
huu ni ujumbe tulioletwa na ras twin toka washington metro wa agosti 27 mwaka huu
Ndio Michuzi,
Ndio Michuzi,
Eee Bwana huyu Lucky Dube amefanya onesho moja hapa Washington DC Metro Area usiku huu (sasa ni saa tano usiku wa kuamkia Jumatatu ya tarehe 27/8) ambalo kwa hakika ni kati ya maonesho bora kabisa kufanywa hapa kama ilivyoelezwa na wengi waliohudhuria. Hao kinamama anaoimba nao wamefanya uchezaji wa "kufa mtu" pale wanapochanganya midundo yao ya Reggae na uchezaji wa muziki wa asili wa ki-Afrika. Wimbo wao wa 'Ding Ding Licky Licky Bong' ndio uliotia fora zaidi katika onesho lao ambalo lilidumu kwa takriban masaa mawili. Hizo ni baadhi ya "taswira" nilizoweza kukamata yapata saa moja lililopita.
Blessings
Ras Twin


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...