leo jk amemtangaza mh. brigedia generali jaji wa mahakama ya rufaa augustino ramadhani kuwa jaji mkuu kuchukua nafasi ya mh. barnabas samatta ambaye anastaafu rasmi keshokutwa baada ya kuitumikia mahakama kwa takriban miongo mitatu na ushee.
ikumbukwe jaji mkuu mteule mh. ramadhani amepata kuwa jaji mkuu wa zenj, na pia makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi bara na kisha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zenj katika nyakati tofauti.
pia amekuwa mmoja wa majaji wa kwanza kwenye mahakama ya jumuiya ya afrika mashariki.
anatarajiwa kuapishwa rasmi julai 20, 2007 ambayo ni siku moja tu baada ya mh. jaji mkuu anayestaafu samatta kuagwa rasmi katika sherehe rasmi iliyoandaliwa kwa heshima yake siku ya alhamisi mahakama ya rufaa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2007

    Naomba close-up, picha ni ndogo mno, lete kubwa kama ile ya bi Kidude ulipoenda sauti za busara.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2007

    Mbona ameshakula chumvi nyingi hakuna wenye umri mdogo kuliko yeye? Miaka 61, angewaachia vijana yeye akacheze na wajuu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2007

    Kwa kweli uteuzi wa Jaji Ramadhani ni mwafaka. Ninavyomfahamu ni mchapakazi, mtu wa watu, mwadilifu, na pia muumini mzuri wa dini yake.Tutamiss piano kanisani!Au kwani Jaji Mkuu anaruhusiwa kupiga piano kanisani? Sheria inasemaje?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2007

    Naamini JK amefanya jambo la maana kumteua mtu mwenye uzoefu kama Jaji Augustino. Kilichobakia kwa jaji ni kuwa kiongozi wa mabadiliko ndani ya mahakama kwa kuwatumia vizuri wanataaluma alio nao na pia kwa kiuongo muhimu kati ya watawala la wananchi katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka na mazingira mazuri yenye kuchochea maendeleo yanajengwa. Hongera Jaji!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2007

    Mbona nchi haijawahi kuwa na CJ muislamu kwanini?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 18, 2007

    huyu jamaa karudi tena kwenye uislamu? alitulia kidogo sasa naona kaamua kuchagua jirani zake haya tutaona mwisho wake....!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 18, 2007

    Hapo JK ametumia technic ya kufanya "balancing" ya dini kwa majina, maana wengine walishaanza kuchonga oh awe muislamu sasa, ohh kwa nini ma JM wote wanakuwa wakristu tu! Ingawa wanajua wazi kwamba innji yetu hii haina udini.
    Sasa ukitunmia jina la kwanza pekee kumu-address yaani Mheshimiwa AUGUSTINO, basi wakristu wataridhika.
    Na ukitumia surname pekee kumu-adress yaani Mheshimiwa RAMDHANI basi waislamu nao wataridhika. Ngoma droo!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 18, 2007

    Asante sana JK kwa uteuzi huu MAKINI. President kama nilivyo kupongeza kumteua Margareth Sitta kuwa waziri wa elimu kweli you know what you are doing despite a few set backs here and there.

    Namtakia afya njema Jaji Mkuu mpya na sina shaka kabisa kwamba atawatumikia watanzania kwa uadilifu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2007

    hongera mzee wetu kwa kuula tena katika serikali ya awamu ya nne.
    Lakini kilio chetu vijana bado kipo palepale, ulaji ni mzuri, hata sisi vijana tunautaka jamani wazee wetu si mtuachie na sisi tuuonje kama qualification tayari tunazo huo uzoefu tayari tunao, au mpaka na sisi tule chumvi nyingi ndio msikie kilio chetu.
    I wish if I could be one of the nominee of that post with this age I have.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 18, 2007

    Heheheee sikujua kuwa Jaji Mkuu ni mwanajeshi pia.
    1.Raisi na Mwenyeti wa CCM ni Luteni Kanali
    2.Katibu Mkuu wa CCM ni Luteni
    3.Jaji Mkuu ni Brig Jen
    4.Wakuu wa mikoa ndo usiseme

    Atapona mtu hapo na amri za kijeshi kwa kwenda mbele

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 18, 2007

    Nadhani Rais amefanya uteuzi mzuri tu, na pia mkumbuke jamani mbamba ngoma uvutia kwake, ndiyo maana bwana Kikwete anavuta Waislam wenzake bwana.... Bwana Ramadhani ni mchapakazi mzuri sana

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 18, 2007

    Asante JK kwa uteuzi wako, achana na washamba wanaongalia majina na kutafuta ni dini gani watakula fikra zao. Hongera baba J. Ramadhani

