), nayo imepaa ghafla. Ile bei ya kuku na samaki iliyokuwa imepaa kwa sababu ya RVF nayo imebakia huko huko juu hata baada ya watu kuanza kula nyama.

    Kwa maana hiyo, kusema kwamba eti Aprili mfumuko wa bei ulishuka kwa asilimia 1.1, ni jambo gumu kidogo kuingia katika akili ya kawaida kwa sababu hakuna nafuu ya maisha inayomfikia mwanachi moja kwa moja.

    Kila wakati nimekuwa nikirejea mfano huu unaoweza kuonekana kama wa kitoto, lakini pengine ndio ukweli halisi kuhusu uchumi. Ukichukua sh 100,000 sasa hivi kwa mkazi wa Dar es Salaam ukaenda kununua vyakula sokoni Kariakoo ambalo ni kati ya masoko yanayouza vitu kwa bei nafuu sana, hakika ukijaza kapu moja la wastani, ujue na sh 100,000 imeondoka.

    Hizi ni bidhaa kama karoti, nyanya, nyama, samaki, sukari, mchele, unga na mbogamboga nyingine pamoja na matunda; vyote vya kutosha wiki moja kwa familia ya watu watano. Hapa ninakuhakikishia hutarudi na fedha yoyote ya maana. Ukigusa na kuku wa kienyeji ambaye jogoo mmoja sasa ni zaidi ya sh 10,000, unaweza kuomba kukopeshwa kwani hiyo laki itakuwa imekwisha kuota mbawa.

    Kwa maneno mengine, BoT inapotoa takwimu zake za mfumuko wa bei au kama takwimu hizo zinatolewa na Mamlaka ya Takwimu, zinamsaidia nani hasa kama si wananchi wa kawaida?

    Nilifungua mjadala huu kwa kusema kwamba, Rais Museveni alielezwa kwamba muasi yeyote kutoka msituni anaweza kuwa rais, lakini si kila muasi anaweza kuwa muhadhiri wa chuo kikuu. Ni kwa maana hiyo hiyo ninashindwa kujua kama Balali anaisaidia BoT kuwa chombo kisichofungamana na siasa, au naye amekuwa sehemu ya siasa? Ninasema haya kwa sababu kila kukicha wabunge wanalia naye, kwamba anapotosha mambo, kwamba haonyeshi kuwa mtaalamu zaidi ila anaegemea kwenye siasa, kulikoni Balali?

    Hivi BoT ikiamua kusimama kwenye ukweli na kueleza hali halisi ya uchumi wetu ili nasi akina yakhe tujue ni kwa nini tukivunja mwekundu mmoja wa msimbazi (yaani noti ya sh 10,000) inakuwa kama imewashiwa moto, itakuwa imefanya kosa gani? Kwani nafasi ndani ya BoT siku hizi ni za kisiasa na si za kitaalamu tena, zimekuwa sawa na udiwani, ubunge au uwaziri. Kuna nini BoT?

    Kuna waasi wangapi wanaotaka kiti cha kisiasa, na kama wapo kwa nini wasitupishe hasa katika zama hizi ambazo jengo jipya la BoT linaashiria kwamba wakaao ndani yake si watu wa porojo ila watu weledi, waliojaliwa bongo na wasiosukumwa kwa shinikizo zozote za kisiasa kwa sababu wao ni wataalamu. Balali mbona hutaki kuliona hili? Unaogopa nini, kiti kimekuwa kikubwa kuliko uwezo wako au unalipa nini?

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 06, 2007

    Comprehensive reports kwa serekali are important. But tukiona numbers e.g uchumi umekuwa 6% tunaridhika zaidi au tunaamini zaidi kuna maendeleo? Tuliaambiwa shule enrollment ni X%, madarasa Y hundreds but quality ilikuwa si nzuri, hamna textbooks etc. Sa zingine tusiaamini statistics sana. Lets give the 'green' boy a chance, akivurunda, tutabaki kulalamika tuu. Tatizo is its like we never learn from past mistakes, we cover them up and make new ones!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 06, 2007

    we michuzi huna maana picha za watoto wa wakubwa mbiombio breaking news lakini picha za taifa stars vs senegal zimekushinda utafikiri hiyo game imechezwa mwezini, unatuletea picha za mazoezini nani anataka.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 06, 2007

    MICHU NAWE KWA KUJIKOMBA! SASA HIYO NAYO NI BREAKINGNEWZ UNAONA. MI NIKAJUA SIJUI NINI. BASI WOTE WALIOCHUKUA FORM WAWEKE BREAKING NEWZ. TUMIA VIZURI BLOG YAKO. TUTAKUCHOKA SASA.
    RIDHI NAONA KIDUME UNAYOYOMA SASA KWENYE SIASA, SAFI NI MWELEKEO MMOJAWAPO WA MAISHA. SHULE HUKO UNASOMA KWELI? UKIFANYA MCHEZO UTAONDOKA NA GPA MBOVU KAMA ULIYOONDOKA NAYO UDSM. VIMWANA ACHANA NAVYO VITAKUMALIZA KUNA UKIMWI WE MWENYEWE WAJUA.AU NIMWAGE MTAMA KWENYE KUKU WENGI?

