
mdau anatutambulisha kitabu chake kipya cha 'watanzania kuelekea kwenye nchi ya ahadi - Tanzaniana to the Promised Land' ambacho kinachambua uongozi wa siasa wa bongo kwa awamu zote tatu zilizopita, na kinatathmini pia kasi mpya, nguvu mpya, na ari mpya ya awamu ya nne. ukitaka nakala kutoka 'TANZANIA PUBLISHING HOUSE" kwa wale walio hapa nchini au wale walioko nje ya nchi kupitia www.lulu.com/ijwerrema au watembelee http://www.ijwerrema.info/ ama tuma email kwa mwandishi author@ijwerrema.info
Ni hatua nzuri, manaake vitabu vipya Tanzania vimepungua sana. Siku hizi waandishi sijui wamechoka? Najua najua wengi watasema kuwa hakuna soko, lakini mwandishi mzuri anatakiwa kufanya utafiti kwanza soko linapenda mambo gani then aandike kuhusu hayo mambo. na internet adevrtising kwa Tanzania bado uwanja ni mpana sana saaana. Kwa kuwa Wabongo wengi hawana credit cards yaani bado hawajajikita kabisa katika internet advertising
ReplyDeleteana nini jipya humo,au ndo usual bla bla tu ?
ReplyDeleteTANZANIA TO THE PROMISED LAND? man not in a million years!
ReplyDeleteTo the promised land ! my a--e!!!!
ReplyDeleteAh mijitu mingine bwana eti,"To the promised land ! my a--e!!!!".
ReplyDeleteYaani miwazo hasi tu na chuki zisizo na msingi. Yaani hata sijui nani kafanya makosa kukupa computer. Mtu kama wewe inatakiwa ufungiwe stoo uwe unabeba maboksi maisha yako yote.
Kazi njema hii ingawa wanasema tusihukumu kitabu kwa kusoma mai hedingi au mai kava yake.
ReplyDeleteNyakatakule
SIYO (AHADI) NI MATARAJIO.. KENYA NA UGANDA WATATUCHEKA...WATATULETEA HATA WAKARIMANI.samahani sawahili yangu mbofumbofu.
ReplyDeleteHongera Ndugu Mwandishi JAPO SIKUJUI NA WALA SIJASOMA HICHI KITABU LAKINI NI HATUA NZURI
ReplyDeleteMimi nilibahatika kupata kopi ya kitabu hiki hapo TPH. Kwa kweli mtunzi amejitahidi sana kutoa mawazo yake kwa uwazi na bila woga. Anaonekana sio ana mtazamo tofauti kidogo.
ReplyDeleteDOLE MTUNZI
Nyie wote wenye kulaumu, tuonyesheni vitabu vyenu mlivyoandika!
ReplyDeleteKazi kulaumu tu na hali hamuwezi hata kuandika kurasa kumi zikasomeka!
Ni heri zaidi mkaenda maktaba, kama hicho kitabu kimeishawekwa, mkisome vizuri na kutuandikia, angalau, "review" yake!
Kumbukeni, na liwajae akilini mwenu: One Tanzania, many voices!
Sio lazima Tanzania yetu ipimwe na mawazo yenu tu, ambayo pengine mkiyaandika yasomwe na wengine, watayakuta ni pumba tupu!
Yaelekea mwandishi anawaona Watanzania wanavyopiga hatua kufikia "promised land". Sisi amabo hatujakisoma kitabu hicho hatujui mwandishi katamati namna gani!
Hata kama kitabu hicho kimeandikwa "one-sided" kupendelea uongozi wa CCM, kisomeni mkikosoe kwa kutoa upnde wenu manaofikiria kutufikisha kwenye "promised land"!
hii tittle mimi wala haijanipendeza. Anafanya kumdhalilisha baba yetu wa taifa mwl Nyerere. Yaani ina maana the more we have new leaders the more we are walking towards the promised land. Kama sio kinyume chake?
ReplyDeleteMimi naomba tu kumuuliza Michuzi kama tunaweza kupata japo uchambuzi tu wa sehemu ya kitabu hiki. Maana watu wanasema tu bila hata kujua kitabu kinasema nini. Lakini inaelekea kuna amabao wameishakipata kama mtoa maoni mmoja hapo juu ambaye yeye anasema anavutiwa na mwandishi.
ReplyDeleteJamani mbona, hizo rangi za bendera zimekosewa?? Au kipo apsaididauni!!
ReplyDeleteJAMANI HIYO BENDERA MBONA IKO APSAIDIDAUNI?? AU NDIO YALIYOMO HUMO NDANI FEST IMPRESHENI MUHIMU.
ReplyDelete