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 18, 2007

    Hongera, kwa wadhifa stahilifu, prefekti mwenza Tabora School (Biscoe House - Upper School - 1964/65) na koleji-mate Mlimani (Class of 1970)!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 18, 2007

    TUNATIA AIBU-----Nimeona hii headline news Tanzania: Impassable Roads Cut Short Museveni's EA Trip Around East Africa - Aides

    Bad roads in northern Tanzania forced President Yoweri Museveni to fly back to Uganda, cutting short a road trip to the country through Kenya.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 18, 2007

    Kaka michuzi nimekumiss sana leo mzima lakini.unajua nini nakumbuka kuna wakati nilienda ofisi kwa msure wangu nikakukuta tukaambiwa tukuamkie eti ahhaa sasa hivi tulivyokuwa wakubwa wengine tukikuhamkia unaweza kututoa baruti ile mbaya but all in all I respect u Bro genius.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 18, 2007

    Kwa taarifa yenu Jaji Augustino Ramadhani ni Mkiristu na ni mwana kwaya mzuri na mpiga kinanda mzuri sana pale Kanisa la Anglikana jijini Dar es Salaam

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 18, 2007

    Michuzi wacha kutupa maoni ya watu, au huyo jaji ni ndugu yako???, wewe ni mjumbe hauwawi weka maoni ya watu ili wanaosoma wawe wachambuzi wenyewe. huyo jamaa japo kachaguliwa si mtu wa haki kwani alichezesha mechi Zanzibar kwa upendeleo sasa usiweke na hii, mi nakulenga wewe binafsi. Kuwa fair basi au umeahidiwa uzee wa balaza mahakama ya rufaa??!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 18, 2007

    Justice Ramadhani holds an LLM degree from the University of Dar es Salaam and a 1970 LLB degree from the Dar es Salaam University College of the then University of East Africa. A devout Christian and church pianist, Justice Ramadhani is married with four children.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 18, 2007

    Who cares na tofauti itakuwapo kweli?

    Dotto yupo mtaani anatembea tu kama vile hatukuwa na jaji mkuu before.

    Hawa viongozi wetu basi tu God knows

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 19, 2007

    mimi sizungumzii udini au majina najua ramadhani ni mkristu na si mwislakmu. umefika wakati watu wasiangalie majina waangalie utendaji wa mtu. ramadhani is not competent alikuwa jaji mkuu zenji ameharibu sana huko! afterall kwani hakuna majaji raia wa kuteuliwa kuwa majaji wakuu lazima watafutwe wanajeshi? kila post mwanajeshi kuanzia rais mawaziri wakuu wa mikoa wakuuu wa wilaya hata majaji?

    huu ni wakati wao wanajeshi wanapeta tu. yetu macho!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 19, 2007

    Halafu Michuzi acha wivu na roho mbaya! Huyu Jaji licha ya kuwa na sifa kemkem pia ni bonge la handsome boy! Ndio nini kutuwekea picha hiyo uliyoiharibu kwa makusudu kabisa! He is the most sexiest Jugdes in TZ ebboh! Weka picha yake halisi yenye mvuto!

    ReplyDelete
  22. Hivi huyu nae alikuwa ktk ile panel ya majaji waliong'ang'ania kwamba jamaa wa CUF walipanga "kuipindua" serikali ya Zenji ktk mid-1990s hadi Nigerian judges wakaja ku-rule kwamba Zenji sio dola?

    Hakuna majaji waliowahi kuchemka vibaya kama wale. Lakini huyu jamaa pia amekuwa ktk tume za chaguzi za Muungano na Zenji ambazo wote tunajua "utendaji" wa hizo tumez. Tusubiri tuone kama ktk zama zake serikali itakuwa inashindwa ktk kesi tena kama zama za Samatta zilivyokuwa.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 19, 2007

    Mh hizi comments!.Sasa wewe unaesema sexiest judge una maana gani..Hii ni serios biz..Bibliography yake iwekwe official..Mke na watoto watajwe majina.Elimu na historia, etc..Sexiest ndio nini..Focus on serios things. Hata kama sexy au mbaya kama pichani, yeye ni judge mkuu kinachotakiwa nikuperform akiwa mzigoni-mahakamani.

    Ni hayo tuuuu!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 19, 2007

    Nyie nyoote mnaosema Jaji mkuu Ramadhani ni Muislam, oooh Kikwete kamchagua Muislaam mwenzake, fanyeni kwanza uchunguzi msikukuruke wanangu! Kwani Jaji Augustino Ramadhani ni MKRISTO mwanglikana pure tunasali nae na anatupigia kinanda kanisani! Waosha vinywaaa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...