

waziri wa madini na nishati mh. nizar karamagi ametangaza sasa hivi hapa dar kwamba atamfikisha mahakamani mbunge wa karatu (chadema), mh. dk. wilbroad slaa kwa madai ya kumkashifu na kumchafulia jina lake baada ya kumtuhumu kwa ufisadi katika mkutano uliofanyika septemba 15, 2007 katika viwanja vya mwembeyanga temeke.
mh. karamagi, ambaye amewasomea waandishi taarifa hiyo hapo juu ofisini mwake, amesisitiza kwamba yeye ni muadilifu na ameamua kwend mahakamani ili kutafuta haki yake dhidi ya wale wote ambao amesema wameshiriki na wanaoendelea kushiriki katika vitendo vya kumpaka matope.
amesema ameshawaelekeza mawakili wake kufungua kesi mahakamani mara moja dhidi ya mh. dk. slaa, gazeti la mwanahalisi na kwianda cha printech ambacho anadai kilichapa matokeo ya gazeti hilo lililobeb kashfa hiyo.
Watu wengine wanapenda makesimakesi! Mmmekuwa Mrema? Si uwashiti tu?
ReplyDeletewatakuMUDHIHIR wewe! Shauri zako.
Ushauri wa bure huo nakupa.
uyo karamagi asijidai kwenda mahakamani wala nini yote yanayosemwa juu yake ni kweli, anajitajirisha tu na fedha za wananchi tena viongozi wengi wa serikali ni wala rushwa tu wasijidai nini wala nini.
ReplyDeleteHaa jamaa hana sela leo ameamua kwenda mahakani yeye ajui aende bungeni akamshitaki bungeni ili na yeye afukuzwe sio aende mahakamani, Unajua hayo yote bila shaka angejiuzuru leo yasingetokea haya yote ila kwakuwa yeye ni mbishi watu watamwambia mpaka ajue watu hawana imani nae, Hapa kuna mashaka hata Raisi nae anakubali uongo wa huyo jamaa sasa hata wanakosa imani na raisi kuhusu huyo jamaa lakini samaki akioza mmoja wote wameoza. Sasa raisi hata kama ameziba pamba masikio au jamaa alikuwa kwenye mtandao ndio maana anambeba lakini ajue wananchi wamechoshwa na huyo jamaa. Kaka Michuzi huu ni ushauri wa bure kwa huyo jamaa huu sio wakati wa kwenda mahakani huu ni wakati wa yeye kujiuzulu ndio suluisho ya haya yote yasitokee.
ReplyDeleteNADHANI HII NI HATUA NZURI KWANI MAHAKAMANI AT LEAST TUNAWEZA KUSIKIA MENGI AMBAYO WAJANJA KAMA MH. MKONO HAWAKUTAKA YASIKIKE
ReplyDeleteKwa sheria za nchi yetu Mh. Karamagi ana haki ya msingi ya kufungua mashitaka mahakamani kama anaona hajatendewa haki. Wasiwasi wangu ni pale atakapotakiwa kuthibitisha uongo uliotolewa dhidi yake kwa nyaraka. Naamini mahakama itahitaji documents kutoka kwa Dr. Slaa na yeye atatakiwa kuwasilisha documents zake kuonyesha how genuine are they. Mahakamani hakuna longo longo ya wingi wa kura kama bungeni. I presuppose the Pandora box is now open!!!!
ReplyDeleteBy the way nimesikia Mh. Kapuya kapata ajali, je ni kweli? Kama ni kweli nampa pole sana na kumtakia apone mapema.
hakuna jambo lisilo wezekana kujastify inapolazimu....hapo jamaa kaona ajustify tu ila ukweli anao...na ivo ashawajuwa wadanganyika basi wala hata haimgharimu...haya bwana tuone...
ReplyDeletehata mbakaji akifumwa live hakosi sababu..ivo hata jamaa uwezo wa kukanusha uko wazi bwana...
ReplyDeleteUjinga mtupu, utawashtaki wangapi? Haya sasa huko mahakamani kutakuwa kutamu ukiambiwa elete ushahidi watu wanamwaga hapo ndio jasho litakutoka.
ReplyDeleteMasikini Karamagi! Mpaka hiyo kesi ije imalizike mahakamani nadhani hata uwaziri atakuwa kamaliza na pengine CCM imeshatoka madarakani siku nyingi! Hajui mpaka kina Slaa wameamua kutake risk kubwa hivyo wamejiandaaje. Haoni mpaka mabalozi wameanza kutoa tamko? Hapo dawa ni JK kujibu hoja kwa hoja period.
ReplyDeleteSAWA SAWA KABISA MIMI NILITAKA NA YEYE AJUE KUWA HATUNA IMANI NAYE NA KWA HILI LA BUZWAGI AJIUZULU
ReplyDeletekaramagi unachemka sana wewe binadamu gani unaweza kuingia mikataba ya aibu vile harafu unaweza kubisha wewe sio mla nchi,...nenda mahakamani tutakufata huku huko kuja kutoa ushahidi'
ReplyDeletetatizo mmefanya watanzania wajinga hawezi kufikiri now its a time fight for fruits of being tanzanian
.
Only in Africa where a minister can sign a contract worth millions of $ not only outside the country but also in a hotel while Embassy offices are available. This is absurd and unacceptable.
ReplyDeletePIMA MAJI TU BOSI
ReplyDeleteHII SASA NI HATARI
ReplyDeleteHivi kuna nini ama ni adhabu ya Mungu kuwaokoa watu wake?
Baada ya ubabe ndani ya Bunge na kumuondoa bwana Zitto Bungeni na Bunge kuvunjwa wale wote walio msakama na kumfanyia nyodo wamesha kutwa na haya yafuatayo
Kwanza alianza Ruth Msafiri wa Muleba Kaskazini. Mumewe alipata ajali mbaya ya pikipiki na kukimbizwa Muhimbili na alifia hapa Mhuhimbili lakini haikutangazwa .Baadaye Peter Selukamba akiwa anaendesha mwenyewe alinusurika kifo baada ya gari lake kuwa kama chapati yaani ile VX yake ya Ubunge na hadi sasa gari halitamaniki lakini akapona kuumia . Hawakuandika kokote wakafanya siri. Siku hiyo hiyo Mbunge Malima akiwa anaendesha yeye mwenyewe akapata ajali pale uwanja wa JK Nyerere akanusurika kuumia lakini gari inahitaji matengenezo makubwa waandishi wa majira kimya hawajasema lolote .
Baadaye akaja Mudhihiri wote mnayajua ya kwake .Juzi kapata ajali mbaya sana ndugu Kumchaya Selemani wa Lulindi.Watu 2 wamekufa na yeye kanusurika .
Je hiki ni kitu gani ? Mungu kutupigania Watanzania ? Je kwa nini vyombo vya habari visiandike ? Au watu wa Kigoma si mchezo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
vizuri kwenda kutafuta haki bwana, kuliko kukaa unabishana na watu na blabla nyingiii, sasa tu mahakamani wasijefanya uamuzi wa kesi kwa kumuogopa mtu hapo, wafanye haki ......haya Michuzi, vipi hali ya waziri Kapuya, nasikia professor kichwa imeumia na ajali..??
