si dar pekee inayopigwa sop sopu. hapa ni a-taun. pia si vibaya kama utapitia globu ya mtani mmoja wa jadi juu ya shirikisho la ist afrika mashariki hapo chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. We Michuzi,
    hapa sio Kigogo round about?

    Toka lini Arusha kuna minazi? ningeona Acacia tree ningekubali lakini sio mnazi.

    leo wadanganye wengine sio mimi.

    hapa sio A-Tauni, hapo ni Kigogo-Dar njia panda.

    ./

    ReplyDelete
  2. Michuzi hiyo ni A-Town sehemu gani? Naona imekaa kama round-about ya Kigogo vile.Naona Arusha kuna minazi mingi sana siku hizi!

    ReplyDelete
  3. Hii roundabout ni ipi tena jamani?Maani nimezaliwa A.City lakini hapa mmenipiga doba.

    ReplyDelete
  4. MICHUZI HAPO SIO ARUSHA... HAPO NI DAR ES SALAAM... KAWAWA ROAD ktk ROUND ABOUT ya KIGOGO enzi zile kulikuwa na sanamu ya Twiga pale...Si waona kibao chini kushoto... Ha ha haaa Arusha hamna sehemu kama hii kwanza nilidhani ROUND ABOUT YA IMPALA lkn sioo... please verify Michuzi...

    ReplyDelete
  5. JAMANI MSIMBISHIE KAKA MICHUZI UNAWEZA KUKUTA HIYO MINAZI NI YA PLASTIC WAMEICHIMBIA KWA AJILI BILL CLITON AKIJA AONE TUMINAZI.
    SI UNAKUMBUKA BILL ALIPOFIKA FESTI TAIMU ARUSHA BARABARA ZILIPIGWA DEKI AU MMESAHAU

    ReplyDelete
  6. ya leo kali misupu,yaani wazee wazima unataka kutufunga kamba mchana mchana,mhhh nimekushtukia.hapa ni kigogo roungabout mjomba,tuombe radhi mshikaji kabla hatuja kunanihii.

    ReplyDelete
  7. Kwakweli hata mimi kakamichu na kukatalia hapo si arusha kwa sababu ya minaza na arusha hakuna barabara yenye double lane, ila sibishi kuwa roundabouts za arusha zimenakshiwa na city clocks ikiwa ndio ilipelekea kutuwekea picha kama hii, wadanyanyika tuko makini!

    ReplyDelete
  8. Nimefurahi kuona wabongo wamejifunza kuona vilivyoko kwenye background maana ni watu maalum wenye kuweza kuchambua picha kuona kila detail iliyomo. hongera uliyeona minazi maana wengi huona kilichokwenye focus ya mpiga picha tu watu kama nyie mnaweza kabisa kutumika katika picture forensics.

    ReplyDelete
  9. Hiyo picha ni A-Town pale mnara wa saa, karibia na shule ya msingi ya Uhuru. Ukienda mbele Sheikh Amri Abeidi. ACheni Kubisha

    ReplyDelete
  10. Duh, Michuzi noma, kauchuna kama vile hajakosea.

    Haya bwana misupu, jambo kimoyo moyo unajua kabisa umechemsha hapa, waombe radhi wadau mshkaji, Mimi aah, sijui lolote, Arusha sijawahi fika hivyo nilikubali kama ulivyopendekeza, lakini kwa maoni ya wadau wengine, mh!

    Huu sasa mzozo michu!

    ReplyDelete
  11. Mmmmmh!!!!!Nafunga mjadala. Yani michu leo umenipata kwelikweli.Yani umenipa changa la macho.Mimi na ujanja wangu wote nshaamini kama hapo ni A town.Nimeoka A town miezi 6 ilopita sijui nilikuw nawaza nini na kuamini kama hapo ni A town.Ila Anon wa kwanza katufumbua macho.Am sure kama yeye angeingia mkenge basi ungevunja mbavu kwa kusoma mlolongo wa maoni ya kuchemsha.Wadau, Geografia hamkuibia nini mlipokuwa sekondary.
    Big up misupu
    Majita

    ReplyDelete
  12. Shida yenu mnadhania minazi inakua tu Dar na Pemba, mkae mkijua kuwa hata mikoani minazi pia inakua, inaweza kuchuka miaka lakini pia inakua, Arusha minazi ipo moja moja, na inategemea, sometimes si minazi inayozaa bali ni miti tu, kwa hiyo hiyo inawezekana kabisa, na saa nyingine miti mingine(mfano wa minazi) inapandwa kwa urembo jamani eg Pine trees, mh kwa kukosoa hamjambo, fanyeni research kwanza!!!!

    ReplyDelete
  13. Arusha kuna mnazi mmoja tu, tena upo maeneo ya Mianzini kama sikosei. Sio kwamba hawapendi iwepo, ila nafikiri hali ya hewa ya Arusha hairuhusu (sina uhakika msije nimeza bureee, sijasomea kilimo ebo!)

    Piga ua, hii sio Arusha nitakataa mpaka kesho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...