je, una habari kwamba idhaa ya kiswahili ya bbc london ilianzishwa na mmbongo? basi huyu hapa hayati oscar kambona ambaye ndiye aliyekuwa mtangazaji aliyerusha matangazo ya kwanza ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC tarehe 27 mwezi Juni mwaka 1957. Alifariki Uingereza akiwa na umri wa miaka 68. kwa habari hiyo na nyingine bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Alikosana nini na mwalimu mbona nasikia mlokuwa vijana enzi hizo mlimuimba sana "huyo mjinga!!! Kambona!!! Huyooo huyo!!! Kambona, Kambona!!!"

    ReplyDelete
  2. kuna wazushi fulani kila wakikutana na sie eti wanadai watoto wadogo tunaofisi kubwa!

    ReplyDelete
  3. Yeah Anon ni kweli tulimuimba sana maskini kambona wa watu. "kambona, ameolewa, wapi? huko ulaya, na nani? na Mwingireza.

    Nifikiri ilikuwa vibaraka waliokuwa hawajui vizuri ni kitu gani hasa kilimfanya Kambona aende ukimbizini ndio waliokuwa wanapandikiza mbegu mbaya na kumuimba vibaya hivo. Nafikiri alipaswa aheshimiwe kwa uamuzi wake kwani alikuw ana haki ya kutofautiana na mwalimu na kama alihisi usalama wake uko hatarini alikuwa na haki ya kwenda mahala alipokuwa anafikiri ni salama kwake yeye na familia yake.

    ReplyDelete
  4. Alianzisha BBC au alitangaza kiswahili kwa mara ya kwanza?

    ReplyDelete
  5. Kambona, Kamaliza, Mataka, Sizya, Dr. Mtawali, Shaba wote na wengine wengi...Wa-Malawi wa kwetu Malawi kwa Ngwazi!

    ReplyDelete
  6. Ninachofahamu Kambona alipinga Azimio la Arusha ambalo ni pamoja na utaifishaji wa mali za raia na Mwalimu alikuwa ni wa 'uko pamoja nami au wewe ni adui yangu'.

    ReplyDelete
  7. Inafaa sana kuandika kitabu juu ya "The Rise and Fall of Oscar Kambona".

    Hata sisi watoto wa Ngwazi tuliyafuatilia hayo ya Kambona wetu!

    Mambo ya Kambona yalikuwa hayakuanza na Azimio la Arusha!

    Kwanza, alikuwa ni Foreign Minister wetu wa kwanza. Katibua!

    Kafanywa kuwa Waziri wa Elimu. Katibua!

    Kafanywa kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa. Kakasirika kuwa Nyerere alikuwa anamteremsha cheo!

    Hasira zikazidi cha kuanza ugomvi na Waziri Mkuu Kawawa. Ugomvi ukazidi kiasi!

    Mnakumbuka "Majambazi wa Uwongo" (watano au sita) majina yao yakitangazwa redioni kwa muda wa juma moja kufuatia habari za jioni?

    Kati ya eti "uwongo" huo ni kisa cha kutwangana ngumi kati ya Kambona na Kawawa mkutanoni!

    Azimio la Arusha linatangazwa when Kambona was already falling from the grace of Nyerere & Co.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...