Mzee Michuzi,
Najua wewe ni mpenzi wa Twanga, ila Nilikuwa naomba muda kidogo ili nimwelimishe bwana Ali choki kuhusu kitendo chake cha kusema mziki wa twanga pepeta ni watanzania.

Ningependa kusema kweli muziki wa kitanzania ni mziki wa Msondo Ngoma, DDC Mlimani park au Taarabu au mziki wa Asili. Mziki wa twanga pepeta ni sawa na muziki wa Gen Defao lakini bado wanashindwa kupiga kiuhakika.mziki wetu wa Tanzania na Congo unatoka kwa mama mmoja na baba moja yaani Cuba.
Ukisikia nyimbo za kale kwa mfano salum abdalaha, nuta jazz band, na Wendo kolosy,Rumba nela au shikamoo jazz au Tabora jazz au jamuhuri jazz band na Grande kale au Franco miaka ya 50 na 60 alafu usikie na mbaraka mwinshe hakuna tofauti ila hawa ndugu zetu waliuchukuwa huu mziki kutokana na kuwa na studio nzuri miaka ya 60,sabini,mpaka80.

kutokuwa na studio na kuwa na siasa mbaya za biashara miaka ya nyuma iliufanya mziki usijulikane,miziki ya Tanzania ilikuwa haijulikani mpaka leo bado tuko chini tunajurikana Kenya na Uganda kidogo au Rwanda na BurundiNaomba sana bwana choki aangalihe vizuri na atafute historia ya muziki wa Tanzania intokea wapi.
Nyimbo ya Dada Asha na ilikuwa moto wa konea mbali kule kinshansa miaka ya sabini.Nacho taka kusema fitina na chuki katika hii biashara ya muziki au kusema maneno yasiyo na manufaa hayafai waCongo waTanzania ni ndugu zetu kama walituacha mbasi tujfunze kutoka kwao ile nasi tuwe imara.wanamuziki wengi kutoka congo wanaokaaa ulaya wanakwambia ni nchi moja tu Africa ina wanamuziki ambao wanaweza kupiga muziki wa kiafrica na watu wakaukubali ni Tanzania.
kwahiyo bwana choki mziki wa twanga ni wa kiafrica na unatokea cuba yaani cuban rumba,na rumba yenyewe inatokea kwenye neno la kabila la bakongo kutoka kule congo,mziki huu unatokea kwenye ngoma za kiasili na neno la kwanza walilio kuwa wanatumia kabla ya kuchukuliwa na kuwa watumwa lilikuwa nkumba watumwa walipokuwa kule cuba walianzisha vikundi vya muziki walikuwa wakitumia ngoma za kiasili walipoingiza vyombo vya wazungu kama gita na saxponi na vyombo vingine ndipo wakatoa neno rumba na kutokea wakati huo mziki ukaanza kuitwa rumba na ukarudi Africa na jina lingine la rumba miaka ya 35s and 40s.

kwa hiyo Ali choki naTwanga pepeta msilete mambo ya uswahili au mambo ya kiuni muanze kupinga mziki uliojaa mziki wenye maneno safi na muwe wenye heshima na muache watu wachague wenyewe mziki wenu si mbaya lakini una makosa lazima muyarekebishe muziki uwe na radha ya kucezwa kwenye club africa.

Bendi ambayo zinauwezo wa kupambana na fm academia ni msondo ngoma na ddc, na akudo.bwana michuzi soon nitakuwa na network ambayo itautangaza na kufanyia mziki wa Tanzania markert.

Bwana michuzi Fm academia ni bendi nawapiga muziki uliojaa. msondo ngoma ni bendi kongwe katika ukanda wa africa mashariki na kati mpaka kusini na mziki wa msondo wacongo wanakwambia msondo ngoma ni TP OK JAZZ YA AFRICA KUTOKANA MPAGILIO WA VYOMBO NA SAUTI NA MZIKI WAO UWA UMEJAA.

