mstaafu wetu mh. bwm tulikuwa naye beneti tofauti na inavyodhaniwa. wengi tumesikitishwa kwa yeye kukosa tuzo ya rais bora inayotolewa na kibopa mo ibrahim ambayo imenyakuliwa na rais mstaafu wa msumbiji, joachim chissano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. We Michuzi wewe, usimlinganishe Chissano na Mkapa! Chissano mwanaume wewe!
    Mkapa pamoja na mazuri yote aliyoyafanya hawezi kumfikia Chissano kiuongozi na kidiplomasia pia. We vipi wewe!
    Mkapa hizi tuhuma za ufisadi ndo zimemchafulia maskini!
    Lakini all in all Chisano alistahili na yuko juu.

    ReplyDelete
  2. Michuzi wacha masihala bwana, wewe ulidhania Ben atapata tunzo lile, huyu jamaa corrupted than any president in Tanzania history. Wangempa mkapa nadhani watanzania tungekuwa wa kwanza kuprotest against it.

    ReplyDelete
  3. Mi sioni tatizo lolote kwa yeye kukosa hiyo tuzo kwa kuwa hakustahili kuipata. kwa hiyo Bw. Michuzi usihuzunike sana kwa sababu ndugu yetu huyu amejikosesha mwenyewe hiyo tuzo kwa kufanya mambo ambayo yalikuwa kinyume na uongozi bora. Kama wananchi wake tu wanamtuhumu kuwa ni miongoni mwa mafisadi walioiweka nchi katika matatizo Mf. kwa mikataba mibovu, kununua ndege ya raisi kwa mabilioni ya fedha pia kununua rada kubwa ilhali nchi haina ndege zinazostahili kuongozwa na hiyo rada then tulalamike tu kuwa jamaa amebaniwa tuzo?

    I'm sorry Michuzi ila siwezi kuwa Mnafiki kiasi hicho.

    Lengo langu kwako ni wewe unielewe no matter kama utayapost maoni yangu au la!

    Siku njema.

    ReplyDelete
  4. Pole sana kaka michuzi kwa Anko Beni kukosa mamilioni ya Mo Ibra. Lakini wengi wetu tumefurahi maana tumegundua kwamba Ben alitupiga bonge la changa la macho, tukadhani yupo poa kumbe anapiga dili za kutuibia. Afadhali hakupata hiyo mimilioni.

    ReplyDelete
  5. Michuzi "wengi" wewe na nani? we sema umesikitika mwenyewe not wengi!

    Huyo jamaa alishajilimbikizia za kutosha hahitaji pesa za MO! Ngoja zienda kwa wanaozihitaji!

    ReplyDelete
  6. hongera comrade chissano ulistahili ila kwa upande wa mzee wetu sijui imekuwaje lakini hili la juzi la kukataa kujibu tuhuma haiwezi kuwa sababu kweli? mbona wazungu wanamfagilia sana raisi wetu mstaafu mkapa?

    ReplyDelete
  7. Michuzi,
    Kukaa serikalini ndo kumekugeuza vile? Nauliza Mkapa kupewa Mo Ibrahim prize itokane na nini? kiburi alichokuwa nacho? kung'akia waandishi wa habari? kutolea mimacho mtu akimuuliza maswali kadhaa? kufanya biashara ikulu? no way hakustahili

    ReplyDelete
  8. Michuzi hivi huyo fisadi wenu mlitegemea kweli ashinde hiyo award ???????? kwangu mimi Mkapa ni mwizi nambali wani.

    ReplyDelete
  9. Afadhali amekosa!maana hizo biashara zake alipokuwa Ikulu na kutozojibu nadhani wakaona kuna ukweli wakampiga chini.."u can fool some ppl some time but you cant fool all the ppl all the time"..hakujua kwamba magazeti yanafika embassy? na embassy wanapeleka summary ya magazeti yote kwao! jibu tuhuma kama unataka uwe mtu safi ata kama katiba inakulinda..its for ur own good not MINE.