ReplyDeleteHeee mie nilipo ona breaking news nikajua kwamba Karamagi kajiuzulu, kumbe anakwenda mahakami?!!!
ReplyDeleteViongozi na wanasiasa wa nchi za dunia ya tatu wakikumbwa na kashfa wanakimbilia mahakamani badala ya kujiuzulu! Very shameful!!!!
TUNGELIKUWA SISI WAO, TUNGELIFANYA NINI? (Gazeti la Kulikoni)
ReplyDeleteNa. Mjenga Hoja
Mpendwa msomaji ni matumaini yangu unafuatilia kwa kina kile kinachoendelea katika Tanzania hasa katika ulimwengu wa siasa. Unaweza kushiriki mijadala mbalimbali kwenye mtandao wa kiintaneti ambapo Watanzania wenzako kutoka kila kona duniani wanashiriki masaa 24! Tembelea tovuti ya jamboforums na ujiunge nasi katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu na pia kupata habari zinazohusu Tanzania mara nyingi kabla habari hizo hazijatokea magazetini, kuonwa kwenye luninga au kusikika katika radio za Tanzania.
Katika makala mbili zilizotangulia za mfululizo huu wa “Tungelikuwa sisi wao, Tusingelifanya vile vyao” nimeonesha kwanza ni kitu gani “wao wamefanya ambacho sisi hatukukifanya” na pili “ni nini ambacho sisi tumefanya ambacho wao hawakukifanya.” Katika sehemu hii ya tatu nitaelezea kuhusu kile ambacho kama sisi tungelikuwa wao au katika nafasi zao “tungefanya ambacho wao hawatathubutu kufanya.”
Katika hili la tatu niseme wazi kuwa siku moja Watanzania wataamka asubuhi na mapema na watasikia kuwa CCM siyo Chama Tawala tena. Siku hiyo ipo na inakuja. Na kama mwelekeo wa CCM sasa hivi utaendelea kwa mtindo ule ule basi siku hiyo inafanya hima kutufikia. Siku hiyo watanzania wengine watapata dhamana ya kuiongoza nchi yetu kuelekea kule kwenye neema ambayo tuliahidiwa tangu tulipojikomboa. Siku hiyo Watanzania wataelewa kuwa nchi ile yenye neema si lazima iletwe na CCM na wala haitatokana na ridhaa ya Chama hicho kilichowahi kuwa cha Mapinduzi.
Kwa yeyote anayefuatilia siasa za nchi yetu ataona kuwa Chama cha Mapinduzi kinapitia katika mawimbi ya bahari ambayo ni wao wenyewe wameichafua, wanafanya hivyo huku wakitaka watu wapuuzie uchafuzi huo wa bahari kwa sababu tu wao ndio wenye merikebu! Bahati mbaya wasichokijua ni kuwa kwa wao kuichafua bahari ya utawala bora na kusababisha mawimbi ya ufisadi ambayo ndani yake kuna kila aina ya uchafu wa wizi, ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi, kiburi cha madaraka n.k wametuchafulia na sisi wengine wenye vimtumbwe vyetu. Hata hivyo kama wao wanataka kuzama na merikebu yao wazame, sisi wengine tunataka kupiga kasia hadi tufike kwenye nchi ya neema, hata kama vingalawa vyetu hivi ni hivyo visukumwavyo na upepo!!!
Hivyo kama sisi tungepata nafasi ya kuwa walipo wao katika nyadhifa zao au kuwa juu yao kimadaraka, katika kusafisha bahari hii ambayo imechafuliwa na CCM na katika kuliongoza Taifa katika kuelekea neema kuna mambo ambayo tungeliyafanya ambayo CCM haiwezi kuyafanya na haijawa tayari kuyafanya.
Hivyo katika makala hii na zitakazofuata baadaye nitajaribu kuonesha ni vitu gani ambavyo tungevifanya kama sisi tungelikuwa katika nafasi waliyonayo CCM leo au tungelikuwa na nafasi juu ya viongozi na watawala waliopo sasa. Tutaangalia mambo mbalimbali kwa kadiri tutakavyoweza tutaangalia maeneo mbalimbali kama uongozi bora, Elimu, Sheria na Katiba, Makazi, Kilimo, n.k Kwa maneno mengine badala ya kuendelea kukosoa tu utendaji mbaya na ubovu wa sera za CCM tutaonesha kuwa kuna mawazo yaliyo bora zaidi na yenye kuifaa nchi yetu na mawazo hayo yako nje ya CCM. Hivyo nakushauri ndugu msomaji hasa kama wewe ni mtunga sera au unayefuatilia sera za vyama vya kisiasa kutafuta kijidaftari ambapo unaweza kujiandikia hoja nitakazokuwa nikiziporomosha humu.
Nina uhakika mambo mengine tayari yameshafikiriwa na mengine yamezungumzwa tu pembeni lakini hakuna kiongozi wa CCM mwenye ujasiri wa kuyafanya yawe kweli. Kuna mengine ambayo yanaweza kuwa mapya na yenye kufaa, ni matumaini yangu kuwa watawala wetu hawataona haya kuyachangamkia hayo na kuanza kuyatekeleza kama wanataka kunusurika na wimbi la Tsunami linalokuja bila kelele mwaka 2010. CCM wana uchaguzi mmoja tu, kubadilika ama sivyo watabadilishwa.
Tutafanya nini?
Kwanza kabisa kama sisi tungelikuwa katika nafasi walizonazo wao au kama tungelikuwa juu yao, kitu cha kwanza ambacho tungelifanyia taifa letu ni kuwatimua wote kazi na kuwataka warejeshe funguo za maofisi yao mara moja, huku tukiwaweka walinzi wawatazame wanapokusanya vikorokoro vyao kutoka kwenye meza zilizowahi kuwa zao. “Maafande” hao watawasindikiza mpaka kwenye magari yao na kuhakikisha kuwa wanaondoka maeneo nyeti ya serikali yetu. Tutawapa muda wa siku thelathini kuhama kwenye nyumba za serikali na kuziacha zikiwa safi na samani zote zikiwa katika hali nzuri, uharibifu wowote kwenye nyumba hizo utawasababishia waende kulala Keko au Maweni. Watakaokuwa wamechanganyikiwa tutawatafutia nafasi Mirembe!
Wa kwanza ambao kwa hakika tutawatimua ni watumishi wote wa kuteuliwa ambao wanafanya kazi kwa ridhaa ya Rais (serving at the pleasure of the President). Miongoni mwao bila ya shaka ni Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali na wale ambao majukumu yao ni ya kisiasa na ambao uteuzi wao unaweza kutenguliwa na Rais. Ninaowafikiria hapa ni watu kama Mhe. Lowassa, Mhe. Msolla, Mhe. Karamagi, wakuu wa mikoa n.k
Bila ya shaka unajiuliza kwanini tungewatimua “wateuliwa” hawa? Sababu kubwa ni kuwa Taifa letu linahitaji mwanzo mpya kabisa kwani hii timu ya zamani ambayo imekuwa madarakani tangu “enzi na enzi” imeshindwa kabisa kuiongoza Tanzania kuwa nchi ile ya ahadi na badala yake wamekuwa wakitutongoza kwa ahadi zenye ukaidi. Kwa miaka karibu hamsini sasa, watawala wetu wameendelea kutuimbia wimbo wa “Tanzania inayowezekana” na wakitugeresha kwa vitu vya hapa na pale kama vile watoto wanaopewa pipi wamung’unye wakati wana njaa ya chakula. Watawala wetu hao, wakati wanaendelea kujijaza mamilioni ya shilingi kwenye hazina zao na za watoto wao, wanatuimbia sisi wengine wimbo wa “sisi ni nchi masikini” wakati wao wanaishi kifahari huku wengine wakiendelea kumalizia mahekalu yao huko ughaibuni.