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 06, 2007

    Wanablogu tafadhalini pitieni hii habari kama inavyopatikana kweneye http://kumekucha.blogspot.com/2007/03/top-kenyan-journalist-in-date-rape.html

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 06, 2007

    Nyie wote mlitoa maoni katika kulaumu Ridhwan kugombea ujumbe wa ccm tu! inalekea mpo zero katika siasa!Mbona hamshangai George Bush Kuwa Rais wa Marekani kama alivyo baba yake mnashangaa Ridhwat Kikwete!
    Nchi nyingi duniani tena za kidemokrasi viongozi kibaa wanatoakna na kidamifiilia za Kisiasa,Inndia.Nehru binti yake Indira Ghandhi Rajiv Ghandi binti sasa mbunge ,pakistan-Bhuto,Indonesia Sukarnos,nk nk
    Acheni chuki leteni hoja za akili

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 06, 2007

    Si jambo geni hili kutokea hapa kwetu na hata duniani. Mheshimiwa Rais Aman Karume naye ni mtoto wa muasisi na Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Adam Kighoma Malima naye ni mtoto wa aliyekuwa waziri nyadhifa mbali mbali, naye Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere mtoto wa Mwalimu JK Nyerere. Takriban wote watajwa hapo juu wemejitahidi kaisi chao katika uwanja wa siasa hapo nchini na yote kupitia "umaarufu" wa wazazi wao. Kamwe haitotokea historia kujirudia eti Bwana Makongoro Nyerere kuwa ama hata kumkaribia Marehemu Mwalimu JK Nyerere kwa lolote lile!!! Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa Ridhiwani, maana Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja tuu!!! Hivyo mikiki yote ya kujiingiza kwenye siasa bado haitamfanya awe kama JM Kikwete, na wala yeye sio kigezo cha JM Kikwete. Hivyo wapiga kura wote wa CCM hili lazima liwe ndiyo dira ya kuwapima hao mnaowachagua. (aDk)

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 06, 2007

    Usulutani umeanza sasa Tanzania. Kule Visiwani nasikia nako Dk, Hussein Mwinyi nae anaandaliwa kuwa Raisi katika awamu ijayo.
    Haya. Yetu macho!

    ReplyDelete
  37. Hongera sana Comrade,
    tatizo la watanzania wengi ni kukosa ila tabia ya "KUTHUBUTU" na hiki ndicho kitatugharimu hata katika shirikisho lijalo la africa Mashariki.

    Mwenzetu huyu nafanya kile nafsi yake inamtuma akiamini kua uwezo na nia anayo kwahiyo sidhani kama kuna dhambi katika hilo.

    Nakutakia mafanikio comrade na changamoto iliyoko mbele yako ni kuongeza umakini na ufanisi katika utendaji wako ili wale walio na mawazo potofu dhidi yako wakose la kusema..Mimi naamini unaweza kwani Ari,nguvu na Kasi pia unayo..

    Michuzi mpe salamu huyo comrade mwambie sie tumejichimbia huku kisiwani tukitafakari jinsi ya kutoka na kuunga mkono jitihada zozote za kimaendeleo zinazofanywa na vijana wenzetu....

    Msalimu pia huyo mpiganaji hapo kando bwaba Hassan Mwamweta mwambie aongoze mpambano vyema ili nia ifanikiwe.....

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 06, 2007

    Guys stop crying.... Bwana mdogo amechukua umri unamruhusu pia Elimu anayo, sasa wabongo mnapiga kelele mwenzenu huyu kachukua fomu pia atashinda tu....

