ghafla bin vuuup wabongo wameibuka na uzalendo wa kuipenda bendera yao kiasi kwamba tofauti na ilivyokuwa awali sasa inapatikana kila mahali kama njugu na kuwekwa popote, hasa hasa mechi ya jana na msumbiji ilipokuwa inakaribia. wadau mnalionaje swala hili?


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Uzalendo ni jambo zuri, na nivizuri watanzania wakajivunia nchi yao

    ReplyDelete
  2. Michuzi uzalendo poa, tena nasikia siku hizi wanafunzi wa darasa la saba au wale wakwenda form five wakipasi mitihani yao basi wanatundika bendera na schoolbag nje ya nyumba.
    WE LOVE TANZANIA

    ReplyDelete
  3. Walionunua hizo bendera sasa zitakuwa mzigo baada ya kuwa "kichwa cha mwendawazimu" kimechemsha safari ya kuelekea Ghana! Na kwa wale wajasiriamali ambao michuzi anawaita mechandize ambao bado hamjauza hizo bendera tegemea hasara.

    ReplyDelete
  4. HIVI UZALENDO WA UNAPIMWA KWA KUPEPERUSHA BENDERA TU? MBONA WENGI WA HAO WAPEPERUSHA BENDERA NDIO WALA RUSHWA WA KWANZA? HAO NDIO WANAOIDUMAZA NCHI.

    ReplyDelete
  5. Broza Michu! Hiyo picha juu ni nini? TTCL kuna watu kibao hivyo au ni msongamano wa watu wa kila siku ...duh Bongo????!!

    ReplyDelete
  6. Siku za nyuma ilikuwa ni kosa kuwa na bendera ya Taifa au kuitumia kwa namna yoyote ile kinyume cha maagizo. Sijui nani alilegeza sheria hiyo.

    ReplyDelete
  7. Mtikila alishawahi kuipeperusha bendera ya Taifa lakini akaambiwa kwamba ni kinyume cha utaratibu kwa kuwa bendera ni nyara ya taifa, na yeye kuipeperusha hiyo bendera ni kosa la jinai.

    Vilevile, Mbowe wa CHADEMA aliwahi kuipaka helikopta yake rangi za bendera ya taifa na akaambiwa hivyohivyo.

    Michuzi, mimi binafsi nafikiri serikali yetu ina u-double standard wa hali ya juu. Bendera ikitumika na wanasiasa ambao si wana CCM inakuwa dhambi.. Ikitumiwa na wengine kuisifu serikali inakua ruksa.... Nakuomba michuzi utumie taaluma yako ya uandishi wa habari vizuri kwa kwenda kumwuliza hili swali waziri anayehusika na mambo ya ndani then uje utupatie jibu. Wakati unamwuliza hilo swali ugusie pia na mifano ya Mtikila na Mbowe halafu utupatie jibu kadri atakavyokueleza.

    Shukran

    ReplyDelete
  8. Kaka Misosi hizo foleni za nini tena hapo? mbona sielewi kidogo? hilo jengo lenye TTCL sidhani kama nalikumbuka, hebu nielezeni wadau kuna nini hapo? wamejipanga kwa sababu gani?
    Chikaka

    ReplyDelete
  9. Anonymous wa September 9, 2007 1:45:00 PM EAT, unataka kujua ni nani kalegeza mwongozo huo?

    Ni adui wa Ujamaa. Jina lake anaitwa Ubepari!

    ReplyDelete
  10. NAHISI HII NI JEIFONGO AU NIMEKOSEA Sir MICHU

    ReplyDelete
  11. UZALENDO ni jambo la msingi sana, lakini uzalendo wa MSIMU ni jambo la kipuuzi sana.
    nionavyo mimi, watz wengi tu wazalendo wa msimu. tena pale tu ambapo neema au dalili za neema zinapoonekana. otherwise, we are by-standers.

    kwa kudhihirisha hili, Michuzi na wadau wengine mtakubaliana nami nikibashiria kwamba itachukua muda sana kwa umati uliofurika jana neshno kuijaza neshno mpya kama ilivyojaa jana. labda waje Real Madrid!

    Kiwango cha uzalendo kilichoonyeshwa ktk siku chache zilizopita ni vyeme kiendelezwe na kamwe tusirudi nyuma. na la msingi kabisa ni kwamba tuuhamishie uzaendo tuliouonyesha ktk masuala ya maendeleo ya jamii na tenda kwa VITENDO na si kwa kkuishia kuvaa na kupepea bendera ktk magari na sehemu nyinginezo

    ReplyDelete
  12. Huyo aliyezuia alikuwa mwendawazimu na mlimbukeni. Maana viongozi wetu kwa ulimbukeni na uzandiki hawajambo. Huku nje wenzetu kuanzia mtoto mdogo anafundishwa uzalendo ikiwa ni pamoja na kuwa na timu anayoi-support na bendera ndio kielelezo cha uzalendo uliotukuka. Wenzetu wanashonea nguo kabisa utasikia hata mtoto akisema I'm proud of an American, proud of being British. Sisi wengine ni kung'aa macho una ujasiri kusema I'm proud of being Tanzanian? Kwanza haijulikani ikijulikana ni kwa matatizo ambayo yamekuzwa zaidi hapa Ulaya.

    Huku wabongo utawaona kama kuku walionyeshewa, watoto wasio na baba. Sasa ndio usikie viongozi wetu wanatupa rasimali zetu bure. Kwa kweli tunapata uchungu kwa kiwango cha kutisha. Hawa wajamaa wanatudharau na kutunyanyasa sana.

    Jamani tuwe wazalendo maana ndio sehemu pekee utaheshimika. Siku moja tulienda kuangalia mechi, mi na Mganda moja tulikuwa tunashabikia ManUTD. Siku hiyo ManUTD ilishinda kwa mabao mengi. Tulivyokuwa na sisi tunashangilia kuna wazungu wakatuuliza kwanini na sisi tunashangilia ManUTD inatuhusu nini? Pamoja na mambo mengine tuliumia kiaina. Mtu kwenu jamani, huku sisi wakupita tu!

    ReplyDelete
  13. bendera ni heshima tosha hata watalii watu jua sasa kwamba uzalendo upo bongo hii ndio inatakiwa

    ReplyDelete
  14. jamani ubepari ni jambo moja zuri sana yaani jk ni bomba. enzi za nyerere kuwa na bendera ya taifa ni noma siku hizi ni kama kumpeleka mleve vile. sasa kilchobakia tu ni kwamba jk aruusu kuwa na DUAL CITIZENSHIP.....ILI WAZAWA WALIOKO NJE WAPETE TUUUUUUUUUUUUUUUUUU
    kasera
    kc,ks

    ReplyDelete
  15. Feedback ya annon wa September 9, 2007 3:55:00 PM EAT, utaileta lini kaka? Mbona siku zinaisha? Au ndio ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya nini?

    ReplyDelete
  16. Misoup lini utatoa feedback? Picha hizi zitapotea kesho na tutashindwa kufahamu tutapataje jibu. Toa basi usemi wako tujue lini utatuletea majibu kutoka kwa wahusika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...