Viongozi hawa ambao wamelewa ugimbi wa madaraka utafika wakati wakae pembeni kwa lazima na kuwapa watanzania wengine nafasi ya kuitumikia nchi yao. Kama kuna mtu anayefikiri kuwa CCM imezaliwa upya na ya kuwa watabadilika mtu huyo yuko njozini. Tangu walipoamua kuacha fikra za Mwalimu na kuongozwa na kitu kingine ambacho hakifanani na itikadi inayoeleweka viongozi wetu wamekuwa wakiongoza nchi yetu pasipo mwelekeo.
Tukishawaweka watu hawa pembeni, tutafanya kitu kingine ambacho wao CCM hawako tayari kufanya. Tutawachunguza wale wote wanaotuhumiwa kuliingizia taifa letu hasara ya aina yoyote. Tutaanza na wale ambao kutokana na nafasi zao walikuwa na uamuzi wa kuzuia na kuingilia kati masuala mbalimbali ambayo yangeweza kuokoa mabilioni ya shilingi. Sisi hatutawaambia wananchi “wapuuzie” hoja zinazotolewa dhidi ya watu hao. Na kwa hakika hatutawataka wananchi wasitilia maanani kama wanavyofanya CCM sasa.
Zinapotolewa tuhuma nzito dhidi ya Benki Kuu, Ikulu, na taasisi nyingine nyeti, sisi hatutazibeza au kuziangalia kwa mwanga wa kisiasa. Tutazipa uzito unaostahili. Kama tungeamua kuichungua Benki Kuu, tusingefanya kwa mazingaombwe kama wanavyofanya CCM sasa. Badala ya kwenda miaka miwili nyuma tu na kuangalia akaunti moja tungeenda zaidi ya hapo ili kuhakikisha kuwa hakuna jiwe ambalo halitageuzwa. Tungeenda miaka nane nyuma na kuangalia akaunti zote nyeti na shughuli zote ambazo zinatuhumiwa kuhujumiwa. Tusingeishia hapo tu, yule ambaye ni mdaiwa mkuu wa masuala ya Benki Kuu yaani Gavana, tungehakikisha anakaa pembeni kwanza ili kupisha uchunguzi huru (tukiendelea kumlipa). Kwa hiyo kwenye suala kama hili la BoT tusingemfumbia macho mtu yeyote. Na kwa hakika tusingesubiri kwenda nje ya nchi kuzungumzia na wafadhili jinsi tulivyo makini na suala hili. Tungetumia mojawapo ya hotuba zetu za mwisho wa mwezi kulizungumzia suala hili hapa hapa nyumbani.
Kwenye suala la Mkapa kwa mfano, sisi tusingewataka wananchi “wamuache mzee apumzike” na badala yake tungelipa suala hili uzito unaostahili. Inapotokea kuwa mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania anatumia nafasi hiyo na ofisi hiyo (majengo pia) kuandikisha biashara yake na kujiita “mjasiriamali” sisi tungechunguza kama hajakiuka maadili ya uongozi. Inapotokea mtu huyo anaweza kuomba mkopo wa karibu dola nusu milioni akiwa katika kiti cha Taifa hili, ingebidi tumuulize alikuwa aulie mkopo huo kwa njia gani na ni kitu gani alikiweka dhamana (Isijekuwa mbuni wetu na tausi wa Ikulu waka wamewekwa rehani). Tungemchunguza Mkapa na wasaidizi wake kuona kama walipokuwa katika nafasi za uongozi hawakutumia vibaya nafasi hizo kujinufaisha wao wenyewe kwa kisingizio “cha kuonesha mfano wa kukopa na kulipa”. Tungemuuliza kama alikuwa anataka kuonesha mfano, mbona hakutuambia anaenda kukopa, ili tumfuate na tujifunze anavyokopa? Na alipo lipa mbona hatukuambiwa ameenda kulipa mkopo huo? Iweze “funzo”hilo lipatikane baada ya waandishi kugundua biashara hiyo?
Tusingeishia hapo tu, baada ya kuchunguza na kuona kuwa alichokifanya kimekiuka maadili, tungemfikisha Rais huyo mstaafu kwa Pilato! Ili asimame ajieleze na kujitetea kuwa alichokifanya kwa kutumia ofisi yake ya Urais kilikuwa ni kwa manufaa yake binafsi na ya watoto wake. Na wakati tunaulizia suala hilo tungemtaka Rais huyo mstaafu aitishe mkutano na waandishi wa habari (kabla kesi yake haijafikishwa mahakamani of course) na azungumzie suala hili na tuhuma hizi nzito dhidi yake. Tusingemwacha azunguke zunguke duniani hadi atoe maelezo ya kutosha vinginevyo mali yake na ya mkewe ingetaifishwa. Hiyo yote ili kumpa funzo yeye na viongozi wengine wa baadaye kuwa ukichaguliwa kuwa Rais, fanya kazi ya urais na urais peke yake. Ukitaka kuuza mitumba na vitumbua subiri hadi utoke Ikulu!
Tungemuuliza pia kuwa kwanini hakututangazia wananchi kuwa mwenzetu ana hisa katika kampuni ya nishati ambayo wakurugenzi ni wanafamilia wake na ambayo yeye kama Rais alihakikisha kampuni hiyo inapata mkataba wa kuiuzia Tanesco umeme? Ni nasibu gani hii ambapo kampuni inayomilikiwa na familia ya Rais ambapo mmoja wa Wakurugenzi wake ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiyo ipate tenda ya kuuza umeme wa Kiwira kwa Tanesco. Hili chini ya utawala wetu angelijibu, vinginevyo mkataba ule ungevunjwa au kusainiwa upya baada ya kampuni hiyo kuuza hisa zake kwa wananchi, ili na wao wajinome na nchi yao!
Kama sisi tungelikuwa wao kuna watu ambao kwa hakika wangejibu maswali ya Watanzania, siyo majibu ya kihuni na ya kisiasa bali majibu ya ndani tena mbele ya kiapo ambacho adhabu yake ni kifungo! Kina Chenge, Mkono, Mramba na washirika wao wote wangesimamisha kujibu tuhuma za kutumia vibaya ofisi zao na kuhujumu uchumi!
