Bendi ya FM Academia Band “Wazee wa Ngwasuma” na Msondo Ngoma zitatumbuiza katika tamasha la taasisi za elimu ya juu litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pia kutakuwepo na wasanii wengi wa bongo flava. Kiingilio ni bure.

Wadhamini wa tamasha hili linalojulikana kama Intellectuals Gala 2007 ni pamoja na benki ya NMB kupitia “Student Account”, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Ndovu,kampuni ya Macmillian Aidan Ltd, Alphatel na Ultimate Security Limited.

Alivitaja vyuo vilivyothibitisha kushiriki kuwa ni Chuo cha Ardhi (ARU), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Uandishi wa Habari (IJMC), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), Chuo Kikuu cha Tumaini na Chuo Kikuu cha Kairuki.

Vingine ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Biashara (CBE), DIT, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chuo cha Maji, Chuo cha Uhasibu (TIA), COET na Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS).


Washindi wa jumla watapata shilingi laki tatu pamoja na kikombe wakati washindi wa pili wa jumla watapewa laki mbili.

Washindi kwenye mpira wa miguu wa watu saba (seven-a-side) watapewa kikombe na T-Shirts. Wachezaji 12 wa soka kwa timu iliyoshinda watafunguliwa akaunti yenye fedha kiasi cha shilingi 25,000/- kwa kila mmoja.

Washindi wa pili kwa upande wa soka watapewa kikombe na jezi 12 za timu ya Taifa ya Soka, Taifa Stars.

Washindi kwenye kuvuta kamba watafunguliwa akaunti yenye thamani ya shilingi 10,000/- kila mmoja na jezi tano za timu ya taifa, Taifa Stars.

Washindi wa pili katika kuvuta kamba watapewa fulana na kufunguliwa akaunti kwenye beni ya NMB.

Watakaoshinda katika mbio za mita hamsini za magunia kwa upande wa wanaume na wanawake watafunguliwa akaunti yenye thamani ya shilingi 30,000/- kwa kila mmoja.

Washindi kuanzia wa pili hadi wa tano kwa upande wa wanaume watapewa fulana na kufunguliwa akaunti benki ya NMB wakati kwa upande wa wanawake watapewa vitopu vyenye nembo ya NMB.

Washindi wawili katika mbio za mita 50 watafunguliwa akaunti zenye thamani ya shilingi elfu thelathini wakati mshindi wa tatu hadi wa tano kwa upande wa wanaume watapewa fulana. Wanawake watapewa vitopu vyenye nembo ya NMB.

Washindi kwenye mashindano ya kuimba na kucheza watapewa fedha taslimu shilingi 15,000/- na zawadi nyingine kutoka kwa wadhamini.

Watakaovaa mavazi ya ajabu (funniest dressed) kwa upande wa wanaume na wanawake watapewa shilingi elfu 20,000/- taslimu. Washindi watachaguliwa bila kufuata utaratibu maalum.

Zaidi ya wanafunzi 70,000 na wananchi wa kawaida wanatarajiwa kuhudhuria katika tamasha hilo ambalo halijawahi kufanyika hapa nchini kwa wanafunzi. Tamasha litaanza saa tatu asubuhi na kumalizika saa 12:30 jioni.

Tamasha hilo limeandaliwa na kampuni ya Capital Promoters International (CPI) kwa lengo la kuwaleta pamoja wanafunzi. Pia makampuni ya biashara yatatumia fursa hiyo kutangaza biashara na huduma zao.


MAWAZO WAZIRI
MRATIBU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. basi dada na kishanga chako chekundu cha kiunoni weeee

    ReplyDelete
  2. duu demu anaonekana ana mnyata kama kaburi la kitoto kichanga

    ReplyDelete
  3. HA HA HA HA HAAAAAA yaani tangu Blog hii ianzishwe sijawahi kucheka ktk Blog hii kama leo duh.... sasa uliyetundika huo mtundiko hapo juu Mnyata ndio nn??

    ReplyDelete
  4. ANTI UMEPENDEZA..NAONA UKO WET..

    ReplyDelete
  5. SINA MBAVU.KWELI MNYATA BAB KUBWA
    YANI NIMECHEKA HADI MBAVU ZINAUMA

    ReplyDelete
  6. Hao ni kachupi ka njano kenye pindo dogo jekundu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...