Jumuiya ya Watanzania UK yaipinga kampuni ya WTM Ultility Services
.Yaiomba Serikali kusitisha mkataba.
.Yataka TBS Itambue MOT ya Uingereza
.Watanzania waombwa kusitisha maandamo Alhamisi
JUMUIYA ya Watanzania Uingereza imeitaka Serikali kusitisha kampuni ya WTM Ultility Services iliyopewa jukumu la kukagua magari yanayokwenda Tanzania na Shirika la ViwangoTanzania(TBS), kwa kuwa utaratibu huo hauwezi kukidhi matakwa ya wengi.
Uamuzi huo uliotolewa Jumapili iliyopita baada ya kamati ya utendaji ya Jumuiya ya Watanzania kukutana kwa dharura kuzungumzia tatizo la kampuni ya WTM Ultility Services {wakisema kuwa kampuni hiyo} inachofanya ni sawa na utaratibu wa kawaida wa kukagua magari unaofanywa na mawakala wengi wa Serikali ya Uingereza unaofanya kazi ya ukaguzi magari (MOT).
Kamati imependekeza iwapo TBS inahitaji magari yote yaliyotumika kutoka Uingereza kuwa na cheti cha ubora wa gari husika ni bora kutumia cheti cha MOT kama ilivyokuwa ikifanya huko nyuma, kwani viwango vya MOT vinakwenda sambamba na matakwa ya TBS.
Uamuzi wa kukubaliana na MOT ya Uingereza umetokana na mtandao wa mawakala wa MOT ni wengi na wamesambaa nchi nzima, tofauti na kampuni ya WTM Ultility Services ambayo inadaiwa kuwa ingeweza kutumia huduma ya kumfuata mteja alipo " mobile Unit Services" kufanya kazi za walio mbali na London.Jumuiya pia imeelezea wasi wasi wake iwapo ni kweli kwa kufanya ukaguzi wa magari kwa kutumia utaratibu wa kumfuata utakidhi matakwa ya vigezo vya ukaguzi kutokana na hofu kuwa vifaa vinavyotumika kwa ukaguzi wa MOT sio rahisi kuhamishika kwa ukaguzi.
Utoaji kibali hiki kwa WTM Utility Services haukuzingatia mfumo mzima wa ukaaji hapa Uingereza na hivyo kufanya zoezi zima kuwa la gharama kubwa kwa mtuma gari huko Tanzania.
Aidha Kamati ya Watanzania hapa Uingereza imependekeza, ingeweza kupewa kampuni ambazo zina mtandao nchi nzima kwenye kila kitongoji cha hapa Uingereza na kuwa na historia ya muda mrefu katika fani hii na wangetoza bei ya paundi 35 hadi 45 na ilichotakiwa ni TBS kufanya makubaliano na kampuni hiyo kwa ajili ya kutoa vyeti vya ukaguzi wa magari kama hawakubaliani na vyeti vya MOT.
Kama kamati ya Jumuiya ya Watanzania hapa Uingereza kazi yetu kubwa ni kuhamasisha Watanzania kuwa pamoja, kuwa na mahusiano mazuri baina yao kwa kujitahidi kusikiliza kero zao na kuwa kiungo muhimu kati ya Watanzania na Serikali (Ubalozi).
Wengi wa Watanzania hapa Uingereza wameonesha kutokubali TBS kuipa kazi ya ukaguzi kampuni ya WTM Ultility Services .Hili linatokana na vigezo vingi na kamati imechukua uamuzi huu kutokana na matakwa ya Watanzania walio wengi.
Ukaguzi wa magari Uingereza (MOT) unatozwa paundi 35 hadi 45 tu, wakati kampuni ya WTM Utility Services wanatoza paundi 100 kwa kila gari dogo na gari kubwa wanatoza paundi 180, kiasi ambacho kinalalamikiwa na Watanzania wengi.
Huu ni utaratibu ambao haukubaliki, Watanzania waishio Uingereza wana dhamira kubwa ya kuwekeza nyumbani kama Rais Jakaya Kikwete alivyokuwa anawahimiza kuwa wasijisahau kuwekeza nyumbani. Lakini si kuwaongezea mzigo wa gharama zisizokuwa na msingi na pindi gharama zinapokuwa nyingi, zinawakatisha tama Watanzania walio wengi.
Utaratibu huu wa kampuni ya WTM Utility Services ulianza rasmi tarehe 14. 05. 2007, lakini utaratibu mzima kampuni hii ulitangazwa tarehe 26.05.2007, hivyo kamati ya Jumuiya ya Watanzania umeiomba Serikali kusitisha adhabu zinazokusudiwa kwa magari yaliyotumwa baada ya tarehe 14.05.2007.
Kamati imependekeza kwa TBS kuangalia uwezekano wa kutumia utaratibu wa ubora wa magari Uingereza (MOT) ambao unafahamika ili iwe sheria kwamba kila gari yenye cheti cha MOT iwe haihusiki na uchunguzi huo.
Kamati pia inawasihi wale wote ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano kwa ajili ya kuipinga kampuni ya WTM Utility Services hadi ubalozini kwa lengo la kuwasilisha malalamiko yao kwa Mheshimiwa Balozi, Mwanaidi Maajar siku ya Alhamis, kusitisha maandamano hayo hadi hapo Serikali itakapotoa tamko rasmi.
Wajumbe wa kamati waliohudhuria ni Mwenyekiti Abubakar Faraji, Makamu Mwenyekiti, Bi Zubeda Mahug, Katibu Mwenezi, Juma Pinto, Wajumbe:Bi Nora Sumari, Bw. Haruna Mbeyu, Bw. Dessa Makoko, Bw. Jumapili Kassongo na Bw. Saidi Yakubu.
- Abubakari Faraji, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Uingereza Kwa niaba ya Jumuiya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

