TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO MKUU WA WANATAALUMA WA TANZANIA SIKU YA TAREHE 29th July 2007

Kumekuwa na makubaliano ya baadhi ya wahitimu wa elimu ya juu, wasomi na wanataaluma kwamba uitishwe mkutano mkuu utakaowakutanisha wasomi na wanataaluma wote Tanzania siku ya Jumapili Tarehe 29th July 2007 jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa NSSF Water Front kuanzia saa 8.00 Mchana.
Inakadiriwa kuwa karibu watu 500 watahudhuria mkutano huu. Katika mkutano huo Mtandao wa Wanataaluma wa Tanzania utazinduliwa baada ya rasimu ya katiba itakayopendekezwa kuboreshwa na kasha kupitishwa.. Viongozi wa kwanza wa kuendesha chama watachaguliwa.
Mkutano pia utajadili mbinu mbalimbali za za kutunisha mfuko na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo itakayobuniwa. Ili uweze kuhudhuria mkutano jiandikishe kupitia tovuti ya http://www.peersgroup.org/register.php au tuandikie subscribe@peersgroup.org. Kwa maeleze zaidi tembelea tovuti ya: www.peersgroup.org

Peers Group ni kundi linalofanya kazi chini ya kivuli cha chama cha SCOPE 2000 ambacho kimesajiliwa. Jina Peers Group limekuwa maarufu zaidi kwa kuwa awali kundi hili lilijumuisha wahitimu wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam waliokuwa na mawazo ya kimaendeleo ambao walimaliza chuo katika kipindi kimoja.
Kwa sasa kundi hili limekuwa na lina wanachama wasio rasmi zaidi ya 300 wa ndani na nje ya nchi ikijumuisha Wahitimu wa elimu ya juu, wasomi na wanataaluma. Wanachama wasio rasmi wa Peers Group ni wanataaluma kuoka nyanja mbalimbali na wenye nyadhifa mbalimbali wakiwepo watendaji wakuu, Wakurugenzi, Mameneja, Wafanyabiashara, Maofisa waandamizi n.k..
Peers Group haijishughulishi na siasa na wala haifungamani na chama chochote cha kisiasa. Dira ya Peers Group ni Kusaidia kuibadilisha Tanzania kuwa Taifa la Jamii yenye maarifa ya juu ifikapo mwaka 2050.

Dhima ya Group Mission ni Kuchochea na kukuza matumizi ya NGUVU YA AKILI miongoni mwa Watanzania katika kuyaelewa na kuyatatua matatizo mablimbali ya Kijamii, Kiutamaduni, Kiuchumi, Kimaendeleo na kisaikolojia.
Madhumuni
1. Kuwafundisha na kuwaandaa Watanzanian katika ujuzi wa Ujasiliamali na kuwafanya wawe wanajitengenezea ajira na kuongeza uzalishaji na hivyo kujenga uchumi imara.
2. Kuchochea na Kukuza uanzishwaji wa Vijiji na vituo vya Elimu ya Ujasiliamali katika kufanikisha shughuli za maendeleo ya Uchumi na Kijamii.
3. Kuchochea na Kukuza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Tanzania.
4. Kuchochea na Kukuza shughuli mbalimbali za Michezo, Burudani,na Utamaduni katika jamii ikiwemo Tamasha la Carnival.
5. Kujenga na kuleta vichocheo vya mabadiliko ya kudumu baada ya muda kuelekea katika kujitegemea kupitia juhudi za pamoja.
Uanachama wa Peers Group
1. Wahitimu wa Elimu ya juu, wasomi na wanataaluma wenye mitazamo ya kimaendeleo.
2. Uanachama wa heshima unaweza kutolewa kwa mtu yeyote, kikundi au Shirika au kampuni yoyote ambayo inaunga mkono Dira, Dhima na Madhumuni ya Peers Group..
Sanctus Mtsimbe, B.Sc. University of Dar Es Salaam, M.Sc. University College London – UK)
Mratibu wa Muda wa Peers Group (0754 833 985)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2007

    Brother Michu, mimi nimejaribu kufuatilia kwa muda jitihada za hawa wenzetu. Nimegundua kuwa wako very genuine na si wababaishaji.

    Pia nimeona members wengi ni wanataaluma ambo wana nafasi mbalimbali muhimu wakiwepo Mawaziri, Ma CEO's n.k. Sasa hivi ukijiandikisha kwenye mtandao wao wa www.peersgroup.org unawekwa automatically kwenye email circulation ambayo ni forum ya discussion. Aisee jamaa they are in serious business, no jokes.

    I suggest Wataaluma wote waliomaliza Diploma, Advances Diploma, Degree, PhD tukusanye nguvu. I believe hii ni association ya kwanza inayokutanisha wataalamu wote wa fani mbalimbali kama Waandisi, Madaktari, Wasanii, Wajasiliamali, Wafanyabiashara n.k.

    Let us join the forces and see the impact.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...