    ReplyDelete
  10. Hii inaonekana ni mwanzoni mwa utawala wake, alikuwa hata hajanenepa na wengi wenu mnaonekana makinda. Ukweli ni kwamba Ben aliwadharau waandishi wa Tanzania na pengine kuwachukia kabisa. Tanzania ilipofikisha miaka 40 ya uhuru aliwaita wahariri anaowataka yeye kumhoji na kuwadharau wengine kwa kuogopa kupigwa maswali mazito. Kukosa kwake tuzo ni halali kwa kuwa hafikii ubora wa Chissano ambaye ameongoza nchi kwa kuweka misingi mingi mipya ambayo yeye Ben alishawekewa na hata kama angejaribu kubadili watu wasingekubali, mfano ukomo wa urais. Aidha ikumbukwe kuwa mafanikio yake yanayotajwa ni kutokana na kufuata maagizo ya wakubwa wa magharibi lakini mlalahoi hana chake. Pamoja na utajiri wote wa Tanzania, kama madini na utalii na kilimo, hakufikia ukuaji wa uchumi wa Msumbiji nchi ambayo haina kitu na ilikuwa vitani kwa miaka zaidi ya 20. Ben ameishindwa kabisa Zanzibar na kashfa zake zinajulikana. Wiki iliyopita gazeti moja la nje liliandika baadhi yake na kwa kuwa Mandela na Salim wanamfahamu, isingewezekana yeye kushinda.

    ReplyDelete
  11. Michuzi, hembu acha utani bwana, be serious. Utasikitishwaje na huyo jamaa kukosa Mo Ibrahim award? He does not deserve it, after all the ufisadi that took place not only under his watch, but he was also an active participant. ever heard about good governance? we are only receiving a pity out of our mineral wealth, thanks to this guy and his cohorts.

    ReplyDelete
  12. Michuzi unaweka post kama vile hujui POLITIKI za kiafrika!

    Hapa BWM ndo alikuwa kalamba ofisi, waandishi lazima awaweke beneti kwani mlikuwa wote ktk kampeni.

    Mlipoanza KUMJUNGUA tu ndo urafiki ukaota mbawa. Na of-coz rais akishaingia madaraka kumuona ni hadi PROTOKALI zifuatwe.

    Na sasa BOYZ II MEN wameshaanza kuwa-chenjia, hawalongi na nyie -waandishi - kama ilivyokuwa awali. Tena siku hizi cowboy (PM) ndio kawa kimya kama mbu vile.

    itafika mahali mtakuwa kama paka na panya!.
    si unakumbuka mziki wa BWM na gazeti la RAI???... Sasa sijui gazeti gani litalipiku RAI sasa. maana Habari Corps wazee wa Netweki wameshainunua, na sasa ipo mdebwedo. ni chombo cha itikadi na uenezi cha chama

    Mungu ibariki TZ

    ReplyDelete
  13. Zawadi ya Mo Ibrahim inaenda kwa watu walioongoza kwa kufuata misingi ya utawala bora kwa maana ya kutoendesha nchi kwa maslahi yao binafsi bali maslahi ya wananchi wao,sidhani kama hiyo sifa ndugu yetu bwm alikuwa nayo! nakubali kazi zake zaidi kuliko utawala wa sasa wa awamu ya nne lakini nakiri pia kwamba tamaa pia inawezekana aliiweka mbele akasahau majukumu yake halisi kama kiongozi wa wananchi.

    ReplyDelete
  14. Michu mbona kakugeukia wewe?Lazima alikutwisha kigongo na wengine wakacheka...ha ha haa

    ReplyDelete
  15. Mi nimesema akome nashangaa umetoa comments zangu. Akome alidhani ni mashindano ya kucheza sindimba hayo.

    ReplyDelete
  16. Ngoja niwaambia, kwenye kamati ya uteuzi yupo mshikaji wangu. Mkapa alikuwa mmoja ya wanaotegemewa kupewa hiyo zawadi. Ila walianza kuchambua mambo ufisadi mwingi ukaibuka hadi noma. Wakamwita hadi Washinton DC, Dr Slaa atoe ushahidi wake. Akaanika hadharani mambo, dokumenti kibao hadi mahoteli sauzi huko yaani balaa..mchezo ukaisha Chissano akachukua.

    ReplyDelete
  17. Anko michuzi unajua wewe umezaliwa siku nyingi sana na umeona mengi sana na unajua sana mambo ya diplomasia kuhs hilo mi sina ubishi HILA ubishi wangu ni kwamba labda BEN akuwa na bahati au amezisiwa tu nahuyu chisano hila ben alivyo kuwa ikulu amefanya mabo mengi sana hila kwa sababu sisi wasomi wa siku hizi atujui chochote na tumekalia ushabiki ndio maana watu wanamuona afai hila kwa kweli amejatihi sana mimi naamini hivyo na atatokea km yeye kwani mambo yake yanaonekana hivi unajua MICHUZI mi nimetoka LINDI saa 12 asubuhi na nimefika DAR saa 9:30 na sio huko tu nenda kila shule kuna darasa moja amejenga kwa mpango wa MMEM na angalia miradi ya barabara pia angalia BUNGE letu na uwanja wa TAIFA MPYA pia angalia wanafunzi walivyokuwa sasomi wengi kwa kweli kwa sababu alikuwa apedwi toka ameingia madarakani basiwaswahili wanasema amekuwa na DAMU YA KUNGUNI! hila ben amefanya sasa walioingia ndio wanatafuna kila kitu

