Hello michu za siku?
kuna issue naomba muifanyie kazi ili itoke gazetini issue yenyewe ni kwamba kuna mshelisheli mmoja alikuwa na shamba lake kubwa huko kibamba ambalo baadae aliamua kuuza viwanja nami ni mmoja ya walionunua kati ya watu wapatao 30 walionunua na kati yetu kuna watu wangine ambao washajenga nyumba na wanaishi hapo kuna wangine ndio wapo ktk ujenzi nami ni mmoja wapo. sasa chaajabu miezi mitatu iliopita walitokea watu wa benki na kudai mwenye hili shamba anadaiwa na benki sasa sisi tumepauza mnatakiwa muondoke kingine cha kushangaza benki wameliuza hilo shamba milioni 12 napale ktk hilo shamba kuna nyumba zenye thamani kubwa zingine hadi milioni 30 tulipofatilia ktk ofisi za benki wanadai hawana hizo taarifa sasa sisi wangine tupo mbali tuna shindwa kuelewa sasa nakuomba ndugu yangu michuzi lifatilie hili swala au mkabizi mwana habari yeyote ili aliweke hadharani na habari hizi mtazipata vizuri kwa diwani wa kata ya kwembe pamoja na mwenyekiti wake wa serikali ya mtaa kwani hili swala hivi sasa lipo mikononi mwao.
naomba msaada wako mr michu kwani ujambazi sio tu kushika bastola huu nao ni ujambazi
mdau mkereketwa


Hili ni fundisho kwa wanaoparamia vitu bongo bila kujua background yake. Na hivi vitu vipo sana bongo watu wanauziana vitu kienyeji tu.
ReplyDelete1.Maswali ya kujiuliza ni je huyo mshelisheli alikuwa anawapa hati za viwanja, yeye anadhamana gani katika viwanja wakati wizara ya ardhi ipo.
2.Wakati wananunua hivyo viwanja walimuhusisha mwanasheria yoyote?, au waliona ubwete kupimiwa viwanja kama kibaba cha unga yaani hela yako tu ukitaka cha Shs 300,000 unapata cha Shs 1,000,000 unapata.
3. hapo bwana muhesabu mmeliwa yaani hata mahakamani mtashindwa na kama ni wizi ni huyo mshelisheli ndio wa kumkaba kama hajarudi kwao, Bank wao wameuza kulipia deni lao jamaa alilokopa akaweka kiwanja "collateral" dhamana.
Swali kwa serikali yetu, Je huyu mshelisheli inakuwaje apate kiwanja nchini mwetu na kutumia kukopea bank, wakati sheria inasema viwanja ni mali ya Rais.
Yeye alipaswa kujenga nyumba ndio aweke dhamana bank na sio kiwanja (Shamba) ambalo halijaendelezwa
Je kwa bank nao ilikuwaje wakubali dhamana ya kiwanja toka kwa mgeni na kumkopa fadha wakati wanajua kuwa huyo jamaa si mtanzania.
Na kama bank walikuwa serious na dhamana yao walikuwa wapi wakati watu wanaanza kuporomosha ma bangalow yao kwa hela za kudunduliza leo hii wanakuja kupauza kwa mtu mwingine.
Ushauri:
hapo ni kufungua court injuction kwanza, halafu wafungue kesi kusikiliza hilo shauri, kama wanaweza watafute mpatanishi(awe eithe wizara ya ardhi, kuweza kuvipima hivyo viwanja na kupewa hati kwa malipo ambayo yatalipa hilo deni la bank na serikali ipate chake)
ONYO:
Jamani tuache kupenda ubwete, Hii tabia watanzania wengi tunayo na ndio mwanzo wa kukosa haki zeti, unakuta watu wanauziana gari Bar, na kukabidhiana funguo, jina la kadi halibadilishwi na kama wewe ni mtu wa nne kuuziwa basi hata huyo wa mwenye jina humjui, je kama la wizi si utaishiwa segerea au ukonga ukape KAKA YAKO?!!!!.
we tuliza mshono huo, hizo nyimbo tulishachoka nazo we kwa nini ulinunua kiwanja bila kufuatilia ardhi? kama unauchungu sana tia timu mwenyewe ufatilie
ReplyDeleteDuh ndugu yangu pole inshaallah mungu atakusaidia michuzi kweli fatilia ila kunajamaa anaitwa baghdad huyo nitapeli wa viwanja ashawahi kufungwa katoka mwaka jana tu, inaonesha ni kama huyo mshelisheli watu kama hao bora wateketezwe mnaponunuwa viwanja msiingie tamaa vikiwa rahisi sana, bora mfatilie kuliko ukiwa nje mtu akwambie kunakiwanja bongo million 7 tu vingi ni bomu bora uone mwenyewe na ufatilie na mikataba yake. pole mzee mungu atakupa zaidi ya hivyo. michuzi msaidie kufatilia jamaa.
