Mbiu ya mgambo ikilia ujue ina jambo. Haya tena! Haya tena! Watanzania walioko Marekani nao wanajiandaa kutoa mlimbwende wao, na mrembo wao wa Mwaka.
Mrembo huyo atakayejulikana kama "Miss Tanzania USA" atachaguliwa baadaye mwaka huu baada ya mchujo wa ushindani utakaofanyika nchi humo.
Wale wote wanaotaka kujua zaidi na wangependa kujiandikisha kushirika nafasi hiyo na kujua ni zawadi gani zitatolewa na masharti ya kuingia kwenye mashindano hayo watembelee http://misstanzaniausa.com/ au wawasiliane na waandalizi wa mashindano hayo info@misstanzaniausa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. halafu mshindi anaenda kushindanishwa na RICHA? au mnajifurahisha tuu!
    Kweli UK ni mme wa dunia, USA labda kiranja mkuu!!!!
    wenzenu tumempeleka mrembo wetu miss TZ na kashindana barabara...

    ReplyDelete
  2. Mbona hawasemi watafanyia wapi hayo mashindano au nani waandalizi? Isije ikawa front for Exotic Escort business!

    ReplyDelete
  3. Idea ya Miss TZ USA is very good. Ila potrayal ya tangazo na hicho kichupi mungekitoa, maana hayaendani na maadili ya kiTZ. Bora huyo dem kwenye picha hapo juu angevaa kakanga hivi, kafupi kiushikaji hivi, eeenh, si mnaelewa ninachomaanisha! Lakini kichupi no no! Wazungu walisema, 'first impression is last impression'!

    ReplyDelete
  4. Baada ya kusoma link iliyotolewa kwenye hiyo habari nikajiuliza je inamaanisha wale wasio na makaratasi hawatagombea? Maana wakienda bongo kushindania MISS TZ ndio hawatarudi tena.....

    Link ilisema hivi:
    We are currently searching for contestants to participate into Miss Tanzania U.S.A.
    We accept applications from all Tanzanian young ladies who resides in the united states and all over the world under the age of 26. This event will take place in U.S.A sometimes in November 2007 (state TBA).

    In addition to the trophy and other goodies, the winner of Miss Tanzania U.S.A will get a ticket to go and compete with MISS Tanzania (In Tanzania). Miss Tanzania U.S.A will be an ambassador for Tanzania and will undertake several projects to promote Tanzania as an investment and tourist destination of choice.

    ReplyDelete
  5. Muite miss atlanta Tz, miss md us, au miss tx usa...msijifanye kuita miss usa tz...okay

    ReplyDelete
  6. Anon hapo juu hebu kuwa na positive mind.

    Acha kufagilia kivuli..read betweens line umeambiwa kuwa mshindi atakwenda kushindana na Miss Tanzania kunako 2008. atashindana vipi na Richa while richa ameshachukua taji?...Inaelekea English is not reachable.

    ReplyDelete
  7. sasa miss TZ usa mbona umeweka picha ya Cynthia masasi na kivuli cha bendera ya Tanzania au ndo ameshashinda tayari?

    ReplyDelete
  8. mnajisumbua kwani washindi wanajulikana nawakina lundenga kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  9. Watu wengine bwana, eti kichupi kitolewe.Utadhani hapendi kumuona demu kwenye kichupi,acheni unafiki.Mtu kama anon 7:24 ndiyo wale wale wenye majarida kibao ya ngono chini ya magodoro yao

    ReplyDelete
  10. hatu support hii kabisa..habari za haya mambo ya kuiga haraka haraka tuuuu na anayeandaa haya mambo hafuati maadili ya TZ kabisa....kwanza kaweka vitu juu juu tu sijui alilala usiku akaota akaona nitawachota wengi...wewe ni nani unayeweka haya mambo na tutakuamini vipi? Mind you umri unaoutaka hapo kwa wengi wanaishi na wazazi wao hapa USA. mahali itakapofanyika hapapo...heee jamani kama mnataka kufanya vitu vya maana muwe makini ...mipango yeyeyewe ni November...miezi hata sio miwili unataka watu wasafiri hukooo kwako...museme sehemu...kama ni huko TX, Ohio, Michigan, Minnesota au DC mwanangu hakanyagi ng'ooo..No offence kwa watu wanaoishi huko lakini from my personal experience ....sitasema mengi

    ReplyDelete
  11. HUYU DADA KWENYE PICHA ANAMVUUTO WA AINA YAKE.