    ReplyDelete
  18. mkapa kafanya mengi lkn alikuwa apendwi tu michuzi minakuambia jana nimetoka mtwara na jana hiyo hiyo nimefika dar mpaka saa tisa nipi dar kwa mara ya mwishi nilifika siku ya tano hapa dar nikiwa niuza nguo zangu zote na kutoa ahadi ya kutokwenda huko hila mkapa maenifanyisha niende kila siku

    ReplyDelete
  19. MICHUZI
    MKAPA kafanya mambo mengi sana na alistahili sana tuzo hii lkn kwakua si mwenye bahati toka utawala wake mpaka anamaliza kwahiyo watz tumezoea sana kuponda mambo bila kuangalia kwakweli benn wameponza baadhi ya mawaziri wake na watendaji wake wakuu na mkewe lkn amefanya mabo mengi sana kajenga uwanja wa kisasa,amejenga daraja kusini,barabara ya singida mpaka shinyanga,bunge,kila shule ya msini kuna jengo lake,amepunguza madeni ingawa wazee sasa wanenda kila asubuhi ulaya kukopa na mengine mengi kwakweli mi nafagilia BEN kwani nafikiri amekuwa wa PILI kwenye hii tuzo

    ReplyDelete
  20. Mkapa hakustahili hiyo tuzo kabisa ,kwani kishajilimbikizia mali nyingi sana zinamtosha.

    ReplyDelete
  21. hivi wewe michuzi unafikiri hiyo zawadi wanatoa kibongobongo,wamepata mawazo tofauti ya kidplomasia mkapa ni mwizi tu kama viongozi wengine wa tanzania hayo mazuri aliyofanya kama raisi ilikuwa ni wajibu wake na mabaya ni mengi na anabahati mchonga alifariki.

    ReplyDelete
  22. michuzi mambo mengi ya serikali unaandikaaga kiushabiki tu sababu na wewe upo serikalini we unajua jamaa kashfa zimemuandama na magazeti yanasomwa na ofisi zote za ubalozi we unafikiri watampa kura kweli,"halafu anaambiwa ajibu tuuma yeye anaongea kiburi" viongozi wa africa wanakera sana,hebu tuuambie sababu zinakufanya uone mkapa anstahili hiyo zawadi pleaseeeeeeee!labda sisi hatuzijui.

    ReplyDelete
  23. Kaka Misupu Naona Sasa Upambe Unakushinda...Huyo Ankal Ben Ni Noma Yaani Angepata Hio Tunzo Tungeandamana Kwani ankal Ben Ndo Rais Pekee Mstaafu Alietajirika Na Wazifa Wake Africa....Na Unitupe kapuni kama ulivozoea

    ReplyDelete
  24. Unafiki mtupu. Eti "tumesikitika" wewe na nani mlisikitika? Mtu mzima ovyooooooooooooo

    ReplyDelete
  25. Michuzi! Michuzi! Michuzi! What are you talking about man!!! Huyo mwizi nani ampe award. Hana chochote alichofanya zaidi ya kuiba. atasahaulika in a minutes man. Huyo ni one of corrupted president in our history. Angepata hiyo tunzo mimi ningekuwa wa kwanza kuipinga. Tanzania hatuna mtu hata huyu wa sasa hivi utombo mtupu sijui wizi lakini i am sure about his performance.
    Mkapa utaishia motoni baba, binadamu tu wapita njia tu, lakini umetuibia, na kutunyanyasa vya kutosha. Ahsante sana.

    ReplyDelete
  26. Mzee BMW alikuwa bado mwembamba sana. Enzi hizo alikuwa bado hajapata msosi wa kutosha. Sijui kama angepata ile tuzo ya Mo Ibrahim ingekuwaje.

    ReplyDelete
  27. At least a glimps of justice has been shown a a commitee under Koffi Annan

    ReplyDelete
  28. Mzee naona picha ya kipindi, na umemkumbuka Mzee. Lakini mbona wengi walikuwa wembamba sasa wamebeba mizigo mizito matumboni mambo safi nini kwa waandishi? Umeona Blog yangu? nilipoteza password sasa mambo safi!

