Mr II live in concert in Houston Texas
Saturday, June 16, 2007

Baada ya show kali ndani ya Boston MA weekend iliyopita, sasa mashambulizi yanaelekea Houston TX ndani ya Safari Party Hall


Album mpya na ya tisa ya Sugu inayoitwa "Coming of Age(Ujio wa Umri)" ipo sokoni tayari. USA inapatikana kupitia
http://www.ngome.com/ na pia atakuanayo siku ya show Houston kwa $10.

Shukran!

Kitova
Ngome Entertainment
http://www.ngome.com/
Wakilisha Tanzania to the Fullest

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

 1. AnonymousJune 07, 2007

  Huyu chalii kaacha bangi?Ajibu yeye mwenyewe kama bado basi mimi siji kwenye concert.

  ReplyDelete
 2. AnonymousJune 07, 2007

  Wafanyakazi 1,500 Sunflag wagoma, wapiga bosi

  2007-06-07 10:17:26
  Na Cynthia Mwilolezi, PST Arusha


  Wafanyakazi zaidi ya 1500�wa Kiwanda cha nguo cha Sunflag, mkoani Arusha eneo la Njiro, wamegoma kufanyakazi na kuamua kuwapiga maofisa wa kiwanda hicho, akiwemo Ofisa Mwajiri Mkuu.

  Sakata hilo lilitokea mara baada ya wafanyakazi hao, kukatwa mshahara kutoka Sh. 40,000 hadi Sh. 27,000, bila ya uongozi huo kutoa taarifa zozote kwa wafanyakazi hao.

  ``Hawa maofisa wetu wanatudharau sana�hasa hawa Wahindi. Wanakata pesa hovyo halafu hawatoi maelezo ya makato hayo, sasa leo tumeamua kuchukua hatua�mkononi maana inaudhi sana,`` alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

  Wakiongea na waandishi wa habari kiwandani hapo, wafanyakazi hao walidai kuwa walikuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu na kwa malipo yasiyolingana na kazi.

  Mmoja wa wafanyakazi hao aliyeomba kutotajwa jina lake, alisema kuwa uvumilivu�una kikomo na hawatakuwa tayari� kupunjwa mshahara, wakati mshahara wenyewe ni Sh. 40,000 tu.

  ``Tunalipwa shilingi 27,000�badala 40,000 na kila siku� tunasema kuwa kiwango cha mshahara wa sh. 40,000 ni kidogo na tumevumilia vya kutosha. Hebu oneni jamani tunavyolipwa na hawa Wahindi? Hii kweli ni sawa?`` Alilalamika mfanyakazi mmoja.


  MICHUZI NAOMBA UITOE HII TUJADILI:

  TUMESEMA TANZANIA TUNAVUTIA WAWEKEZAJI ILI KUONGEZA AJIRA. TATIZO KUBWA SANA AMBALO MH. RAIS KIKWETE ANATAKIWA ALIVALIE NJUGA NI HILI LA AJIRA ZISIZOFAA. NASEMA HATUTAKI AJIRA ZISIZOFAA, TUNATAKA "QUALITY JOBS". HAWA WAWEKEZAJI UNAWAPA "TAX HOLYDAYS" NA VIVUTIO VINGINE KIBAO ILI KUTENGENEZA AJIRA, JE HII NDIYO AJIRA TUNAYOTAKA?

  HIVI KWELI 40,000 FAMILIA INAWEZA IKAISHI? MAJUZI WAFANYAKAZI WA SUPERMARKETS WALIANDAMANA WAKALALAMIKIA MISHAHARA MIDOGO, WA MAHOTELI NAO VIVYO HIVYO, JE WAZIRI ALICHUKUA HATUA GANI?. KWANINI TANZANIA LEO TUNARUHUSU HAYA? KILA SIKU TUNALALAMIKA "KUTOKOMEZA UMASKINI, MKUKUTA, MKURABITA, MENGI TU, LEO HUKO KWENYE G-8 WANAONGELEA "POVERTY IN AFRICA", ALAFU SISI LEO TUNARUHUSU MAELFU YA WATANZANIA KUNYONYWA NDANI YA NCHI YAO KANA KWAMBA SIO NCHI, KWANINI?

  WAZIRI WA KAZI ANAFANYA NINI HASA? HII NDIYO KASI MPYA ALIYOTUMWA NA RAIS?

