akijibu swali kuhusu tuhuma zinazomwandama rais mstaafu mh. bwm kwamba alijipatia mkopo akiwa madarakani, jk alisema hana hakika na hilo na kwamba si utaratibu mzuri sana kuwachunguza wastaafu wetu na kwamba likitokea lililo wazi na kubwa litachunguzwa. swali la yeye kujiingiza katika biashara aliweka wazi kwamba fani hiyo haiwezi na kwamba yeye atajishughulisha zaidi na ukulima na ufugaji na tayari ana shamba la mananasi huko kwao bagamoyo pamoja na mifugo. aligusia pia swala la mechi ya taifa staaz na senego amapo aliwapiga vijembe viongozi wa vilabu kwa kuwataka waweke maslahi ya vilabu mbele ya yao binfsi na kwamba timu ya taifa ni mahali ambapo mchezaji anakwenda akiwa tayari kaivishwa kilabuni kwake. aliweka wazi pia safari ya kwenda ghana bado ni ndefu na ngumu hivyo wabongo wasitegemee maajabu. ila alitoa rai kufanyike juhudi za makusudi kupata wachezaji watakaokwenda nje kucheza kuongeza maarifa na uzoefu kama senego ambao wachezaji wake wote ni wa kulipwa nje.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2007

    JAMANI HUYU MWANAUME NI MZURI SANA MIMI YAANI NAMUONEA WIVU SANA MKEO SIJALI UNAENDESHAJE NCHI MIMI WEWE TU UTAMU WA SURA YAKO HIS FIT,HAS GOT BRAIN IAM COMPLETELY SPEECHLESS FOR THIS MAN AGE DOESNT MATTER MWAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2007

    1.Interesting,how Jakaya doesn't want the press to investigate on Mkapa's shady dealings.Could it be because Kikwete is also involved in 'em?

    2.To the poster above,you need to get out more LOL.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2007

    Hongera Rais Kikwete kutoa jibu la Kuhusu mkapa na Mkopo wake.

    Muuliza swali alimtegeshea. Raisi angejibu kuwa analijua sekta nzima ya benki Tanzania ingeingia matatani.

    Angesema analijua. Swali lingekuwa taarifa za Mkapa kukopa kazitoa wapi yeye kama Raisi,Sababu kwa taratibu za uendeshaji mabenki (Duty of Secrecy) hayaruhusiwi kutoa siri ya mteja wake kwa yeyote awe mwandishi wa habari au Raisi.

    Raisi angetoa hizo taarifa kuwa anajua mabenki yalimkopesha Mkapa.Sekta ya benki ingeporomoka sababu watu wangeanza kuhamisha mapesa yao na kuyapeleka Uswisi n.k kwa kukosa imani ya utunzaji siri wa mabenki ya Tanzania.

    Kwa kuogopa kuwa hakuna siri za fedha na akaunti zao kwenye benki za Tanzania wateja wangeanza kutorosha fedha kwa kuzibadilisha haraka kwenye fedha za kigeni na kuzitorosha na kukimbiza kuweka nje ya nchi kwenye mabenki ya nje na nchi wanayoona yaweza tunza siri.

    Ghafla nchi ingejikuta ina upungufu wa hela za kigeni,na soko bubu la fedha za kigeni lingeibuka ghafla na fedha za kigeni zingeuzwa kwa bei kubwa na kufanya shilingi yetu iporomoke ghafla kwa kiwango cha kutisha kutokana na kuongezeka ghafla kwa mahitaji ya wahamishaji fedha ambao wangeenda kuchukua fedha za Tanzania kwa wingi kwenye mabenki kwenye akaunti zao na kwenda nazo mitaani kwenye soko bubu na kununua fedha za kigeni kwa wingi na kuzitoroshea nje ya nchi kuweka huko wanakoamini siri za wateja zinatunzwa.

    Pia lingeweza zuka tatizo lingine nalo ni kuwa kwa mabenki kuogopa wateja kuwakimbia kwa kutuhumiwa kuwa hayatunzi siri za wateja mabenki yangejikosha kwa kumjia juu Raisi Kikwete na kumkana kuwa hayahusiki na alichosema na kuwa yenyewe hayajampa taarifa za Mikopo ya Mkapa,sasa hapo Raisi angeonekana Mwongo mkubwa mbele ya wananchi kitu ambacho kingemwingiza matatizoni pia.Na angeonekana anamwandama Mkapa kwa kumwonea.Kitu ambacho kisiasa kingekuwa kibaya kwake.