 1. AnonymousJune 06, 2007

  THE SILENT STALKER Says......Kusema kweli am so happy kusikia tumeungana na hili swala maana wakati napost the 1st two malalamiko nilipata faraja sana kuona wenzangu tumeungana mkono kwenye hili suala, sasa tukae tusubiri tuone Serikali itasemaje??? Jumuia ya WaTZ UK, nawasukuru sana kwa kukaa pamoja na kulijadili hili suala kwa dharura BIG UP 2 U all, Am all in Ur favor tusibiri matokeo, lakini kama maandamano yatakuwepo count me in even thou i havent done any maandamano in my entire life

  ReplyDelete
 2. AnonymousJune 07, 2007

  Baada ya kubainishwa kwamba address waliyotoa WTM huko Dagenham inatiliwa mashaka katika blog hii, leo hii wametoa address mpya ambayo pia ina utata kama zoezi ambalo wanakusudia kulifanya. Hatimae address yao imezaa address mbili kwa moja barking/dagenham kama inavyoonyesha kwenye tovotu yao, katika maisha yangu kukaa UK, sijawahi kuona address ina address mbili kwa moja, inadhihirisha wazi kwamba hii kampuni hawajui wanachokifanya na wanachokikusidia kukifanya, bali ni sehemu ya kitengo cha kuchukulia wafanyabiashara pesa zao bila kuwa na mantiki au taratibu za kuaminika katika kufanya zoezi hilo.


  Hata hivyo leo hii WTM wametoa press release, ambayo inaongelea kuhusu zoezi hilo la ukaguzi wa magari, ambalo litaanza tarehe 06 June 2007, na siyo tarehe 14 MAy 2007 kama ilivyoelezewa hapo awali, walipoingia mkataba na TBS.

  Kama tulivyoolezea hapo awali wafanyabiasha lazima, wapeleke malalamiko yao kwenye vyombo vya sheria hapa UK na huko Tanzania kupata uwazi wa huu utaratibu mzima wa hili zoezi gharamu ambalo mpaka muda huu, hakuna taratibu kamili ambayo iko wazi kwa wananchi, hususan kuhusu hili swala la gari kuwa MOT, inakua vipi tuwapelekee hawa jamaa kukagua gari hilo hilo.

  Hii licence yao, kama wanvyodai wamepatiwa kuweza kuanzisha hili zoezi, lazima iangaliwe upya na malalamiko lazima yapelekwe VOSA uk, na vyombo vyengine husika vya kiserikali UK.


  Mpaka hivi sasa sina Clue WTM ina maana gani kwa urefu ?? SAY NO DUBIOUS COMPANY SAY NO DUBIOUS DEAL

  ReplyDelete
 3. AnonymousJune 07, 2007

  Je kampuni ya WTM inabiashara ya kukagua na kusafirisha magari, hiki si kujichanganya na kuwapendelea zaidi, wateja wao wa wenye kusafirisha magari.

  Waungwana hili ni swala la kuliangalia.