  HAYA MAKAMPUNI AMBAYO YANAMILIKIWA ZAIDI NA WATU WASIO WATANZANIA YANAPATA FAIDA KUBWA, KWANINI WASILIPE MISHAHARA YA KUTOSHA? KUNA FAIDA GANI KUWA NA EXPORT FIGURES NZURI HUKU WATU WAKO JEHANAM NDANI YA NCHI YAO?

  MAKAMPUNI MENGI ULAYA GHARAMA ZAO KUBWA ZAIDI KATIKA "VARIABLE COSTS" AU GHARAMA ZA UENDESHAJI,AMBAZO NI MISHAHARA NA BENEFITS NYINGINE. AJABU NI KWAMBA SISI TANZANIA(AFRIKA) TUNARUHUSU GHARAMA ZAO ZA UENDESHAJI ZIHUSIANAZO NA MISHAHARA KUWA NDOGO SANA, TUNAWARUHUSU KUTUNYONYA, KITU AMBACHO HUKO WALIKOTOKA SHERIA ZAO HAZIWARUHUSU.

  TUNARUHUSU HAWA WATANZANIA WANANYONYWA, LAKINI TUTAISHIA KUJENGA MATABAKA YA WATU. HAWA WANAONYONYWA WATAKUWA MASKINI ZAIDI, WATOTO WAO WATAKUWA NDIO KABISA, MWISHO TUTAKUWA KAMA BRAZIL, AU AFRIKA KUSINI, AMBAPO UJAMBAZI UMEONGEZEKA SANA KWASABABU WASIO NACHO LAZIMA WAFANYE UJAMBAZI AU WAFE. WHAT DO THEY HAVE TO LOOSE? WAKATI HUO, HAO WENYE VIWANDA NA MA- SUPERMARKETS TUNAOWARUHUSU KUNYONYA LEO WATAKIMBIA NCHI, AU WATAJITENGA NDANI YA NCHI, JE SISI WATANZANIA TUSIO NA PA KUKIMBILIA KUWAKWEPA WATANZANIA WENZETU TUTAKWENDA WAPI?

  HILI SWALA SIO LA MISHAHARA PEKE YAKE. NI SWALA LA KUJIULIZA, TUANAJENGA JAMII YA AINA GANI? TUNASEMA UCHUMI UNAKUWA, LAKINI TUNAWASAIDIAJE WATANZANIA? KWANINI MTU ATOKE NJE AMBAKO ANALAZIMISHWA KULIPA MSHAHARA WA KUFAA AJE KWETU NA TUMRUHUSU KUTUNYONYA?

  TUSIPOJIBU HAYA MASWALI KWA UHAKIKA NA UJASIRI LEO, TUTAJIBU KWA MATATIZO MAKUBWA SIKU ZA USONI.

  ReplyDelete
 3. AnonymousJune 07, 2007

  we sugu na ma prodyuza wako,hivyo vichupi vya nini kwenye tangazo.ndo tuseme.....?

  ReplyDelete
 4. AnonymousJune 07, 2007

  Sir Issa MIMI NITAKUWEPO KAMA KAWAIDA.."..SUGU FANYA MAMBOOO KAMA WEWE ANON HAPO JUU ACHAWIVU KWASABABU BONGO HAKUNA "...PRISKRIPTION..." YA BANGI."..I WISH SUGU ANGEZUNGUKA STATE NYINGINE ZAIDI.."

  ReplyDelete
 5. AnonymousJune 08, 2007

  Vandumweh! Huyu si alishawahi kutangazaga kwamba ameachan na kupafomu muziki, atabaki tu kuwa prodyuza sijui! Sasa imekuwaje tena?
  Watu wengine mbona vigeugeu namna hii!?!

  ReplyDelete
 6. AnonymousJune 09, 2007

  Kwakweli bongo hatujipendi: yaani tunajiruhusu kulipwa mishahara mbuzi wakati tunajua kabisa kwamba ni ya kinyonyaji?

  Namuunga mkono muandishi hapo juu, kwanini haya makampuni yanapata faida zaidi siku hizi kutoka kwetu sisi maskini?. Wanaita emerging markets, huko ndio kuna pesa, and yet wanatulipa mishahaa ya ajabu, ina maana sisi ndio tunawapa faida....THINK, THINK, THINK MAN!

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...