jengo la makao makuu ya shirika la bima la taifa lililopo kona ya mitaa ya pamba na samora huenda likapigwa mnada hivi karibuni kufuatia amri ya mahakama ya kazi kuliamuru shirika hilo la umma kulipa wafanyakazi wake 1634 malimbikizo ya mishahara yapatayo shilingi bilioni 3 na ushee ambayo wanalidai.
pamoja na kupigwa mnada jengo hilo ili kulipa deni hilo, mahakama hiyo pia imeamuru akaunti kadhaa za shirika hilo zizuiwe na mali kadhaa kuuzwa ili kufidia malimbikizo hayo. amri hiyo imetolewa majuzi oktoba 12 kufuatia hukumu ya kesi ilofunguliwa na wafanyakazi hao mwaka 2002 kudai mishahara mipya kuanzia januari 1, 1997 ambapo mnamo oktoba 8, 2007 walipeleka ombi mahakamani hapo kukazia hukumu hiyo ya awali ilotolewa mei 23, 2004 ambayo wafanyakazi walishinda lakini shirika lilidai halina uwezo wa kulipa mishahara hiyo mipya.
mahakama hiyo katika uamuzi wake wa juzi imetoa mwezi mmoja kwa shirika la bima kulipa malimbikizo hayo ama sivyo jengo hili la makao makuu lipigwe bei na akaunti zake kadhaa kuzuiwa ili kufidia malipo hayo.


Safi sana, wache lipigwe mnada tununue. Jengo kubwa hela za kuwalipa wafanyakazi hamna. Akili gani hiyo?
ReplyDeletePiga, ua, garagaza hilo jengo litanunuliwa na MANJI tu hilo.
ReplyDeleteNyie subirini tu
Ann...9:09:umesema ukweli..jamaa ana uchu na majengo huyu... wakiona AIBU SAAANA wataliuza kwa NSSF... nao kwa kupenda kudandia MKUKI KWA MBELE... cjui kama wataliachia....
ReplyDeleteHapo ndipo Tanzania tunapoonekana vituko.Watu wanaua shirika halafu wanadai waongezewe mishahara.Watu wanaua kiwanda halafu wanaandamana hadi kwa Raisi au mahakama kuu kudai walipwe mafao ya kuondoka kiwandani au shirika baada ya kuua.
ReplyDeleteWatanzania tuache uhuni huwezi kuua kiwanda au shirika halafu udai mafao uwe meneja mkuu au mesenja.Huna haki kabisa.Hata kama sheria zipo za kukutetetea sheria kama hizo ni za kihuni na hazitakiwi kuwepo katika mfumo wa utandawazi wa sasa.
Hivi ni halali kweli hata kwa majaji kukubali watu wanaoua shirika au kiwanda kuwa walipwe mafao au mishahara iongezeke? Utamlipaje mafao mtu aliyekuulia biashara yako? Huyo ni muuaji anayetakiwa aondoke mikono mitupu ukimhurumia apelekwe jela kwa kuua mtaji wa walipa kodi waliolipa kodi kuanzisha shirika hilo la Bima.
Kwangu mimi naona shirika la BIMA ni marehemu na waliooliua ni wafanyakazi wenyewe.
Mawakili naomba mtetetee walipa kodi kwa kuwapinga wafanyakazi wa bima kuongezewa mishahara baada ya kuua mtaji wa walipa kodi na kuliacha shirika likiwa hali mbaya.Hivi Tanzania ni lini itakuwa na mawakili wenye uchungu wa kuwatetea walipa kodi ambao mali zao kama hilo Shirika la Bima zinapokuwa hatarini?
Mawakili wa Tanzania ni vizuri waamke.Wakati mwingine wainuke watetee walipa kodi dhidi ya Wafanyakazi wa sekta za Umma wanaokalia vibaya mali za umma na mashirika.Wasingoje tu kesi za kulipwa.Uzalendo wa mawakili wa Tanzania uko wapi?
Wafanyakazi wa Bima wanatakiwa si waongezwe mishahara bali wanatakiwa wapunguzwe mishahara na kutimuliwa wote bila mafao yoyote sababvu shirika wamelifikisha mahali pabaya na wamezamisha kwenye shimo mtaji wa wenye hisa wa bima ambao ni walipa kodi wan chi hii.
Wanasiasa mko wapi amkeni dhidi ya mwenendo wa wafanyakazi wa bima wanaotaka nyongeza za mshahara wakati shirika linadidimia chini.Kila moja anahitajika kuwa mzalendo awe Jaji,Wakili,Mwanasiasa au mlipa kodi ni vizuri tuwe wazalendo.