  Scenario,

  Nina malori mawili na magari madogo mawili, ninakusudia kuyasafirisha kuyapeleka Tanzania, vile vile meli nitakayoitumia inaondoka siku tatu kutoka leo, ninawapelekea hawa WTM kukagua haya magari kwa bahati mbaya yote yamefeli, lakini sasa ninarudi tena na kuwapa hii deal ya kusafirisha haya magari yangu kwa kutumia kampuni yao, kwa gharama kama paundi 6000, na wao watapata chao kama paundi 2500 mpaka 3000. Je WTM hawayatayachukua haya magari na kusafirisha kwa kutumia kampuni yao ?? hali ya kuwa wata issue hizo TBS certificates kwa magari ambayo yamefeli MOT na TBS Standards???

  Hili tatizo nina uhakika litazua mengi hapo mbeleni, ni swala ambalo tuliangalie kwa makini

  ReplyDelete
 4. AnonymousJune 07, 2007

  Nafurahi sana kusikia hili...way to go guys...ingawaje siye tulio USA hatuhusiki kwenye hili zoezi lakini wakianza huu upuuzi huko kwenu watamalizia kwetu na mabara mengine pia. Ni heri tuwakomeshe mapema

  Na mimi nawaambia tu serikali kuwa msiendeshe mambo kimiaka ya ukoloni...tutasimama kila siku kwa miguu yetu miwili kudai haki zetu na kuyaongea hadharani mnayofanya kwa siri

  Kazi mliwapa utility toka 14 of may lakini mmekuja kutangaza mwishoni kwanza kwa kupitia kwa blog...sound fishy to me...

  ReplyDelete
 5. AnonymousJune 07, 2007

  mambo ya ulaji.com wa-TZ tunapeleka mpaka ughaibuni. kama TBS walishachukua chao mapema hapo watajiju. hapo kuna kila dalili ya rushwa, yaani gharama ya ukaguzi iruke toka paundi 35-45 mpaka paundi 100-180 (almost mara 3 ya gharama za kawaida) kwa mwendo huu sijui kama tutafika!!
  Big Up wana Ukerewe kwa kuonyesha njia!

  ReplyDelete
 6. AnonymousJune 07, 2007

  Tukisha wawajibisha hawa WTM inabidi tuwaangalie TBS ili tuone kama taratibu za kutoa zabuni zimekiukwa. Mtu lazima awajibike, a buck stops at TBS. Hongera wadau wa Ukerewe.

  ReplyDelete
 7. AnonymousJune 07, 2007

  TULIAMBIWA MIKATABA YA MADINI IMEKOSEWA.SASA HUU WA WTM SERIKALI HAIKUUPITIA VIZURI????


  JAMANI TUMECHOKA NA HUYO JK NA SERIKALI YAKE.KILA SIKU NI ISSUE MPYA.

  TUTAFIKA KWELI?HAO WATU WALIOWAJIBIKA KWENYE HUO MKATABA WAFUKUZWE KAZI ILI TUEPUKE HAYA MAMBO YA KIJINGA.

  KEEP IT UP WANA UK.TENA JK ASIJE TENA HAPO KUWAPA HOTUBA ZA UONGO TU.

  ReplyDelete
 8. AnonymousJune 07, 2007

  Kama mkazi wa Ukerewe nilikua sioni haja ya kuwa na affiliation yoyote na umoja wetu hapa UK coz i was thinking baadhi ya watu walikua wanajitengenezezea mianya ya ulaji tu,lakini my opinion has now changed. Well done guys, how do i join?
  It is clear that tutakua tunalipa extra ili ku cover gharama za hawa jamaa kumove around na mitambo yao.Naamini kama they will never be able to justify the fees they are chrging kama tutawapeleka mbele ya vyombo husika.Bado pia nina wasiwasi na quality ya service yao. Is it going to be any better compared to MOT za waingereza?
  Hapa kunakuka rushwa na naona kama wamepata hii deal kwa njia ya rushwa basi hawa ni watu wa rushwa na serikali itegemee mikweche zaidi kutoka UK coz watakua hawakatai gari kama ukiwakatia kidogodogo.
  Together we stand, cheers brothers and sisters!

  ReplyDelete
 9. AnonymousJune 07, 2007

  Jamani mjue kwamba hiyo WTM ni ya Twine Mutabazi ambaye mama yake mzazi(sasa marehemu) mpaka mwaka huu mwanzoni mauti yalipomkuta alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS hivyo hilo ni pande kapigiwa mtoto tangu mama akiwa hai na alipofariki ndipo Mkurugenzi Mkuu Bw. Mwakyembe kaamua kutoa dili hilo kama kifuta machozi!!!!

