WTM Press Release : 06 June 2007

This is to inform the general public that with effect from 6th June 2007, WTM UTILITY SERVICES has been granted a licence to operate on all ports of the United Kingdom i.e Tilbury , Sheerness, Felixstowe, Southampton.
Our new Inspection Office at the port of TILBURY is :
UNIT 7A TILBURY DOCKS INDUSTRIAL ESTATE
TILBURY,
ESSEX. UK
RM18 7HB

Our Administration office still remains at
UNIT 1A ,
Maybells Commercial Estate, Off A13
Barking/ Dagenham, Essex ,UK
IG11 0TT

*Please note, We must be notified 3 days before the vehicle arrives at the port to arrange for inspection.

*Inspection fees must be paid in advance

*Proof of ownership is required ORIGINAL LOG BOOKS and SHIPPING NOTES are required (no photocopies) to avoid further delays.

* Failure to present the documents will result in non Inspection of your vehicle. This is a
LEGAL SECURITY REQUIREMENT as we need to know the status of the vehicle.
An additional charge for lack of documents and other fees will be levied to the vehicle owner.

For and on behalf on WTM Utility services.
Mr. Chande Kondo
Operation Manager
WTM Utility Services
http://www.wtmutilityservices.com/index.php

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2007

    Nyie huko mgome au myasafirishe hayo magari kupitia bandari za Kenya halafu muyaingize from there tuone watafanya nini...

    Juat my idea

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2007

    UK mshikamano uwe huo huo la sivyo mgome

    Halafu wanamuelezea nani kwenye website yao. Wanazania watu wote wanasoma habari kwenye net...

    Watu wataangalia information on a directory

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2007

    Now wameona ulaji unakuja na kwenda kuinspect hayo magari na kufanya secretarial duties hawataweza tena...Yaani walikua hawana hawa watu kabla ya kupewa zabuni

    Hivi hiyo experience wanayo au basi vifaa vikiwako basi watafanya kazi kwa ki %%%&&&$

    Hii kazi inanipa utata.

    I am very disapointed for really. badala ya 45 keli mtu alipe 100 tanzania nyie viongozi machozi yetu msiyachezee

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2007

    Watanzania wa UK msitie shaka, kama serikali haita withdraw huu upuuzi wake ni kama vile wamesema watanzania sasa basi kuingiza magari kutoka uingereza. Mi nilikuwa nina mpango huo lakini wallah nimeahirisha kupeleka gari naliuza halafu naagiza kitu japan, kama hao utility watakuwa na japan sawa.

    Hawa wapuuzi tu wanataka kuchezea watu akili, yaani hesabuni maumivu na hela yenu mlihonga haitarudi mpaka miaka 20 ipite ndio mtaanza pata faida.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2007

    yaaani hata kizungu ni cha shida kweli tumeliwa. Maana naona Operation Manager na sio Operations haya basi tusamehe hilo eti For and behalf on hahahahahahahaha!!! Bwana wee ni for and behalf of!!!!!!! sasa tuibieni salama nyie wajanjaa lakini jasho la mwanadamu haliendi bure.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2007