    ReplyDelete
  29. Mzee naona picha ya kipindi, na umemkumbuka Mzee. Lakini mbona wengi walikuwa wembamba sasa wamebeba mizigo mizito matumboni mambo safi nini kwa waandishi? Umeona Blog yangu? nilipoteza password sasa mambo safi!

    ReplyDelete
  30. Michuzi
    I have to few scandals for you on Mkapa
    1) Ununuzi wa rada (30% commission)
    2) Ununuzi wa ndege ya Rais($49mil)
    3) Privatisation of NBC, TANESCO and many more State firms.
    Mkapa witnessed all these and didn't do anything. End of the story.! and these few scandals disqualify him from any nomination.

    ReplyDelete
  31. HAYA MICHU....KAMA NI KUSIKITIKA BASI NI WEWE NA FAMILIA YA BEN, MANAKE HAKUNA MTANZANIA MWENYE AKILI TIMAMU NA MWENYE UCHUNGU NA NCHI HII AMBAYE ALITAKA HUYU FISADI ASHINDE HIYO TUZO!! BEN NI MWIZI MWIZI MWIZIIIIIIII! JAMANI, I HOPE ANASOMA HII BLOG ILI AT LEAST AONE JINSI TUNAVYO MFIKIRIA! YOU ARE A SHAME TO ALL TANZANIANS! INSHALAH, HAKI ITATENDEKA TU.

    ReplyDelete
  32. Michuzi acha politik,huyu mtu apate award kama hii kwa sifa gani aliyo nayo?kumbuka katauachia msemo wa "kutoka baba wa taifa mpaka baba vibaka"!mtu gani huyu asiyekuwa hata na huruma na wananchi wake ati anakuwa na minista anayesema "hata kama watu watakula nyasi/maani kama ng'ombe rada lazima inunuliwe"yeye anacheka tehe tehe!ati rada kwa ndege gani zinazotua bongo?then ndege ya rais afu nasikia ni mbovu!AnaBen co!aibu aibu rais mzima na akili zake timamu anaanzisha biashara akiwa Ikulu wapi good governance? wakati mpambe wake baba wa taifa alikemea sana kuhusu hili!
    Nadhani tangu kuzaliwa kwa taifa hili hatujawahi kupata rais fisadi kama huyu sasa award kama ile apewe ya nini?

    ReplyDelete
  33. Hongera sana Chisano.

    Hakika alistahili kupata hiyo tuzo kutokana na jinsi alivyo watumikia watu wake.

    Malipo ni hapa hapa Duniani,kwa Jah tunaenda kufunga hesabu tu.

    Nampenda pia kwani ni miongoni mwa viongo kwenye huu ukanda wetu anayependa kutumia lugha ya kiswahili.

    Kila la kheri afaya njema,Chisano kula bata sasa kivurini bila bugha...

    Mzee wa Lupaso ingawa naye taalum yake ilikuwa ni masuala ya ze upaparazi lakini nashangaa jinsi alivyowageuka wenzake baada ya kuingia madarakani..

    Kweli kuna watu na viatu..

    Naomba kuwasilisha..Tuzo zimetolewa kwa haki bin sawiya.

    ReplyDelete
  34. wewe mchuzi vipi unampennda sana huyo mkapa ,sasa ingekuwa zawadi za wizi bora angepata na muuwaji lakini ya heshima .

    ReplyDelete
  35. Nakumbuka yalisemwa mengi wakati wa Hasan Mwinyi, eti nyakati zile kila jengo jipya iwe hotel au vipi la Bi Siti Mwinyi..hiloo, eti yeye na mzee wanajiandaa wasiumbuke baada ya kibarua kuisha! Hebu tufikiri makini, sijaona baya sana alilofanya Mkapa, lakini amini nawaambia punde tu tutaanza kumsafisha kama tulivyofanya kwa Mwinyi, hata kuna baadhi walithubu kuanza kumsema Mwalimu kabla haidhihirika kuwa, walikuwa watu safi

    ReplyDelete
  36. Mkapa hawezi hata kuwa wa pili au wa tatu!

    Rais Mkapa alianza vibaya kwa kusema uwongo! Je, mnakumbuka tuhuma za mafuta ya kupikia zilizomwangusha Waziri Prof. Mbilinyi?