    Pia Mkapa angeweza kuishitaki benki na Kikwete na kuwadai mabilioni kwa kuvunja kanuni ya duty of Secrecy ambayo mabenki dunia nzima yanatakiwa yaijali kwani hayaruhusiwi kumwaga siri za mteja kwa hovyo hovyo kwa waandishi na wanasiasa Raisi akiwemo.

    Baadhi ya Waandishi wetu wa habari ni waandishi uchwara.Huyo aliyesema Mkapa kakopa, Mkapa angekuwa hana huruma na anayetaka utajiri wa haraka angelifilisi hilo gazeti na kuchukua mali binafsi za hao waandishi wa habari kwa kuwapeleka mahakamani na kuwashtaki kwa kumchafulia jina.

    Hata sasa Mkapa akiwabana hao waandishi wa habari waeleze walikozitoa hizo habari watakwama tu.Benki zitawakana hao waandishi wa habari, sababu hakuna benki wala mfanyakazi wa benki aweza toa taarifa yoyote ya mteja kwa waandishi wa habari.Ni jambo lisilowezekana kabisa.Halipo na haliji kuwepo mwandishi kupata habari za mteja toka benki au mfanyakazi wa benki.

    Ikitokea Mfanyakazi wa benki akathubutu kutoa habari za mteja kwa mwandishi wa habari habari atafukuzwa kazi mara moja bila kukawia na bila maruprupu yoyote na aweza pia shitakiwa kwa kuihujumu benki kuifanya ionekane haitunzi siri za wateja ili waikimbie na kuvujisha trade secrets kwenye public.

    Benki ya NBC kupitia wanasheria wake imtafute huyo mfanyakazi aliyewapa waandishi wa habari taarifa za Mkapa kukopa atafutwe atimuliwe kazi ili kuiokoa benki isionekane kuwa haitunzi maadili ya benki.

    Njia ya kumpata huyo mfanyakazi ni kwa kumbana mwandishi wa habari aliyesema Mkapa kakopa abanwe aeleze chanzo cha hizo habari zake,akishindwa kudhibitisha au kuonyesha hicho chanzo yeye binafsi achukuliwe kuwa ndiye mwanzilishi na mpishi mkuu mwandamizi wa hayo majungu na ashitakiwe kwa kuchafua jina la benki na mteja wao Mheshimiwa Raisi mstaafu Mkapa na adaiwe hayo mabilioni kama fidia pamoja na kufilisi mali za gazeti na zake binafsi pengine ndiyo itasaidia kuwafanya waandishi wawe serious wanapoandika habari zao.

    Raisi Kikwete kusema hana taarifa ya Mkopo wa Mkapa kumemwokoa kwenye domo la mamba la waoteaji waliochomekea hilo swali kwa huyo mwandishi wa habari ili Raisi anyinyonge mwenyewe kwa mdomo wake.

    Waandishi chambueni habari vizuri kabla ya kuandika ili kuepusha madhara kwenu na wengine.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2007

    Koloboi,

    Mchanganuo wako ni mzuri, lakini si kweli kwamba benki hazitoi kabisa taarifa za wateja. Siku hizi ukifungua account utasainishwa form ya kuruhusu TBA (Tanzania Bankers Association) kutoa data za account yako kwa mtu au chombo watakachoridhia. Kwa ufupi serikali ikitaka kupata data za account yako haina kipingamizi.

    Same goes for the USA also, kupitia The Patriot Act. Bush akitaka kucheki account yako anywhere in the world anaweza kwa kigezo cha kupambana na ugaidi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2007

    Hakuna chombo duniani kinaweza toa taarifa ya mteja wa Benki bila document ya kimahakama au kisheria iwe TBA,George Bush,Kikwete au yeyote.Hata TBA haiwezi toa taarifa kwa waandishi wa habari au Rais kwa kisingizio eti yaweza mpa yeyote hakuna kitu cha aina hiyo koloboi yuko right.

    Hizo taasisi zote unazozosema zinapewa hizo taarifa,zinapewa si kwa ajili ya public au jounalists consumption Zinapewa kwa kusudi maalum na zikishapewa hazitakiwi kuzitoa kwa third party bila document za kisheria au mahakama.

