msanii klyiin akikuonesha jalada la albamu yake mpya 'klyinn:crazy over you' anayotarajia kuiingiza sokoni hivi karibuni. mengi kuhusu mrembo huyu na albamu hiyo nenda ://www.klyinn.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. Hivi huyu si ndio yule alisema hataki picha zako huku kwenye blog sasa wewe hukusikia au huyu ni mwingine manake majina yao ya kisanii hayapishani.....????

    ReplyDelete
  2. sorry natoka nje ya mada.. ya klynn

    Tanzania yamshangaa Museveni kuhusu Shirkisho

    Written by Faraja Mgwabati
    Sunday, 16 September 2007
    TANZANIA imeshtushwa na taarifa kwamba Rais Yoweri Museveni wa Uganda ana mpango wa kuendelea na uharakishwaji wa Shirikisho kati ya nchi yake na Kenya na kuiacha Tanzania kinyume cha makubaliano ya nchi hizo tatu mwezi uliopita.

    Vyombo vya habari vya Afrika Mashariki viliripoti jana kuwa Rais Yoweri Museveni ameitaka Kenya na nchi yake ziendelee na mpango wa kuharakisha uanzishwaji wa Shirikisho na kuiacha Tanzania mpaka itakapokuwa tayari.

    Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ali Iddi, aliliambia HabariLeo mwishoni mwa wiki kuwa ameshangazwa na habari hizo kwa kuwa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki walishaamua kusimamisha uharakishwaji wa Shirikisho hilo.

    Balozi Iddi alisema hajapata taarifa rasmi kuhusiana na madai hayo, lakini watamuuliza Rais Museveni kujua kama ni kweli.

    “Tutamuuliza kupitia Balozi wetu kule Uganda. Kwa sasa hatuwezi kusema zaidi kwa sababu hatujathibitisha,” alisema Balozi Iddi. Naibu Waziri alisema ingawa kisheria inaruhusiwa nchi zilizokuwa tayari kuendelea na zisizokuwa tayari kusubiri Shirikisho, lakini alihoji kwa nini Rais huyo wa Uganda hakusema nia yake hiyo kwenye kikao cha wakuu wa nchi hizo. Alisema serikali itatoa maelezo baada ya kuzungumza na Museveni.

    Inasemekana Rais Museveni hakufurahishwa na matokeo ya kikao cha wakuu wa nchi za Afrika Mashariki kilichofanyika Arusha mwezi uliopita ambacho kiliamua kusimamisha mpango wa uharakishwaji wa Shirikisho hilo na badala yake kuanzisha soko la pamoja na sarafu moja ifikapo 2012.

    Habari zinasema baada ya uamuzi wa kikao hicho, Museveni alituma ujumbe wake kwenda Kenya kumshawishi Rais Mwai Kibaki kwamba Kenya na Uganda ziendelee na mpango wa
    kuharakisha shirikisho na kwamba Kenya itafaidika na mpango huo mpya hata kama Tanzania haitakuwapo.

    Katika kikao hicho cha Arusha, Tanzania iliweka wazi kuwa kutokana na maoni ya Watanzania wengi kukataa mpango wa kuharakisha Shirikisho, ingependa ijiimarishe kwanza kiuchumi ndipo baadaye Shirikisho lifuate. Wachambuzi wa mambo wamekuwa wakisema kuwa Museveni alikuwa na hamu ya kuwa Rais wa Shirikisho hilo na ndiyo maana anataka kuanzishwa kwake hata kama wajumbe watakuwa nchi mbili tu.

    Kwa mujibu wa wachambuzi hao, kukwama kwa uharakishwaji wa Shirikisho kumemfanya atafute mbinu nyingine ikiwa pamoja na kuiomba Kenya waungane. Katika hotuba yake ya hivi karibuni mjini Arusha, Museveni alinukuliwa akiwataka Watanzania kutoogopa Shirikisho na
    kwamba ardhi na ajira yao vitalindwa.

    Hata hivyo ,Waziri wa Kenya anayeshughulikia Afrika Mashariki, John Koech alisema haiwezekani Kenya na Uganda kuendelea na Shirikisho la Kisiasa na kuziacha Tanzania, Rwanda na Burundi.