    NASHANGAZWA SANA NA PRESS RELEASE YA WTM UTILITY WALIYOTOA KUPITIA KWENYE BLOG HII YA MICHUZI.
    NAJUA ITAKUA IMEPITISHWA BURE NA BILA KUTUMIA SENTI MOJA.
    KWANZA KABISA KIU YANGU NA WABONGO WENGINE WAISHIO HUKU, TULITARAJI LILE DUKUDUKU LILILOTUKABA MUDA KUHUSU UHALALI WA BIASHARA HIYO NA VIKWAZO VYAKE, VINGEPATIWA MAJIBU YA KURIDHISHA ILI KUONDOA MIGONGANO ISIYO NA MSINGI.
    KWA UTARATIBU WA KIBIASHARA, WANANCHI AMBAO WANALAZIMISHWA KUTUMIA HUDUMA HIYO, WANAYO HAKI YA KUTAMBUA VIGEZO VILIVYOTUMIKA KUHALALISHA BIASHARA HIYO NA KUVIWEKA PEMBENI VITUO VYA UKAGUZI WA MAGARI HAPO UK.
    SI VIBAYA KWA MZAWA KUWA NA BIASHARA KAMA HIYO LAKINI NI VYEMA PIA TUNAOLAZIMISHWA KUTUMIA CHOMBO HICHO,(CHA WTM) TUKAFAFANULIWA KWA KINA FAIDA NA MADHARA YAKE BADALA YA KUTOA PRESS RELEASE ILIYO NA VITISHO NA FAINI ZA JUU.
    VITUO VILIVYOTAJWA HAPO JUU VYA SOUTHAMPTON NA VINGINEVYO NI VYA USAFIRISHAJI WA NJIA YA MELI, JE WANAOSAFIRISHA KWA NDEGE (NDANI YA KONTENA) WATAFANYIWA UKAGUZI WAO WAPI?
    JE TAARIFA ZA KUKAGUA MAGARI YAENDAYO BONGO, IMEWAFIKIA NA MAWAKALA WENGINE AMBAO HUSAFIRISHA MAGARI YETU? NA KAMA NI HIVYO, CHAJI YA UKAGUZI INAPASWA ILIPWE KWA NANI? KWENU AU KWA WAKALA WANGU AMBAYE HUPELEKA MIZIGO YANGU AIRPORT KWA USAFIRISHAJI?
    NILIJARIBU KUONGEA NA MMOJA KATI YA MAWAKALA WANAOSAFIRISHA MIZIGO YANGU MARA KWA MARA KWENDA BONGO AKADAI KUWA HANA TAARIFA NA WALA HAITAMBUI KAMPUNI YENU.
    HAMUONI KUFANYA HIVYO NI KAMA KUJITIA MATATIZONI KWA KUFANYA BIASHARA YA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA NGUVU?
    KAMA KWELI BIASHARA YAO INAKUBALIKA NA WANATAKA KUWATANGAZIA WABONGO WOTE WAISHIO UK, KWA NINI WASITUMIE VYOMBO VYA HABARI KAMA ITV, CHANNEL 4, CHANNEL 5 NA MAGAZETI YA THE SUN, DAILY MAIL NA MENGINE AMBAYO YANASOMWA NA WENGI.
    KWA JINSI WANAVYOJIELEZA WAO NI KWAMBA BIASHARA HIYO ILISHAANZA MAY 26, 2007. NIAJE IBADILISHWE NA KUANZA JUNI 6, 2007?
    KWA KAWAIDA TAARIFA KAMA HIZO MUHIMU WANANCHI HUPEWA ANGALAU MIEZI MIWILI, MITATU ILI KAMA KUNA UTATA WOWOTE UTAOJITOKEZA UWEZE KUREKEBISHWA.
    VIPI PRESS RELEASE ITOLEWE JUNI 8, WAKATI UTARATIBU TAYARI UMESHAANZA SIKU MBILI KABLA; YAANI JUNI 6?
    KWA VILE SUALA LA USAFIRISHAJI MAGARI HALIWAGUSI WABONGO WAISHIO HUKU, PIA KUNA WAINGEREZA WANAOTAKA
    KUSAFIRISHA MAGARI HUKO BONGO UKIWEMO UBALOZI WAO, JE WANAYO TAARIFA YA KUKAGILIWA MAGARI NA WTM UTILITY KABLA HAWAJAPELEKA HUKO?
    KAMA TUTAKUWA TUNAENDESHA BIASHARA KIENYEJI KAMA HII YA WTM UTILITY, KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA VYOMBO VYA DOLA KUINGILIA KATI NA KUANGALIA UHALALI WA KIBIASHARA (BIASHARA HURIA) WA CHOMBO HICHO.
    HII INAWEZA KUSABABISHA UKIRITIMBA SIYO TU KWENYE MAGARI, PIA UTAINGIA KATIKA NYANJA NYINGINE KAMA YA KUSAFIRISHA NGUO, VIATU, MASHINE NA VITU VINGINE.
    NASEMA HIVYO KWA SABABU WTM WAMESHADAI WAMETUMIA FEDHA NYINGI KUANZISHA BIASHARA HIYO. SIDHANI KAMA WALIPATA WASHAURI WAZURI WA KUELEZA MADHARA NA FAIDA YAKE KWA INAONYESHA DHAHIRI WAMEINGIA KWENYE SHIMO LINALOKALIWA NA CHATU!
    TUNGEFURAHI SANA KAMA MNGEJIBU MASWALI YA WANANCHI YALIYOULIZWA MWEZI ULIOPITA. HII INAONYESHA JINSI GANI MLIVYO VIBURI, WAKAIDI NA MSIOTAKA KUSAHIHISHWA. MSIPOANGALIA MTAPELEKA MAGARI YENU YENYEWE NA KUAMBULIA HASARA MWAKA HUU.
    WATU KUFANYA MGOMO NI KITU KIDOGO SANA. HAKUNA KUTUMA GARI NA UONE UTAPATA NINI.....MANYANG'AU NYIE

