
kuna mdau ambaye sasa hivi kaniletea usongo huu....
MICHU,
KAMA UNAVYOKEREKA NA TATIZO LA MAHANDAKI NA MINYORORO, NDIVYO INAVYOTUGUSA WOTE. MATATIZO HAYA MAWILI YANAHUSIANA SANA NA NI VIGUMU KUYATENGANISHA.
CHANZO HASA NI NINI?.
1 KUCHANGANYA SIASA NA UTAALAM
2 KUTOWAJIBIKA KWA WATENDAJI
3 SHERIA HAFIFU ZA MATUMIZI YA BARABARAMAAMUZI MENGI YANAYOHUSU MIPANGO MIJI YANAFNYWA NA WANASIASA ZAIDI KULIKO WATAALAM,LICHA YA UKWELI KUWA TUNAO WATAALAM WENYE UWEZO WA KUFANYA HIVYO.
MAJIBU YA HOJA ZA KITAALAM HUISHIA KATIKA KAULI MASHUHURI 'HATUNA FUNGU' HATA KAMA ZIPO LAKINI ZINAELEKEZWA KATIKA SEMINA ENDELEVU NA PEVU.
TUNAO WABUNGE AMBAO POSHO ZAO ZINAPANDA KILA UCHAO, WAKUU WA MIKOA NA WILAYA NA MAMEYA, LAKINI HAKUNA HATA MMOJA ANAYESHUGHULISHA KICHWA CHAKE KUANGALIA NINI KERO ZA WANANCHI. WAO NI WAANDAJI WA ZIARA ZA VIONGOZI. HAWA NDIO CHANZO CHA MATATIZO. HAKUNA DEREVA ATAKAYETUMBUKIZA BALOON LAKE KATIKA SHIMO LA ASKARI MONUMENT NA KWINGINEKO, MATOKEO YAKE MWENDO WA MAGARI UNAKUWA NI WA KUSINDIKIZA HARUSI.
SWALI HAPA NI KUWA HIVI KONOIKE WANATUMIA WATAALAM KUJENGA LAMI VIPI LAMI HIYO HIYO IZIBWE NA VIBARUA KWA MCHANGA, JIBU NI RAHISI MHANDISI AMEAGIZWA ATIE KIFUSI NA MWANASIASA AU BARAZA LA MADIWANI! MAEGESHO YA DALA DALA KATIKATI YA BARABARA YANAJULIKANA HATA KWA POLISI, NA HASA NDIO CHANZO CHA FOLENI HASA RUSH HOURS LAKINI INAOKENA IMA POLISI HAWAJUI AU WANAJUA ILA KAUZEMBE TU KAMETAWALA. MUHIMU KWAO NI KUZUIA MAGARI VIONGOZI WAPITE.
HIVI MKUU WA KITENGO CHA USALAMA BARABRANI HAJUI HILI AU HALIONI NA YEYE ANAISHI WAPI. KAMA HAWEZI KULITATUA ANAFANYA KAZI GANI ZAIDI YA KUTOA TAKWIMU ZA AJALI KWA SIKU. BARA BARA ALIZOJENGA MKOLONI NI ZILE ZILE KAMA SAMORA N.K. MJI WAKATI HUO UNA WATU LAKI 6, SASA NI MILLION 5 UNATEGEMEA NINI.KULUNDIKANA OFISI SEHEMU MOJA. WIZARA ZOTE ZIPO DOWNTOWN, KANA KWAMBA ZIKITAWANYWA HAZITAFANYA KAZI. KWANI KUNA SHIDA GANI WIZARA, KAMA MIFUGO ILIYOPO TEMEKE, NA ILE YA AFYA, UJENZI N.K ZIKATWANYWA KATIKA MANISPAA ILI WATU WASIELEKEE SEHEMU MOJA KILA MARA.
