
usiku huu tulikuwa ukumbi wa diamond jubilee holi kuning'inia na kuchanwa mbavu na mark curry a.k.a. bw. cooper ambaye aliingia na wapambe wa kimasai huku yeye mwenyewe kala lubega. shoo hiyo ya masaa mawili ilifana na umati wa wadau uliohudhurika uliondoka umeridhika. ukitaka kujua mengi ya mchekeshaji huyu bofya hapa

karibu na mwisho wa shoo bw. cooper alikaribisha wadau jukwaani kubanjuka

bw. cooper aliongelea mengi katika maisha na jamii, huku akisisitiza watu wavae kondom wakati wa kunanihii kama kinga ya maradhi

kila aliyepanda jukwaani alieleza anafurahia nini siku hii. huyu mdau alisema kuwa anafurahia kuanzisha mradi mpya ambao hakutaja ni wa nini...



Mmeshaning'inia na Mista Kupa shwali au vp.Turudi kwenye ishu za Tizi,mambo ya list of shame, Buzwagi na tamko na Mheshimiwa Butiku alilolitoa alhamisi kuhusu mafisizz mbona umelibania hebu tuletee mezani tuoshe vinywa,maana nasikia ni heri uliwe na simba ndugu zako wanaweza kupata kajiutambulisho kuliko fisi aka fisadi
ReplyDeleteBW. MITHUPU KWANZA HONGERA KWA LIBENEKE MAANA NAON WALIENDELEZA HADI DEI BREKI. MIE NATAKA KUMJIBU HUYO MDAU JUU, WE WALA USIHANGAIKE NAYE. TENA NAKUSIFU KWA KUTOINGILIA MIJADALA YA NAMNA HII, UKIDHIHIRISHA USEMI WAKO KWAMBA GLOBU HII SI YAKO NI YETU WOTE.
ReplyDeleteMIE KWA MUONO WANGU NAONA STAILI HII INAFAA SANA KWANI UNATOA NAFASI KUBWA YA KUONESHA MAMBO AMBAYO KWENYE VYOMBO VINGINE VYA HABARI HUONI. KWA LUGHA INGINE NAMWAMBIA HUYO MDAU HAPO JUU AKITAKA MAMBO YA BUZWAGI NA AENDE ZAKE KWENYE WEBU ZA MAGAZETI ALIKOSOMEA HAYO MAMBO YA KINA BUTIKU. HUMU TUACHIE SIE AMBAO HATUPATI NAFASI YA KUONEKANA SEHEMU INGINE NA KUTOA MAONI BWELELE BILA NOMA WALA NINI.
MTU AKITAKA MAMBO YAKINA SIJUI NANI AMBAO WANAANDIKWA KILA SIKU NA AENDE HUKO HUKO. HII NI TOVUTI YA WALE WANAOSAHAULIKA NA VYOMBO VINGINE VYA HABALI. UPO HAPO WE MDAU WA HAPO JUU????
Asante mdau wa hapo juu. Si saa zote watu wanataka kuongelea Buzwagi issues.Some people needs to live a little!!!
ReplyDeleteGreat job Issa
jamani si nilisikia kwenye kipindi cha kina fina kuwa mr kupa atavaa nguo za masudi?? ile jeans ni ya masudi kweli au uzushi tuuuu????
ReplyDeleteSasa ilikuaje huko kwa inglishi iz not richabo pipo?
ReplyDeleteNaikia Paris Hilton naye anaptia bongo akitenda South Africa.
ReplyDeleteNaona tangazo la JK linafanya kazi au ni mchemko tu.
Kila mmarekani anatafuta makao yake ya kustaafu. Michial jacson kashapata kwake. Sasa hawa wengine wnnatafuta huko...Angelina ameshasucure namibia...sasa....hawa...ulaji bongo...
Kweli sio siri, mnacheka lakini najua hola... sina maana ya kusema nyie ni Maimuna, bali ni kwamba hawa blacks lugha yao ni ya mtaani zaidi kuliko ya vitabuni ambayo ndo tunayojifunza sisi. Na msijisikie vibaya ni kawaida tu, samtaimz unafoji tu, so what! mradi mmechill out au siyo? give me hi five...
ReplyDeleteDOH! Hao wamasai walitumia deo kweli au Mr. Cooper anafaidi kikwapa hapo?
ReplyDelete