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2007

    Duh, hawa jamaa wa WTM ni wasanii tu, na hasa huyu jamaa Chande mie nafahamu kwamba jamaa ni msanii. Sasa ndugu zangu wa UK, mbinu hapo ni moja tu. Ukitaka kupeleka kijigari chako bongo pitisha Mombasa kwa watani zetu wa jadi halafu ingizia Namanga. Walahi jamaa wameula wa chuya, kwa sababu watabakia ofisi wazi wakati hakuna deal zinazoendelea. Pumbuwasha wakubwa nyie.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2007

    Your Excellency President Jakaya Kikwete, please put a stop to this TBS/WTM nonsense!Otherwise tell TBS to appoint agents in Iceland,Honduras,Papua New guinea,Kazakhstan,Bhutan and The Maldives. There also Tanzanians there wishing to export cars to Tanzania,aren't there?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 08, 2007

    wallah inauma wallah! hivi hivi mtu unaibiwa,tena in the Governments name? haki kweli?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2007

    Hawa watu walizania itakuwa simple sana kwa vile wabongo ni Yes sir people all the time.

    Time has changed

    Wao ndio walikua wanafanya uagenty wa kuingiziwa magari bongo. Walikua wanashughulikia papers zote sasa naona kwa nini tusikamue na hii MOT pia.

    1. wanaotumia airways wao watakaguliwa na nani?

    2. Watu ambao hawasomei Michuzi blog watapata habari wapi?

    3. Kwanini mambo yameanza kabla ya press release.

    4. Reasonable time kwa watu kuelewa nini kinatakiwa ni miezi mitatu...wao wametoa api.

    5. Je mtu yeyote anayeishi UK akipiga simu ubalozini kuomba viza ya bongo na kutaka kupeleka used car lake bongo hii habari wanayo. Je mtu huyu ataambiwa kacheck gari lake kwao?

    Wameaona walala hoi ndio wananunua use cars sasa wanataka wachukue jasho lao lote.

    Kama wanauhalali kwa nini hawajibu shutuma zote? Si wametoa maelezo humu basi wangekuja kujibu mambo yao humu humu kwenye blog

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2007

    Kwanza niwaambie kitu sijui nyie hukou kwenu lakini huku USA kipeleka container Mombasa ni cheper kuliko kupeleka Dar Es Salaam. na hata Ticket ya ndege JFK to Nairobi na JFK to Dar ..cheaper ni kupitia Kenya...

    Fungueni macho na muwe wajanja...

    Penny uliyoitolea jasho sio mchezo mtu akiichukua tu hivi hivi...

    Niulizeni mimi mara ya mwisho kushukia Dar airport ni 1999...Japo saa nyingine na save dola 250 to 300 lakini it is something

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2007

    napenda kutoa pongezi kwa wakereketwa wenzangu, kwa kulipiga vita hili swala, lakini angalieni na mnapotoa malalamiko yenu kwani hapo hapo ndipo mnapowapa "Idea" na mbinu za kujiimarisha zaidi, cha muhimu naona watu tushikamane na kulipeleka hili jambo mahakamani kusitisha hilo zoezi zima, tunaomba chama cha watanzania waishio uingereza chini ya mwenyekiti wao Abuu Faraji kulipeleka swala hili mahamani.