    Wakitaka kugawa hizo taarifa waandishi wa habari na wanasiasa akiwemo Raisi hawako katika kundi la kupewa hizo taarifa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2007

    Salma kasafiri vipi? maana baba kawaida havai hivi na protocol je?

    Anon hapo juu yeah ni mzuri,men wakitanzania kwa ujumla ni wazuri na wajua mahaba lkn waswahili weeeeee acha tu hawashikiki. Shauri ako

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2007

    Koloboi umejinarrow yourself halafu unajifanya unajua sana kila kitu.
    Soma sana ili upate kujua na upande mwingine wa shilingi. "No research, No right to speak."
    Inawezekana kwa upande wa sekta ya benki hali ndo hivyo unavyosema, lakini sivyo ilivyo kwa upande wa sheria za makampuni.
    Fahamu kuwa taarifa zote hizo za mikopo ya kampuni huwa zinasajiliwa kwa Msajili wa Makapuni chini ya Sheria ya Makampuni. Na fahamu pia kuwa chini ya sheria hiyo taarifa zote za makampuni(isipokuwa correspondences) ni for public consumption. Any member of the public anaweza kupekua, kupata na hata kutoa nakala ya taarifa ya kampuni yoyote iliyoko kwa Msajili wa Makampuni, kwa kulipia fee iliyowekwa kisheria. Sasa una uhakika gani kama hawajazipata huko? Usiandike tu kabla hufanya research exaustivelly!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2007

    I agree fully with the above two commentetors. Proper channels should be followed to investigate the matter, this will eventually lead to all culprits, be it former presidents, bank managers or clerks...that is the rule of law, if there is any in Tz anyway. In my opiniojn I guess it is the rule of the jungle!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2007

    Kilichoandikwa na magazeti toka lilipoanza sakata hili kinasema Mkapa akopeshwa siyo kampuni yake yakopeshwa.

    Kisheria mtu na kampuni ni vitu viwili tofauti.Kisheria ukisema Mkapa kakopa na kampuni imekopa unaongelea vitu tofauti.

    Huyo koloboi alikuwa anaongelea kuhusu Mkapa na kusema Kuwa huwezi toa akaunti ya Mkapa na mambo ya Mkapa as individual kirahisi.

    Mimi binafsi naona koloboi yuko sahihi.Au wewe uliyefanya utafiti Sheria ya makampuni hukufanya utafiti usome hayo magazeti yaliyoandika huo mjadala yalichoandika.Nenda hata leo kasome kila gazeti uone yanaongelea individual au kampuni.
    Umejichimbia kwa msajili wa makampuni umesahau kwenda maktaba utafiti.Wewe ndiye hujui kitu.

    Na wewe hujafanya research ya yaliyoandikwa magazetini toka mwanzo so you also don`t have the right to speak.

    Magazeti yanaongelea Mkapa wewe unaongelea kampuni ambayo yeye ni mkurugenzi.Wewe umeibua topic ambayo ni new topic ambayo siyo kiini cha vyombo vya habari ambavyo wanaandika.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2007

    HUKO NI KUFICHIANA UOVU TU.TUMECHOKA NA MAELEZO YAKO KAMA UNAWAELEZEA WATU WASIOKWENDA SHULE.

    ULAYA MARAIS,MAWAZIRI WANACHUNGUZA WAKIWA MADARAKANI,SEMBUSE WAKISTAAFU.

    DONT TELL US RUBBISH.TUMEKUCHOKA WEWE BABA/

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2007

    Mkapa deal la Rada lazima litabumbuluka tu, angalia jamaa wa Saudi Arabia waliokuwa wanachunguzwa kwa deal zile zile na BAE, kilakitu sasa nje.
    soma hapa chini;

    Saudi prince 'received arms cash'

    Arms deals with the Saudis have been worth billions to the UK


    BBC investigation
    A Saudi prince who negotiated a £40bn arms deal between Britain and Saudi Arabia received secret payments for over a decade, a BBC probe has found.
    The UK's biggest arms dealer, BAE Systems, paid hundreds of millions of pounds to the ex-Saudi ambassador to the US, Prince Bandar bin Sultan.

    The payments were made with the full knowledge of the Ministry of Defence.

    Prince Bandar would not comment on the investigation and BAE Systems said it acted lawfully at all times.

    The MoD said information about the Al Yamamah deal was confidential.

    Sir Raymond Lygo, a former chief executive of BAE, told the BBC's World Business Report that there had been "nothing untoward" about the arms deal.