LAKINI LA MUHIMU HAPA NI KUWA MEYA ANAFANYA NINI KATIKA JIJI LAKE MAANA YEYE NDIYE 'CITY FATHER' KAMA HAPANGI NYUMBA YAKE VIZURI NANI AMSAIDIE.? HIVI BAJETI YA JIJI KUHUSU MAPATO NA MATUMIZI MBONA HAIWEKWI WAZI, IL HALI TUKIJUA KUWA CITY INAKUSANYA MABALION SASA, NINI MCHANGANUO WA PESA HIZO ILI TUJUE ZINATUMIKAJE. MFANO ZILE KODI ZA BIASHARA, MATANGAZO, MAEGESHO, STENDI N.K ZINAFANYA KAZI GANI BAADA YA KUNUA SHANGINGI LA MEYA NA MAJOHO YA MADIWANI PAMOJA POSHO.
WAKATI MAMEYA WA MAJIJI KAMA MADRID,TOKYO WAKIFIKIRIA MIJI YAO INAJIANDAA VIPI KWA OFFER YA OLYMPIC 2016,SISI MEYA WETU AMESHINDWA KUSIMAMIA UZIBAJI WA VIRAKA NA MINYORORO YA MAGARI.
WAKATI MAMEYA WA CAPE TOWN, LONDON,DELHI, NEW YORK WAKIAGIZA SERIKALI ZAO ZIFANYE NINI,WAKWETU ANAFUNDISHWA KUFUNGA TAA ZA BARABARANI, NI KWA MANTIKI GANI JIJI LISIWE NA VURUGU !!!!!
KIFANYKE NINI.
1 WATAALAM WAPEWE NGUVU ZA KIUTENDAJI NA SIO WANASIASA KAMA MADIWANI.
2 WANANCHI WAWAWEKE KITIMOTO WAWAKILISHI WAO WATOE MAJIBU YA TATIZO
3 SERIKALI FUTA HALMASHAURI YA JIJI,WEKA TIMU YENYE KUFIKIRI4 JIJI LIWEKE WAZI MATUMIZI NA MAPATO NA MIPANGO YAKE
5 JESHI LA POLISI'TRAFIKI' LIFUMULIWE NA LIATAKLOUNDA LIPEWE MALENGO KWA MUDA FULANI
6 PANUA BARA BARA NA IMARISHA ZILE ZA KUINGIA NJIA KUU
7 TAWANYA OFISI HASA ZA SERIKALI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA UELEKEO.
8 SHERIA ZA MATUMIZI YA BARABARA ZIWE KALI SANA
9 MAJENGO YA GHOROFA YAWE NA MAEGESHO FLOOR YA CHINI KUEPUKA WATU KU EGESHA MAGARI BARABARANI, ANGALIA KARIAKOO KWA MFANO TU.
KIMITO.
BARUA YA WAZI KWA MICHUZI
ReplyDeleteTUNAKUBALI MICHUZI NA JITIHADA ZAKO HIZI ZA KUYALIDIA DIP MAHANDAKI BONGO.
LAKINI HII YOTE UNAFANYA HIVYO ILI KULIPIZA GHARAMA ULIZOTOZWA KWENYE GEREJI BAADA YA KUVUNJA SASPESHENI YA GARI YAKO ULIVYOKUWA UNATOKA HARUSINI USIKU UKIWA MBWIII.
SI VIBAYA UKAENDELEZA LIBENEKE KWENYE KAMPUNI BUBU YA WTM UTILITY AMBAYO INAFANYA SHUGHULI ZAKE ZA KUJIINGIZIA PAUNDI ZA WABONGO KIMABAVU.
KWA MUDA MREFU SASA WA TZ WAISHIO UK WAMEKUWA WAKILALAMIKA NA PIA KUOMBA MSAADA WAKO IKIWA NI PAMOJA NA KUWAULIZA (TANZANIA BUREAU STANDARD) TBS UHALALISHAJI WA KIBALI CHA UKAGUZI WA MAGARI KWA WTM PEKE YAKE HAPO UK.