    “Ni vizuri kujiimarisha katika ushirikiano wa kiuchumi kabla ya kuunda Shirikisho la Kisiasa,” alisema Koech. Tayari Rwanda na Burundi zilishaweka msimamo wazi kwamba kwa kuwa wamejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki hivi karibuni wanahitaji muda zaidi wa kuwashirikisha wananchi wake.

    ReplyDelete
  3. Keilin jamani umeolewa?????
    Jamani hivi wewe hata chooni unaenda kweli!!!!!!!
    Uko bomba mbaya ya kufa mtu.
    Shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  4. kinjeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee unaona maneno hiyo?

    ReplyDelete
  5. DADA UNAVUUTIA PICHA MURUA KABISA HII, SAFI SANA.ISSA HAYO MAKAVA YA CD YAMESHAZIBA MOJA YA ENEO MUHIMU HAKUWA NA HAJA YA KUVAA SIDIRIA, HEBU IEDITI ISSA MVUE SIDIRIA ABAKI NA MAKAVA, BIBIE UNAMVUUTO.(samahani issa nafahamu huu ni mwezi wa toba)

    ReplyDelete
  6. DU AISEE KUMBE KLYINN NI BOMBA EEH.

    ReplyDelete
  7. Album hiyo inapatikana wapi jamani kaka michuzi maana sijaona mahali ulipoandika inauzwa wapi?

    ReplyDelete
  8. is it crazy over you or about you.Just thinking HGL.Over kupita about kuhusu.Or you mean all over him/her.too bad.Next time cover up sis,you are already beautiful don't sell baby,is out of you culture

    ReplyDelete
  9. Yarabi toba,
    Michuzi umeshaniharibia swaumu yangu.Anyway nitalipiza kwenye sita.Du!!Yani mnataka kusema huyo Kinje wewe anon uliyeandika hapo juu kabanjua mzigo au?Mtoto kaumbwa.Huyu hakuzaliwa.
    NooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooHakuzaliwa

    ReplyDelete
  10. Klyn unavutia sana dada na hilo tumbo lako flat,niliwahi kukuona mara moja long time sana wakati uko O'bay...nakumind sana lakini niko mbali sana na hapo,nikirudi hakika nitakueleza ....hiyo pua tuu ndio inanimaliza,njoo States utapendeza zaidi na mambo yako yatanyooka zaidi maana huku wanapenda wazuri kama nyie,hapo milango yote ya bahati watakufungulia kutokana na uzuri tuu

    ReplyDelete
  11. HAKUNA MVUTO WALA NINI NI MKOLOGO TU NA KALIKITI. UNAPIGA YOWE KIIINJEE! YES MIMI KINJE NI ALWATANI DOGO, PESA MINGI NA NI HANDSOME, YOU CAN TELL TO YOURSELF I AM A HOT CAKE,NAPATA ILE FIRST CLASS UKIONA NIMEACHA BASI JUA KINA JACKIE PEMBA WANAPONEA PALE...MICHUZI WAELEZE VIJANA KUHUSU MIMI SUPER STAR...

    ReplyDelete
  12. Aibu aibu aibu. Kylin unatia aibu. UPO UCHI KABISAAAAA BORA UNGEMALIZIA TU. SIONI SABABU YA KUUZA CD ZAKO UKIWA HUJAVAA NGUO. UTANDAWAZI HUUU UTATUMALIZA!!!!!
    YAANI NI VIGUMU MTU AKIKUAMBIA HUYU DADA NI CHA... UKATAE KWA JINSI ALIVYO VAA. mmh

    ReplyDelete
  13. ISSA NAONA UNATAKA MWEZI WA TOBA TUSISOME HII BLOG. MAMBO GANI HAYA??
    MARA TSHIRT ZA CARSBERG MARA UCHI WA DADA ZETU MMH

    ReplyDelete
  14. Huyu dada ni mtamu sana,
    Natamani atokee mtu atoe ushuhuda kama alisha wahu kunanihii maeneo yake.
    Namtamanigi toka anaanza kuchipukia katika ulimbwende,
    Nampenda sana,

    ReplyDelete
  15. Jamani hiyo mishipa ya shingo na mishipa chini ya mashavu imekakamaa, Loh!!

