idadi ya wadau wanaojizolea nondozzz yazidi kuongezeka. safari hii ni mdau lilian mbaga iundi (shoto) ambaye kala nondozz ya master in international communication management chuo kikuu cha the hague university of professional education, uholanzi. hongera sana lilly.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Michuzi si umetuambia kuwa wadau hawavai majoho huko uholanzi mbona hii picha wamekula majoho? Au yule wa kwanza amezuga kula nondozz?

    ReplyDelete
  2. Wewe Anonymous wa 2.56.00AM EAT Septer 19.

    Hicho Chuo ulichosoma wewe ambacho hawavai majoho ni chuo chako sio Uholanzi yote. chunguza

    Dada Hongera sana kwa mafaniko na Mungu akuzidishie katika utendaji wako ili ukabiliane na matatizo ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  3. kama anony 2:56 asemavyo si vyuo vyote hawavai majoho. Kwa maelezo kiduchu ni kuwa vyuo ambavyo ni vya Kidachi (asilia) hawavai majoho isipokuwa maprofesa wao. Ingawa si lazima, kawaida, kwenye dondo ya Ph.D wanaume wanavuta suti zenye mikia za penguini wakati akina dada nao wanakula tu vitu vya nguvu (mara nyingi rangi zitumikazo ni nyeusi na nyeupe). Sasa Wadachi kama zilivyo nchi nyingi ulimwenguni leo wanakuwa 'globolaizidi' hata wanatoa sasa 'Masta Digriiz' kitu ambacho hakikuwepo katika mfumo wa vyuo vyao asilia, hivyo utaona kuwa nyuo kadhaa vya kimataifa nchini uholanzi ambavyo asili yake ni UK, US n.k wanakula majoho kama kawa. Potelea pote, majoho au hakuna majoho chini ya msitari ni JE MWANADAMU AMEFUTA UJINGA ZAIDI NA KUONGEZA UJANJA ZAIDI?
    Hongera Dada!
    Nikitonya kutoka kwenye wanja la Amsterdam Schiphol mimi ni Nyakatakule- unyilisya echalo.

    ReplyDelete
  4. NI KWELI SIO VYUO VYOTE ULAYA(NJE YA UINGEREZA) HUVAA NAJOHO. MIMI NIMEKULA NONDOZZ SWEDEN NA MAJOHO SI DILI. HII INATOKANA NA UTARATIBU WAO WA ELIMU AMBAO UNABADILISHWA SASA. UTARATIBU WAO ULIKUWA KWAMBA HAWANA BACHELORS DEGREE, WEWE UKIINGIA CHUO NI MIAKA MITANO UNATOKA NA MASTERS, WAO HUWA WANAZIITA UNDERGRADUATE DEGREE, KWA WAO POST GRADUATE(AU GRADUATE SCHOOL) MAANA YAKE PHD. NA WALA KWENYE VYETI VYAO HAWAANDIKI "DEGREE", WANAANDIKA "DIPLOMA". DIPLOMA SIO LEVEL YA CHETI KAMA TUNAVYOELEWA SISI BONGO, ILA NI JINA LA CHETI CHOCHOTE, NDIYO MAANA UNA HIGH SCHOOL DIPLOMA, UNIVERSITY DIPLOMA (IN ENGINEERING, SOCIOLOGY, U NAME IT), NDIYO MAANA UNAONA WATU WANASEMA DEGREE YA ENGINEERING AMBAYO NI "DIPLOMA" UJERUMANI NI SAWA NA MASTERS KWENGINE....

    NCHI NYINGI ZA ULAYA KAMA GERMANY, SWEDEN, NORWAY, FINLAND, DENMARK ELIMU IMEKUWA NI BURE KWA MIAKA MINGI, NA KWA HIYO HAWANA UTAMADUNI WA KU-DRAMATIZE GRADUATION. UK NA MAREKANI, ELIMU IMEKUWA IKIUZWA MIAKA MINGI, NDIYO MAANA WANA DRAMATIZE NA MAJOHO KWA SANA, NA PIA "LEVELS" KIBAO KAMA CERTIFICATE, DIPLOMA, DEGREE, POST GRADUATE (CERTIFICATE,DIPLOMA), MASTERS DEGREE...PHD! WANAVYOTENGENEZA LEVELS MBALIMBALI NDIVYO WANAVYOUZA ZAIDI!!!(MARKET SEGMENTATION).

    NA SISI BONGO HATUKO NYUMA KU-DRAMATIZE NA KUVAA MAJOHO, NAAMBIWA SIKU HIZI HATA CHEKECHEA WANA GRADUATION NA MAJOHO KIBAO!! OFCOURSE, TUNAUZA ELIMU PIA, SI TUKO NYMA YA UK?!

    NDIYO MAANA UKIWA SCANDINAVIA AU GERMANY HAKUNA SWALA LA CHUO KUTAMBULIWA AU HAPANA, KWASABABU HAKUNA VYUO VYA UBABAISHAJI KUTAFUTA HELA...

    HATA KWENYE PHD MAJOHO SI LAZIMA, ILA UNAWEZA KUONA SUTI NDEEEEEFU(WATAALAMU NIAMBIENI ZINAITWAJE?) NA KOFIA NDEFU.

