Mcheza soka chipukizi na anayeinukia kwa kasi kubwa, Derek Marwa, wa kwanza kushoto (walio simama) akiwa na timu yake ya yosso iitwayo "PrillRed" ya Bethesda, Maryland inayoshiriki katika michuano mikali ya ligi ya soka ya Montgomery County (Washington D.C. Metropolitan). Uchezaji mahiri na ufungaji magoli wa Derek katika ligi hiyo umemfanya aanze kuzongwa na makocha wa timu za daraja la juu chipukizi ziitwazo "Classics" ili afanye majaribio ya kuzichezea. Derek anataka siku moja awe katika kikosi cha Taifa Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AaaaaaameNNNN Na iwe hivyo katika jina la YESU!Inafurahisha sana na ni baraka kuchochea vipaji vya wadogo hawa!

    ReplyDelete
  2. Yosso, umenikumbusha mbali, enzi zile nilipokuwa ka binti kadogo wadada wa Sekondari walikuwa wakipiga raba fulani hivi za kitambaa zimepanda kiaina hadi kwenye kianzio cha leg zikiitwa Yosso.

    Derek mungu akujaalie ufikie malengo yako, umetambua kipaji/ajira yako mapema basi wewe zingatia mambo yote muhimu ili uje kuwa naninhii wa Bongo.

    Kazi nzuri!

    ReplyDelete
  3. Tayari tumeshapata kaserengeti boy
    Baadae huenda akachezee kwenye club kubwa kama Madrid, Milan na nyengine.

    Endelea kijana, HONGERA

    ReplyDelete
  4. Marekani hakuna mpira, kama kweli wazazi wa huyo dogo wako serious wamuhamishie mapema europe, napendekeza UK au Germany zaidi coz mpira wao wa shughuli, akienda Italy soka la bongo hataliweza.

    ReplyDelete
  5. Pongezi nyingi kwa wazazi wa kijana huyo kwa kuona umuhimu wa kumruhusu mtoto wao kuonyesha kipaji chake na wao wakashirikiana kukiendeleza. Changamoto kwa wazazi wengine tusiwabanie watoto wetu.

    Kijana hongera sana na Mungu azidi kukupa nguvu na hekima.

    ReplyDelete
  6. ASANTE SANA MZAZI WA USA HAWA NI MOJA KATI YA WATOTO WENGI WA WABONGO WANAOCHEZA NICHEZO MBALIMBALI HAPA USA.

    ReplyDelete
  7. Hongera nyingi sana kwanza kwa Dereck halafu hongera kwa wazazi wake.
    Naomba mwendelee hivyo hivyo,mkiweza mpelekeni Ulaya huko mbeleni,nakubaliana na anonymous wa Sept 22,2007 3:29pm, kuwa ni heri UK au Ujerumani.Italy waachieni wa South America msipoteze muda wenu.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Derek ;-)! Keep it up!

    From Aunty Nzota.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...