jengo la makumbusho ya taifa (la mjini, mkabara na ifm) linafanyiwa matengenezo kugeuzwa kuwa makumbusho na kituo cha utamaduni ambapo kutakuwa na ukumbi mkubwa wa kisasa wa kubeba watu 500, studio za kurekodia muziki na mazoezi, galeri za maonesho ya sanaa na vikorombwezo kibao vya kupafanya mahali hapo pachangamke. tayari uzio wa bati umeshaanza kuzungushwa na vifaa vya ujenzi kuletwa. hivi tunavyoongea nyaraka za ujenzi huo zinatarajiwa kutiwa sahihi wakati wowote baina ya menejimenti ya makumbusho na shirika la misaada la uswidi ama sida na ujenzi utaanza mara moja na kuchukua takriban mwaka mmoja kukamilika ambapo kilio cha wasanii kukosa mahali pa kuoneshea kazi zao vinatarajiwa kwisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2007

    jamani tunazidi tu kuongeza msongamano usio wa lazima,hivi kweli tumekosa washauri wa kuwashauri nini cha kufanya hapo.kweli tanzania tumefilisika kimawazo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2007

    Kwakwelitumengoja muda mrefu mno kupata hiyo national theatre, kama mambo ndiyo hayo basi tunashukuru na ninaamini sanaa itazidi kukua-Mlewa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2007

    waache kukandamiza majengo mapya huko town. mbona nafasi zenyewe hazipo? watafute maeneo nje ya mji sio kiola kitu huko town hivi hakuna wataalamu wa kupanga miji? ukumbi wa kubeba watu 500 hilo ni eneo kubwa watafute nje ya dar hata bagamoyo au kibaha au chalinze sio kila kitiu dar waache ushamba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...