  ReplyDelete
 10. AnonymousJune 07, 2007

  wanangu ughaibuni komaa nao hao matapeli hadi kieleweke. bongo tuko nyuma yenu.bahati mbaya local media hapa bongo naona imepewa mshiko maana big as it is hii story wameibania hapa nyumbani.

  ReplyDelete
 11. AnonymousJune 07, 2007

  Nazipongeza jitahada za kuomba serikali ya Tanzania kuzuia dhuluma na wizi huu wa wazi. Lakini isipochukua hatua yeyote nini kifanyike? Naomba tufungue kesi mahakamani na kuweka pingamizi dhidi ya hawa walaji hadi kesi itakapokwisha. Tunavyo vigezo na ushahidi wa kutosha kuwashinda hawa walaji katika vyombo vyetu vya sheria. Nia tunayo, uwezo tunao, tutawashinda.
  Naamini sheria itahukumu kwa manufaa ya maslahi ya watanzania na si ya hao walaji na wezi wakubwa wa mchana.

  ReplyDelete
 12. AnonymousJune 07, 2007

  Video maalum ambayo imepostiwa si punde tu katika blog hii tbswtmuncovered kwa ajili ya kuleta furaha ndani ya nyuso zetu baada ya wiki ndefu bila maombi yetu na malalamiko yetu kutolewa japo tamko na TBS au serikali.

  Ni mategemeo yangu itakuwa ni yenye kuleta himasa zaidi, hali yakuwa tuna tabasamu. Ni mategemeo yangu mutaipenda.

  ReplyDelete
 13. AnonymousJune 08, 2007

  Kwasababu hii issue inazihusu nchi mbili, tunaweza kuwapeleka hawa TBS mahakamani Uingereza kwani hawawezi kuleta rushwa zao kama wanavyofanya Tanzania. Na hii itakuwa somo kwa walarushwa wote. We have to give them a lesson. "anticorruption 101" from Zambia.

  People, we must protest this kind of crruption, we must oppose it, and we must try to alter it. Someone must take responsibility.

  Let my people go! United we stand, divided we fall!

  Mdau from USA.

  ReplyDelete
 14. AnonymousJune 08, 2007

  Mmmoja wa watu wa karibu wa hao wezi wa WM utility alisikika kwamba wm utility ni kinyozi kwamba ukitaka kunyolewa lazima umfate kinyozi......despicable!!!!!

  ReplyDelete
 15. AnonymousJune 08, 2007

  Comrades, it is obvious hii ishu ya WTM ni mradi wa wakubwa. Ni ulaji tu!! Nothing else. Kama ishu ni inspection ya magari, MOT ya Ukerewe is qualified and sufficient enough to do the job competently. Kuongezea hapo WTM is simply duplicating efforts and shamelessly exploiting Tanzanians in the diaspora. Huu ni unyonyaji wa kishamba na kipuuzi sana. Surely our leaders can come up with more creative ways of exploiting the public.

  As always, huo mradi utekelezaji wake utakua mbovu na vimeo vitaendelea kuingia nchini kama kawaida. Hapa Tanzania kuna mpango wa kukatia magari road licence kila mwaka subject to passing police inspection. Lakini magari mengi nnayoyaona barabarani yana hali mbaya mno kiasi kwamba kwenye nchi ya kistaarabu ukionekana unaliendesha unaweza fungwa jela miaka 40. Wiki hii tu hapo barabara ya Kawawa kuna lori (nadhani modeli ya mwaka 1954, body lote kutu, halina taa hata moja) limeshindwa kupandisha mlima likarudi nyuma na kuua dereva wa gari ndogo iliyokua ikifuata. Kama kuna magari ya aina hii yanatembea kwenye barabara zetu, Trafiki wanafanya kazi gani? (Vimeo vingi ni vya matrafiki wenyewe na mabosi wao). Zoezi la kure-new road licence limeambulia nini? TBS wako wapi? Tanzanians, lets wake up and be serious. Hivi vimradi vya kijanjajanja vya kutafuta ulaji havitatufikisha mbali. Let us take pride in progressing through hard work.

  ReplyDelete
 16. AnonymousJune 08, 2007

  Hivi ndugu zangu wa UK, mmefikiria uwezekano kwamba hawa jamaa wa WTM wanataka muwalipe pound 100 kisha wao wanaweza chukua gari lako na kulipeleka MOT ili likafanyiwe inspection? Kule MOT wao wanalipa pound 35 halafu pound 65 wanatia mfukoni. Nadhani hiyo ndo plan yao...na hiyo tunaita kanyabwoya.Wizi wa kimachomacho.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...