    ReplyDelete
  12. Safi sana, sio kila mwaka ni miss TZUK, haya na wale watz wa China, Uganda, SA, Canada na kwingineko andaeni mashindani ya kumsaka Miss TZ huko mliko mana'ke Lundenga anatuyeyusha tu huku.

    Je watanzania walioko ndani ya Tz wanaruhusiwa kuja huko nakushiriki?

    ReplyDelete
  13. Annon wa September 17, 2007 10:28:00 PM EAT, naona kama una some points ulipozungumzia usiri wa venue ya mashindano haya ya ulimbwende... Ila umeniuzi ulipozungumzia issue ya mwanao, maana mi nazani atakua disqualified kwenye raundi ya kwanza.. kisa = kichogo. Miss Tanzania haiwezekani akawa na kichogo kama kile mamaa..

    ReplyDelete
  14. I would like take this opportunity to reply to your few questions kwa yule aliyeuliza kuhusu mavazi ya khanga.
    Keep in mind this is not Miss Bantu ni Miss Tanzania and a winner anakwenda kushiriki kwenye miss tanzania then miss world kama akishinda..basically hatuwezi kumvalisha kanga umeshanielewa mpaka hapo?.
    Na pia mind you mavazi yanayoshindaniwa ni kama swimming costume,evening dress,could be traditional attire you name it

    And in regard to the site..Hii site kwa sasa hivi imeandaliwa kwa kusearch or contestant ila in meantime site bado ipo in progress our site designer bado anaitengeneza tunaongeza more stuff ili iwe dynamic.We know right now site ipo static with no flash...Ila it will be done soon and we will keep you posted.

    Thank you
    The organization

    ReplyDelete
  15. Oh, you like to see other people's daughters walking their tails from side to side,right? Now is your daughter's turn to shake that booty in front of us.Don't worry. We'll be there watching her close and personal.Let me give a hint.When ya daughter asks you a permission to go to cancun with friends, guess what she'll be coming to D.c,Houston,Colombus,Detroit,etc.You know why I know that,nobody goes to cancun during the Huriccane season.Anway, we'll send you her pictures on her lovely bikinis.
    Yeah, we'll peep on your daughter's behind with a enormous lust, bro.We'll eye-balling her every step of the way.We will be doing her with our hungry eyes.Ha ha ha ha ha ha ha.Now how does it feel,old head?
    Oh, yeah Mbigiri said that.
    Holla back.

    ReplyDelete
  16. Jamani jamani tusiwe tunafuata mkumbo. Last 2 weeks Hashim Lundenga alikuwa anahojiwa channel 10 akiwa na Richa na dada mwingine mwandishi wa habari sikumbuki jina.

    AKAULIZWA: Dhana ya kushindanisha uzuri mabinti ni nini?
    Akajibu: ni sanaa
    AKAULIZWA: sanaa ni nini?
    Ndugu zangu kweli jamaa alishindwa kujibu alizunguka zunguka bila kufaka. Ukichukua tafsri ya sanaa kuwa ni kioo cha jamii. Hebu niambieni kwenye suala la urembo jamii inajifunza nini??? Je!
    ni ni mavazi ya magharibi? Nywele za bandia, maumbo slim au ni nini?
    Akaulizwa kuhusu sifa.
    Alisema hata mwanamke mnene anaruhusiwa kushiriki katika umiss mradi awe na vigezo kama ubunifu n.k. sasa mimi napata utata kidogo, kinacho wasababisha wembamba peke yako kushiriki ni nini?

    ReplyDelete
  17. Aaa... sijui hebu muulize Richa maana ya sanaa?
    Manake sisi tukijibu kuna atakaye sema tunamuonea wivu mdosi wa watu bure..!!

