Kanisa la wa Tanzania na watu wote wanaotumia lugha ya kiswahili wanapenda kuwatangazia wadau wote wa blog hii popote walipo kwamba yule mwanamzuki machachari wa nyimbo za injili kutoka nyumbani Tanzania Dada ROSE MUHANDO atakuwa na onyesho kabambe katika kanisa hilo.
Onyesho hili la aina yake litaanza saa kumi kamili jioni siku ya jumapili tarehe 21.10.2007.Dada ROSE MUHANDO ni muimbaji aliyetokea kupendwa ndani na nje ya Tanzania, uimbaji wake wa nguvu na hisia kali unavutia watu wengi.
Rose Muhando ameshashinda tuzo mbali mbali za uimbaji.
Kwa wale watakaopenda waandaliwe malazi tunaomba wawasiliane nasi kupitia:
Email: umojachurch@yahoo.com,
Simu: 214 554 7381,
682 552 6402,
au 214 341 7287.
Kanda zote za Rose zitauzwa moja kwa moja kutoka ukumbini.
Kanisa lako ulipendalo la Umoja.


Kaka, Texas kubwa kama Tanzania in terms of land area. Sasa Rose Mhando yupo Texas jiji/mji gani?
ReplyDeleteUmoja Church lipo jijini Dallas, Texas.
Watanzania hua tuko shady sana kanisa hakuna cha adress wala ni na namba za simu hizo mara unapiga zimekatwa,jamani kwa nini tunapenda kuishi kitapeli?
ReplyDeletehuyo dada atakuwa TX ipi?kama alivyouliza huyojamaa hapo juu fafanueni ili watu wajue kama wataweza kwnda au la tangazo halijakamilika hilo
ReplyDeletehawa watayarishaji wajifunze wengine wanavyo weka matangazo na hata ikiwezekana wawe na website inayoelezea kila ktu kuhusiana na show hiyo. Sasa je atakuwa Texas tu au anaenda na state zingine
ReplyDeleteJamani tour yake ni vipi? Atakuja East Coast? Nina kanda zake nyingi tu na ni muimbaji mzuri sana. I hope atatembelea sehemu za huku.
ReplyDeleteWEWE DADA ROSE MHANDO UNAJUA KUIMBA...HASWA MALIZA HIYO SHOO HUKO TEXAS..SISI TUNAKUTAFUTA/KUSUBIRI KWA HAMU...SEMA BEI YAKO NYIMBO ZAKO ZINALIPA..halafu nyie wachungaji mnaoandaa hiyo shoo wekeni address basi ya hilo kanisa..."..NYIE HAMPENDI WAUMINI JAMANI ?? kumradhi lakini msije sema nina "..mapepo.." NI ADDRESS TU INAYOHITAJIKA WATU TUJE KUJIMWAYAMWAYA KWA YESU AU VIPI...
ReplyDeleteLabda ni kutokana na ushamba au ufinyu wa ufahamu nilionao juu ya mambo ya kidini yalivyo hivi sasa kwa kuwa niaishi kijijini sana. Hivyo naomba kuelimishwa kwa kina "HIVI HATA INJILI INAFANYIWA SHOO?" Nitashukuru endapo wenye ufahamu juu ya masuala haya ya injili mukinielimisha.
ReplyDeleteXP