Mimi binafsi nimeamua kuandamana kuanzia sebuleni kuelekea Chumbani kwangu kupinga hiyo hukumu ya wafanyakazi kuongezewa mishahara wakati shirika linadidimia chini na mtaji wa walipa kodi unapotea.
Pamoja na heshima niliyonayo kwa mahakama hukumu hiyo haijanifurahisha imekosa uzalendo wa utetezi wa mali za walipa kodi inatetea waua shirika wafanyakazi wa Bima Kama sheria zilizotumika ziko sahihi basi sheria hizo zimepitwa na wakati inabidi zibadilishwe haraka ili mtu akiua shirika au akilifikisha mahali pabaya asilipwe nyongeza za mshahara bali apunguziwe mshahara au afukuzwe kabisa.
koloboi@yahoo.com
Hivi jamani hua vitu kama hivi inakua no lose kwa taifa hua nani anastahili kua responsible,maana kuna uzembe wa mtu,ingetakiwa waliokwisha kua wakurugenzi woote watoe maelezo inakuaje mpaka watu wanakosa kulipwa na kama wana vimali mali vyao watoe maelezo wamepataje.Hizi ni mali za uma zinanunuliwa na Manji.
ReplyDeleteKweli kuna watu waropokaji,wewe koroboi...huelewi msingi wa maamuzi ya mahakama ya kazi....ila sikushangai sana maana ndio utamaduni wa baadhi yetu hupenda sana kudandia mambo yasiyowahusu....mahakama haiwezi kutoa uamuzi huo bila kuwa na sababu za msingi...kwa taarifa tu kesi hii ni ya muda mrefu....haki hii ya watumishi wa shirika ilistahili ilipwe tokea mwaka 1997....lakini kama tujuavyo..rizki ya mtu ipo tu...hucheleweshwa na baadhi ya watu...fanya utafiti kabla ya kutamka utumbo wako
ReplyDelete...acha walipwe pesa zao bwana na hilo jengo halitusaidii chochote acha lipigwe bei tuu na kampuni yenyewe ni upuuzi mtupu maana ni kama miradi ya watu binafsi kula tuu bila uchungu wowote huku tukidanganywa ni mali ya umma na bora bima ife kabisaaaa!
ReplyDeleteWafanyakazi wa Bima wamelila shirika la Bima wamelimaliza sasa wameenda kortini waliuze wafunge mahesabu wagawane na kutawanyika na kulirudisha Ground ZERO.
ReplyDeleteWatu walitoa moanoi kupinga maamuzi ya mahakama, hawajafnya utafiti ya kutosha. Kusema kwamba wafanyakazi wameua shirika ni ujinga . Kwasababu shirika lilikuwa lnaendeshwa na management , chini ya bodi ya wakurugenzi, wakifanya kazi chini ya wizara ya fedha. Kama ni kuua shirika waliliyoliua ni wasimamizi, ambayo ndiy waloikuwa na dhamana ya kusimamia kuendeshaji wa shirika, kumtuisha mfanyakazi wa ngazi ya chini lawama ya kuliua shirika ni kosa.
ReplyDeleteCCM na sera zake holela, pamoja na wizara, bodi ya wakurugenzi, na management, inabidi wawe responsible kwa shirika hilo kufa pamoja na kuwa na monopoly for more than 25 years! wao ndo wameharibu, sasa it is not fair watu wengine hasa wafanyakazi waliyoitumkia shirika kwa uadilifu wabebe athari za uzembe wa watu wachache.
Koroboi...yaani wewe unasupport kiwanda au shirika ambalo halilipi watu wake. Nini faida ya kufanya kazi kama hulipwi? Au wewe ni mmoja ya wanaokula jasho la watu? Au wew ni mfanyakazi uanyependa kuonekana umebeba briefcase lakini huna hata senti mfukoni mwako?
ReplyDeletekama hawalipi wafanyakazi inamaana kuwa hawaingizi pesa, kama waningiza pesa basi wanawanyonya wafanyakazi otherwise funga biashara. Atakuja msouth atafungua bima yake na watu watakoma. Watalipa mpaka wachoke. Na upuuzi ni wao wao..wameshindwa kufuatilia bima nyingi. Ni magari mangapi na majumba mangapi yanaunguzwa na watu wanalipwa kuliko gharama ya gari au nyumba.
Well, ikija bima ya wenzetu watu wataendesha kwa heshima barabarani. Kwa vile hawatakua wakilipwa juju juju tu na wafanyakazi wananyimwa mishahara.