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 06, 2007

    JAMA EH! YAMESEMWA MENGI SANA HUKO JUU, BILA UPENDELEO WA HALI YOYOTE NI HIVI, KWANZA KUCHUKUA FORMU NI HAKI YA KILA MMOJA WETU, SEMA NYADHIFA YA MZEE WAKE ITAMFANYA ALAMBE DUME! USIFIKIRI MIMI NA WEWE ETI TUKACHUKUE FOMU TUPATE,NG'O HATA KIDOGO, TENA SIJAWAI ONA MTOTO WA CHIFU, AU MANGI AU RAIS ANA MPINZANI AFU APIGWE CHINI NA MPINZANI KAMA YUPO NIPENI MFANO, PILI KWA KWELI ARI MPAYA, NGUVU MPYA,...VITATUTOKEA PUANI, LAITI NYERERE ANGEKUWA HAI...WE ACHA TU, ALOMKUMBUKA NYERERE APO JUU KANIFURAHISHA SANA, SIJUI ANONA HAYA! ANAWEZA KUMDANGANYA BWANA GOD AMPE CHANSI YA KUSHUKA ULIMWENGUNI KWA SIKU KADHAA AIONE IKULU YA LEO ILIVYO, KAZI YETU WALALA HOI KUIMBA TU KASI MPYA, ARI MPYA....TUTAIMBA SANA! FIKIRI TU KWANZA UNAVYONG'ATWA NA MBU UMEME UKIKATIKA, FIKIRI TU UNAVYOENDA MAILI KUSAKA MAJI .. MBONA WAKATI HUO HUSIFU MSEMO WA ARI MPYA......?????NIPENI JIBU WAZALENDO WENZANGU!

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 06, 2007

    NYIE MNAOTETEA HAWA WATOTO WA VIONGOZI KUCHUKUA FORM AU KUGOMBEA UONGOZI KWENYE VYAMA WOTE HAMTUMII AKILI. WENGI MNAULIZA JF KENNEDY, GEORGE BUSH NA WENGINEO NI KWELI WATOTO WAO WAMEINGIA KWENYE SIASA LAKINI WAMEGOMBEA UONGOZI BAADA YA BABA ZAO KUONDOKA KWENYE UONGOZI

    HUYU MTOTO ATAKUA NA PRIVILEDGES NYINGI TU KWA AJILI YA JILA LA BABA YAKE. KAMA AKIPATA HII KAZI KITU CHOCHOTE ATAKACHO PENDEKEZA AU KUFANYA KITAPITISHWA MOJA KWA MOJA. NA ATAKAYE MKATALIA MTAJUA NINI MADHARA YAKE YATAMPATA HUYO MTU ANAWEA HATA KUPOTEZA KAZI YAKE KAM MWANAYE AKIMWAMBIA BABA YAKE.

    KAMA BABA YAKE ANGEKUA MSTAAFU HALAFU YEYE AGOMBEE WALA NISINGESIKITIKA LAKINI BABA BADO YUPO RAISI....KWELI HII MNAONA NI VIZURI?

    NA PIA KAMA AMESOMEA MAMBO YA UONGOZI AU POLITICS AS HIS MAJOR HAPO NITAELEWA KIDOGO NA KAMA NINGEKUA MZAZI WAKE NINGEMWAMBIA AFANYE KAZI NYINGINE KIDOGO KUPATA UJUZI BY THE TIME BABA URAISI UMEISHA BASI ANGEINGIA KWENYE HAYA MAMBO.

    YOU GUYS HAVE TO LEARN TO SEE THING IN BLACK AND WHITE NOT JUST IN GRAY COLOR ONLY.

    HIVI UCHAGUZI MWINGINE NI LINI WA KUCHAGUA RAISI MPYA

    ReplyDelete
  41. Dhuu...! sijasoma comments zote hizo nasikia kizunguzungu.

    Kuna mahali tumelauumu wazee kupewa madaraka kila leo na vijana competent wanaachwa, sasa mbona tena kama kuna vijana wana jitahidi kuendela mahali fulani tunalalamika pia? Let us not waste time on that let us be supportive wawe watoto wa vigogo (as u call them) or not they are tanzanians. Tubadilike jamani let us look things on positive side! otherwise wazee watachukulia tu "vijana hawana lolote..kelele tupu..." which I doubt

    ReplyDelete
  42. Hey Ridhiwani, HONGERA! Nilijua utafuata nyao za Mzee!

    Best Wishes to you. Holla at chemiche3@yahoo.com

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 06, 2007

    Well,I knew CCM were corrupt,but this is a new low for them.

    I suppose when my father becomes president I too shall "Apply" for a position in the Government huh?

    My message:Wake up Tanzanians,don't tolerate this patronage AT ALL,if you can't see the big picture Kikwete is painting with all these little ongoings then do not expect Tanzania to advance in ANY way for the next two decades.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 06, 2007

    "Mbona hamshangai George Bush Kuwa Rais wa Marekani kama alivyo baba yake mnashangaa Ridhwat Kikwete!"

    Sorry,but how on Earth does George Bush relate to Tanzania?You do know that there WAS another president in between Bush senior and junior,right?

    And please,don't try and defend this child by saying "It's just a small position!Nothing major!",Mkapa started out as a bloody reporter,this game Kikwete is playing is ONLY aimed at making his son the future president of Tanzania.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 06, 2007

    "Guys stop crying.... Bwana mdogo amechukua umri unamruhusu pia Elimu anayo, sasa wabongo mnapiga kelele mwenzenu huyu kachukua fomu pia atashinda tu"

    Elimu anayo?Tell me,what proof do you have that he has ACTUALLY graduated and attained a proper degree in this field he's applying for?