    UTARATIBU HUU WANAUBADILISHA SASA ILI KUWE NA BACHELORS(3YRS) NA MASTERS(2YRS). MPANGO HUU UNAITWA "BOLOGNA PROCESS" NA UTAKAMILIKA MWAKA 2010. SAMBAMBA NA MABADILIKO HAYO ITAKUWA NI KUANZA KUUZA ELIMU HASA KWA WAGENI, NA LABDA TUTAANZA KUONA MAJOHO ZAIDI.

    ReplyDelete
  5. jamani Uholanzi hawavai majoho kwa bachelor ila kuanzia masters na PHD wanavaa na sana sana Universities sio hizo hogeschool wanazoziita .Na kingine inategeema na shule yenyewe na aina ya degree uliyosomea.

    ReplyDelete
  6. HONGERA SANA SANA BI LILIANI. KWELI PENYE NIA PANA NJIA, NA WAKATI NI ILLUSION KWANI MARA HII TAYARI!
    WADAU TOKA AFRICAONLINE WANAKUPONGEZA SANA (THEMISTOCLES)

    ReplyDelete
  7. Nataka kusomamesha mtoto wangu degree ya kwanza Marekani au Uingereza vyuo vya bei rahisi ni vipi? Nisaidieni.

    Mwanangu kakosa admission vyuo vikuu vya Hapa Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Du, ni kweli jamani, kweli tembea uone mengi..sisi tumeiga UK kwasababu ya ukoloni,kumbe wazungu wengine wanaona UK kama nchi nyingine tu, wao wanafuata utamaduni wao....Sweden na Finland party kubwa zaidi ni High School... degree kawaida tu wala hawahangaiki na majoho ya Kiingereza. Unakula tai, unapewa ua na cheti chako unaanza!

    ReplyDelete
  9. Does 'joho'make any difference?Not to some of us.

    ReplyDelete
  10. hee! Watu mnaongea? Kwani issue hapa ni Nondoz au majoho!

    Hongera Lily na wengine mliohitimu, basi njooni nyumbani mtumie Elimu yenu kuelimsisha wengine ambao hatuna uwezo wa kujaku-nondo huko au kutumia Elimu hiyo kuendeleza kainchi ketu, hasa sekita ya IT na Sheria mana'ke hapa nyumbani haki zipo kama hazipo vile (kwa vile raia wa kawaida hatuzijui haki zetu).

    Hongereni sana wote mliokama nondoz.

    ReplyDelete
  11. ushauri wa bure kwa anon wa sept 19 at 2:09.achana na biashara ya kupeleka watoto Uk na USA,kwanza ni very expensive halafu kibaya zaidi ni high risk maana huko madawa ya kulevya nje nje na mwanao akiingia kwenye wrong group kwisha kazi,unless uwe na mtu mzima wa kumwangalia ajue nini kinaendelea.watoto kibao UK na USa wanaletewa school fees na wazazi wao wanazibwia unga.ushauri wa bure: viko vyuo vizuri sana sasa hivi kwenye nchi kama south africa,india,malasyia,australia ambavyo gharama zake ni nzuri na elimu ni quality.mtoto asikudanganye eti ataanya kazi na kusoma,uwongo mtupu,it is too taxing na hawezi kufaulu mitihani kwa sababu ya presha.

    ReplyDelete
  12. KWAKO NYAKATAKULE UNYILISA-ECHALO.
    Yego mwamba,nimekubaliana na hoja zako za msingi.Sasa kwa majibu zaidi napenda nikukosoe ila kwa kutumia email na maongezi yawe ya mimi na wewe.Tafadhali nipe email address yako kwa juice41@gmail.com
    Majita Bin Bugunda

    ReplyDelete
  13. DINAH, ISSUE HAPA NI MAJOHO, SIO NONDO, KWASABABU WABONGO WANALALAMIKA UTAPATAJE NONDOZZ BILA JOHO? UKWELI NI KUWA NJE YA MAREKANI NA UK, WATU WANACHUKUA NONDO BILA MAJOHO...ILA WAKIMALIZA FORM SIX WANAPATA KOFIA MAALUM NYEUPE...HIYO WANAITUNZA SANA NA KILA MEI MOSI WANAIVAA NA KUNYWA HADI ASUBUHI....HASA SWEDEN NA FINLAND.

    ReplyDelete
  14. Majita;
    Ambe kaluka,
    Yaani eti watu tuache shughuli zetu kukalia kujadili majoho tuu wakati hata kale kashule ka anthropodisi ka Doni Bosko nyumbani nako wanavaa majoo wakati wanahitimu!
    Majita nakuandikia sasa hivi tuongee mambo ya maana na baadaye ikiwezekana tuonane hapo the Hague!

    Nyakatakule

    ReplyDelete
  15. Hivi kuna Chuo ubelgiji wanavaa majoho?

    ReplyDelete
  16. HONGERA SANA DADANGU UTUFUNDISHE HIZO MBINU ZA MAWASILIANO UJUE KWAMBA WABONGO WENGI TUNAHITAJI HIZO KWANI MAOFISINI UNAKUTA MTU ANAKWAMBIA SUBIRI KAMA UNAWEZA KAMA HUWEZI ISHIA.

    KIPEPEO TOURS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...