    "I was the one who won the contract," he said. "I don't know anything about him (the prince) at all. I would have remembered that name."

    When asked about the secret payments, Sir Lygo said that it was not going on when the deal was signed.

    "I would have known if it was going on at the time. I was not aware of it, so as far as I am concerned it was not occuring.

    "Yes, we paid agents. Nothing illegal about that. It was absolutely in accordance with the law at the time... there was nothing untoward about the deal whatsoever."

    Private plane

    The investigation found that up to £120m a year was sent by BAE Systems from the UK into two Saudi embassy accounts in Washington.

    There wasn't a distinction between the accounts of the embassy or official government accounts

    David Caruso
    American bank investigator


    Timeline: BAE Systems probe

    The BBC's Panorama programme has established that these accounts were actually a conduit to Prince Bandar for his role in the 1985 deal to sell more than 100 warplanes to Saudi Arabia.

    The purpose of one of the accounts was to pay the expenses of the prince's private Airbus.

    David Caruso, an investigator who worked for the American bank where the accounts were held, said Prince Bandar had been taking money for his own personal use out of accounts that seemed to belong to his government.

    He said: "There wasn't a distinction between the accounts of the embassy, or official government accounts as we would call them, and the accounts of the royal family."

    Mr Caruso said he understood this had been going on for "years and years".

    "Hundreds of thousands and millions of dollars were involved," he added.

    Investigation stopped

    According to Panorama's sources, the payments were written into the arms deal contract in secret annexes, described as "support services".

    They were authorised on a quarterly basis by the MoD.


    Prince Bandar was Saudi ambassador to the US for 20 years

    It remains unclear whether the payments were actually illegal - a point which depends in part on whether they continued after 2001, when the UK made bribery of foreign officials an offence.

    The payments were discovered during a Serious Fraud Office (SFO) investigation.

    The SFO inquiry into the Al Yamamah deal was stopped in December 2006 by attorney general Lord Goldsmith.

    Prime Minister Tony Blair declined to comment on the Panorama allegations.

    But he said that if the SFO investigation into BAE had not been dropped, it would have led to "the complete wreckage of a vital strategic relationship and the loss of thousands of British jobs".

    Prince Bandar, who is the son of the Saudi defence minister, served for 20 years as US ambassador and is now head of the country's national security council.

    Panorama reporter Jane Corbin explained that the payments were Saudi public money, channelled through BAE and the MoD, back to the Prince.

    The SFO had been trying to establish whether they were illegal when the investigation was stopped, she added.

    She believed the payments would thrust the issue back into the public domain and raise a number of questions.

    'Bad for business'

    Labour MP Roger Berry, head of the House of Commons committee which investigates strategic export controls, told the BBC that the allegations must be properly investigated.

    If there was evidence of bribery or corruption in arms deals since 2001 - when the UK signed the OECD's Anti-Bribery Convention - then that would be a criminal offence, he said.

    He added: "It's bad for British business, apart from anything else, if allegations of bribery popping around aren't investigated."

    Liberal Democrat Treasury spokesman Vince Cable said that if ministers in either the present or previous governments were involved there should be a "major parliamentary inquiry".

    "It seems to me very clear that this issue has got to be re-opened," Mr Cable told BBC Radio 4's The World Tonight.

    "It is one thing for a company to have engaged in alleged corruption overseas. It is another thing if British government ministers have approved it."

    Panorama will be broadcast on Monday 11 June 2007

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2007

    "Unlike American law where law enforcement agencies, the judicial system, and private citizens can gain access to all kinds of financial information under Swiss law, except for extraordinary circumstances neither the bank's officers or the bank's employees are allowed to reveal any information, relative to any account to anyone, including the Swiss government.

    No private citizen, or their legal representative can ever receive any type of information about any one's Swiss bank account under any set of conditions. That includes all types of legal proceedings that the Swiss classify as "non-criminal behavior."

    The Swiss consider tax evasion and many other "crimes" under US law as "political offences." Things like divorce, inheritance disputes and bankruptcy cases are examples of "private matters," and as such the secrecy of the account is protected from any legal action to verify the presence of, or attempts to seize any assets.