    God,it's people like you who are apart of the problem with Tanzania,the "Let's just let him be!Nothing will happen!" logic is not only idiotic but is highly FALSE.This is EXACTLY why Tanzania is still among the poorest nations of the world,number 4 to be exact(If you need proof feel free to ask for it).

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 06, 2007

    Mi nafikiri suala la form lisituumize kichwa. Tusubiri uchaguzi, tuone watoto waote wa vigogo wamepita?, au tuone kama majina yote ya watoto wao watayarudisha?, hapo sasa ndio tuanze kuchambua mambo.

    Unajua kuchukua form hata mtu ambaye 'antena imetua kunguru' yaanu akili chenga chenga, kwa wenye tivii wanajua naongea nini, anaweza chukua tu kigumu kushinda.

    Michu majina yakirudi tuwekee orodha ta watoto wao wote hapo tuone kama baba zao kweli hawana upendeleo?,

    Hapa mi naona inawezekana JK anataka kucheza mchezo amabao wote mtashangaa ni pale atakapomkata jina dogo lisirudi, ili aweze kuwa na kisingizio kama mwanangu nimemkata jina iwe wewe?, ndio ngoma ya mchezo mtakapoiona sasa.

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 06, 2007

    Waridi tatizo siyo vijana hapa tatizo ni vijana wapi? Huyu siyo kijana kama akina Zito, huyu ni kigogo. Maana hakuna mtu anayeweza kumchallenge. Akimwambia baba yake umekwisha. Huyu siyo sawa na akina karume, bush na wengineo, huyu anatumia mgongo wa baba yake.

    Sitashangaa kuona pia mdogo wake akichukua pia form next time hizi ndizo tunaziita hira za watanzania waliomadarakani/walio na nafasi.

    Hii inaitwa Kombolea mwanangu! butua.Baaada ya baba kupigana na kufika, sasa njia ni nyeupe kushika kila mahala.

    Ndio maana sitashangaa kuona baadhi ya watu makini kuangalia alternative.

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 06, 2007

    tatizo nyie wotw mliocomment hapo juu hamjui hicho cheo kina maan gani.
    ni chao kidogo sana, ayani mtu unakua nacho na unaendelea na kazi nyingine, sio full time kama some of you wanavyothani.
    afu msipende kummix sana dogo na baba yake,dogo ameanza politics kabda baba yake hajawa waziri, sasa inakua vipi aache leo just because baba yake ni rais?
    then kumbukeni hiyo ni haki yake kikatiba, and instead of kulalama eti anachukua fomu mtoto wa rais, nenda wewe kachukue kwenu uone kama utaweza au hutaweza.
    afu mbona hammsemi amina shifupa, baba yake hakuwa na cheo cha maan CCM, ila coz ana damu ya politics kafight kivyake kawin, regardless ametumia njia gani!

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 06, 2007

    I once asked, "What has your country done for you so far?" I am asking again!

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 06, 2007

    Dah kwanza naomba nimpongeze bwana Ridhiwani kwa uamui wake wa kuchukua fomu,, ni haki ya kila mtanzania kwa hiyo na yeye akiwa mtanzania ana kila haki ya kuchukua form hizo,, pili nitoe dukuduku langu kwa hawa wananchi waliochangia kutoa maoni humu ndani ya blog hii maridhawa,,,, Mimi nawapongeza wote mliochangia humu ndani pia napongeza wale wote waliotoa comments ambazo ukizisoma basi utaona kweli kabisa huyu mtoa maoni ameenda shule hongereni sana,, ila kuna MPUUZI mmoja hapo juu ameandika pumba ambazo sijawahi kukutana nazo, hivi kweli unaweza ukaspare some times kuja kutueleze majigambo yako kuwa WAZAZI WAKO WALIENDA SHULE NA SISI WANANCHI TUSIO NA WAZAZI KWENYE HII SERIKALI TUTABAKIA HIVI HIVI KAMA TULIVYO TILL WE DIE,, kumbuka we dogo huyo baba yako au mama yako au nani yako aliyeko madarakani ni kutokana na kura za huyo hyuyo mlala hoi unayemtukana leo.... kwa hiyo jaribu kujirekebisha ndugu haya ni maisha bwana na maisha ni kama mbio za kijiti kuna leo na kesho bwana,,,, Majigambo hayafai

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 06, 2007

    CONGRATS THE SON OF MY EX PARTNER

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 06, 2007

    Wakubwa wanataka kuhakikisha wanalindwa pale wanapotoka madarakani ndio maana wanahakikisha watoto wao wanachukua fomu ili wawaoe nafasi na baadae wawalinde na kuziba madhambi yao.Katibu mkuu wa chama Makamba alihakikisha Kijana wake yuko na Kikwete ndio akamsaidia kumuombea Ubunge wa kuteuliwa na sasa ameshaanza vikao vya kampeni ya mtoto wake Mwamvita ili awe mbunge viti maalum 2010.

