mdau wa kigamboni anatupasha kwamba katika sehemu za mjimwema wanachi waliamua kufunga barabara kwa magogo kuishinikiza serikali kuweka matuta, kufuatia mwanafunzi kugongwa na gari na kufa. inasemekana uzalendo umewashinda wakazi wa huko kutokana na matukio mengi ya ajali za watu kugongwa watu katika barabara hiyo yenye lami kutoka kivukoni feri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2007

    HUU NI UKOSEFU WA UTAWALA WA SHERIA KWA VITENDO NA SERIKALI(VIONGOZI) KUTOKUWAJALI WANANCHI WOTE(WALIOPIGA KURA ZA NDIYO NA HAPANA).WATU KUMCHOMA MSHUKIWA WA UHALIFU NI ISHARA YA WATU KUTOIAMINI SERIKALI YAO KUWA ITATENDA HAKI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2007

    Hivi ujenzi wa daraja la kigamboni utakuwepo kweli?????....Hivi Serikali inahitaji tu kura za wananchi wa sehemu hii ya kigamboni?..jamani huu ni unyanyasaji,lakini kuwapatia maendeleo ni mgogoro....watu wa kigamboni wanapata taabu sana pale kwenye kwenye kivuko..mapantoni mabovu,kweli serikali inashindwa kuwajengea daraja??...au kwa vile inapata sana fedha kutotokana na mapato ya pantoni???

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2007

    Kwani kigamboni kuna uchumi gani wakufanya serikali ipeleke mabilioni kujenga daraja. Ni kwa vile hao watu wachache wamejenga nyumba huko sasa wanaona ni kazi kuzunguka kupitia mbagalla?

    Tunahitaji kujifunza jinsi ya kuallocate hela ya umma. Ingekua kuna viwanda au maofisi yanayohitaji watu kuenda kwa haraka haraka kweli.

    tufikirie kwanza sio kuona george washington bridge basi nasisi tujkakamue tujenge.

    I don't see the need of that bridge for real for now.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2007

    Sio kwa vile serikali inapata mapato kwa ajili ya pantoni. Ikiwekwa daraja pia wataweka toll ya kuimaintain. Na watu wakiona toll tena wataanza kusema ni nyingi bona pantoni letu....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...