ligi kuu ya soka bongo ijulikanayo kama vodacom premier league imeanza kwa vigogo vya soka kuyaanza mashindano hayo kwa kwikwi baada ya yanga na simba kutolewa nishai kwenye michezo yao ya ufunguzi. jana yanga kalizwa 1-0 na watoto wa mjini ashanti uwanja wa jamhuri morogoro wakati simba nao pia wamebenjuliwa na coastal union kwa 1-0 uwanja wa mkwakwani.
huko morogoro leo ni polisi morogoro na moro united na manjago wameshinda 2-0. hii inaashiria kwamba ligi kuu safari hii si ya kuchezea magazetini ama redioni...
Hapa wana Yanga inabidi kujiuliza mara mbili, kuna haja gani ya kutumia mamilioni kusajili wachezaji kama Kabanda, Mwalala, Sunguti, Lukunku, chuji nk baadaye kuwalipia vibali na mishahara mikubwa halafu kufungwa na timu ambayo bajeti ya usajili mzima hailingani na mchezaji mmoja wa Yanga inatia sana uchungu!!!!
ReplyDeleteMpira hauna guarantee ndugu yangu hata usajili vipi bado kuna kufungwa pia.Haina maana ukisajili kwa mamilioni ndio hufungwi.Katika usajili mpya wa Yanga Kabanda ndio afadhali kidogo wengine tumeuziwa Kanyaboya.Tumesajili majina na sio uwezo ndio maana sasa tunaanza kushikana mashati.
ReplyDelete