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 06, 2007

    Most of you watanzania ni wajinga, ndio nimesema wajinga. Mtu akiiba Tsh 1000 mnampiga mawe mpaka kufa lakini hao wakuu wanaoiiba mamilioni na mnajua hamfanyi lolote bali kuwafagilia. Mtakufa maskini na kuchomwa moto.

    ReplyDelete
  54. AnonymousJune 06, 2007

    Kikwete amechemsha. Kama mzazi na mshauri wa huyu mtoto angemwambia asichukue form wakati yeye yupo madarakani.

    Kuna uongozi na uongozi...Mtoto wa raisi kugombea NEC????

    TZ viongozi wamesahau kuwa hiyo na kazi sio ukingship. Hii nchi ni yetu wote na babu zetu waliijenga pia sio kwa vile hawakua kwenye mambo ya siasa basi mjisahau kiasi hi.

    Wengine mmeshaanza kutoa email zenu mkijua kesho basi huyu kijana atanisaidia kazi ...acheni ushambenga....kama ni rafiki yako wasiliana naye in private...ulikua wapi siku zote hizo.

    ReplyDelete
  55. AnonymousJune 06, 2007

    WATANZANIA WENZAGU FUNGUENI MACHO KARINE YA 21 INAENDA HIYO NA NCHI YETU INATIMIZA MIAKA 46 TANGU TUWE UHURU MAMBO YA MZEE KASEMA NDIYO YAMETUFANYA TUWE WACHEKESHAJI HATA KWA MAJIRANI ZETU AMBAO HAWASTAHILI KUTUCHEKA...HIYO SYSTEM YA MWALIMU YA KUWEKA WATU WAKE WA KARIBU ILI HASIJE AKAPINDULIWA YAMEFANYA NCHI ISHINDWE KUJIMUDU KWA MAMBO MENGI TU MATOKEO YAKE TUMEBAKI KUWA OMBA OMBA NA KUISHI KWA MISAADA KAMA WAZUNGU HAWAJAFURAHI BAJETI HAITOKI... MIE SIKIONI KITU AMBACHO WATANZANIA TUNAWEZA KUJIFUNIA UKIONDOA WHAT WE CALL (PEACE) AMBAYO INAELEKEA KUONDOKA SOON KAMA MAMBO YENYEWE NI HIVI NA KARIBU TUTAANZA MAMBO YA RWANDA...NYIE SUBIRINI TU HIYO INAKUJA KWA SABABU WATANZANIA WA 1990 SIYO WATANZANIA WA 2007 UTANDA WAZI UMEFUNGUA WATU MACHO .....WATANZANIA WAMEISHA JUA NINI MAANA YA KUISHI BAADHI YAO WANASAFIRI WANAONA DUNIA INAVYOENDA WATU WANAUCHUNGU NA MAISHA. WATANZANIA WALIMCHAGUA KIKWETE WAKIWA NA MATUMAINI YA KUWA MKOMBOZI WA WATU WA CHINI MATOKEO YAKE AMEANZA KUWAFUNJA MOYO WALIO WENGI KWA UWAJIBIKAJI WAKE NA UTENDAJI KAZI, SASA UKIONGEZEA TENA SYSTEM ILE YA KUPEANA PASI.... MPAKA WATOTO''' BASI HAPO AMECHEMSHA SANA HATA NUSU YA MUDA WAKE WA KUKAA IKULU BADO ALISHA ANZA KUVUTA KIZAZI... BONGO '''' KWELI NCHI YA KISANII .
    KWANINI ATUIGI MIFANO YA WAFADHILI WETU MTU MUDA WAKE UKIISHA ANAFUNGA VIRAGO ANAWAACHIA WATU WENGINE WAFANYE KAZI..NANI ALIKUAMBIA KWAMBA PRESIDENT IS PROFESSIONAL????????? MTU ALIRIDHISHA WATOTO WAKE UDAKTALI AU UHANDISI HUYU ANAHESHIMIKA SIYO URAISI HIYO NI POSITION AMBAYO UNAPEWA NA WANANCHI KWA MUDA SIYO MILELE...KAMA TUNAVYOFANYA AFRICA MATOKEO YAKE NI VITA VYA HAPA NA PALE NA KURIMBIKIZA UMASIKINI..
    HUYU MTOTO WA JK ANAWEZA KUONGEA NINI KUHUSU POLITICS.. JAMANI'''' POLITICS IS REALLY PROFESSIONAL AMBAYO WATU WANASOMEA SIYO MAMBO YA LONGO LONGO ZA C.C.M ETI SIASA.. HALAFU NYIE WATU WENGINE MNA UNGA MKONO VITU VYA AJABU.. HAO WATU BWANA WANAFUJA HELA ZA WAZUNGU WANAZOTUPA KUTEGENEZA BARABARA NA KUWEKA MAJI KWA WATU WA CHINI WENYEWE WANANUNULIA MAGARI YA KIFAHARI ...HILI GANI JAMANI MNAJUA BEI YAKE LAKINI??????? HIYO NI LATEST BMW INAANZIA 65 KWENDA JUU UJAWEKA MADIKO DIKO...ANATEMBELEA MTU AMBAYE ANA FAIDA YOYOTE KWA NCHI...WAKATI WAGONJWA MUHIMBILI HAWANA HATA ASPRIN , KITANDA KIMOJA WANALALA WATU WAWILI HIYO BAHATI ...MARANYINGINE CHINI HALAFU SOMEBODY IS DRIVING BMW LATEST.....INATIA HURUMA SANA INGAWAJE MIE SIISHI BONGO LAKINI YANAYOTOKEA BONGO YANATIA SANA MAJONZI KWANINI JK AENDA KUTEMBELEA WAGONJWA AKAONA WATU WANAVYOLALA KWENYE SAKAFU...HALI MPYA KASI MPYA....NYIE MLIO BONGO MSIPO AMKA NDIOO HIVYO TENA IMETOKA.. NAFIKILI WENGI WETU WAMESOMA LITERATURE KUMBUKENI(THING FALL APART AU KWA KIWAHILI MKENI SI SWALI TENA ) GOOD LUCK GUYS....MKEREKETWA UGHAIBUNI..