    ReplyDelete
  18. tafsiri ya sanaa sio kioo cha jamii.tafuta ujue

    ReplyDelete
  19. Nyie waTZ wa huko UK mnyamaze tu. Yooote mnayosema against Miss TZ USA ni uoga tu...au tunasema "You are Chicken!". Tunafanya haya mashindano na tutampeleka mwakilishi wetu kwenye the next Miss TZ. Je mnataka kuanzia sasa wawe wanashinda wadosi tu? Maana baada ya Richa kushinda (kama ni kweli ameshinda au kuna mtu ameshushiwa Escalade au Hummer nyumbani kwake!), sasa wadosi TZ yote wataingia kwenye mashindano! And guess what you ignorant, back-stabbing, development-wrecking people out there it is out Tanzanian identity ALL OVER THE WORLD that will be in jeopardy. We have to come together in order to succeed. And that means giving out positive, encouraging and corrective comments in order to improve an idea or a person.

    Sasa huyo anonymous anaemuelezea binti wa watu...why do that? Sasa kama wazazi wa huyu binti (ambaye..mind you! anaweza akawa ni Miss world kama akishindana na akashinda mpaka huko) wakisema NO, HATUTAMRUHUSU binti yetu kushiriki because there's a pervert out there, utakuwa unamfaidisha nani? Kila siku wajapani, wa south-africa ,a wamarekani ndiyo watakuwa wanashinda tu. Give Tanzania a chance...BE KIND, BE POSITIVE AND BE INFORMED!

    ReplyDelete
  20. Lete tasfiri ya sanaa
    Mheshimiwa BAKITA

    ReplyDelete
  21. eti miss tz usa!!?wasichana wenyewe age zimekatika,mimi sijaona msichana mwenye sifa hapa usa,naona wote wamekomaa ka madume.

    ReplyDelete
  22. Art (As sanaa) is beauty and beauty is art.
    The expression of ones unique love, immagination, vision, and interpretation of beauty through eyes, sensation, smell, sound, taste, and God....
    art has a lot of meaning could be yourself..it's hard to define art basically you don't have to Blame Mr Lundenga.

    Thanks
    Miss Tanzaniausa Organization.

    ReplyDelete
  23. Wewe Anonymous ulosema...
    "eti miss tz usa!!?wasichana wenyewe age zimekatika,mimi sijaona msichana mwenye sifa hapa usa,naona wote wamekomaa ka madume".

    Hivi uko jimbo gani la USA? Jamani...isije ikawa kwamba uko bush, na tokea uje hapa marekani hujatoka kwenda popote! Na kama kweli unaamini kwamba HAKUNA wasichana wazuri, na wenye umri unaofaa hapa, basi wewe umefilisika kimawazo, kiteknolojia, kiuchumi na kijamii! Pole zako Anonymous;-)!

    To ALL the haters...Bring it on!
    To Miss TanzaniaUSA Organization...keep it up! and
    To all those prospective contestants...show us what you can do girls...and good luck!

    ReplyDelete
  24. anon wa 2 31 anatutisha, kasign off na neno THE ORGANISATION hii nini MAFIA COSA NOSTRA

    ReplyDelete
  25. contestant atakuwa huyo huyo aliyekubali picha yake iekwe hapa. kwanza umri nadhani umeshakatika kama alivyosema mdau hapo juu...

    wangeweka MRS USA-TZ....wako ma mrs huku wee wacha bwana..watu wana watoto watatu lakini ukimwona bado saa sita saa sita

    ReplyDelete
  26. kama jamaa alivyosema hapo juu, nimetembea sehemu kibao hapa usa lakini wasichana hapa ni vichekesho,tusubiri tuone!!

    ReplyDelete
  27. cynthia masasi hana muda wa kuingia kwenye mashindano ya miss tanzania usa..so for all u haters just know she is not interested in miss yanzania usa..i dont think she even know that her pictures is being used..

    ReplyDelete
  28. Who are you? Where are you? Where is the venue? How can we join or get involved with anything when no information is available about the hosts? You actually expect us to divulge personal information about our business to link to your website? How do we know you are legitimate? Are you registered? What is your federal ID number? Every organization, association, business etc makes themselves known. We all know who organizes all the beauty pageants in the US! So who are you? And why should anyone sponsor, support or get involved with you if we don't know who you are? This might well be a scam! There have been so many scam "non-profits" taking our money and putting it in their pocket claiming that they are helping "our people" in TZ! If you are legitimate and honest --- make yourself known!!! Why are you hiding behind the generalized term "WE"? Who us "WE"?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...