    There are some notable exceptions. Three types of activity which the Swiss consider illegal, and are bound by treaty with the United States to "open" the account for possible legal proceedings are: organized crime activities, drug trafficking, and "insider trading" of securities. In instances of this kind, the Swiss authorities have the final say on whether or not to reveal any information".


    kwa kifupi kijana "koloboi" ni kwamba sio ukifungua account Uswiss basi hauwezi kutolewa information zako la hasha koz kuna makosa ambayo chombo cha sheria kikiwasilisha serikalini Uswiss basi info zako zote zinatolewa,watu wanapenda kufungua uko kwasababu kuna makosa machache sana ambayo yanasababisha watoe info zako ukilinganisha na the rest of the world na pia account number hazina majina bali special numbers and mtu anaejua majina to those numbers ni bank managers and only few selected staff in that bank..(Bank zote swiss ziko registered serikalini)

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2007

    Perez,
    Kula tano wakwetu. Huyu Koloboi anajidai anajua kila kitu kumbe hamna lolote. Anadahani mambo yanaendeshwa kienyeji kama jinsi ki-accout chake binafsi kinavyoendeshwa.
    Hutamuona tena kurudi kwenye mada hii kutoa pumba zake.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 08, 2007

    Kikwete kakiri kuwa anafanya biashara akiwa Ikulu kwenye hotuba yake.

    Biashara yenyewe anayofanya ni ya kilimo cha mashamba makubwa, kule Bagamoyo.

    Anachofanya kama alivyosema kwenye hootuba analima mashamba makumbwa na kuuza mazao yake.Hivyo anafanya biashara ya mazao ya Kilimo akiwa Ikulu kama alivyokiri mwenyewe alipoulizwa kama naye atakuwa mfanya biashara au la akiwa Ikulu.


    Ili kuweka rekodi vizuri waandishi wa habari msimsumbue tena Kikwete sasa na akistaafu mkiona kanunua ghorofa la mabilioni,mjue pesa za hilo ghorofa zitakuwa zimetoka kwenye biashara ya mazao toka kwenye mashamba yake makumbwa kule bagamoyo kama alivyowaeleza kwenye hotuba.

    Tofauti ya Biashara za Kikwete na Mkapa wakiwa Ikulu ni kuwa Mkapa kakopa kanunua nyumba na kuwa anapangisha(Ameamua kuwa mfanyabiashara wa kupangisha majumba) Wakati Kikwete yeye kaamua kuwa mfanyabiashara wa Mazao.

    Wote wawili ni wafanyabiashara wakiwa Ikulu tofauti yao ni aina za biashara wanazofanya.Wananchi na waandishi wa habari muelewe hivyo.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 08, 2007

    Jamani mbona mnalumbana na watu wanaohusika wala hawana habari. hivi mnadhani bongo hii kuna MKUBWA anayefanya dhambi? Mbona wote ni watakatifu? Angalieni yenu waachieni yao, THIS SYSTEM hamuiwezi. Mtamaliza maneneo yote wenzenu wanakula kwa RAHA ZAO.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 08, 2007

    Zote hizo ni pesa za wananchi wanatumia.

    Mbona Nyerere hakuwa na vyote hivyo???????????

    Jamani huu wizi wa macho macho tumechoka.

    Na Sumaye nae atasema mashamba ya Kibaha ndio yanamfanya awe na ma-account yenye pesa Uswiss.

    Mhhhhhh kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 08, 2007

    Raisi kufanya biashara sio tatizo. tatizo kama hawi mfano bora wa kulipa kodi na kulipa mshahara mzuri wafanyakazi wake..

    Kila mwazno wa mwaka tunaonyweshwa BUsh na mkewew income yao kwa mwaka ni ngapi na wamelipa tax kiasi gani...Na kwasasa hivi baada ya kuingia kwenye uongozi ili kuondoa maneno waliachia biashara zao zote...kuongoza nchi ni kusucrifise kama unataka ungozi uwe tayari kuachia mengine yote kwa kipindi unachoongoza

    Shamba likiungua kazi itafanyika vizuri kweli???? Hata kama yuko ziarani si atakatiza ziara yake...

    The is is how much you will be able to fully work if you have all these other things.

    Kama mtu anatakak uwa mfanya biashara basi achia uongozi...

    Ndio yale ya viongozi wa njuma aliweka biashara kwa majina ya ndugu zake

    Tanzania Tanzania... Mungu anaona ...kama kweli mnaenda kusali kila siku halafu mnayofanya hivyo nakuona ni haki yenu Mungu atawwateketeza ... remember that

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...