    ReplyDelete
  56. AnonymousJune 06, 2007

    Si mnataka uongozi wa vijana hata kama hawajaiva so long as ni vijana?????????????????????????????

    Sasa kelele za nini na huku ninyi mnekunja mikia kuchukua fomu!!!!!!!
    !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    Bado mmeweka matako chini????????
    ???????????????????????????????????

    Nendeni huko Bagamoyo au kwingineko mkachuke fomu!!!!!!!!!!!
    !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  57. AnonymousJune 07, 2007

    Michuzi kweli usifiwe kwa vile solidarity ya wa bongo inaonekana kwenye mambo mengi tu sasa hivi. Lakini haya na mengine mengi yangepita chini chini tu bila kujulikana au kujadiliwa kama sio hii blog yako. Hata yakijulikana kwenye vyombo vya habari TZ watu wengi wanasoma na kusema hii halinihusu mimi kwa hiyo kwa nini nijisumbe. Na pia TZ ni forbidden kumweleza ukweli kiongozi wako , baba yako au mkubwa wako pale anapokesea kitu.

    Niwape hongera sana kwa vile wengi wao wanaongea point sana tu the only difference here ni huyo mtu anaoingelea hoja yake akiwa amekaa upande gani???.

    Na wengi nawaona hapa wanaongea point zao kulingana na mazoea na sehemu wanazoishi. Inaelekea wengi hamjakulia bongo au kama mliweza kuishi na kusoma bongo basi labda mliondoka muda mrefu tu au hamjaenda bongo muda mrefu.

    Kwa taarifa yenu bongo uliyoiacha ni ile ile. Kama uliondoka awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu na hii ya nne zote ni sawa tu.

    Kama huna unayemjua hufiki mahali popote.

    Kushughulikiwa bado ni kidogo kidogo wanataka. Hongo bado ipo mbele tu. Angalia hizi passiport mpya kwa wale mlioenda bongo na kutakiwa kuchukua mpya kabla ya kutoka nje ilikua ukimkatia mtu dola 50 unaambiwa njoo mchana kuchukua passiport yako. Usipotoa sijui ulikua unasubiri mpaka sijui lini.

    Na hata hizi office za maubalozi yetu nje ya nchi yaani wao wanaziendesha kibongo bongo tu. Piga simu kwenye ofisi za ubalozi wako kuulizia jambo wakipokea simu wakijua tu wewe ni mtanzania basi na sauti inabadilika halafu utaanza kuzungushwa wee …na mwishowe utaambiwa hold on….hold on….. hold on….Wananyodo sana…

    Michuzi siku moja tuwekee mjadala kuhusu maubalozi yetu yalioko nje ya nchi na jinsi wanavyo toa customer service kwa raia wao wakiwa wanahitaji informations au jambo lolote…compare to other nationalities

    ReplyDelete
  58. AnonymousJune 07, 2007

    kazi kwelikweli huko Tanzania.