ReplyDeletekaka Michuzi namuunga mkono asilimia 200% huyo Skraga aliyetoa maoni hapo juu.
ReplyDeleteWatanzania tunapaswa tuamke sasa na tujue angalau requirements ndondogo za sheria ambazo sio lazima sana uziendee darasani.
Kuna usemi wa kisheria unaosema "CAVEAT EMPTOR" yaani BUYER BEWARE!
Kimsingi ni kwamba usemi huu unamtaka mnunuzi yoyoye kufanya upekuzi kwenye mamlaka inayohusika juu ya uhalali wa umiliki wa Mali hiyo wa huyo muuzaji, yeye mnunuzi anayotaka kuinunua. Lakini kwa sababu ya haraka haraka zetu hatufanyi hivyo.
Mimi nilitaka kuingizwa mjini na kundi la vijana fulani kule kitongoji cha MAPINGA-Bagamoyo.
Eti wanadai wamepewa ardhi na uongozi wa Kijiji, ni mali yao kwa hiyo wanakata na kuuzia watu. Cha kushangaza ni kwamba unaweza kuuziwa heka moja hata kwa Tzs. 80,000/=!
Wakanikuta nami mjanja. Nikawaambia twende kwenye serikali ya Kijiji/Mtaa kwanza. Wakaanza kujiuma uma. Nikaishia zangu.
Ningalikuwa n-jinga chi ningekula maapi!
Namshukuru Skraga kwa maelezo mazuri ambayo yanafaa kusomwa na kila mmoja wetu. Suala la kununua viwanja vilivyopimwa ni suala ambalo sio tu litamnufaisha mnunuzi bali pia ni chachu ya uendelezaji wa makazi bora nchini. Naomba watanzania wenzangu popote walipo waunge mkono juhudi za serikali za kupima na kugawa viwanja ni pia kuwezesha mazingira bora kwa taasisi zinazojiweza kujenga nyumba kitaalamu na kuziuza au kupangisha kwa wananchi. Huo ni mwanzo wa hatua muhimu ya maendeleo nchini Kwetu. Nampa pole ndugu yetu aliyepata matatizo lakini pia namtakia uvumilivu na umakini katika kufuatilia jambo lake.
ReplyDeleteJuly 19, 2007 10:05:00 PM EAT SKRAGA ushauri wako mzuri sana mimi kama mtanzania mwingine yeyote yule nadhani tunawatu wanao somea sheria au wahitimu hapa kwenye hii blog sio? jambo la busara lingekuwa kumsaidia ushari wa kisheria huyu jamaa hapa maana hata kama ukimlaumu kimeshatokea na wengine tutajifunze kupitia kwake naamini katika ushari 10 kati ya 1 litamsaidia mawazo au sio
ReplyDeletejamani siku hizi ukitaka kununua kiwanja nenda Wizarani wao watakuambia nani mmiliki au ni sehemu halali au siyo na uhakikishe wanakupa GO AHEAD na unapewa Hati...uswahilini acheni kwenye vitu vinavyohusisha pesa mambo lazima yaende kiofisi la sivyo utapeli hautaisha,na mliodhulumiwa fuateni ushauri wa jamaa hapo juu SKRAGA.
ReplyDeleteAisee skraga hata mimi naungana na wewe kwa maelezo yako ila naomba wewe na wadau wengine msome tena hayo malalamiko ya huyo mdau kwani amedai walikwenda bank kuulizia hilo swala lkn bank hawana taarifa hizo sasa hamuoni hapo kuna ubabaishaji? inawezekana ni ofisa mmoja tu wa bank ndio anacheza mchezo huo na ofisini hawajui.
ReplyDeleteAnon wa 5:53:00PM EAT
ReplyDeleteNi kwamba Bank hawana taarifa kuwa kiwanja kiliuzwa na mshelisheli, ndio mimi nafikiri na wadau wengine walivyoelewa.
Halafu kumbuka kuwa ofisa mmoja wa bank au kundi la watu matapeli hawawezi kwenda kwenye makazi ya watu na kuzusha ni kiwanja cha bank kwani wanajua ni issue nzito na itaishia kwenye vyombo vya sheria.
Hapo ni kwamba bank wanasema hawana taarifa kama "kihamba" kimeuzwa hiyo tafsiri sahihi ya hiyo mail.
Pole mdau, ila nakubaliana na ushauri wako wa vyombo vya habari kuiripoti kupitia msaada wa michuzi ili jamii, ijifunze kutokana na makosa hayo yaliyofanyika na watanzania wenzetu