Baada ya kumaliza na hao wakuu tungeenda kwa wale waliokuwa Makatibu na Wakurugenzi mbalimbali ambao wamelisababisha Taifa hasara. Hapa tusingekuwa na Mswalia Mtume wa kina Kikwete na Lowassa. Asingekuwepo mtu wa kuonewa haya. Halmashauri zote ambao katika ripoti yake ya fedha ya Mwaka kuna mapungufu yasiyoelezeka ya kiasi cha shilingi milioni tano tu, wakurugenzi wake na weka hazina wangefutwa kazi! Tusingesubiri hadi ziwe fedha za chama ndio tuchukue hatua kama wanavyofanya CCM sasa.
Kwa ufupi ni kuwa kama sisi tungelikuwa wao kwenye upande wa uongozi na utawala tungehakikisha kuwa tunasafisha utumishi wa serikali na kuajiri watu safi, kuwachukulia hatua watu wachafu, na kutowaonea huruma hata rafiki na washikaji wetu. Tungerudisha nidhamu ya utawala na nidhamu ya kufuata taratibu. Tungehakikisha kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria hata kama ana bendera saba zinapepea kwenye gari lake! Tungefanya hivyo kwa sababu tunatambua kuwa bila kusimamia utawala wa sheria na taratibu Tanzania yenye neema haiwezekani isipokuwa kwa watu wachache. Tungelikuwa sisi wao, tungefanya hivyo. Wiki ijayo tutaanza kuchambua mengine ambayo tungeyafanya kama sisi tungekulikuwa katika nafasi zao au juu yao kimadaraka. Usikose wiki ijayo ambapo tutaanza kuja na mambo mengine mengi ya kuonesha kuwa nje ya CCM kuna mawazo yaliyo bora.
Katika mapambano haya ya kifikra, fikra zetu ni lazima zishinde kwani wao CCM wameziacha fikra zile za Mwalimu na sasa hawana cha kushikilia isipokuwa wanatafuta pa kukimbilia. Katika Tanzania ambayo sisi tungelikuwa wao, tusingevumilia uzembe na kwa kweli tusingezawadia ubabaishaji.
Hapa Patamu,
ReplyDeletewakati wa watanzania kujua nani mchawi na nani Mganga umewadia.
Tatizo ni kwamba hii ngoma ikiingia kwa pilato ndio inakuwa mwisho wa uhundo. manake vyombo vya habari ndio zinakuwa vimeshapigwa STOP ku-report zaidi.
Masikini Karamagi,huu sasa huenda ukawa mwisho wake kisiasa,laiti angelisoma alama za nyakati angejiuzulu ili kulinda jina na hadhi yake ni wazi sasa anawashiwa taa ya kijani na muda si mrefu atawashiwa taa nyekundu,hata Rais Kikwete hawezi kuendelea kumtumia mtu anayeichafua serikali yake kwa kiasi hiki...wananchi sasa wamemchoka kila siku kuonekana mwizi ni yeye tu,sasa mahakamani ndio itaonekana mbivu na mbichi na ninaamini hata kama kesi itachukua miaka 10 lakini haki itatolewa tu..tunashukuru leo kwenye magazeti tumeona mkataba wa Buzwagi ulivyo wa kitapeli,jinsi watanzania tulivyouzwa na ndio maana wakakataa katakata kuupeleka bungeni sasa nguvu ya umma inamrudi karamagi...ninamwonea huruma sana Karamagi kwa ujanja wake kuumbuliwa lakini sina cha kumsaidia zaidi ya kumlilia na kusema MASIKINI KARAMAGI.
ReplyDeleteKARAMAGI OOOH KARAMAGI MWISHO WAKO SASA UNANUKIA...MAANA KILA MAHALI WATU WANAKUZUNGUMZIA WEWE NA KWA BAHATI MBAYA KILA MTU ANAKUONGELEA KWA UBAYA....KARAMAGI OOH KARAMAGI UMEAMUA KWENDA MAHAKAMANI KUJISAFISHA LAKINI UNATAPATAPA TU MAANA JINA LAKO HALISAFISHIKI TENA...LAITI TUME INGEUNDWA BUNGENI KAMA SHUJAA ZITTO KABWE ALIVYOOMBA YOTE HAYA LEO YASINGEKUKUTA...KARAMAGI OOH KARAMAGI POLE SANA.......LAITI UNGEJUA KILA MTU ANGEKUZOMEA BARABARANI KAMWE USINGEINGIA KWENYE SIASA UNGEBAKI TU NA BIASHARA ZAKO....LAKINI MAJUTO NI MJUKUU...POLE KARAMAGI NAONA SASA MKATABA UTAUANIKA MAHAKAMANI BAADA YA KUUFICHA KWA SIKU NYINGI KWA MASLAHI YAKO.....KARAMAGI OOH KARAMAGI POLE SANA BABA...WATANZANIA TWAKUPA POLE ILA JUA TU KWAMBA JASHO LA WATANZANIA HALIPOTEI BURE.....
ReplyDeleteNaaende mahakamani lakini akijua kwamba ndio anazidi kumpa umaarufu bwana Slaa.
ReplyDeleteWanaogopa wafadhili waulaya wanavyosema ndio maana wanahaha sasa.
Kumfikisha Slaa mahakamani bado hakutawapa wafadhili kuiamini serikali mpaka waonyeshe vielelezo sahihi vya kukanusha.
Slaa ni jiwe la moto, walipa kodi wameamka sasa.
Ninamuunga mkono Mh Karamagi kwa hatua hiyo aliyoamua kuichukua ya kwenda mahakamani. Ni lazima wote tuelewe kuwa kila raia ana haki zake za kimsingi zinazomlinda kwa mujibu wa sheria. Ni vema kabisa kwa Mh. Karamagi kwenda mahakamani ili mtoa tuhumu asibitishe madai yake mahali ambapo ni muafaka na wala siyo kwingineko.
ReplyDeleteNA WEWE SUBIRI AJALI YAKO KUNAWATAALAM WANATEGA VYUMA BARABARANI. HALAFU WATANZANIA ACHENI LIFT ZA BURE BURE ZA MAGARI YA WAKUBWA. KUMBUKA CHUMA KIKIMKOSA YEYE MHESHIMIWA, LAZIMA KIONDOKE NA MTU MMOJAWAPO KWAKUWA NDIVYO KILIVYOTUMWA. LASIIVYO KITAUDHURU MGUU AU MKONO AU KIUNGO CHOCHOTE CHA MHESHIMIWA, LAZIMA KIZIKWE/UZIKWE ILIKU SYMBOLIZE MAZISHI AU KIFO. samahani jamani kama nimevuuka mipaka " kama unaamini walokole wa kweli waambie wakuombee" kumbuka kuna walokole wa uwongo.
ReplyDeleteZITTO MUAMBIE FUNDI MITAMBO HUKO KIGOMA AENDELEE KUWEKA MAMBO SAWA, SASAHIVI NCHI IMECHAFUKA, WATU WANADONDOKA NA MAGARI, BALAAA,,WANAHANGAIKA, WENGINE WANAPELEKANA MAHAKAMANI SASA, WATU WANAHAHA UTADHANI WANAUMWA UCHUNGU WAKWENDA KUZAA,MMH NA BADO,,,,ZITTO EEH, HEMU MPE OFF HUYO FUNDI MITAMBO KIGOMA, APUMZIKE KIDOGO, MWEZI MTUKUFU UISHE NDO AENDELEE KUITIKISA SIASA............