    ReplyDelete
  59. AnonymousJune 07, 2007

    HABARI NILIZOZIPATA HIVI PUNDE NI KWAMBA KIPA WA ZAMANI WA YANGA BERNARD MADALE AMEFARIKI DUNIA JANA 6/6/2007 MICHUZI LETE NEWS.

    ReplyDelete
  60. Acheni wivu wabongo mnakuwa kama hamjasoma? Kha! kwani na nyie mmenyimwa kwenda kuchukua form? Vibaya hivyo, mwacheni Ridhiwani asonge mbele, mtasema mtachoka lkn mjue elimu inamata sana, mnakuwa waswahili waswahili yaani sijui moje hata. Songa mbele Ridhiwani usisikilize maneno ya wabongo, wasikukatishe tamaa!!

    ReplyDelete
  61. AnonymousJune 07, 2007

    NYIE KWELI MMELEMAA. MNAANGALIA RIDHI ANACHUKUA FOMU WAKATI NCHI INADAIWA KUTUMIA MAMILIONI YA FEDHA KUHUDUMIA MAGARI YA KIFAHARI.
    HIYO GARI ALIYOENDA NAYO KUCHUKUA FOMU HATA MTOTO WA MALIKIA HUKO UINGEREZA SIJUI KAMA ANAWEZA KUTAMBA NAYO MITAANI.
    KWANZA ATAPIGIWA KELELE NA WALIPA KODI KWA KUTUMIA 4X4 NA KUCHAFUA MAZINGIRA. HIYO GARI INAGHARAMA YA MILIONI NGAPI JAMANI.
    HIVI KWELI TUNABANA MATUMIZI AU TUNAMWAGA RADHI KUONYESHA NANI ALIYETUMIA DOLA NYINGI IKULU.
    ACHENI JAMAAA. HAYA MAGARI HATA WABUNGE WA UINGEREZA SIDHANI KAMA WANATHUBUTU KUWA NAYO INGAWA NI NCHI TAJIRI NA YA KIBEPARI. BMW X5...SIYO BMW X3!!! HATARIII
    KAMA HUYO MTOTO ANASOMA HUKO UK, ANACHUKUA MFANO GANI KUTOKA KWA WABUNGE WA NCHI HIYO, WANAVYOTUMIA USAFIRI WA KAWAIDA, WANAVYOISHI NA MAMBO MENGINE.
    MIMI NILIDHANI UNAPOKUWA NJE UNAANGALIA JINSI GANI WENZETU WANAVYOJITAHIDI KUJENGA NCHI ZAO NA KULETA MIFANO HIYO NYUMBANI. LAKINI HAPA....NATIA SHAKA.

    ReplyDelete
  62. AnonymousJune 07, 2007

    Kwa nini tuko suprise! Kwanza alikuwa mama Migiro asiyo na diplomacy experience alikuwa in charge of mabalozi. It was simple message JK, first lady and my friend Migiro run the country. Kila picha ukiona the President is taking a tour introducing the foreign minister to the world. Suku pata kuona that the Foreign Minister of any country given that kind of publicity.Huya mama kawa cha bad blood everywhere. She could not build bridges between Tanzanians living abroad with their embassies. She was in charge of career diplomats who have been serving our country for years. People where fired, majungu majungu tu. People were afriad to say anything becuase she was president's friend. London Balozi rafiki wa president, qualification yake a lawyer. Picha kwa ma pich tu, attending mashuli mashuli tu.
    Here comes his son. How many sons get publicity kama hiyo. Tanzania is not America. CCM is in trouble
    it is divided into majungu majungu tu. His son should set an example by volunteering, working with NGOs
    lakini hiyo si culture yetu! Mtoto neda kwenye JAMBO FORUM upatia mafunzo!

    ReplyDelete
  63. AnonymousJune 07, 2007

    ROSE inaelekea na wewe ni mtoto wa vigogo. Anoy hapo juu amesema kweli hapa watu wanajadili hii habari na idea zao zinategemea umekaa upande upi wa meza.

    Wenye kufikiria kuwania hizi kazi wakati baba zao bado wako kwenye hizo nyadhifa wanaona hapa wanachomewa utambi.

    Elimu ni yeye tu anay? Amesomea nini huyu kijana lets be honesty ...

    ReplyDelete
  64. AnonymousJune 07, 2007

    Sasa wewe Chemi ndo nini kutoa email yako?, Grow up dada, wewe ni mtu mzima sana maana umesoma na dada zangu walionizidi miaka 10. Hata nikiwaambia umemwambia mtoto wa Rais akutumie email watakushangaa.
    umemsifia kwanza ukidhani akisoma sifa ndo ataku email?, kama alikuwa hakujui kabla sahauu dada kupata email from him.

