
baba wa taifa akiwa anapiga stori na mdau mwandamizi freddy macha ambaye leo nimepata mshtuko wa furaha kukuta kumbe naye ana globu yake. kumtembelea bofya hapa na pia kwenye tovuti yake bofya hapa
kwa kweli nimehemewa kugundua globu ya gwiji huyu wa lugha, muziki na utamaduni. tangia niko kinda nimekuwa nikisoma maandiko yake kwenye sunday news na sasa kwenye guardian. ni mmoja kati ya walionihamasisha kuivamia hi fani ya uandishi. na kama hiyo haitoshi mdogo wake, ndesanjo macha, ndiye aliyeniambukiza hili gonjwa la globu...
mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni; freddy na ndesanjo macha ni kioo cha uandishi bongo
kaka Michuzi nadhani kidole kiliteleza wakati "unabonyeza kibara."
ReplyDeleteNadhani kwenye maelezo haya ulitaka kuandika BLOG na sio GLOB kama ilivyojitokeza mara 2.
Kama sivyo basi nisamehe bure!
Hata mimi alinihamasisha sana kupenda na kuingia kwenye maswala ya pafomansi aat.
Hivyo hivyo hakika wanyonge wanyongeni haki yao wapeni. These talents funika bovu. Globu ya Freddy ni darasa tosha kama ilivyo wavuti wake/yake.
ReplyDeleteSorry to ask you this Ndugu Michuzi, are you a journalist or a cameraman? because sometimes, I get confused by people saying you are more cameraman than a "professional journalist". I'd appreciate your kindly answer.
ReplyDelete