BWANA ISSA MICHUZI NITARUDI TENA.

asante
yusef uk.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MHESHIMIWA UMEJARIBU KUELEZEA KUHUSU MUZIKIWETU NA WA KONGO, LAKINI BAHATI MBAYA INAELEKEA HIYO MIAKA YA 50 NA 60 ULIKUWA HAUJAZALIWA AU ULIKUWA KIJIJINI HIVYO UMESHINDWA KUELEZA KIUSAHIHI. MBARAKA MWINSHEHE YEYE ALIKUWA AKIMUIGA FRANCO, VIVYO HIVYO BENDI ZETU NYINGI ZILIKUWA ZIKIIGA NYIMBO ZA KONGO,KUIGA HUKO NDIKO KUMETUFANYA LEO TUWE NA BONGO FLAVA BAHATI MBAYA ZAIDI NDIO UNAOTUKUZWA KULIKO ULE WA AKINA SISI TAMBALA. MUZIKI WA AKINA BOSCO AMBAYE ALIKUWA MKONGO NDIO ULIOTAMBA SANA, UTASHANGAA KUONA WAKONGO NA WAKENYA ENZI HIZO WALIPENDA SANA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA MUZIKI, TANZANIA TULIKUWA NA WANAMUZIKI WACHACHE SANA WALIOTUNGA NYIMBO ZAO BILA KUIGA MMOJA WAO NI FRANK NA DADA ZAKE, KIKO KIDS! SALUM ABDALLA NA MTUNZI WA MALAIKA. HIVYO UTAONA KUWAQ WATANZANIA BADO TANATANGATANGA KIMUZIKI KAMA TUNAVYOTANGATANGA KIVAZI HATUNA MWELEKEO WA KITANZANIA ZAIDI YA KUJIVUNA KUWA MUZIKI WETU UMEKUA! NI UPI? MIMI, WEWE NA YULE TUTAENDELEA KUBISHANA MPAKA MILELE BILA KUPATA UFUMBUZI. BONGO HATUPENDI KUSUMBUA UBONGO TUNATAKA SIMPLE SIMPLE, CHAP CHAP, KANYAGA TWENDE, OKOA MUDA. JE, TUTAFIKA?

    ReplyDelete
  2. haina tatizo muziki kufanana, vitu vidogovidgo sana vinatofautisha muziki kati ya bendi au nchi .

    Muziki wa twanga pepeta ni
    watanzania;... kama vile muziki wa Salum Abdalah ulivyukuwa wa Tanzania bila kujali jina lake Cuban marimba au midundo yake ya Rhumba na chachacha .

    Music is music, music is universal , ....kuna bendi za zaire zilitumia chorus za wimbo ASHA toka Bongo kutengeneza album ya Lagos night au Nairobi night kama sikosei .
    Muziki unaongea lugha moja . Labda ndo sababu UB40 wamefanikiwa kimuziki .

    ReplyDelete
  3. yusef uk.>>> Au Choki alipoimba .... NINA MDODO WANGU NAANGUSHA MOJAMOJA LEOOO INAMA INUKA WEEE NANGUSHA MOJAMOJA LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO LEOOO Anadhani ndio mapigo ya kipimo chake cha kusema mziki wa twanga pepeta ni watanzania. Ha ha ha haaaaa!!!

    ReplyDelete
  4. Mi nafikiri hayo ma drum machines wanatumia hawajajua kuya arange sawasawa ndio maana inakua kama wanapiga madebe tu hakuna mapangilio
    Inabidi waweze kuandika na kusoma muziki

    ReplyDelete
  5. Muziki wote ni do,re,mi,fa,so.la,ti,do'
    Kinachohitajika ni arrangement ya Instruments na vocals.Sijui kama maproducer wetu wana huo utaalam,
    Na wana muziki wetu wana papara sana kurekodi nyimbo . Mtu utatoaje album mbili kwa mpigo?

