Home
Unlabelled
soko mjinga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ah mbona iko wazi. Hilo linaitwa soko mjinga kwa sababu toka lianzishwe wanaokwenda kununua vyakula hapo ni wajinga. Ni wajinga kwa sababu wanabamizwa mibei mikubwa mikubwa lakini hawashtuki. Wangejisumbua kwenda mbele kidogo mpaka Kariakoo wangepata vyakula hivyo hivyo kwa nusu ya bei.
ReplyDeleteSoko lisilo na akili hahahaha, nafikiri maana yake ni soko lisilo maalum au soko dogo.
ReplyDeleteNilikuwa sijui kama hilo la Kisutu ni mjinga kwa vile nijuavyo mimi soko mjinga mara nyingi huwa nje ya soko kuu/maalum na mara nyingi bidhaa zao huwa zinatoka moja kwa moja shambani na ni nafuu ukilinganisha na za masoko makuu/maalumu.
Mfano Kariakoo, Tandika na Tandale kabla hujaingia kule ndani unakutana na jamaa nje ya soko wamepanga bidhaa zao kwenye sandalusi(kipande cha kiloba), Ukienda kule Brixton, Liverpoor st au Rochester utakuta wana mobile shops/market muda wa mauzo ukiisha wanaondoka na maduka/soko yao.
michu naona leo umeamua kuniumiza roho yangu na kunifanya nipate uchizi, kwa picha zako za kunifuta hisia ya nyumbani. soko hili nilikuwa naliona expensive na la akina sunche bai, lakini nilikuwa na enjoy ninavyo katika katika maeneo yake.
ReplyDeletenafunga virago nirudi nyumbani maana ushanitamanisha uhondo wa kwetu.
majuu sometimes choo kichizi
KWA WALE WANAOFAHAMU HADITHI YA SOKO MJINGA HILO HATA HALIWAUMIZI KICHWA.
ReplyDeleteMOJA KATI YA SABABU KUBWA KWA SOKO KUITWA MJINGA, NI KWA SABABU YA WAUZAJI KUTOPIGA KELELE KAMA WAFANAVYO WAUZAJI KWENYE MASOKO YALICHANGAMKA.(MFANO; KARIAKOO, TANDIKA,ILALA NA KINONDONI).
MARA NYINGI UKIINGIA KWENYE SOKO LA KISUTU, WAUZAJI HUWA HAWAPIGI KELELE KUNADI BIDHAA ZAO. WAO HUSUBIRI MTEJA KWENYE UBAO WAO NA KUMPA BEI ZA BIDHAA ANAYOHITAJI.
SABABU NYINGINE INASAIDIKIWA KUWA IMETOKANA NA IDADI YA WATU WACHACHE WANAOKWENDA KUPATA MAHITAJI YAO KWENYE SOKO HILO KULINGANISHA NA YALE MASOKO YALIYOCHANGAMKA.
anony 10:56 noooooo point yako nooo soko mjinga kwasababu halina kelele...arusha lipo na lina kelele asubuhi
ReplyDeletemimi nitakubaliana na wanaosema bei zao ni ghali...na ni shida ya haraka au kutofikiri ndio kutakupeleka hapo..
Linaitwa soko mjinga kwa sababu kulikuwa na mjinga(mwendawazimu) alikuwa anitwa kikono kwa wale wa zamani kama mnamkumbuka alikuwa analala pale sokoni ndio watu wakawa wanaelekezana pale sokoni kisutu kwa mjinga anapolala...mwisho ndio ikawa tena soko mjinga.kalagabaho!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHILO soko silisahau kamwe,mganga wa kienyeji akikupa masharti kwamba anahitaji umletee njiwa mwenye makengeza au njiwa zeluzelu,hapo unawapata bila wasiwasi
ReplyDeleteanony 5:17 sikubaliani na wewe...!
ReplyDeleteMbona masoko mjinga mengine yameanza huku tukiyaona na hakukuwa na mwendawazimu wala kichaa? Na pia nadhani kichaa si sawa na mjinga. Ili uwe mjinga sharti usiwe kichaa.... Mwasemaje wadau?
Nakubaliana na wanaosema soko mjinga ni lile lisilo rasmi, na mara nyingi huwa karibu au pembezoni mwa soko jingine kubwa..hivi kumbe hata kisutu ni soko mjinga!
It is called Soko mjinga mainly because the sellers are never sure of the selling price. You will find that most of the time the buyers will be buying the merchandise on a very low price than what the market is looking for. And the Sellers never complain. But this was then. I dont think this still applies as the sellers are sharp upstairs now:) So the name 'Mjinga' has been carried accross since those old days.
ReplyDelete