ReplyDeleteYaani nimetokea kuichukia hii serikali ya JK, wamekaa kijanja-janja na kulindana. sijui lini Watanzania tutaamka na kujaribu kuipa madaraka uongozi mwingine tofauti na huu wa CCM
ReplyDeleteGari jipya linatengezwa mwaka huu bei yake ni kubwa kuliko la mwaka jana, lakini wao hata baada ya miaka 100 hao Barrick hawalipi chochote! Hata bei ya dhahabu ikifika $5,000 per ounce mwaka 2050 hawa Barrick wanaendelea kuchukua dhahabu yetu bila kulipa chochote! Huu ni upumbavu wa hali juu! Mkataba huo na ile ya nyuma pia ifutwe mpaka hapo kutakuwa na maslahi ya kweli kwa Watanzania.
ReplyDeleteMkataba wa Mgodi Buzwagi kumnufaisha zaidi mwekezaji
Na Mwandishi wetu
SUALA la uwekezaji wa katika mgodi wa madini wa Buzwagi uliopo mkoani Shinyanga linazidi kunyumbulika ambapo imebainika kwamba mkataba kati ya serikali na Kampuni ya Barrick ni wa zaidi ya miaka 50.
Kwa mujibu wa mkataba huo, uliosainiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nizar Karamagi na Mwakilishi wa Kampuni ya Barrick, Gareth Taylor, Februari mwaka huu London, Uingereza, kampuni ya Barrick itachimba madini katika mgodi huo kwa miaka 25 na kwamba itaongezewa tena miaka mingine 25 baada ya kipindi hicho.
"Waziri atatakiwa kutoa leseni maalum ya uchimbaji kwa kampuni haraka iwezekanavyo na kwa vyovyote vile kwa kipidi kisichozidi siku 60 tangu kampuni kuwasilisha maombi ya leseni na leseni atakayotoa waziri itakuwa kwa kipindi cha mwanzo cha miaka 25,
"Kampuni itakuwa na uhuru wa kuongezewa muda wa leseni kwa masharti yale yale kwa kipindi kingine cha miaka 25 na endapo kipidi cha nyongeza kitaisha na kampuni akaomba kuongezewa tena, basi kama waziri ataona ni kwa maslahi ya taifa ataweza kutoa kipindi kingine kwa kampuni atakachoona kinafaa," sehemu ya mkataba huo ambayo Mwananchi imeiona inaeleza.
Kwa upande wa mrabaha, mkataba huo unaonyesha kwamba kampuni hiyo imeruhusiwa kuchimba madini mengi zaidi ya dhahabu.
Kifungu hicho cha mkataba kinaeleza kuwa kampuni Barrick kupitia kampuni yake tanzu ya Pagea italipa asimilia tatu ya mrabaha wa madini yote yatakayochimbwa baada ya kuondoa gharama za uzalishaji, isipokuwa katika madini ya almasi ambayo yatalipiwa asilimia tano.
Kuhusu mapato halisi ambayo yanatarajiwa kupatikana kutoka katika mgodi huo, vifungu vya mkataba huo vinaonyesha kuwa nje ya malipo ya mrabaha na kodi ya zuio, serikali ya Tanzania pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama ulipo mgodi huo, itakuwa inalipwa jumla ya dola za Marekani 583,980 kwa mwaka.
Baadhi ya kodi ambazo zitalipwa ni pamoja na asilimia tatu ya thamani ya madini baada ya kuondoa gharama za uzalishaji kama mrabaha kwa madini yote yanayochimbwa eneo la Buzwagi.
Pia mkataba huo unaonyesha kwamba kampuni hiyo itakuwa ikilipa ushuru wa stempu kama ulivyoanishwa katika Sheria ya Ushuru wa Stempu namba 20 ya mwaka 1972, kuanzia tarehe ya kuanza kwa mkataba wa Buzwagi.
Hata hivyo, kuna uwezekano wa kampuni ya Pangea Minerals kutolipa hata senti tano kwa ushuru wa stempu kwani kifungu cha 5 (1) cha sheria ya ushuru wa stempu kimsema: "Hakuna ushuru wowote utakaolipwa kutokana na waraka wowote uliosainiwa kwa niaba au kwa taarifa ya serikali," ambapo kama kifungu hiki kisingekuwapo, basi serikali ingekuwa na wajibu wa kulipa ushuru huo kuhusiana na waraka huo.
Agosti 14, mwaka huu Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, lililimsimamisha Ubunge, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kujishughulisha na shughuli zozote za Bunge hadi Januari mwakani baada kubainika kuwa alisema uongo kuhusu uwekezaji katika mgodi wa Buzwagi.
Zitto aliwasilisha hoja binafsi akitaka maelezo kuhusu kusainiwa kwa mkataba huo wa mradi wa mgodi wa Buzwagi kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick, wakati serikali bado inafanya durusu ya mikataba.
Spika wa Bunge, Samwel Sitta, alisema Mbunge huyo atasimamishwa kwa vikao viwili hadi Januari mwakani kushiriki shughuli za Bunge kuanzia siku azimio la Bunge lilipopitishwa, yaani jana, zikiwamo zile za Kamati za Bunge.
Zitto alipotakiwa kujibu hoja, alisimamia msimamo wake wa kwanza na akasema yeye ni mwanademokrasia na kwamba angekuwa tayari kwa uamuzi wowote ambao Bunge lingeuchukua.
Akiwasilisha hoja hiyo, Kabwe alilitaka Bunge likubali kuunda kamati hiyo teule ili kuchunguza mwenendo mzima wa kusainiwa kwa mradi huo kulikofanyika jijini London, Uingereza Februari mwaka huu.
Alidai kuwapo kwa ukiukwaji katika baadhi ya taratibu zinazosimamia kuongoza sekta ya madini nchini ikiwemo haraka iliyomfanya Waziri Karamagi ausaini mkataba huo akiwa nje ya nchi bila kusubiri ripoti ya tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) kuhusiana na mradi huo ambao kwa kawaida hutolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (Nemc).
Hata hivyo, baada ya Ziito kusimamishwa ubunge vyama vya upinzania vilianza ziara mikoani kuwaeleza wananchi uonevu aliofanyiwa.
Ziara hiyo imesababisha wapinzania kuibua tuhuma nyingine kubwa kwa baadhi ya viongozi wa serikali kwamba wanahusika na ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma.
NINAKUBALIANA NA MTOA HOJA NDEFU HAPO JUU KUHUSU JAMBO FORUMS KWA HOJA NZITO,DATA,HABARI MOTOMOTO.MFANO HII HABARI YA AJALI YA KAPUYA NILIIPATA JAMBO FORUMS JANA JIONI(SAA ZA NY,NY) NA MTOA MAONI MMOJA AKASEMA MDAU "MASATU" HUWA ANATAARIFU JAMBO FORUMS HATA KABLA YA BLOGS,RADIO,TV NA MAGAZETI KURIPOTI.........HII NI KWELI KWANI SIKUAMINI ILE HABARI NA KUPITIA VYANZO VYA HABARI MBALIMBALI NILIVYOVITAJA JUU SIKUONA JAMBO KAMA HILO.