    ReplyDelete
  65. AnonymousJune 07, 2007

    Anoy 1.44pm wajifunze wapi wakati wakimaliza shule tu hawataki hata kufanya kazi kidogo huko huko ili wapate work experience. wanaogopa kwa vile huko hamna upendeleo...
    Halafu wanamiss kufuliwa nguo, kutandikiwa vitanda na the only thing ni "what's for dinner" chakula kinakuja mezani.


    Ninachosema kufanya kosa sio kosa, kosa kirudia.

    1. Vijana wengi hii iwe changamoto mlioko home go and get those forms too iwe challenge najua wasomi wako wengi.

    2.Vijana watu wazima kikubwa ni siku ya kuvote go and vote. Uchaguzi wowote ni muhimu uwe ni wa nyumba kumi, wabunge au raisi go and vote...

    I hope by next time wanavote tena watakua na system ya watu kuvote nje ya nchi. Nchi nyingine nyingi tu ingawaje wako nje ya nchi lakini wao wanavote kama raia wengine.

    ReplyDelete
  66. AnonymousJune 08, 2007

    UMENIFURAHISHA SANA ANONY ULIYEMSHUSHUA CHE MPONDA I COULDN'T IMAGINE SUCH AN ACT FROM HER ETI ANATOA EMAIL ??!!! HA HA HA HA VERY FUNNY. KWANZA WE MTU MZIMA SANA ACHA KUJIAIBISHA I NEVER THOUGHT YOU ARE THAT CHEAP!! HALAFU KUNA ANONY ANASEMA ETI RIDHIWANI KAANZA POLITICS KABLA BABA YAKE HAJAWA WAZIRI...JAMANI JAMANI ONGEENI WITH FACTS AU MNATETEA TU HADI PUMBA?, IVI UNAJUA ANA UMRI GANI? YEYE ANA 27, BABA YAKE AMEKUWA WAZIRI KWA MIAKA 17 (reference kitabu cha kumtambulisha kikwete if am not mistaken kiliandikwa na ben mtobwa wakati wa kampeni) BACK TO THE POINT INAONESHA BABA YAKE AMEANZA UWAZIRI YEYE AKIWA NA MIAKA 10, UNATAKA KUSEMA ALIANZA POLITICS AKIWA NA MIAKA 9 AU 10? GET WELL INFORMED BUDDY!! HATA IVO RIDHIWANI KUGOMBEA NEC SIO ISHU NAMUONA KALOST TU AACHE KUFANYA SHUGHULI ZA MAANA KUMJENGA KIMAISHA ANAFUATA MKUMBO!!LOOSER...

    ReplyDelete
  67. AnonymousJune 08, 2007

    Tena huyo CHEMI huyo hivi karibuni tu tena alikuwa anajipendekeza, anajipitisha, anaji "cheap-isha" na kujimove-zisha kwa Sumaye kule Marekani.
    Angalia! Shauri zako. Ohoo!

    ReplyDelete
  68. AnonymousJune 09, 2007

    JAMANI HUYU ROSE SIYO MTOTO WA VIGOGO HILA CHAUPELE...CHUPI MKONONI HUYU ANALOLOTE ....HALAFU FOR YOUR INFORMATION GUYS TANZANIA HAKUNA KOGOGO HAO WATU TUNAO WACHAGUA WANAKULA HELA ZETU ZA MISAADA...LEO MMAREKANI KACHEKA KWENYE G 8 SUMMIT AFRICA BILLION 60 YEYE PEKE YAKE ANATOA 30 SASA BMW (XX 5) NAONA JK ATANUNULIA MPAKA WAPISHI WAKE... HALAFU KILA SIKU WAZUNGU WANAANGALIA NA KUCHEKA TUNAVYO NYENYEKEA MISAADA...LAKINI SIYO MBAYA KAMA NUSU YA MISAADA TUNGELITENZENEZA ANGALAU DAR AMBAKO WAZUNGU WANAFIKA KUANGALIA MATUMIZI YA HELA ZAO NA KUKUTA MAANDAKI NA FUMBI HUKU CADILLAC NA BMW ZINABEMBEA KWENYE MITARO..MAMBO MAPYA NA HALI MPYA

    MKEREKETWA UGHAIBUNI/////.

    ReplyDelete
  69. AnonymousJune 09, 2007

    I know huyu mdada is too much. Kila kingozi au mtu mzito wa bongo basi anajilamba kwao kweli.

    Kwani mzee mjinga huyu...ukiingia mjini lazima data uzipate kwanza ...nani asiyejua Boston wanawake za watu wengi tu wanamamiwaya...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...