
bosi wa taasisi ya utangazaji dunstan tido mhando (kati) akila stori na mabosi wa gtv. taasisi hiyo ambayo inaendesha televisheni ya taifa, redio tanzania dar na prt fm leo imeingia mkataba na kampuni moja ya ughaibuni itayotoa huduma za mtandao ambapo kuanzia ijumaa ya wiki ijayo tvt, rtd na prt zitaweza kupatikana kwenye mtandao
Safi Tido kwani hiyo TVT, RTD walikuwa nyuma sana, sio MD aliyekuwepo mambo yake ya kishamba na ya kizamani. Inyanyue labda itaendelea.
ReplyDeletehiyo bomba, michu usisahau kutumwagia linki.
ReplyDeleteBwana asifiwe sana!! Na wote tuseme Amen. Usisahau kutupa link kaka Michu, I cant even wait!
ReplyDeleteHiyo Ni Hatua Moja Mbele! TUT Inastahili Kuungwa Mkono Na Watanzania Wote Popote Walipo.Kwani Mechi Ya Msumbiji v/s JK Boyz Itaonekana Mtandaoni!
ReplyDeleteIzz Wa
Hayo maneno! Inaelekea kuna mwanga mpya Taasisi ya utangazaji. Keep it up!
ReplyDeleteNAKUPONGEZA BRO TIDO.
ReplyDeleteILA MSIWE MNAJISAHAU KUBALANCE HABARI.HIVYO VYOMBO NI VYA UMMA SIO VYA KWETU SISIEMU TU.
ENE WEI TUTAFIKA TU MWANZO MZURI.ALAFU TIVITI MPUNGUZE VIPI VYA NJE HASA CHINA.
TUNATAKA TUANGALIE IPOGOLO,LUPASO,NDANDAIMA,NYANGUGE,IBITABAGUMBA N.K
Safi mlikuwa wapi hata kuzidiwa na radio Maria inayopambana kuzuia tu kondomu bila kujua kuwa wapo wasio waaminifu ambao kondomu inakuwa ni jibu la kuwaokoa au pia hata kwa waaminifu bado pia kondomu ina matumizi mazuri tu ya mpango wa uzazi n.k.
ReplyDeleteAidha mpango huu wa kuwa mtandaoni utasaidia kuleta pande zote za shilingi na kubalance taarifa kamambe za mwanakijiji kama mtaweza kujadili hoja kwa hoja!
Hongera Tido Mhando, maana Redio One, Clouds FM, Radio Free Africa zimeshindwa kutumia technolojia ya mtandao. Redio Maria ilionyesha njia na sana Radio za Serikali zinaonyesha kwenda na wakati. Tunasubiri kwa hamu kuona matangazo ya TVT, PRT na radio TZ live kwenye mtandao bila kupitia kwa viji kampuni vya ulaya kama TVT ifanyavyo sasa. Tunataka Tanzania iwe hewani dunia nzima kwa kutumia wataalamu wetu hapo nyumbani.
ReplyDeleteMdau
London
duuu hongera sana tido maana nilikua nashangaa kuona nchi nyingi tuu zina tv kasoro tanzania hata radio hatuna ilikuaa inanipa shida kidogo, kwa maana hiyo hata mpira wa taifa staz na msumbiji tutauona live kupitia tvt au sio michuzi
ReplyDeleteKukaa ughaibuni kuna faida zake na mwenye nguvu usimkinge, ungana nae. Tido anaipeleka baruti kishenzi taasisi na nnajua kuna watu fulani hiyo kasi hawaiwezi, watachomoka soon.
ReplyDeleteTVT sasa hivi safi sana, tunaona soka mtu wangu, sio kila siku makala za wanyama tu. Yani hata kuangalia tamthilia siku hizi tunalipwa, dah, udumu Tido.
Pale kwenye mahojiano live kati ya studio za Dar na wabunge kule Dodoma ndio umeniacha hoi kabisa.
Kanyaga twende baba.
Hongera TUT
kama Ni kweli tutanenepa Na hongereni ila angalieni tu tukijaa huwa mnazifunga wenyewe..hehehe kaazi kweli kweli
ReplyDeleteTunampa hongera sana Bwana Tido kwa hatua hii. Lakini hapa kuna walakini kidogo. Maana mpaka sasa hivi TUT haina wavuti wake (website), mimi nafikiri wangekuwa na wavuti ndiyo tungeona mambo yanakwenda safi. lakini sijuiiiiiii
ReplyDelete