Thobias Mwanakatwe wa PST, Chunya, anaripoti kuwa Msafara wa NaibuWaziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantum Mahiza jana ulipata ajali baada ya gari waliokuwa wakisafiria kugongwa na lori.
Msafari huo ulikuwa na maofisa wa Idara ya Ukaguzi Nyanda za Juu,waandishi wa habari na askari.Ajali hiyo ilitokea juzi 11:45 jioni katika kijiji cha Luwanjilowilayani Chunya Mkoani Mbeya wakati msafara huo ukitokea katika ziaramjini Chunya kurudi Mbeya mjini.
Lori hilo lenye namba za usajili T 683 AFK liligonga gari lenye nambaSTK 3170 ambalo lilikuwa likiongoza msafara wa Naibu Waziri huyo likiendeshwa na dereva Abel Mwakatete likiwa limewabeba maofisa hao.
Maofisa wa Idara ya Ukaguzi waliokuwa katika gari hilo lililogogwa niNaibu Mkaguzi wa Kanda, Mama Arevo, Mkuu wa shule ya Sekondari Tukuyu,Bw. Wakili Mwangoka, mwandishi wa habari wa RTD na mwandishi wa habariwa Kampuni ya The Guardian, Bw. Thobias Mwanakatwe pamoja na askari,Sajenti Seif ambao hata hivyo hawakujeruhiwa.
Lori hilo baada ya kuligonga gari hilo la msafara halikusimama nabadala yake aliendelea na safari zake ambapo Naibu Waziri na watuwaliokuwemo katika msafara huo walilazimika kusimama kwa nusu saakutafakari kinachoendelea.
Askari wa kitengo cha usalama barabara Sajenti Seif aliyekuwepo katikamsafara huo alimweleza Naibu Waziri kuwa gari lililogongwa ligeuze ilikumfukuzia dereva huyo wa lori lakini pamoja na kumfukuza dereva huyona kusimishwa alikataa kata kata kusimama na kuendelea na safari yake.
Jitihada za kusimamisha lori hilo ziliposhindikana ilibidi askari huyoawapigie simu wenzake waliokuwepo kituo cha polisi Chunya na kuwaamuruwalikamate gari hilo mara litakapofika ambapo taarifa iliyotolewa janausiku zilionyesha kuwa dereva wa lori hilo alikuwa tayari amekamatwana polisi.
Wakati huo huo, msafara wa Waziri Mkuu Edward Lowassa aliye mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi asubuhi ya leo ulipata ajali baada ya magari kwenye msafara huo kugongana yakiwa yanatoka nyumbani kwa Spika wa zamani Mh. Pius Msekwa kijijini kwake Ukerewe.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Zelothe Stephen, watu sita walijeruhiwa katika ajali hiyo, watatu ambao ni madiwani wa maeneo hayo vibaya sana, na wamelazwa hospitali ya wilaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Temba alishasema huu ni mwaka wa Shetani hamkumsikia, sasa alaumiwe nani???....

    hii haijakaa sawa...

    ./

    ReplyDelete
  2. Kabwe mwezi mtukufu huu, wahurumie manake utawamaliza sasa. Kizizi hicho sio mchezo..

    ReplyDelete
  3. Hii pia ni kutoka jambo forum....Kwa wale msiopitia blog nyingi but this ni vizuri kuona pia na kujiuliza ...labda kuna ukweli ndani yake ...kama upo tumwombe Mungu awasamehe na majanga haya yawapitie mbali

    "Hivi sasa kuna hali ya hatari hapa nchini kwetu,na pia mimi ninaamini kuna adhabu ya Mungu ili kuokoa watu wake.
    Baada ya malumabano yaliyotokea katika kikao cha bunge la bajeti kilichopita ambacho kikapitisha mhe zitto (mbunge wa kigoma kaskazini) wale wote waliomsakama,kushawishi na kumletea nyodo walikutwa na mabalaa na majanga kama ifuatavyo:
    RUTH MSAFIRI MBUNGE WA MULEBA KASKAZINI,mara tu baada ya kikao mume wake akapata ajali mbaya sana ya pikipiki iliyompelekea asafirishwe mpaka muhimbili na baati mbaya akafariki dunia,japokuwa haikutangazwa sana katika vyombo vya habari.
    PETER SERUKAMBA MBUNGE WA KIGOMA MJINI,mara tu baada ya kikao alipata ajali mbaya sana na gari lake aina ya land cruiser vx ya ubunge ambayo ilibaki kama chapati(written off) na haiwezi tena kutengenezeka hata kidogo ila yeye alifanikiwa kunusurika,japokuwa haikutangazwa hata kidogo kwenye vyombo vya habari.
    ADAM KIGHOMA MALIMA MBUNGE WA MKURANGA,mara tu baada ya kikao akiwa anatoka jimboni kwake akiwa na gari lake la kifahari alipata ajali mbaya sana maeneo ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere japokuwa yeye alinusurika ila gari yake hiyo ambayo ni prado new model kama ya marehemu chifupa ilikuwa kama chapati,bahati nzuri yeye alinusurika,ila haikutangazwa sana kwenye vyombo vya habari.
    MUDHIHIRI MBUNGE WA MCHINGA,sina haja ya kumzungumzia mana wote tunajua hivi sasa anapata chakula kwa mkono wa kushoto sio kulia tena

    NA HIVI SASA KAPUYA,

    MWENYEZI MUNGU TUNUSURU"

    ReplyDelete
  4. hii sasa sio mungu mtupu kuna na mkono wa zitto hapa,

    ReplyDelete
  5. hizi ajali zinatokea kwa viongozi hili waweze kuona jinsi gani sheria za barabarani bongo zinatakiwa kufuatiliwa ki sawa sawa hili kuokoa maisha ya watu....

    ReplyDelete
  6. Sheshe/lisheshe babu kubwa na sio kasheshe tena.

    ReplyDelete
  7. Hapo sasa nyoka kamng'gata binadamu,kila siku raia wa kawaida wanakufa kwa ajali no body cares.Tungoje tuone sasa nini kitatokea,lazima wataanza kulaumu barabara ni mbovu,matairi ya magari hayana uimara na mambo mengine meengi and then watamuingiza Shekh Zuberi Kabwe Zitto atlast.Yetu macho.

    ReplyDelete
  8. Mkapa alipoingia madarakani ajali mbaya sana za meli, treni na mabasi ziliua raia wengi(kafara)huyu JK yeye ajali zinawarudi viongozi wenzake.
    Halafu nakumbuka Sheikh Yahya alitabiri mwaka huu watakufa viongozi mashuhuri wa kitaifa au kimataifa, sijui itakuwaje??

    ReplyDelete
  9. WABONGO MNALALAMIKA NCHI YETU MASKINI BADALA YA KUFANYA KAZI NYIE NA RAMLI...
    ENDELEENI KUPIGA RAMLI SISI TUNAFANYA KAZI
    MDAU USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...