    Asanteni wakereketwa wenzangu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2007

    hii press release imetolewa wapi officially? na hivi hili zoezi limepitia bungeni na wabunge wamelikubali? Jee wahusika watanzania walio nje na nyumbani walipewa habari tu au walishirikishwa? Jee serikali walisikiliza opinion za wananchi? mbona mambo nchi yetu bado yanaendeshwa kisultani-sultani tu? ni faida ya kuwa na bunge?
    Rushwa inanuka tena iko dhahiri, kweli tutafika mwendo huu?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 09, 2007

    ANONYMOUS WA June 8, 2007 5:27:00 PM EAT, UMEELEZA MAMBO MENGI KWA UFASAHA, HWA JAMAA LICHA YA KUWA NA VIBURI NA MAFISADI, PIA WANA MAPUNGUFU YA UELEWO WA TARATIBU ZA BIASHARA YA KUHUDUMIA JUMUIYA.

    WATU MBALIMBALI HAPA UK KWA NYAKATI TOFAUTI WAMEONGEA NAO KWA SIMU NA KWA KUKUTANA, LAKINI HAWAONEKANI KUJIBU HATA HOJA MOJA KWENYE PRESS RELEASE YAO KIMSINGI.

    KAMA SIO MALIMBUKENI NI NINI KUSEMA KWAMBA KAMPUNI INATOZA KIASI HICHO KWA UKAGUZI KWA VILE IMELIPA FEDHA NYINGI ILI KUPATA LESENI, SIO TATIZO LETU, SIJAONA LESENI INAKUA GHALI KATIKA MASWALA YA KULINDA MAZINGIRA YA TANZANIA, BASI TUSEME NIA NI KULINDA MAZINGIRA YA TANZANIA BALI NI KUIINGIZIA TBS NA WTM HELA KIBAO.

    UKWELI NI KWAMBA, JAMAA WA WTM WAMETUMIA HELA NYINGI KUHONGA ILI KUPATA HICHI KIBALI CHA KUKAGUA MAGARI, KWANI SIONI SABABU ILIYOWEZA FANYA KAMPUNI KAMA YENU KUWEZA KUPEWA KIBALI, HAMNA HISTORIA YA UTENGENEZAJI NA UKAGUZI WA MAGARI, HAMNA CAPITAL BOTH HUMAN AND FINANCIAL KUWEZA KUWA NA WIGO MKUBWA KWA NCHI NZIMA HADI IRELAND.

    MAMA ALIKUWA NAIBU MKURUGENZI, MKAGUZI MKUU NI WA NYUMBANI, WAKAGUZI WALILIPIWA HELA KUJA KUANGALIA WAKATI FUNGU LILITAKIWA LITOKE TBS KWENYEWE, LAPTOPS WALIZONUNULIWA WATU WA TBS WALIOKUJA HAPA LONDON N.K NDIO SABABU KUBWA YA NINYI KUPEWA CONTRACT!

    NAONA TAYARI MNA OPERATIONS MANAGER, SASA ITABIDI PIA MTAFUTE PUBLIC RELATIONS MANAGER, LABDA ANAWEZA KUWASAIDIA KIDOGO KATIKA KUELEZEA KWA WAKEREKETWA MAMBO YANAYOWASIBU KUHUSIANA NA HILI DEAL LENU........

    UKITAKA KUJUA HAWA JAMAA NI MBUMBU KIASI GANI, KUNA MDAU AMBAYE AMESEMA ALIONGEA NAO NA KUWAAMBIA KWAMBA KISHERIA MTU ANAWEZA KUPELEKA GARI LAKE BONGO BILA YA KUFANYA HUO UKAGUZI NA ASITOZWE FAINI YEYOTE ILE KWA MADAI KWAMBA TAARIFA YA UKAGUZI HAJAPATA, KWANI HAWAJATOA TAARIFA KWENYE GAZETI LOLOTE LINALOJULIKANA HAPA UINGEREZA ISPOKUWA BLOGU YA MICHUZI BONGO NA TOVUTI YA ABU FARAJI UK.

    CHA AJABU NI KWAMBA MPAKA LEO HAKIJAFANYIKA.......

    WEZI WAKUBWA NYIE.......

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 11, 2007

    JAMANI MSIPATE TAABU TUMENI MALALAMIKO YENU KWA RAISI WA TANZANIA.

    WWW.JAKAYAKIKWETE.COM
    AU CHUKUA LINK HII
    http://www.jakayakikwete.com/tanzania/pages/Ask-the-President

    TUSIKUBALI JAMANIIIII.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...