    ReplyDelete
  16. anoni juu kabisa, aliyekataa tusimuone humu hatutaki ni Ray C, atajiju sie tunaendelea kukamua

    ReplyDelete
  17. we sir kinje sikia,wahenga walisema 'ukisusa wenzio wala',sasa kama jak pemba anajitafunia taratiiiiibu mwache kwa raha zake,of course udenda unakutoka,utajiju!

    ReplyDelete
  18. UPO JUU DADA.

    KANYAGA TWENDE.WATIMULIE VUMBI WAPOTEZE LONGOLONGO WOTE.

    NASUBIRI SANA KUIWEKA MIKONONI HIYO CD.

    ILA TATIZO WABONGO KWA KUBURN CD MNANITISHA NDIO BALAA.JAMANI TUWAUNGE MKONO WASANII WETU TUNUNUE KAZI ZAO.

    NI HAYO TU

    ReplyDelete
  19. Kweli watoto wamaharibika,bongo hakuna tena wazee?Mtoto yuko uchi wa mnyama urembo gani huu?Wazee wenzangu nisaidieni.
    Mwinyijuma shoko jumbe alii.

    ReplyDelete
  20. jamani jamani!!mambo ya maovu(nyuchi)hayajakatazwa mwezi wa ramadhani tu,bali hata siku za kawaida!!
    michu tupe mambo!!kitoto bomba sana,yani anaitaji kupewa raha,kwani naona bado ajapata raha,,!!!
    by SEOUL

    ReplyDelete
  21. Msalie Mtume, kaka michuzi!

    ReplyDelete
  22. WHAT A SAUGASAGE WALLETTTTTT, JAMANI TUNAOMBA UWEKE NGUO YOUR SO BEAUTIFUL TO GO LOW LIKE THAT. I THROUGHT YOU HAD A LOT OF CLASS BUT I'M REALLY DISAPPOINTED TO SEE THIS.

    ReplyDelete
  23. Hivi hamuoni mtoto mdogo BESTA anavaa nguo za heshima na anapendeza,ameona kutuonesha tumbo ni deal, labda kama ana biashara nyingine anatangaza zaidi ya hiyo ya music. Vinginevyo AIBU!!

    ReplyDelete
  24. I CAN'T HELP IT BUT TO WONDER. WHAT HAPPENED TO YOU KLYINN. UMEJIWEKA KWENYE POSTI MBAYA SANA NA HIYO PICHA.YOU HAVE CLASS DEAR DONT SELL YOUR SELF LOW LIKE THAT IT DOESNT LOOK GOOD ON YOU.CD UNGEUZA HATA BILA KUTOA NGUO.

    ReplyDelete
  25. Yes, hata mimi naomba radhi natoka nje ya mada kuunga mkono maoni ya Anonymous wa Sept/17/07 10:16pm.
    Kama Rais Museveni ana mpango wa kuharakisha muungano huo basi aendelee tu,hii itaonyesha jinsi ambavyo waBongo hatukukosea kupinga kuharakisha mambo haya.
    Ni wazi kuwa hakuna msimamo wa pamoja.Nini kijakuja baada ya haya?
    Yetu ni bora yawe macho na masikio!

    ReplyDelete
  26. Alipiga picha ana akili sana, inatoa impression hakuwa amevaa kitu at the same time inaonyesha kavaa blazia. CD cover ingefunika hicho kiblazia kwa chini, ohooo udenda ungewatoka wengi

    ReplyDelete
  27. HI DADA WEWE BOMBA TUU WAACHE WASEME " ETI UMEJISHUSHA HADHI" MWILI NI WAKO BIBIE TENA HUNA KOVU KAMA WENGINE NDIO MAANA HAMU WEZIONYESHA MIILI YENU KWA KIGEZO CHA HESHIMA.U GO GAL..

    ReplyDelete
  28. It's true! Klynn! Urembo wa mwanamke wa kiafrika ni mavazi. Una mwili mzuri basi utumie kuvaa mavazi yanayoendana na umri wako! Si lazima uende uchi. I believe Bongo kina madesigner wanaoweza kubuni mavazi ambayo utawafurahisha watu wa umri wote na kutunza heshima yako! Pse be wise.

    ReplyDelete
  29. Michuzi mbona unaruhusu comment ambazo ziko nje na topic??? Huyu jamaa anachomekea habari za Museveni na wewe unaaprove tu??!!
    Hao watu ndio wanaoharibu blog na Forum nyingi tu.
    please uwe unaziblock hizo!!

