jk alizungumzia kirefu masuala ya elimu ambapo alitoa masikitiko yake dhidi ya mimba na utoro wa wanafunzi. akasisitiza kwamba juhudi zinafanywa kukabiriana na hilo na kwamba sasa hata zile sehemu sugu zimeanza kupata mafanikio. aliwataka ma-dc kuwa wakali sana kwa hilo. vile vile akijibu juu ya elimu bora badala ya bora elimu kwa wengi alisema kwa sasa ujenzi wa madarasa pamoja na kuingiza darasani watoto wengi unaenda sambamba na uboreshwaji wa elimu ambapo vyuo vya mkwawa iringa na chang'ombe dar vimepewa hadhi ya chuo kikuu ili kukabiriana na tatizo la ubora wa elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2007

    ni wakati umefika kuwa wazi kwa wanafunzi kuhusu matumizi ya condom,mtawaficha mpaka lini wakati ngono wanafanya tuwe wazi ama sivyo hatutatatua tatizo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2007

    Hivi tanzania kuna polling system ya kurate kazi ya kiongozi .....akiw madarakani kwa kipindi fulani...USA wanamrate bush kila siku...na kila jambo analolifanya wanarate na kuweka matkeo hadharani

    na hata halmashauri kuu inaruhusiw akuhave a vote of confidence or no confidence...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2007

    Nchi hii Wasomi wengi wamejazana katika sehemu ambazo zinaleta umaskini kwao na kwa watanzania.

    Elimu inabidi ipambane na Mazingira.Tanzania elimu hiyo hatuna ya kutosha.

    Sehemu kubwa ya wasomi wetu wamejazana katika sekta ambayo ijulikanayo kitaalamu kama sekta ya kuandika (WRITTING SECTOR). Sekta ambayo kwa sehemu kubwa inatumia kalamu,peni,komputa, makaratasi katika utendaji wa kazi za kila siku.

    Hakuna nchi yoyote duniani ambayo imeedelea kwa kutegemea sekta ya kuandika.Mjapani mmoja aliwahi kuniuliza akasema karibu kila duka ninalopita miotaani huwa linauza peni za kuandikia hivi watanzania huwa mnaandika nini? Inaonyesha peni ni bidhaa muhimu sana hapa kwenu!Kuna waandishi wengi sana wenye vitu vingi sana vya kuandika!!!

    Mazingira yetu ni ya Kilimo,Ufugaji,,Madini na Biashara.Ungetarajia wasomi wengi wawe wamejazana katika fani hizo na vyuo na shule zetu zijazane katika mkondo huo.Lakini wengi wa wasomi wamejazaana katika digrii za Sanaa.Bachelor/Masters etc of Arts akiwemo Raisi wetu.Na arts ni sanaa na anaye-practice arts ni artist au msanii.Kwa hiyo nchi yetu imejaa wasanii wengi sana wanaotoka vyuo vikuu.

    Lakini utakuta Kilimo ambacho ndio kinaitwa uti wa mgongo wa Tanzania kinaendeshwa unaendeshwa na watu waliomaliza darasa la saba au ambao hawakusoma kabisa.

    Sasa kunakuwa na mgongano wa sera na vitendo. Nchi inasema inategemea kilimo hivyo ungetegemea mkazo uende huko wa kielimu lakini unakuta mkazo hauendi huko unakazia kuzalisha wasanii waliojaa digrii za sanaa.Nchi haiwezi endelea kwa kutegemea bachelor,Masters,au Doctors of arts.Nchi siyo sawa na chuo cha sanaa bagamoyo.

    Nyerere aliwahi kusema wasomi wakiingia katika kilimo, kilimo kitabadilika.Na kweli tumeanza kuona sekta kama za ufugaji kuku ambayo wasomi mijini wanaufanya kuna mabadiliko. Ilikuwa si rahisi kuona mtu akiwa anafuga kuku 1000 lakini sasa ni kitu cha kawaida.

    kwenye upande mwingine Mazingira yetu yana madini.Sasa ungetarajia ungetarajia kuona vyuo kibao vya madini hata vya VETA kama vile vya kufundisha kutengeneza vidani,n.k Lakini unakuta watu wanafundishwa umakenika wa magari ya Wajapani!!! (Import Oriented Education)na utengenezaji mashine za kutoka nje ya nchi!

    Matokeo yake madini tunayo elimu ya madini hatuna wala haipewi kipaumbele! Wakati madini ndiyo yako kwenye mazingira yetu na Elimu tupewayo ilistahili iwe ile ya kutusaidia kuyashughulikia mazingira ya madini ili tuondokane na umaskini.

    Biashara ni eneo lingine ambalo lingetiliwa mkazo lakini bahati mbaya Wafanyabiashara wengi wazawa ni darasa la saba na waliofeli sekondari.Wakati sekta hii ni pana na muhimu mno katika uchumi.

    Upande Wa Biashara umebakia mikononi mwa wahindi kwa kuwa wamegundua siri ya Kusoma.Hivyo wengi wao wamesomea biashara barabara ndiyo maana wanawashinda wafanyabiashra waswahili ambao kusoma wanaona kama kituo cha polisi. Kutwa wafanyabiashara wetu wanashinda kwa waganga wa kienyeji!

    Umaskini ni mkubwa Tanzania sababu elimu hii yetu ni mbovu sana haisaidii mtu apambane na mazingira.

    Mfano uuna Pamba kwenye mazingira yetu ungetarajia watu wengi wawe wamesomea mambo kilimo cha pamba,utengenezajinyuzi na nguo na mambo ya viwanda vidogo na vikubwa vya vitumiavyo pamba.Lakini unakuta elimu hiyo haipo watu wamekazana kuandika na mashule yanaendelea kuzalisha wasanii wa masomo ya arts.

    Nikiwa mkereketwa wa maendeleo ya nchi yangu naomba mfumo wa Elimu na mkazo wake ubadilike.Elimu Iwezeshe mtu kuwa na uwezo wa kupambana na mazingira na kuibuka toka kuwa maskini na kuwa tajiri.

    Na ili hili liwezekane elimu bora inayoshughulikia mazingira ni muhimu sana.

    Kama hatutawapa watu wetu elimu ya kuwasaidia kushughuklikia mazingira tutaendelea kuona wageni wakija wakichukua hizo fursa na sisi tutabaki tumetoa macho na kuishia kuwa maskini.

    Napendekeza wapanga sera badilisheni mfumo wa elimu ulenge hasa kwenye kilimo,ufugaji,Madini na Biashara,Na viwanda vidogovidogo vya bidhaa na mazao ya madini kama vidani n.k Tuwe na wakulima wengi wasomi badala ya kuwa na maafisa kilimo wengi wasomi.

    Ili nchi yetu iendelee haitoshi nchi kuwa na maofisa biashara wa serikali wengi wasomi bali nchi inahitaji wafanyabiashara wengi wasomi,pia nchi ili iendelee haihitaji tu maofisa wa madini wa serikali wengi wasomi bali inahitaji wachimba madini wengi wasomi.

    Hayo ndiyo maoni yangu. Wanakijiji mnaruhusiwa kutumia ninayoandika popote.Naona wengine wananiandikia kuomba ruksa kwenye mail yangu.

    Natoa ruksa ya jumla.Ukitaka kutumia makala zangu tumia tu popote upendapo.Niwe nakujua au sikujui ruksa.

    Asanteni


    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...