    Katika hotuba aliyotoa mbele ya Watanzania nyumbani kwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa hapo Mount Vernon, New York, mmoja wa Watanzania alitaka kujua serikali inafanya nini juu ya tuhuma za Waziri Prof. Mbilinyi kuhongwa na wanunuzi wa mafuta ya kupikia ya kutoka nje. Na kwa nini mashirika yetu yaliuzwa kiholela kwa bei ya chini sana kutolingana na “market values”?

    Kwanza Rais Mkapa aliona haya kulijibu moja kwa moja. Baadaa ya muda, alikaza roho na kusema kuwa tuhumu hizo hazina msingi wowote. Baadaye alijifunga kisabuni kueleza kuwa hizo tuhuma mahazima msingi hata kidogo. Kwani karatasi waliyogusha yenye nembo ya Ikulu na nambari za kumbukumbu ilikwa ni ya barua ya kibali kwa wahujaji wa kiislamu kwenda kuhiji Meka!

    Rais Mkapa alitaka kumlinda Mbilinyi kwa kusema eti “wanataka kupaka matope mawaziri wangu bure…Kabineti yangu ni safi sana….imeanza ‘on a clean slate’”!

    Lakini waliporudi Dar es Salaam, kabla ya walioandama naye hawajamaliza kufungua mizigo ya vile walivyonunua ugenini, kulikuja habari kuwa Waziri Prof. Mbilinyi amejiuzulu!

    Kuhusu hilo la kuuzwa kwa bei ya chini mashirika ya umma, kweli kakiri kuwa tulipunjwa sna!

    Kuna utata wa ukweli wa bonge la jiwe lenye dhahabu alilozawadiwa huko Bulyankulu.

    Waziri wa Madini na Nishati Yona alitoa majibu ya kubabaisha.

    Mwisho Rais Mkapa akaja juu kuwakemea waandishi wa habari. Mpaka sasa hilo jiwe halijulikani liko wapi!

    Sijui ni kwa nini “Mzee wa Kiraracha” Augustine Lyatonga Mrema hakuifuatilia tuhuma hiyo, kama alivyoanza?

    Kukaja tena utata wa mkataba na kampuni ya Malaysia kuhusu uzalishaji wa nishati.

    Kukaingia tena tuhuma za ushemeji kwa kampuni ya uendeshaji kutoka Afrika Kusini kuendesha shughuli za Tanesco.

    Yakaingia tena maneno ya kampuni ya wakina Yona na mtoto wa Mkapa, Steven, kuhusu maliasli ya mkaa wa Tanzania!

    Juzi juzi zikamwaga tuhuma nyingine za mikopo ya pesa na kibali cha kuundwa kwa Benki ya M (Mkono/Mkombozi) ambayo inapanga katika nyumba ya Mkapa Dar es Salaam - Benki ya mwanasheria na m-Bunge mtunga sheria aliyedai kuwa ilimbidi ashirikiane na Wahindi kuanzisha benki hiyo kwani sheria za nchi ni kikwazo kwa wazawa kuweza kupewa kibali kama hicho.

    Kama sheria ni mbaya, kwa nini huyu m-Bunge asiweze kuzirekebisha yeye na wa-Bunge wenzake?

    Na mengi yatajitokeza! Mkapa ajitokeze kusawazisha!

    ReplyDelete
  37. I KNOW THAT THIS IS AN OPEN BLOG, AND THAT EVERYONE CAN PUT OUT THEIR OPINIONS, BUT I AM TARGETING THIS PERSON ...JOMABE.... HIVI WEWE UNAISHI NCHI GANI WEWE? WE NI MTANZANIA WEWE? AU NDIO NYIE WATOTO WA MKAPA AU NDUGU ZAKE? MIE NADHANI NA WEWE UKO USHIRIKA MMOJA NA MKAPA, ILHALI WEWE NI MKURUGENZI WA MOJA YA MAKAMPUNI ALOFUNGUA MR & MRS MKAPA!

    KWENYE DUNIA NYINGINE, MIE NADHANI MKAPA NA FAMILIA YAKE WANGEKATWA KATWA MAPANGA KABISA! THIS PRESIDENT WAS ARROGANT, AND HE LOOKED AT EVERYONE WITH DISDAIN, FROM THE TIP OF HIS NOSE!

