
Asalaam alaiykum,
Mimi ni RAMADHANI, Nilimpa ujumbe Rajab akuletee, Nikamtuma na Shaaban akuambie kuwa nipo njiani.
NAKUJA na mke wangu SWAUMU na watoto wetu watatu: 1.Rhma, 2.Maghufira, na3.Tauba. Pia sijamuacha rafiki yangu wa damu QURAAN, na ndugu yake QIYAMU LAIL.
Sitokaa nawe kwa muda mrefu, nitakua nawe kwa mwezi mmoja tu, ukisha tutaondoka kumpisha, EID -EL-FITRI na hatimae Sitat – Shawwal, ambao watawasili kwa kupishana.
Utupokee kwa mapenzi yako yote, na ututunze kwa kipindi hiki kifupi kwani tukiagana huna uhakika wa kutuona tena mwakani.
RAMADHANI MUBARAK !!
“Enyi Mlioamini! Funga ya Ramadhani imefaradhishwa kwenu kama ilivyokafaradhishwa kwa wale waliokuwa kabla yenu ili mpate tauba” (QURAAN Surah Al-Baqarah 2:183) (Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchamungu)
Nakutakia maandalizi ya funga njema ya mwezi mtukufu wa Ramadhan…shahar tauwba..
M.M. Juma


Tutaukaribisha, ila kama unavyojua tunamuogopa kidogo huyo Saumu.
ReplyDeleteMungu atatujaalia Inshaaalah
Kila la kheri wale wote ambao watakuwa katika Swaum. Allah awape nguvu inshaallah
ReplyDeleteJamani huu ni mwezi mtukufu fungeni na mfunge kikweli.Najuwa maboksi na swaumu haviendi pamoja,lakini jinyimeni kwa mwezi mmoja. Kwa wale waongo kuweni macho-angalieni tusije kupigana vikumbo kwenye ma-buffet,mac d's mishale ya alasiri.
ReplyDeleteHuwa nashidwa kuelewa kwanini yule mdudu(kitimoto)anakosa sana wateja Pale sunmarino? Askofu
ReplyDeleteKaribu, karibu mgeni.. unajua eeeh, kama vile umetushitukizia ee... ingawaje kwakweli tulikuwa tumepata taarifa kuwa unakuja, lakini wengine mara wasema utakuja leo wengine kesho.Unajua tena..
ReplyDeleteJisikie upo nyumbani. Ila jamaa wa ukoo wa ulevi, wapo hapa na rafiki zao ukoo wa uzinzi, wamepandisha kile kichaa chao karibu mwaka mzima sasa. Baya zaidi wamewaambukiza na ukoo wa bangi na watoto wao madawa ya kulevya. Hatusemi kitu kwani wake zao, akina usengenyaji,rushwa fitina, chuki na wajomba zao akina ujambazi na wezi wanawasaidia kwa kila hali. Huenda mgeni wetu utatusaidia kuwapa ile dawa ya kuwapoozesha angalau kwa mwezi huu utakaokuwepo, Alhamdullilah, Karibu sana.