ReplyDeleteILA JAMBO FORUMS KAMA HUNA DATA USIJARIBU KULETA LONGOLONGO.
Ultimately monopoly shows
ReplyDeleteAdam Lusekelo
Editor
Daily News; Wednesday,September 26, 2007 @00:02
DECADES of one-party dictatorship are ultimately showing. The mindset of some guys in CCM is still in the mid-seventies. Of late the ruling CCM has shown how rusty it has become.
The thing is these are not the days when people were terrified when told that you will be dealt with by the party (Chama kitakushughulikia!). The late Mwalimu warned his party mates that too much of everything makes you become stupid.
You lie and later you start believing in your own lies and propaganda, ending up looking ridiculous. CCM does not seem to know what to do now. Political advisers like Mzee Kingunge were great in the days of one-party rule. I interviewed him several times and you would have to work very hard to ruffle his feathers.
But a lot of water has passed under the bridge. Times have changed.
Mzee Kingunge called the press to Ikulu and started finger wagging and yelling to the opposition that they were in fact talking rubbish treasonable things.
Mzee Kingunge thunderously said that the opposition should come up with proof that some top guys in the CCM were stealing from fellow Tanzanians.
He called Chadema to substantiate their claims that top CCM guys are busy stealing in the name of Tanzanians. In short he was warning the opposition that 'CCM itawashughulikia!
It was CCM who started it in the form of promoting Chadema's Zitto Kabwe into a national hero. The minister of energy and minerals, Mr Nizar Karamagi, had indulged into some hanky panky which will cost the country millions of dollars.
CCM’s Aggrey Mwanri also claimed that the CHADEMA guys wanted cheap fame. But it was the CCM, using their Speaker Sam Six which gave CHADEMA that fame on a silver platter!
The opposition didn't waste time. They took advantage of this CCM goofing and did a national crest riding. CCM was all the time yelling that the opposition should be ignored.
But you cannot ignore the truth. This time people ignored CCM and turned in large numbers to attend opposition rallies.
Deputy minister of energy and minerals went to Geita to try to explain his boss’s situation. He ended up getting heckled and booed. CCM maintains that the opposition is a bunch of thugs!
What about the Dutch ambassador to Bongo Mr Karl Van Kesteren’s call? He has said that the government should respond to corruption allegations recently leveled against a number of high-ranking public figures. Mwanri should tell us that - is the ambassador seeking cheap publicity?
Delays in government action may delay aid commitments by donor countries and could deter investors,” He has said. Mr Mwanri should tell us if the ambassador is seeking cheap publicity!
When things have been getting out of hand CCM went on panic stations. CCM secretary general, Joe Makamba hit the road to try to go and explain to the wananchi.
The thing is you just cannot call the opposition trouble makers just to get retrospective fame. What is wrong with going for fame anyway? Why are the CCM leaders doing overkill to appear in the CCM owned or influenced media everyday? It’s cool for them to appear on TV everyday but not others eh!
They are seen inspecting this or that project, now kissing babies here or there.
That is not news.
In fact there should be a one-hour show for the rulers and their wives everyday. But as a guy who has been in the media all my life, I might tell the rulers that is not news. It looks like propaganda of the 60s. But if you ask me, that is not news. That only boosts the ego of the rulers.
Many CCM leaders still seem to think that this is a one-party state. For heavens sake it is not! Whether you like it or not Dr Slaa, Zitto and the opposition now sell.
I won't watch or listen to some CCM guy say that the opposition is trouble makers out for fame. The opposition definitely has something to say. Some guys have been looting millions in our name.
If the CCM has something to say they should go to the wananchi and refute the charges. If the charges were lies, then they should go to the courts and sue the opposition to their last penny. But they can’t do that. They know that more dirt will come out if they went to courts.
Ni kigezo gani hasa muhimu kilichomlazimu Karamagi kuweka saini kwenye mkataba katika hoteli wakati ubalozi wetu upo London? Isitoshe inakuwaje saini ziwekwe London wakati Makao makuu ya barrick yapo Toronto? Hii inaonyesha kuwa kuna kitu kilikuwa kinafichwa. Hivi hizi ofisi zetu za kibalozi zinafanya kazi gani?
ReplyDeleteHuyu Karamagi asituchefue waTZ, hivi yeye aliyoyafanya anafikiri WaTZ ni wajinga kiasi hicho? kama si MAfisadi kwanini hawakutaka kuweka mkataba hadharani ukapitiwa kabla ya kusainiwa kama alivyosema mapema JK??? wasitufanye wajinga kiasi hicho, mwisho wao umefika
ReplyDeleteNafikiri na vizuri kwa mheshimiwa Karamagi ajiuzulu na kisha aende mahakamani kudai ushahidi wa madai yaliyotolewa. Kwa hali inavyoendelea, ni wazi kuwa wananchi hawana imani na Mheshimiwa Karamagi, na endapo ataendelea kuwepo, basi hiyo ni wazi kuwa uwepo wake ni kwa maslahi yake binafsi na wale wanaoendelea kumshikiria.
ReplyDeleteMi nafikiri uzalendo unatupoza. HAWA CCM WANAHITAJI MASHUTIZI KIDOGO TUWA VOTE OUT KWANZA NDIO NAONA WATAJIFUNZA. wakae benchi kama awamu mbili hivi ndio wawe na heshima kidogo kwa mabosi wa(wananchi). kwani naona CCM hawa wajui mabosi wao. Wanafikiri wao ndio mabosi na ndio maana wanakosa nidhamu ya kazi.Ila wakijua kwamba kuna kupigwa chini watajifunza.
ReplyDeleteMSAFARA WA LOWASSA NAO WAPATA AJALI MBAYA.
ReplyDelete2007-09-26 16:39:02
Na Geoge Maratu, Ukerewe
Msafara wa Waziri Mkuu Bwana Edward Lowassa uliokuwa ukitokea katika Uwanja wa Ndege wa Ukerewe kwenda nyumbani kwa Spika Mstaafu, Bwana Pius Msekwa umepata ajali mbaya.
Katika ajali hiyo, watu zaidi ya sita wameumia huku watatu wakiwa taabani na wamekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe kuokoa maisha yao.
Majeruhi hao walio katika hali mbaya ni madiwani watatu waliokuwa kwenye msafara huo.
Watu walioshuhudia ajali hiyo wanasema imetokea leo asubuhi majira ya 3:00 katika eneo la Mchirizya mjini Nansio, muda mfupi baada ya Waziri Mkuu kutua kwa helkopta na msafara kuanza safari.
Wamesema magari matatu yaliyokuwa kwenye msafara huo, huku yakiwa katika mwendo mkali, yaligongana.
Magari hayo ni Hiace yenye namba za usajili T 428 AQA, Prado lenye namba za usajili T 986 ANU na STJ 3292 aina ya Toyota Land Cruiser.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, ajali hiyo imetokea baada ya STJ kuigonga Prado iliyokuwa mbele yake na kusababisha Prado nayo kuibamiza Hiace.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Zelothe Stephen amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari hilo la Serikali.
