si vibaya kula uroda wa nyasi za bandia wanja la zamani la neshno

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. wewe mtu una visa wewe

    ReplyDelete
  2. Wajameni, tutoeni tongotongo sisi wengine ambao hatujui maana ya nyasi bandia! Na kwanini wasiweke nyasi zenyewe wakaweka bandia? Je kuna chochote kisayansi kinaweza kueleweka kwanini tuliamua kununua nyasi bandia kwa zaidi ya TSHS 340ml wakati nyasi zipo za kumwaga mikoani za bure tu!? Je hizo nyasi bandia zinaota na zinahitaji kumwagiliwa?!!? Mhhh, makubwa haya.

    Tuelemisheni wenzenu. Kwa wale wanaojua maana ya nyasi bandia tafadhali! Maana najua kuna watu wataamua kukurupuka tu na kuweka uwongo hapa.

    Asateni sana na wabeja sana!

    ReplyDelete
  3. Hehehehe, URODA gani tena na wewe ,ebu fafanua vizuri? Unaonaje league sasa, Arsenal moto ule ule kazi kwa wajinga wajinga sasa

    ReplyDelete
  4. wewe unapoza swaumu tu, usituzuge

    ReplyDelete
  5. Anon at 7:57 Pm. Nyasi za bandia ni nyasi za plastic kwa kiingereza zinaitwa turf. Hizi nyasi huwa zinatandazwa uwanjani kiutaalam kiasi kwamza tofauti kati ya original nyasi na hizi za bandia huwa ni ndogo sana. Baada ya kutandaza layers za mchanga maalum chini hizo nyasi hufuatia huku zikiwa na mchanganyiko wa vimpira vidogo vidogo vinavyo act kama mchanga. Kama mchezaji tofauti ya turf na mchanga halisi kidogo ni impact kati ya miguu na uwanja au mpira na uwanja. Katika turf impact huwa ni kubwa zaidi kwa hiyo ni rahisi sana kwa wachezaji kupata maumivu "injuries".
    Kuhusu gharama hukutakiwa kuhoji kabisaa na hata hiyo milioni 360 sijui umeipata wapi. Hizi nyasi ni udhamni maalum wa FIFA ambao unaendelea katika nchi nyingi za dunia ya tatu Tanzania ikiwemo. Kwa hiyo Kaka/Dada baada ya kulaumu hebu shukuru maana siku moja mwanao au hata mjukuu wako atacheza hapo Taifa. Akhsante!!

    ReplyDelete
  6. Bwana misupu,mbona watupotosha? Urodo tena?
    BONYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!

    ReplyDelete
  7. Sanet anon Sept 24; 9:02 hapo juu kwa ufafanuzi. Sikujua maana ya nyasi bandia.
    Unasema ni udamini wa FIFA? MBona tena walikuwa wanaomba kwa Kikwete waondolewe VAT!? Umeshahau? VAT YENYEWE ilikuwa 65ml. Sasa thamani halisi ni mara tano ya hizo. Au siyo?!

    Asante lakini.

    ReplyDelete
  8. URODA VIPI MBONA UPO MWENYEWE HAPO HATUONI HATA SABUNI ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...