CULTURE ZIARANI ULAYA

Na Kwame Mchauru

Kikundi maarufu cha muziki wa taarab asilia kutoka Zanzibar kimeondaka usiku wa leo tarehe 18 Oktoba kwa ndege ya shirika la ndege la Uswisi kuelekea Zurich kwa ajili ya kuanza ratiba ya maonyesho kadhaa katika nchi mbalimbali ulaya.
Safari hiyo inayoratibiwa na kampuni ya Jahazi Media iliyopo chini ya bwana Werner Graebner itawachukuwa wasanii hao kipindi cha mwezi mmoja na nusu kabla ya kurejea tena nchini.
Culture Musical Club ni moja ya makundi ambayo yanaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kufanya maonyesho mengi zaidi katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Kiongozi wa msafara huo bwana Tainur Rukun amesema kuwa katika safari hiyo kutakuwa na wasanii 12 na watatu kati yao wakiwani wanawake watakaoongozwa na mwimbaji maarufu wa taarab bi Rukia Ramadhani.

Ratiba kamili ya maonyesho yao ni kama ifuatavyo:

CULTURE MUSICAL CLUB OCTOBRE / NOVEMBRE 2007
20, MARSEILLE, Festival Fiesta des Suds (France)
26 oct ANVERS, Zuiderpershuis (Belgium)
27 oct AMSTERDAM, Royal Tropical Institute (Netherlands)
30 oct DIJON, Théâtre des Feuillants (France)
02 nov COLOGNE Philharmonic Hall (Germany)
03 nov DARMSTADT Zentralstation ( (Germany)
04 nov ZURICH Moods (Switzerland)
05 nov WIEN Konzerthaus (Austria)
06 nov LUXEMBOURG Philharmonic Hall (Luxembourg)
07 nov BREMEN Radio Bremen (Germany)
09 nov HANNOVER Pavillon(Germany)
12 nov ABBEVILLE, Centre Culturel (France)
13 nov LE MANS, Palais des congrès (France)
14 nov BESANçON, Opéra Théâtre (France)
15 nov BOURGES, Maison de la Culture (France)
16 nov BELFORT, Le Granit scène nationale (France)
17 nov AULNAY SOUS BOIS, Le Cap (France)
18 nov MASSY, CC Paul Bailliart (France)
22 nov LAS PALMAS, Festival Womad (Spain)
23 nov LAS PALMAS, Festival Womad (Spain).
Wasanii wa kundi hilo kwa majina ni kama ifuatavyo:
Rajab Suleiman (qanun, kidumba) kAli Hassan (‘ud, bandmaster) Ramadhani Khamis (first violin) Juma Abdallah (violin) Makame Faki (vocals, violin) Taimur Rukun (accordion), mkwasa Mahmoud Juma (double bass, cherewa) Foum Faki (bongos, kidumbak) Amour Haj (dumbak, sanduku) Rukia Ramadhani (voc;als, chorus) Nuru Raphael (chorus, rika, dance); Asha Othman (chorus, dance).
Bofya linki hizo hapo chini uwaone na kuwasikiza wafalme hawa wa bashraff:

http://www.bbc.co.uk/radio3/womad2004/taarab_dezanzibar.shtml

http://www.bbc.co.uk/radio3/worldmusic/onlocation/zanzibar1.shtml

http://www.mondomix.com/en/videos.php?artist_id=764&reportage_id=2215

http://www.seattlechannel.org/videos/video.asp?ID=4057

http://depts.washington.edu/kexp/blog/?p=1367

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wallahi watu wa Seattle USA mlifaidi mambo, nadhani na hata bara ulaya yote mtafaidi taarab original toka Culture, naomba muiangalie link ya seattlechannel.org ya urefu wa dakika 55(hamsini na tano)nzima kama Michuzi alivyotuwekea hizo link.
    SeniorJumior
    London.

    ReplyDelete
  2. kwa nyie msiojua TAARAB ukisikia taarab basi ndio hii

    siyo MATUSI YALIYOJAA KWENYE HIZO NYIMBO MNAZIITA MIPASHO

    yaani hapa maalim Michuzi umenipeleka mbali sana mzee

    hii ndio taarab bwana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...