Kamanda amewataja majeruhi hao kuwa ni Juma Mbassa, diwani wa kata ya Ilugwa, Bernad Polisi, diwani wa kata ya Kagunguli na Christian Nabigambo ambaye ni diwani wa kata ya Bwino ambao hali zao zimeelezwa kuwa ni mbaya.
Hata hivyo Kamanda amesema gari la Waziri Mkuu halikuguswa hata kidogo na anaendelea na ziara.
Anon wa 1:08 PM EAT CCM hata muwanyime kura bado watachukua nchi. Kama wangejua kuwa kuna kupigwa chini wasingefanya hivi wafanyavyo sasa, Ona tony blair baada ya kuona LABOUR PARTY inazama kwa ajili yake kaachia ngazi kwani anajua masanduku ya huku yana sauti kubwa kuliko Vyombo vya dola. ila CCM wanafimbo yao nzuri "Rungu la Dola" mkiwapiga chini kwa kura watajitangaza washindi kwa kula na mkileta fyoko mnapigwa virungu na mabomu ya machozi na kumwagiwa maji ya upupu. Hapa kilichopo ni kuwakoromea tu wasipate usimgizi ili wawajike lakini kwenye sanduku sahau ndugu yangu.
ReplyDeleteDk. Slaa azidi kukabwa koo
ReplyDelete2007-09-28 09:07:16
Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa anazidi kukabwa koo na vigogo aliowataja kuhusika na ufisadi ambapo jana Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Bw. Patrick Rutabanzibwa naye ametangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi mbunge huyo na wenzake.
Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Bw. Rutabanzibwa alisema madai aliyoyatoa Dk. Slaa na wenzake Septemba 15, mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini si ya kweli na yamemharibia heshima yake mbele ya Watanzania.
Alisema katika mkutano huo walimtaja kuwa yeye (Rutabanzibwa) ni fisadi na kwamba hata katika toleo la Septemba 19, mwaka huu la gazeti la Mwanahalisi lilichapisha madai hayo.
`Matamshi ya Dk. Slaa na wenzake yamenishangaza, yamenisikitisha na yamenihuzunisha sana,` alisema.
Alisema madai hayo ya Dk. Slaa na wenzake dhidi yake ni uzushi mtupu na kwamba anakanusha vikali tuhuma hizo za kumhusisha na vitendo vya kutumia wadhifa wake kama mtumishi wa umma vibaya au kwa maslahi yake binafsi.
Aliongeza kuwa madai hayo, yanalenga kumchafulia jina na kumshushia heshima mbele ya watumishi wenzake na jamii ya watanzania kwa ujumla.
`Ili nitendewe haki na kwa lengo la kulinda heshima yangu inayotokana na kuutumikia umma wa watanzania kwa uadilifu kwa miaka 28 hadi sasa, sina budi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Dk. Slaa na wenzake,` alisema.
Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Maji, Bw. Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.
Wa kwanza kukanusha tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa ni Mbunge wa Musoma Vijijini na Mwanasheria maarufu, Bw. Nimrodi Mkono ambaye alisema tuhuma zake ni za uongo zenye lengo la kumchafulia jina lake.
Hata hivyo, Bw. Mkono anatofautiana na watuhumiwa wenzake
baada ya kusema kwamba hana nia ya kumshitaki Dk. Slaa kwa kuwa hana fedha za kumlipa.
Aliyefuata ni Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi ambaye aliwaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki kuwa atamshtaki Dk. Slaa kwa kuwa tuhuma alizozitoa dhidi yake hazina ukweli wowote.
Juzi, Katibu Mkuu Kiongozi wa Wizara ya Fedha, Bw. Grey Mgonja naye alitangaza kuwa atamshtaki Dk. Slaa kuwa kumtaja kwa ni mfisadi.
ROHO INANIUMA SANA NIKUKUMBUKA JINSI BIBI YANGU KULE SINGIDA ALIVYONYANG'ANYWA KUKU NA STULI ILI KULIPA MAFUTA YA MWENGE.NAKUMBUKA NILIKUWA MDOGO NACHEKI PICHA ZIMA..HALAFU LEO NASIKIA KUNA MTU ANALIPWA DOLA 500 PER HOUR? JAMANI HUU SIO UFISADI NINI? MUNGU YUPO BWANA WATZ HAWATADANGANYWA HADI MWISHO WA DUNIA.MAISHA YAMESHAKABA SANA SASA.WATU WAMEANZA KUONA UKWELI.MUDA WA CHANGES UNAFIKA SASA.KARAMAGI KUBALI ULIFANYA KOSA KUSAINI MKATABA NJE YA NCHI KAKA.
ReplyDeleteWAFADHILI WATAKA UFAFANUZI WA TUHUMA ZA UFISADI KWA WAANDISHI WANAOTOA HABARI JUU YA RUSHWA ZINAZOENDELEA.
ReplyDeleteSAKATA la tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali na wafanyabiasha nchini linaendelea kutimua vumbi baada ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kutaka serikali itoe ufafanuzi wa kina ili kurejesha imani kwa wafadhili na wananchi.
Katika mahojiano Maalum na Mwananchi, Mkuu wa Mabalozi wa EU walioko nchini, Maddens Peter, alisema hadi sasa tuhuma za rushwa dhidi ya baadhi ya viongozi hazijakanushwa na akaonya kama serikali itaendelea kukaa kimya basi huenda watu na nchi wafadhili wakadhani kuwa tuhuma hizo ni za kweli.
"Tuhuma zinaonekana bado hazijakanushwa. Serikali inatakiwa kueleza vema kazi, sera na hata mafananikio yake. Mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa nchi wafadhili, hivyo ndivyo demokrasia na utawala bora inavyotaka," alisema.
Peter alisema ni kazi ya serikali kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo ili nchi wafadhili ziweze kuwaeleza wananchi wao.
"Nchi wafadhili wanatakiwa kuwaelezea walipakodi wao jinsi fedha zao zinavyotumika katika nchi hii hivyo tunatakiwa kuwa na ripoti sahihi na ya uhakika ili tuendeleze ushirikiano tuliokubaliana," alisema.
Kuhusiana na ukaguzi unaoendelea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Peter alisema nchi wafadhili wana wawakilishi nchini Tanzania wangependa kuona uchunguzi wa kina unafanyika na wakaguzi walioteuliwa.
"Serikali iliwaahidi walipakodi kwamba uchunguzi makini utafanyika na sisi tunasema, si kuwa na ripoti ya ukaguzi tu, lakini pia kuona utekelezaji wa mapendekezo ambayo yatatolewa," alisema.
Kampuni ya Ernest and Young ambayo imepewa kazi hiyo, ilianza kufanya ukaguzi wa mahesabu BoT Septemba 10, mwaka huu na inatarajia kumaliza kazi hiyo baada ya siku 60.
Wakati huo huo; Balozi Msaidizi wa Ujerumani nchini Tanzania, Ingo Herbert, aliishauri serikali ya Tanzania kujibu shutuma zote za rushwa zinazotolewa dhidi ya baadhi ya viongozi wake kwa sababu nchi wafadhili zinafuatilia kwa karibu malumbano yanayoendelea na kwamba zingependa kufahamu ukweli.