NIA NA MADHUMUNI YA KUTAKA KUPATA TAARIFA NI KUONDOA UTATA UNAOWAGUSA WENGI...NASEMA WENGI IKIWA NI PAMOJA NA WASIO WATANZANIA AMBAO WANATAKA KUITUMIA HIYO WTM UTILITY KUPELEKA MAGARI YAO BONGO.
AJABU NI KWAMBA, LICHA YA KUPIGIWA DEBE NA WABONGO JUU YA SUALA HILI, WEWE UMEKUWA UKIZIPA KIPA UMBELE TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE) ZA WTM UTILITY NA KUPUUZA MAONI YA WENGI.
LAITI KAMA WALIKUWA WANATAKA KUTOA TAARIFA YAO KUPITIA KWENYE VYOMBO VYA HABARI, JE WAMETUMIA MAGAZETI GANI NA MANGAPI KUCHAPISHA TAARIFA YAO?
KWA VILE SHUGHULI ZAO ZINAENDESHWA KIMATAIFA (KWA VILE INAWAGUSA NA WANA UK WENYEWE), WAMEITOA KWENYE CHOMBO CHOCHOTE KILE AU KWENDA HATA BBC BREAKFAST, THIS MORNING (ITV) KUWAPASHA WAZUNGU NA WENGINE JUU YA UTARATIBU HUO MPYA?
KAMA KWELI BIASHARA HIYO SI HARAMU NA IMEBARIKIWA KWA MIKONO YOTE MIWILI NA SERIKALI YA JK, KWA NINI WAWE NA HOFU KUTOA TAMKO LAO KWENYE VYOMBO VYA HABARI VYA TAIFA AMBAVYO HAVITAWAGHARIMU HATA PENI MOJA?
LICHA YA KUTUMIA VYOMBO VYA UK KUWAPASHA HABARI HIZO MUHIMU, JE WTM UTILITY WAMETUMIA VYOMBO VYA HABARI TZ, KAMA UHURU, NIPASHE, RAI, MTANZANIA N.K ILI NDUGU NA JAMAA WANYE NDUGU ZAO WA TZ WAWEZE KUWAPA TAARIFA WATUMAO MAGARI KUTOKA UK JUU YA UTARATIBU HUU MPYA?
HIVI MAJUZI ULIENDA KWENYE MKUTANO WA WAHARIRI NA JK KULE IKULU, JE UKIWA MMOJA WALIOHUDHURIA ULITUMIA NAFASI HIYO KUHOJI UHALALI NA UTARATIBU WA WTM UTILITY MBELE YA KIKWETE?
NASEMA HIVYO KWA SABABU, MICHUZI UNAYO HAKI KAMA WALIYONAYO WT-WA UK WA KUTAKA KUJUA HILO LAKINI KAMA UNAJIHUSISHA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, LAZIMA UTASHIKWA NA KIGUGUMIZI NA KUONA KUFANYA HIVYO UTAJIHARIBIA!!
KAMA SUALA LA KUPEWA ZAWADI, IDADI YA WANA-BLOG WANAOTEMBELEA HUMU, WANAWEZA KUCHANGA NA KUZIDI MARA KUMI YA ZAWADI UTAKAYOPEWA NA WTM UTILITY ILI KURIDHISHA MATAKWA YAO.
MIMI NINA IMANI KABISA KUNA WATU WANAOCHANGIA MADA KWENYE BLOG HII, WANAWEZA KUJITUTUMUA NA KUKUTUMIA TIKETI YA NDEGE, MALAZI NA CHAKULA ILI UJE UJIONEE MWENYEWE JINSI GANI NA MAKAMPUNI MANGAPI YANAYOJIHUSISHA NA UKAGUZI WA MAGARI KWA BEI NAFUU KULIKO YA WTM.
