shirikisho la soka bongo leo limetangaza viingilio kwenye mechi ya taifa staaz na msumbiji kwenye uwanja huu hapo septemba 1 dhidi ya uganda.
kasema kutakuwa na sehemu za vip A ambao watalipa 30,000/- vip B ni 20,000/- na vip C ni 10,000/- ambapo kwenye rangi ya chungwa ni 5,000/ na kajamba nani ni 3,000/-
vile vile leo tff imekaa kimya kujibu kampuni ya easy finance iliyotaka kununua mechi hiyo kwa milioni 300 kwa kile ambacho redio mbao zimesema tff inategemeqa kuvuna milioni 800 hivi. yetu macho.taifa staaza wanarejea kesho jioni na kukutana na uganda jumamosi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. MICHU Kajamba nani ndio sehemu gani ktk huu uwanja mbona sehemu zote sawa au kuwa mbali na mgeni wa heshima ndio kajamba nani?

    ReplyDelete
  2. Sasa kajamba nani ndio wapi hapo Michu maana naona rangi ya chungwa imetanda mpaka chini.

    ReplyDelete
  3. Kwa ufafanuzi kuhusu "mkao" uwanja wa neshno stediumu bofya kiunganishi hiki http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=1367

    ReplyDelete
  4. Kaka Michuzi hivyo viingilio bado ni vidogo kama kweli tunataka kuu-mentein huu uwanja wetu vizuri.
    Uwanja huu ni umetumia pesa nying na ni vizuri ukaendeshwa ki-business ili uweze kujiendesha wenyewe na sio kuoneana huruma halafu baadae kuishia kuomba MARUZUKU serikalini. Come on!
    Viingilio hivyo vikiendelea namna hiyo uwanja huo wala hautadumu.
    Mtakuja kukumbuka maneno yangu haya. Shauri zenu.

    ReplyDelete
  5. MICHUZI UMEKOSE HICHO KIINGILIO NI CHA MECHI YA STARS NA UGANDA NASIO STARS NA MSUMBIJI. NI CHA ILE MECHI YA KIRAFIKI SEPTEMBA MOSI. KIINGILIO CHA STARS NA MSUMBIJI HAKIJATAJWA BADO NA NADHANI KWA TAMAA YA TFF KITAKUWA KIKUBWA SANA. MECHI YA KIRAFIKI TUU WANAWEKA KIINGILIO KIKUBWA HIVI JE YA MASHINDANO ITAKUWAJE?? HIYO MECHI NA UGANDA UWANJA HATA NUSU HAUTAJAA NAKUHAKIKISHIA, WATU WATAKUWA NANAHIFADHI PESA ZAO KWA AJILI YA MECHI NA MSUMBIJI. JAMAA WANA TAMAA SANA!!

    MZOZAJI

    ReplyDelete
  6. Jamani wabongo tuache kulalamikia kila kitu hata pasipo sababu.

    Hivi kweli mnataka kusema sh. 3,000 na 5,000 ni nyingi kwa wapenzi wa mpira wa Dar? Hivyo si ndo viingilio vya kawaida kwenye uwanja wa zamani?

    Kilichoongezeka ni viingilio vipya, ambavyo ni kwa viti maalum (vip). Mnataka kuchanganya watu wote, muwachomolee wake zetu gold zao, siyo?

    Viingilio vya sh. 3000 na 5000 vitaingiza watu zaidi ya 40,000 ambao ni wengi mno, kupita kiasi chochote wa washabiki kuwahi kuona mechi moja hapa Tanzania. Kwa statistics tuu, watu walioingia CCM Kirumba kuona mechi ya T-Stars vs Senego ni kama 22,000 tuu. Na viingili vilikuwa kati ya sh. 10,000 - 3,000 kama sikosei. Sasa hao watakaoshindwa kuingia sababu ya kiingilio watatoka wapi wakati nafasi zipo 40,000?

    Viingilio vikubwa lazima viwepo, ili watu wasiotaka vurugu kuingia, kutoka, na wakati mechi inaendelea wakae na nafasi zao. Ndio mana mwingine atakuwa tayari kulipia 30,000 kuona mechi ile ile ambayo mwingine analipa 3,000. Ila hii ina maana aliyelipa 30,000 hatakaa kwenye foleni kwa muda mrefu. Hili ni jambo la kawaida sehemu zote. Wale wanaosafiri kwa ndege wanafahamu kuna business class na economy class ingawa ndege ni ile ile!

    ReplyDelete
  7. YOTE TISA. MIMI NINGEKUWA MDAUWA TEMEKE NINGEFANYA JUU CHINI KUHAKIKISHA WANJA HILO LINAZALISHA MAMILIONI KILA MWAKA.
    KWANZA NINGEWASHAURI WACHINA WAJENGE ARENA PEMBENI KIDOGO YA UWANJA HUO AMBAO UNGEKUWA UNATUMIKA KWA STAREHE ZOTE ZA DISCO, MATAMASHA YA MUZIKI WA DANSI NA HATA MAPAMBANO MAKUBWA YA NGUMI.
    PILI NINGETAFUTA WADAU WAJENGE HOTELI ZA NYOTA TANO (FIVE STARS) ILI WATALII NA TIMU NGENI ZINAPOFIKA WANAPOFIKA WASIHANGAIKE KUTAFUTA HOTELI ZILIZO MBALI NA UWANJA HUO PAMOJA NA ARENA YAKE.
    TATU; NINGEKUWA NAANDAA ANGALAU MECHI KUBWA ZA KIMATAIFA ZITAKAZOSHIRIKISHA TIMU ZINAZOCHEZA LA LIGA, LIGUE 1, EREDIVISE NA PREMIER LEAGUE KAMA WANAVYOFANYA JAMAA WA THAILAND, KOREA WANAKOALIKA TIMU ZA ULAYA NA KUFANYA MASHINDANO MBUZI.
    NADHANI WADAU WANAOANGALIA MECHI KWENYE LUNINGA, WANGEKUWA WANAJIMWAGA KILA SIKU KUSHUHUDIA WACHEZAJI WA TIMU ZAO WANAZOSHABIKIA KAMA VILE ARSENAL, REAL MADRID, PSG, MAN. UNITED, BWAWA LA MAINI, AJAX NA NYINGINEZO.
    NDIYO. KWENYE MITI MARA NYINGI HAKUNA WAJENZI. UWANJA HUO KAMA UTAPATA WATU WANAOJUA KUTENGENEZA FEDHA, WATARUDISHA FEDHA ZOTE ZA GHARAMA ZA UJENZI. WOTE WANAFANYA HIVYO.

    ReplyDelete
  8. that is so damn cheap kwa mwendo huo tutaweza kulimaintaini liwanja letu.
    Sijawahi kwenda kwenye show yeyote kwenye viwanja vyao hata iwe mechi mbovu zaidi kuliko zote....the cheapest you can get ni dollar 35

    Tukitaka usafi lazima tulipe pesa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...