    MIE NASEMA, KAMA AMEJENGA UWANJA WA NDEGE NA BARABARA, HUO ULIKUWA NI WAJIBU WAKE, IN FACT HIZO NI PESA ZA WAFADHILI AMBAO WANA-DICTATE WHAT SHOULD BE DONE. SO HE WAS FOLLOWING ORDERS! IN FACT WE SHOULD BE THANKFUL FOR THE DONORS BECAUSE KAMA ANGEPATA CHANCE KIDOGO TU, I AM SURE ANGEHAMISHA NUSU YA PESA ZILIZOTUMIKA, LABDA AKAJENGA HOTELI NYINGINE SOUTH AFRICA! MWIZI MKUBWA! MAANA VIONGOZI WENGINE HUWA WANAIBA, NA KUONA SONI, LAKINI THIS GUY WAS JUST CHARGING FORWARD, TAKING MORE AND ALL HE CAN TAKE! KUUZA MAKAMPUNI, KUNUNUA RADA NA NDEGE MBOVU, I MEAN WHO THE H_ _ _L DOES THAT? HALAFU JUU YA YOTE ANAKAA KIMYA.

    MKAPA, TAKE MY ADVICE...KAMA ULIVYOKWIBA KUTOKA KWA WANANCHI...(KIMYA KIMYA) TAFUTA NCHI ITAKAYOKUKUBALI, HALAFU TOKOMEA HUKO WEWE NA FAMILIA YAKO YOTE(KAMA IDD AMINI DADA), LA SIVYO TUKIAMUA WANANCHI KUKUPROSECUTE, NADHANI (KAMA MMASAI ALIVYOIMBA)ITAKUWA MBAYA SANA!

    ReplyDelete
  38. Hapo naona waandishi wanafiki wanashindana kucheka kwa nguvu mpaka wanainamia chini (isipokuwa Michuzi na jamaa wawili, wanacheka kwa pozi), kwa kuwa Mkapa katoa joke-utumbo. Bongo bwana.

    ReplyDelete
  39. Hebu acha kututia kichefuchefu! eti mnasikitika! Kwa kipi alichokifanya kwa waandishi wa habari? Si alikuwa anawatukana kila siku au umesahau? Mwizi huyo, mla rushwa na fisadi mkubwa kabisa. Ana tuhuma nzito kabisa dhidi yake anakataa kuzijibu eti, "Niacheni nimestaafu" tutamzomea kila tutakapomuona kwa ufisadi wake mpaka ajute kwanini alituibia na tutashibikiza katiba ibadilishwe ili mvua imnyeshee akamalizie maisha yake lupango.

    ReplyDelete
  40. anamtetea kwa kuwa amipiga picha moja

    ReplyDelete
  41. Hii blog basi tu ishakuwa michezo kwa wote!!!
    Michuzi acha nidhamu ya woga!! BMW hayupo kwenye madaraka!! Speak your mind we ni babu sasa, miaka 45 si mchezo!!Next utasema Karamagi na Mapuri wanastahili tuzo za mawaziri bora waliowahi kutokea Africa.

    ReplyDelete
  42. Mimi nina hasira, naomba huyu mtu ashitakiwe afungwe jela ya Ukonga. Nakuomba Mtikila popote ulipo ushughulikie suala la Ben, jitahidi sana kwenye hili, achana na Ditopile. Mimi nabeba boksi majuu, lakini uchache wa kulipia gharama za kesi ninao. Anayewasiliana na Mrema naomba umwambie aibue tena ishu ya lile tofali la dhahabu.
    Asanti.

    ReplyDelete
  43. Ndugu zangu, watanzania, tunakumbuka kuhusu primitive accumulation? Mkapa katukuta tunavaa viraka, leo tuna wabongo tena weusi kuliko wana weza kuenda majuu kuleta biashara kama kazi! Hivi tunajua sisi wabongo tulitawaliwa na makampuni na sio nchi..? anza na wajerumani hata waingereza! na hizi zilikuwa kampuni binafsi! tusome historia, fedha au pesa ni nini, katengeneza nani, nani anasema zichapishwe, na kwa nini wote tunaziabudu? hivi unadhani kumfukuza kazi mtu ni kama kutupa mpunga ili uote kila pahala? muulize JK alijuta kufanya hivyo! Unajua kuhusu mamlaka ya waziri, katibu mkuu wa wizara? hata Raisi hawezi kutengua maamuzi bila kufanya maamuzi magumu! hivi mnajua nchi zilizoendelea mapinduzi ya kiuchumi yalifanywa na makampun binafs na sio serikali? Na hao wote walipata pesa au fisadi kwa kunyonya wengi? Ndugu yangu hakuna mafanikio bila kuwa fisadi kama mnavyoita siku hizi! hata mababu zetu walikuwa watemi kwa kuwa na watumwa, somemi historia!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...