NAWEZA NIKAWA NAONGEA PUMBA, LAKINI KWA JINSI WA-TZ WALIVYOCHOKA HIVI SASA NA WIZI WA KIMACHOMACHO, KUKUCHANGIA WEWE PAUNDI 10 KILA MMOJA KUJA UK, HAWAONI SHIDA ILI MRADI WEZI WA JASHO LA WANANCHI LAZIMA WAKABWE NA WAKOME.
KWA HIYO, KWA NIABA YANGU BINAFSI NINGEKUSHAURI UTUSAIDIE KWENDA TBS, WIZARA YA MIUNDO MBINU, UBALOZO WA UK-TZ UTUPATIE MAJIBU KAMA YALE YA POSTA, MUSTAFA HASSANALI NA WENGINE WALIOJITOSA NA KUJIBU HOJA ZAO.
NA UKIWEZA CHUNGULIA KWENYE TOVUTI VOSA-UK UONE SHERIA, GHARAMA NA UTARATIBU WA KUKAGUA MAGARI HAPO UK.
NATUMAI WARAKA HUU UTAKUAMSHA USINGIZINI NA KUKUTOA KWENYE HOJA YA MAHANDAKI DAR NA KUHAMIA WTM UTILITY...AHSANTE......MKEREKETWA MOHAMMED ABDULLAH MOHAMMED
mzee tupe latest morogoro
ReplyDeleteor highlight kati ya chipolopolo na taifa stars
HIVI HUYO MEYA WA JIJI ANAPOSAFIRI MARA KWA MARA KWENDA NCHI ZA NJE ANAENDA KUJIFUNZA NINI?KAMA JAMAA ALIVYOSEMA NI KUWATIMUA WOTE,HELA KWA JIJI LA DAR ZIPO,HIVI HAWA VIONGOZI WETU NINI WANAWEZA KUFANYA KWELI?
ReplyDeleteMimi siamini kama mheshimiwa meya anaujuzi wowote wa masuala ya majiji, hawa mabwana wanachaguana kwakuzingatia uzawa(wa dar) zaidi ya utaalam,kumbukeni mheshimiwa Charles Keenja alipokuwa anaoongoza ile kamati yake,mji ulibadilika na mambo yalikuwa makini zaidi, leo huyu mwinyi!? taa za barabarani tu zinamshinda!aibu tupu!
ReplyDeleteHAWA VIONGOZI NINI KWELI WANAWEZA KUFANYA?NI SWALA LA AIBU SANA KWA SISI WADAU KUKAA NA KUJADIRI SWALA KAMA HILI LA MASHIMO WAKATI TANZANIA IMEZUNGUKWA NA MATATIZO LULUKI,NAJUA NI KERO KWA WANANCHI KUPITA KWENYE HAYO MAANDAKI KILA SIKU LAKINI HAWA VIONGOZI KATIKA KARNE HII YA 21 WANASHINDWA KUTATUA SWALA HILI,HIYO NCHI INAKERA SANA!NI WAPI TUNAKWENDA? SIJUI HUKO HOSPITALI KUKOJE,MASHULE VIJIJINI,BARABARA ZA VIJIJINI SIJUI ZIKO KWENYE HALI GANI,KWELI BONGO INAENDESHWA KISANII!!
ReplyDeleteukiona hivyo ujuwe tumefungwa, kwa nn michuzi hutaki kutupa matokeo kati ya Tanzania na zambia ?
ReplyDeletetwambiye tu
ReplyDeleteHivi kweli mtu anaenda nyumbani akisema ametatua hilo tatizo hapo ?Kama si utani ni nini? Kuja kuweka udongo kwenye shimo ni kutengeneza au kuchafua ?Kesho mvua ikinyesha hapo unajua kutakuwa na hali gani ?
ReplyDeleteTatizo letu sisi tumezidhisha dharau hata kwenye mambo ya msingi,na hamna mtu wa kuwafanya waheshimiwa wawajibike.Sijui ni mtaalamu gani aliyefanya kazi hiyo,na sijui elimu yake ni nini hasa,maana inabidi sasa tuanze kuulizana our level of competenti !!