Tuhuma zinazotolewa kuhusu ufisadi ni nzito, nasi tungependa serikali ikatoa tamko lake mapema iwezekanavyo kuhusu tuhuma zilizotolewa na vyama vya upinzani dhidi ya baadhi ya viongozi,� alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam jana, Herbert alisema ni vizuri serikali ikazingatia misingi ya utawala bora ambayo dhana yake ni uwazi, ukweli na uwajibikaji.
Alisema Ujerumani ni mshiriki mkubwa wa maendeleo ya Tanzania, kwani katika miongo minne iliyopita imetumia kiasi cha Euro bilioni 1.8 kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo hivyo hata walipa kodi wa Ujerumani nao wangependa kufahamu kuwa kodi zao zinatumiwa vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.
Herbert alikuwa akieleza kuhusu wiki ya Ujerumani iliyoanza jana, ambayo lengo lake ni kuwatambulisha Watanzania kuwa Ujerumani ni miongozi mwa washirika wakubwa wa maendeleo nchini, hivyo Ubalozi wa nchi hiyo umeandaa maonyesho ya shughuli zake inazofanya Tanzania chini ya taasisi zake za maendeleo ambazo ni Partner for the Future Worldwide (Gtz), Hanns Seidel Foundation (Hsf), Konrad Adenauer-Stiftung (Kas), Friedrich Ebert Stiftung (Fes), Deutsche Welle na Germany Capacity Building International (Inwent).
Alisema serikali ya Ujerumani imeshiriki katika sekta tatu muhimu za maendeleo nchini Tanzania ambazo ni huduma za afya, miradi ya maji safi na salama na uimarishaji wa serikali za mitaa.
Alisema miradi yote hiyo inaendeshwa chini ya mpango wa mashirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania ambao lengo lake ni kutekeleza sera ya maendeleo ya Ujerumani ambayo ni kusaidia kunyanyua kiwango cha maisha cha watu wa nchi zinazoendelea.
Herbert alisema katika makubaliano ya ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania, kipaumbele zaidi kimewekwa katika mpango wa serikali ya Tanzania wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini (Mkukuta), ili kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ambapo nchi hiyo inaisaidia katika nyanja tatu ambazo ni kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato, kuboresha kiwango cha maisha ya watu na huduma za jamii na kukuza utawala bora na uwajibikaji.
Kuhusu suala la utawala bora na uwajibikaji, Herbert alisema wanafuatilia kwa karibu siasa za Tanzania na Ujerumani imeguswa na malumbano yanayoendelea ambayo yanawahusisha viongozi wa serikali ya na tuhuma za rushwa.
Huyu ni balozi wa tatu wa nchi wahisani wa Tanzania kutoa maoni yake kuhusu tuhuma za rushwa na ufisadi zilizotolewa na Dk Wilbroad Slaa dhidi ya viongozi mbalimbali zinazohusisha ufujaji na upotevu wa rasilimali za umma.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Balozi wa Uholanzi Karel van Kesteren, alielezea kukerwa kwake na tuhuma hizo dhidi ya viongozi waandamizi wa serikali na kutaka serikali itoe tamko lake haraka iwezekanavyo.
WAPINZANI WAMJIBU WARIOBA
ReplyDelete2007-09-29 08:40:57
Na Restuta James
Umoja wa vyama vya upinzani umejiingiza katika malumbano na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba kwa kudai kuwa hautishwi na utetezi uliotolewa na kiongozi huyo na kwamba wakigundua kuna ubadhirifu aliowahi kuufanya wakati akiwa kiongozi wa ngazi za juu serikalini watamshughulikia.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Jaji Warioba kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na wapinzani za kuwataja hadharani viongozi wa serikali na kuwahusisha na ubadhirifu wa mali za umma.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za makuu ya CHADEMA, jijini Dar es Salaam, viongozi hao kutoka vyama vya TLP, NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF, walisema wanashangazwa na kauli zinazoendelea kutolewa na watu waliowatuhumu pamoja na ile ya jaji Warioba na kueleza kuwa hawatambui Jaji Warioba alizungumza kwa kutumia utaratibu gani kwa kuwa hivi sasa hashikilii wadhifa wowote.
Viongozi hao wa vyama walisema Jaji Warioba alipaswa kueleza juhudi zake za kupambana na ufisadi na kwamba baadhi ya majina ya watu wanaowatuhumu si mageni badala ya kukaa kimya na kuwashangaa wapinzani ambao wana nia ya dhati ya kutaka ukweli juu ya matumizi ya rasilimali za umma na fedha za walipakodi.
`Sisi tunaamini kuwa Jaji Warioba ni miongoni mwa viongozi waadilifu lakini kauli yake ya juzi inatupa utata sana maana alitakiwa kuwashauri viongozi wa serikali juu ya kutoa tamko kuhusiana na tuhuma hizi kuliko ambavyo viongozi hao wanaanzisha malumbano kwenye vyombo vya habari hivi sasa,` alisema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuza Taifa Bw. Sam Ruhuza.
Katika hatua nyingine viongozi hao walisema wameahirisha kulipua `mabomu mengine kwa kuwa bado wanafanya uhakiki na uchunguzi zaidi wa `mabomu` wanayokusudia kuyalipua.
Walifafanua kuwa kwa sasa wanashirikiana na wataalamu mbalimbali kukamilisha uhakiki wa jambo wanalotaka kuwaeleza wananchi.
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. Victor Kimesera alisema bomu lililopangwa kulipuliwa ni jipya na kwamba halihusiani na yaliyotangulia akitaja Buzwagi na viongozi waliotuhumiwa kujihusika na ufisadi.
`Hili jambo ni jipya hatutazungumzia uamuzi uliofikiwa na watuhumiwa wa kutaka kutuburuza mahakamani maana hilo litatatuliwa kimahakama kama ambavyo wanadai,` alisema.
Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema viongozi wa vyama hivyo wanashirikiana na jopo la wataalam wa kada mbalimbali kujadili suala hilo kwa kina na kwamba siku chache zijazo watawaeleza wananchi.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF ? Zanzibar Bw. Juma Duni Haji , kwa upande wake alisema anashangazwa na watuhumiwa waliotajwa kutokwenda mahakamani hadi sasa, badala yake kuendelea kusema kuwa wamechafuliwa majina na kukashifiwa.
`Wanajifanya kuwa wamechafuliwa majina lakini hawataki kwenda mahakamani. Hiyo janja yao ya kutaka kuwaathiri wananchi kisaikolojia tumeigundua hivyo tunawaomba wananchi wawe makini kwa kufuatilia mambo haya bila kukata tamaa hadi hapo ukweli utakapojulikana` alisisitiza Bw. Haji.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu NCCR-Mageuzi Taifa Bw. Ruhuza aliongeza kuwa wanasuburi kuburuzwa mahakamani ili watoe mambo yaliyotakiwa kuzungumzwa bungeni na viongozi waliotaka kuwasilisha hoja binafsi.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa TLP Bw. Mrema, Bw. Ruhuza wa NCCR-Mageuzi, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Bw. Haji pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa vyama hivyo kutoka bara na visiwani.
Aidha viongozi hao walisema wataitisha mkutano mapema pale kazi ya uhakiki wa nyaraka za `bomu` wanalotaka kuwaeleza wananchi itakapokamilika.