    ReplyDelete
  30. Acheni uzushi watu!!! Dada hayuko uchi wala nini si amevaa kama bikini tu!! ni mambo ya kawaida tu, tena katoka bomba. haterz bwana.

    ReplyDelete
  31. We anony wa 5:12. Usitake kudanganya watu kuwa wanawake wazuri wakija marekani wanafanikiwa kuliko wakiwa Bongo. Unataka kusema Klyn akija marekani ata win kuliko alivyo sasa? Wangapi wazuri kuliko, wameenda huko wakirudi huku home, yaani aibu, hata housegirl wangu anamshinda kwa kunawili. Timua huko mbeba maboxi wewe!!!

    ReplyDelete
  32. WEWE ULIYESEMA unataka kumuoa acha ujinga MADEMU KAMA hawa sio wa kuoa hawa ni viburudisho tuu.

    x_x

    ReplyDelete
  33. anon wa sept 19,9:56:00 nakuunga mkono na kichwa.hapa UK yuko aunt mmoja bomba amelost kinoma na kwa sasa anatandika vitanda.kabla ya kuzamia kule bongo alikuwa matawi ya juu ile mbaya sijui nani alimdanganya azamie.not all that glitters is gold!

    ReplyDelete
  34. wewe ANON UNAYE SEMA WAZURI WANAFANIKIWA USA mbona Hoyce Temu alikuwa Marekani kisha akarudi bongo fasta fasta?au naye kafanikiwa ndiyo akarudi bongo?

    ReplyDelete
  35. sasa ndio mnatusema watandika vitanda ama tujue vipi? manake tupo wengi huku ukereweni twayatandika matanda kwa kwenda mbele sema wengine twapita tu sio kwamba ndio kufika tukamaliza vilivyotuleta basi tunarudi nyumbani ila msione watu wanatandika vitanda mkawazarau watu wapo na ndoto zao vichwani na malengo yao na kutandika vitanda si kulost umesikia we anony wa hapo juu

    ReplyDelete
  36. jack ni mzuri,anaemkandia anaona wivu,nguo aliovaa kwani ina tatozo gani ,tumbo ni kitu cha kawaida,hajakaa uchi , we kama una mikovu jifunike

    ReplyDelete
  37. anon wa 7:57 usikasirike.kinachotia huruma na simanzi ni kuona mtu ambaye bongo alikuwa na biashara nzuri anaiacha na kuja kutumikishwa na watasha ughaibuni,mtu unajiuliza why?

    ReplyDelete
  38. Wewe Kinje! I hope its not you for real. We mwana si umeoa majuzi tu hapa? wajibeza nini kuwa umetembea na so and so. Jembe la mkono shurti kupokezana, mwache binti apite zake huyo. Umeshapitwa na wakati. Kwani we know life in the married territory is boring as hell.

    ReplyDelete
  39. anknon wa September 19, 2007 2:04:00
    ASANTE KWA kuniunga mkono na kichwa ILA hawa watu wanataabishwa sana wangu na sijui kwanini huwa hawajifunzi USTAA unawaponza sana CHECK SASA ni kweli ni mzuri ILA KWA SASA UZUR WAKE ni sawa na bure otherwise WATU WATAFANYA tu kopo la kujazia mamboz na kutimka

    x_x

    ReplyDelete
  40. SABABU KUBWA KWA KUANIKWA UCHI KWENYE MABLOGU NA INTERNET KMA IFUATAVYO:-
    + INAONYESHA KUWA HAKUNA MARKETING SKILLS ZA KUTOSHA TZ NDIO MAANA WATOTO WANAKAA UCHI ILI WAUZE HATA CDS MASIKINI

    + KUIGA KWINGI BILA KUJIJUA WANAFANYA NINI - WANAOIGWA HAWAKAI UCHI KILA WAKATI...

    + UTAMADUNI HUMFANYA MTU KUWA MTU .....IMAGE NI MUHIMU...LAKINI HAWANA MWALIMU MZURI AU HAWAJANIPATA BADO.

    ReplyDelete
  41. jamani Jack what happened? na upole wako wote pamoja na Urundi wako wote how did you endup naked on a national blog?, I heard you were married to a white guy and you went to South Africa kutafuta maisha what happened?? jirani yako na classmate wako Oysterbay primary-karibu England

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...