
seba mtupili (shoto) na wenzie wakibugi ymca enzi hizo. hivi sasa seba ni mwalimu wa tenisi wa vijana klabu ya gymkhana na pia ni mchezaji wa timu ya taifa wa gofu. amewahi pia kuwa bingwa wa tenisi.

seba mtupili (kulia) na rafiki yake wakinionesha picha nilizowapiga miaka ya 80 leo nilipokutana nao klabu ya gymkhana

seba mtupili (kati) na mwenzie (pili shoto) wakila bugi na wenzao enzi hizo ukumbi wa ymca


duuh! enzi hizo suruali "don't touch my shoes"..sisteri ana usongo wa nguuuvu..hapo lazima mwimbo wa "holiday"
ReplyDeleteMICHUZI,
ReplyDeleteHIZI ENZI TULIKUWA TUNAITA-ZA USURE;UTASIKIA WATU WANASEMA YULE JAMAA MSURE KWELI.
Hahahaaa yaani mdau umenikumbusha mbali, Ymca enzi hizo, na hivyo viatu vya kichina wakati huo ndio vilikua vinatamba kama nini,
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteHizi picha za enzi hizo zingeenda poa sana na ule uchambuzi uliouweka pale bongocelebrity.com kwenye habari ya dj seydou.niliupenda sana.
....hivyo viatu vya kichina vinanikumbusha mbali sana,vilikuwa vinaitwa bruce lee.kweli kila kila na wakati wake.
ReplyDeleteMdau wa Tarehe October 15, 2007 4:08:00 AM EAT,kukuweka sawa vile viatu vilikwa vinaitwa "Kung Fu Shoes" na kuvipata ni mtaa wa Pemba au Ilala kwa Muddy Punky nao wana ringa kwenye kuuza suruali unanyoshea wanga hapo duuuh!! Aaaaaaaah David Olela kama namuona.
ReplyDeleteMichuzi bwana wa siku nyingi kwenye fani si mchezo.
Duh nayaona Makopo ya Oki na Korie kwa nyuma na vile viti vya rangi ya Orange bdo vpo Cho kikuu... Du ni cku nyingi saaanaaa...
ReplyDelete