    ReplyDelete
  6. Kuna siku nilisoma mahojiano ya Fresh Jumbe na jamaa wa bongo celebrity.Yule ndio alitoa majibu kuhusu nini kifanyike.ningeshauri wadau wa muziki wayasome
    http://bongocelebrity.com/2007/09/23/tusibweteke-fresh-jumbe/

    ReplyDelete
  7. muziki ni muziki tu, acheni malumbano yasiyo na maana.

    ReplyDelete
  8. Aliyetoa mada mwanzoni anatakiwa ajifunze ku-edit kazi yake.Ingawaje umejitahidi kiufanisi kuelezea lengo lako lakini sentensi zako nyingi zimeishia hewani hazieleweki.

    ReplyDelete
  9. Bw. Anonymous Said!
    Aliyoyasema huyu jamaa ni kweli kabisa kuhusu muziki wa Bongo na wa Kikongo kuwa asili yake ni moja. Na unayoyasema wewe pia ni sawa kwamba sisi wa Tanzania toka enzi na enzi tunapenda sana vitu vya kuja ama kuiga.

    Kumbuka miaka ya 70 wakati Maquiz wana Kamanyola walipoingia TZ walikuwa hawapigi muziki wa kutisha, lakini cha ajabu watanzania wengi walipenda muziki wa Kamanyola bila jasho. Nyimbo zao nyingi ziliimbwa katika kiswahili cha kuboronga na hata mapigo yao yalikuwa si ya kutisha ila watu pamoja nami tulipenda kusikia vitu tofauti. Na muda ule Bongo kulikuwa na bendi kali ambazo zilimpita hata Franco kwa upigaji, bendi kama NUTA, Tabora Jazz, Mbaraka na Moro Jazz, Nyanyembe, yaani nyingi tu za kutisha lakini tulizidharau na kufuatia Maquis kwa sababu walikuwa tofauti na wanatoka nje ya TZ.

    We chukulia mfano wa sasa, Bongo Flava ni muziki wa kijinga (Computer made) lakini wabongo hata mtu mzima na akili yake anaona ujiko kusikiliza Flava. Ukiuliza unaambiwa kwenda na wakati, for what? Sasa muziki wa Flava ndio umekuwa kazi, maana kila kijana akiwa na njaa anajiingiza kwenye Flava ili naye apate hela ya kula na kutanua na ndio maana kwa sasa muziki wa Flava hauna hata radha, maana utakuta kila mtaa kuna watu 50 au zaidi wanajishughulisha na muziki huo matokeo yake unakosa hata msisimko. Lakini kwa kuwa wanawaiga wamarekani weusi sie tunaona ujiko na kuubeza huo muziki.

    Muziki unatakiwa na ujuzi ama kipaji na Flava hamna kitu kama hiki. DJ anachukua beats za watu na ku-mix kwenye computer then anampa mtu kuimba masuala ya pipi pipi sie tunaona ujiko because tunaiga wamarekani weusi, yaani mpaka imekuwa kero. Sie wabongo ni wajinga wa kuiga na hatuna msimamo hta kidogo. Ila kwa kuishia ni kwamba, muziki asili haswa wa Tanzania ni ule wa Msondo, Sagha Rhumba, Sikinde, na bendi nyingine zinazopiga kama hizo nilizozitaja hapo juu, ila kamwe si 'ganga njaa' Flava!

    ReplyDelete
  10. Ufafanuzi sahihi juu ya muziki wa kitanzania waweza kupatikana kwa kufanya utafiti kwa kuwahoji wanamuziki wa zamani kama vile maalim Gurumo, Bichuka, Juma Kakere, Zahirim Ally Zorro na wengine.

    Pia ili kudumisha muziki wa kitanzania ni vema bendi changa kama Twanga pamoja na wanamuziki wapya wakajifunza toka kwa bendi za zamani zilizopo hadi sasa-ninamanisha Msondo, Sikinde na nyingine. Japokuwa ubunifu pia wahitajika lakini tusipoteze asili ya muziki wetu.

    Hata ikibidi ni vema kuwauliza CHAMUDATA kwani waweza kuwa na ufahamu kiasi juu ya masuala haya ya muziki.

    Kwa heri kwa leo.

    MSAHAMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...